COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Nimekwambia tuzijadili kwanza sifa za Mungu kabla ya kuzungumzia mambo ya huu ulimwengu,mambo ya dini yako ya zamani kwamba "ana hukumu watoto na vitu kuu kwa makosa ya mababu zao" hii sio sifa ya Mungu. Sijakwambia uanze kuelezea matukio kwanza.

Kwahiyo tuanze kujadili sifa zake kwanza kwa ujumla wake na utoe tafsiri ya kujipinga.

Twende taratibu tu mkuu.
 

Tukio litatokeaje bila kuruhusiwa na sifa ya mungu?
 
Ndiyo maana mie nataka tujadili kwanza sifa na maana ya kujipinga.

Kujipinga maana yake ni kitu kimoja kuwa na mielekeo miwili tofauti.

Kama vile kuambiwa "mungu ni mwenye rehema isiyo na mwisho" halafu hapo hapo ukaambiwa "hasira ya mungu isiyo kifani itawawakia watenda dhambi".

Au kuambuwa mungu kwa asili ni kilele cha uzuri, halafu akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Nishakueleza kuhusu sifa za mungu na zinavyojipinga hapo.

Imekuwaje mungu ambaye ni kilele cha uzuri akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Inawezekanaje mungu mwenye rehema isiyo na mwisho aumbe viumbe ambao atawachoma katika moto wa milele?

Hususan kama hizo akiki za kujua mema na mabaya wanazotakiwa wazitumie kumjua mungu kawapa mungu yeye mwenyewe?

Mtu akishindwa kumjua mungu kwa akiki ambazo ukomo wake umepangwa na mungu, huyu mtu ana makosa ya kutomjua mungu au mungu ndiye ana makosa kwa kumpa huyu mtu akiki ndogi ambayo imeshindwa kumjua mungu?
 

Twende taratibu.

Umesema kuwa Kujipinga ni kitu kimoja kuwa na mielekeo miwili tofauti,sasa mie kwanza kabisa nianze kujadili hitimisho unalotumia kutokana tafsiri hiyo.

Hicho kitu kuwa na mielekeo miwili tofauti inakuwaje ndiyo iwe sababu ya kutokuwepo hicho kitu?
 

Kwa sababu kinakosa logical consistency.

Nimetoa mfano katika Euclidean geometry hakuna "pembetatu duara".

Kwa sababu kitu kimoja hakiwezi juwa pembetatu halafu kikawa duara hapohapo.

Pembatatu duara haiwezi kuwapo, kwa sababu kabla sijaipinga kuwepo, yenyewe inajipinga. Pembetatu haiwezi kuwa duara na duara haliwezi kuwa pembetatu.

Mungu wako anajipinga kama "pembetatu duara" inavyojipinga katika Euclidean geometry.

Kwa sababu ana sifa zinazom contradict yeye mwenyewe kuwepo kama sifa za "pembetatu duara" zinavyo contradict kuwepo kwake.
 
 

Labda nitoe mfano,tufanye mimi Tz mbongo niseme kuwa mimi ni mpole,mkorofi na mgomvi. Tukitazama hayo niliyoeleza kuhusu mimi ni kama yanatofautiana kwa maana kwamba mpole hawezi tena kuwa mkorofi au mgomvi kuwa mpole, ndiyo inavyoeleweka hivyo. Lakini kwa hayo niliyoyaeleza kuhusu mimi Tz mbongo ambayo yanaonekana hayaendani ndiyo je,ndiyo huniondolea mie uwepo wangu?
 

Wewe TzMbongo "mpole, mkorofi na mgomvi" ni kitu cha kufikirika. Haupo.

Kwa maana ukiwa mpole huwezi kuwa mgomvi na ukiwa mgomvi huwezi kuwa mpole.

Huwezi kuwepo TzMbongo "mpole, mkorofi na mgomvi" kama "pembetatu duara" isivyoweza kuwepo.

Kwa sababu hamna logical consistency katika kuwepo huko.
 

Sasa sipo mimi au haiwezekani kuwa na hizo sifa kwa wakati mmoja?
 
Wewe nani?

Tuende poloepole, hatua kwa hatua.

Wewe mwenye sifa hizo zote kwa pamoja haupo, unakubali au unakataa?

Sasa sipo mimi au haiwezekani mimi kuwa na hizo sifa kwa wakati mmoja?

Swali linaeleweka kabisa.
 


1.Swali nililokuuliza ulitakiwa kulijibu kwasababu majibu yake yalikuwa mawili.uthibitishe au ufanye vyovyote ambavyo tafsiri yake itakuwa umeshindwa kujibu lakini Jinni yupo na huo udakuzi unafanyika.
2.Ukumbuke tangia mwanzo unahitaji uthibitishiwe uwepo wa Mungu.
Lakini ukumbuke Mungu ninaemtaja mimi ni kama muislam ni MUNGU WA GHAIBU.
Sasa nakushangaa unaponambia kwamba umedismiss swali kwasababu swali langu liko irrelevant to the topic.

