nijothemaster
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 324
- 56
This is a contradiction.
Ni kama kuwezekana kuwapo "pembetatu duara" katika Euclidean geometry.
Katika probability kuna kitu kinaitwa "mutually exclusive events", vitu ambavyo vyote haviwezi kutokea pamoja.
Kwa mfano, uki flip coins huwezi kupata heads na tails ( kichwa na mwenge) kwa wakati mmoja.
Lazima iwe kimoja, heads or tails. Kichwa au mwenge.
Wewe unataka mutually exclusive events mbili zote zitokee kwa wakati mmoja.
Unataka kulazimisha pembetatu iwe duara.
Mkuu mfano leo hii ukisikia labda mtu ambaye aliyekuwa akiua watu nae leo ameuliwa. Je,unaweza kuhukumu hao watu waliyomuua kwa kusema hao waliyomuua huyo mtu muuwaji kuwa hawana upendo? Au utawapongeza kwa kitendo chao hicho?
Mungu anaweza yote,
Mungu ana upendo wote.
Kuna mateso (magonjwa, njaa, matsunami, vita na mauaji n.k)
UHURU JR, inawezekanaje sentensi tatu pale juu zile kweli kwa wakati mmoja?
Kwa nini kuna kuua na kuuana?,huyo mungu mwenye upendo wote na sifa zote kwa nini alishindwa kuondoa haya mambo yote?,je aliweza lakini hakutaka?,huyu mungu anaupenso wote kweli?,may be hakuweza je huyu mungu ana uwezo wote?,.
Mungu anayejua yajayo anahaja gani ya kunihukumu tena kwa kunichoma moto?,anafaidika nn?kwa nini anihukumu kwa kitu nilichoshindwa binafsi kujizuia kufanya naye alijua kabla!
Ikiwa kuna mungu wa aina hii basi ni hatar.maana kama mungu anapata hasira,huzuni,ghadhabu,na wivu lakini mnamtanabaisha kama mungu mwenye upendo na ajuaye yajayo !.maana ninavyojua mimi ili uwe na hasira ama ghadhabu lazima upate habar mpya
Mambo gani hayo yaliyotabiriwa na yakatokea?
Na mtu kutabiri kitu kwenye kitabu halafu kikatokea ni uthibitisho kwamba hicho ni kitabu cha mungu?
Ukiambiwa Isaya alimtabiri masiha kuzaliwa miaka 3,000 iliyopita, halafu Yesu akausoma utabiri huo na kujifanya yeye ndiye masiha wakati si masiha, na wala hakuna masiha, utasema kwamba Isaya alitabiri kweli na biblia ni kitabu cha mungu?
Kama ni utabiri tu mbona hata Nostradamus katabiri, kitabu cha utabiri wa Nostradamus ni cha mungu? Nostradamus ni mungu?
Naweza kuwa nauliza haya maswali mtu mwenyewe hata Nostradamus hujawahi kumsikia, judding by your posts here.
jibu maswali yangu kule kiranga....UFUNUO......
Kwa nini kuna kuua na kuuana?,huyo mungu mwenye upendo wote na sifa zote kwa nini alishindwa kuondoa haya mambo yote?,je aliweza lakini hakutaka?,huyu mungu anaupenso wote kweli?,may be hakuweza je huyu mungu ana uwezo wote?,.
Mungu anayejua yajayo anahaja gani ya kunihukumu tena kwa kunichoma moto?,anafaidika nn?kwa nini anihukumu kwa kitu nilichoshindwa binafsi kujizuia kufanya naye alijua kabla!
Ikiwa kuna mungu wa aina hii basi ni hatar.maana kama mungu anapata hasira,huzuni,ghadhabu,na wivu lakini mnamtanabaisha kama mungu mwenye upendo na ajuaye yajayo !.maana ninavyojua mimi ili uwe na hasira ama ghadhabu lazima upate habar mpya
Nipe post number, maswali unataka kujibiwa wewe tu, yangu hujibu.
Kwa nini mungu mwenye ujizi wote, uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu hili swali.
Mkuu mfano leo hii ukisikia labda mtu ambaye aliyekuwa akiua watu nae leo ameuliwa. Je,unaweza kuhukumu hao watu waliyomuua kwa kusema hao waliyomuua huyo mtu muuwaji kuwa hawana upendo? Au utawapongeza kwa kitendo chao hicho?
nimelijibu malanyingi basi angalia hilo #880
Hujajibu swali la msingi. Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mtu anaweza kuua wakati alikuwa na kila uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba ulimwengu ambao hakuna mtu anayeweza kumuua mwenzake?
Kama kuua kubaya hivyo, kwa nini mungu mwenye uwezo wote, unuzi wote na upendo wote karuhusu kuua kiwezekane alipokuwa akiuumba ulimwengu? Ingawa alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kuua hakuwezekani?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ilikuwaje akaumba ulimwengu ambao shetani anawezekana kuwapo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezekani kuwapo?
Mtu alishakuwa anaandika "mala nyi gi" kqanza kabisa napata wasiwasi na elimu yake.
Inaonekana Kiswahili tu shida.
Sasa kujibu maswali kwa logic ya Bertrand Russell tutaelewana?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ilikuwaje akaumba ulimwengu ambao shetani anawezekana kuwapo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezekani kuwapo?
Nina kuwa na mashaka kama kweli kuna Mungu mwenye sifa za upendo wote na uwezo wote.
Kama ni kweli anawapenda sana wanadamu, kwa nini anawaacha wateseke ili hali ana uwezo wa kuyaondoa mateso?
Inasemekana upendo wa Mungu kwa wanadamu ni mkubwa kuzidi ule wa baba kwa mtoto wake, hivi wewe UHURU JR ungekuwa na uwezo wa kuondoa let say magonjwa kwa mwanao ungemwacha augue au hata afe kabisa?
Faza huchoki kuliuliza hilo swali?
ulitaka atengeneze maroboti...? awe anayaamrisha,..sasahivi sikia njaa ukale,sahivi usilale mwezi,sahivi usimpige mwezio,sahivi tengeneza hiki,....ndo utakacho?