Maelezo kuhusu Mungu ni ya kibinafamu zaidi na kwamba si ya Mungu Mwenyewe. Kwa hiyo kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu atathibitisha Mungu mwenyewe.
Na mpaka sasa, kwa kuzingatia uwezo wake unavyosemwa mkubwa wa kuthibitisha bila shaka, na jinsi ambavyo maneno yote ya kuwapo huyu mungu yanavyopwaya ukiyaweka kwenye mtihani wa mantiki, naweza kusema kuwa huyu mungu ni hadithi tu za kibinadamu katika jitihada za kujibu kile ambacho hakuwa na jibu nacho.
Which is very understandable as a coping mechanism.
Dini zilizofundisha kuwapo kwa mungu kwa miaka elfu na elfu kabla ya elimu ya kidunia kukua zilifanya mengi ya kijinga, lakini zilifanya mengi mazuri pia. Kama kuwapa watu a moral compass na kuweka rules of conduct katika maisha.
Sasa mimi ninachoshangaa ni kwamba, sasa hivi binadamu ameweza kuendelea kiasi cha kusoma misahafu na kuona kwamba hawa watu wa zamani walijaribu sana kujibu maswali ambayo hawakuweza kuyajibu, wakatunga habari za mungu ziwasaidie kuishi. Mtu akiona radi anakwambia sauti ya mungu hiyo, anajificha. Si sauti ya mungu, lakini akijificha anajiepusha na kupigwa na radi. It works. Watu hawauani ovyo kama wanyama etc.
Sasa leo, tumneweza kujua radi ni nini, inatokeaje na hatuhitaji mungu kuielezea radi, kwa nini tunamg'ang'ania mungu?
Leo kuna watu hawaamini katika kuwapo kwa mungu wanaishi maisha moral kuliko wanaoamini kuwepo kwa mungu walio Vatican City na Mecca, kwa nini tunamhitaji mungu?
Mungu kwangu naona ni kama mtumbwi uliotusaidia kutoka Kivukoni kwenda Kigamboni katika safari yetu ya kwenda Mjimwema. Sasa tumeshavuka Kivukoni, tumefika Kigamboni, hatuhitaji mtumbwi, lakini kwa woga wetu tunang'ang'ania tuubebe mtumbwi mpaka Mjimwema.
Utatuchosha bure.
Mungu angekuwapo tungekuwa na uhakika kuliko tulio nao sasa, maana ni tabia mbaya mungu kujificha wakati ana kila sababu na uwezo wa kujidhihirisha kwa namna ambayo haipingiki.