Mimi nimekuuli vitu ambavyo wewe kwako ni GHAIBU VILEVILE.Labda uje s
 

Inaonekana kama umepost kwa bahati mbaya ulikuwa hujamaliza kuandika vile.
 
Kiranga

Labda uje useme kwamba jinni haumjui wala udakuzi haujawahi kuusikia maishani mwako.
Lakini kama hivyo vitu umewahi kuvisikia unatakiwa unithibitishie uwepo wake.
 
Last edited by a moderator:


Asante kwa hii Elimu. Umekwenda vyema kweli. Ha ha ha haaa nimefurahi sana kusoma comment yako Mkuu. Very wise.
 


Sasa sipo mimi au haiwezekani kuwa na hizo sifa kwa wakati mmoja?

Wewe nani?

Tuende poloepole, hatua kwa hatua.

Wewe mwenye sifa hizo zote kwa pamoja haupo, unakubali au unakataa?

Sasa sipo mimi au haiwezekani mimi kuwa na hizo sifa kwa wakati mmoja?

Swali linaeleweka kabisa.

Wewe mwenye sifa hizo haupo, unaelewa hilo maana yake?

Maana yake Tz mbongo kama Tz mbongo nitaendelea kuwepo ila haiwezekani nikawa na sifa hizo kwa pamoja??



Haya ni Matokeo ya kitu nakiita. CHOICE. after receiving the Knowledge, You weigh n pick Sides. Kisha unatumia elimu yako, iloyokupelekea kuwa na uwezo ulio nao kufanya Argument against the Existence of GOD Or His Absence.

Hakuna kati yenu mwenye uwezo wa kumridhisha mwenzake maana kila swali unalouliza kuna namna unataka ndio ujibiwe, ukijibiwa otherwise unajenga hoja yako hapo. Tambueni kuwa, katika kuwaza kwenu, pia upo uwezekano mkawa mnatumika vibaya na Shetani kwa wanao amini uwepo wake, lakini pia kwa Asie amini uwepo wake atapuuza uwepo wake na wa shetani, lakini kupinga huko hakumaanishi yupo, lakini pia hakumaanishi hayupo. Tukubaliane kwamba sisi ni matokeo ya ELIMU tuliyonayo juu ya mambo haya Mawili.

MIMI NAAMINI MUNGU YUPO. Wewe usie Amini usinifuate mimi ninae amini yupo uniambie ETI MUNGU HAYUPO. Kwanza hiyo ni Civil Case, NENDA KWA WENZIO WASIO AMINI UWEPO WAKE MKAENDELEE KUJIBISHANA NA KUONGEZEANA UDHIBITISHO KWAMBA HAYUPO. KAMA AMBAVYO NA SISI TUTAKAVYOKUTANA NA TUNAONAMINI TUKAENDELEA KUSHUHUDIANA NA KUJIONGEZEA ELIMU ZAIDI YA UWEPO WA MUNGU HASA KATIKA KIZAZI ENDELEVU KAMA HIKI NA KIJACHO.. Pia Nafasi ya Shetani katika Elimu tunazopata, namna ambavyo anaweza cheza na akili za wachapaji/waelimishaji na hao wenye mamlaka yakutoa machapisho, ama elimu juu ya Jambo Fulani.

We Must be Careful.
 

Swali uliloulizwa hujalijibu, ulilolijibu hujaulizwa.

Choice inekuja baada ya mungu kuanua kuumba ulimwengu huu, na choice itakuwapo, na choice hiyo itakuwa na mipaka gani, hivyo ndivyo maandiko yanavyosema.

Kwamba ulimwengu na misingi yake vimeumbwa na mungu.

Swali langu halihusiani na kutaka kujua kwa nini kuna manaya katika ulimwengu huu, lingekuwa swali ni hilo, ungeweza kunijibu kwamba, kuna mabaya kwa sababu watu wamepewa uwezo wa kuchagua mema na mabaya nao wanachagua mabaya.

Swali langu ni tofauti, na hujalijibu.

Swali langu ni, mungu huyu mnayemsema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, ukiwamo uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kabisaaa, kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani?

Ni kweli alikuwa ana uwezo wa kuuumba ukimwengu huo lakini hakutaka tu?

Kama ni hivyo hana upendo qote basi, maana mqwnye upendo hawezi kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Au, alitaka sana kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, lakini akashindwa tu?

Kama ni hivyo basi hawezi yote, maana alitaka kuumba ulimwengu usiowezekabika kuwa na mabaya lakini akashindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…