Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
kiranga ujuzi wote,uwezo wote,upendo wote ndo sifa pekee za MUNGU wetu, tokea umeanza kumsikia?....
Swali siyo sifa pekee, swali ni, je hizi ni sifa zake?
Hata kama si sifa pekee, kama sifa hizi ni sifa zake, na zinaleta mgogoro wa idea ya mungu wenu kuwapo kujipinga na tunachokiona duniani, ukweli kwamba sifa hizi si za pekee haumalizi mgogoro huu.
Mungu wetu anaweza kusemwa kuwa na sifa ya kuwa katika kila punje ya mchanga.
Lakini sihitaji kuitaja sifa hii kama haina relevance to my argument.
Umeelewa somo?
One mention only the things that are relevant to the case, if you bring something that is not relevant to the case you are wasting everybody's time.
And I am not about wasting time.
Maswali kama haya yananionesha vitu kadhaa.
1. Hujaweza kuuliza maswali mazuri zaidi yanayohusiana na hoja.
2. Hujaweza kufikiri kwa kina kuelewa maswali mazuri zaidi yanayohusiana na hoja ni yapi.
3. Hujaweza kufikiri kwa kina kuelewa pa kuanzia kunipinga ni wapi, ila unauliza maswali tu kwa kutapatapa
4. Hujaweza kuelewa kwamba nikiuhoji uwepo wa mungu kwa sababu tabia yake moja inaleta contradiction kati ya yeye kuwepo na ulimwengu tunaouona, hata kama ana tabia nyingi sana nyingine, kama hii moja haijamalizwa hiyo contradiction yake na kuwa cleared, hizo nyingine zote zinakuwa hazina maana. Kwa maana mungu wenu anatakiwa awe thoroughly perfect.Huwezi kusema "Huyu mungu yuko bomba kwenye tabia zake 999, hii ya elfu moja tu kachemsha tumuachie, tusihoji hii moja".
Huyo atakuwa mungu au katuni wa mungu?