Maswali yako yanauliza kwanini aamue hivi na kwanini asiamue vile. Sioni kama upo sahihi kuniuliza maswali ya aina hiyo.
Ni sawa na kuuliza kwanini Rais Jose Mujica aamue kuishi maisha ya usawa kwa kuwa rais lakini anaishi maisha ambayo hayaendani na cheo chake. Kwanini asingejitenga tu na kuishi maisha yake pekee?yani mbali kabisa na kuishi na watu ambapo kusingekuwa na suala la usawa.
Hakuna anayemlazimisha kuishi hivyo.
Nini kinamfanya aamini maisha ya usawa ndiyo sahihi?
Sijui kama umenielewa maana yangu hapo.
Swali langu linatokana na tabia za msingi kabisa mnazosema huyu mungu anazo.
Ambazo ni kuweza kufanya vyote, kujua yote na kuwa na upendo wote.
Nilitegemea mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mtoto mchanga wa mwaka mmoja hawezi kufa katika mafuriko.
Kwa sababu hata kama unaweka habari ya mtihani, huyu mtoto mchanga hakuna anachotahiniwa, kwani hajaanza hata kuujua ulimwengu.
Hapo tunaona jibu la mtihano ni la uongo.
Sasa kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu huu ambao mtoto mdogo kama huyo anaweza kufariki katika a natural disaster wakati mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao watoto wachanga hawawezi kufa katika hali mbaya kama hiyo?
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao manaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili kimantiki.
Swali ni sahihi. Kwa sababu ulimwengu tunaouona unapingana na tabia za msingi kabisa za huyo mungu mnayesema yupo. Tabia za kuweza yote, kujua yote na kuwa na upendo wote. Sasa nikiangalia maovu ya dunia nashangaa, imekuwaje mungu huyu akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Ina maana alitaka kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani akashindwa?
Kama alitaka ila kashindwa, ni kweli anaweza yote?
Au hakushindwa kuumba ulimwengu usiowezekana kuwa na mabaya ila hakutaka tu?
Kama hakushindwa kuumba ulimwengu usiowezekana kuwa na mabaya, ila hakutaka tu, ni kweli kwamba anatupenda na ana upendo wote?