Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Ukiniambia wewe tajiri, mkarimu, una hekima, huna hasira, msafi, imetembea dunia nzima..
Nikikuomba hela kwa sababu wewe ni tajiri na mkarimu sijatambua sifa zako nyingine?
Far from kitotambua sifa zake nyingine, nazitambua sifa hizo.
Tatizo hata sifa mbili tu zikipingana, mungu wenu kashapata contradiction no matter hizo sifa nyingine zinasema nini.
Tukiambiwa mungu wenu ni mpenda haki upande mmoja, halafu upande mwingine tukaambiwa anahukumu watoto na vitukuu kwa makosa ya mababu zao, hapo tayari huyu mungu kashajipinga mwenye?
Which is which?
Ni mungu moenda haki au hajali haki anahukumu watoto, wajukuu na vitukuu kwa makisa ya mababu zao?
Nikikuuliza swali hili huwezi kumtetea mungu kwa kusema ana sifa nyingine nzuri, sifa nyingine nzuri zinaondoaje hii contradiction?
Mfano wako wa TzMbongo kiwa mwanajeshi na mpole haukidhi kanuni ya kulinganisha vinavyolingana. Hakuna contradiction kati ya mtu kuwa mpole na mwanajeshi, kina contradiction katika mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Huwezi kulinganisha kisicho na contradiction na kilicho na contradiction.
Siga zinazohusika hapa ni, kwa upande mmoja, mungu kuwa mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote na kwa upande mwingine, mungu kuwa muumba wa ulimwengu huu.
Hizi ndizo sifa "material" to my argument.
Kama mungu anazungumza na Putin kwa simu maalum kila Jumanne jioni, sihutaji kuizungumzia sifa hiyo kwenye argument yangu kwa sababu ni immaterial to my argument.
Hizo sifa material to my argument unazikubali?
Unakubali kwamba mungu ni mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wa yote na pia kaumba huu ulimwengu?
Nimekwambia tuzijadili kwanza sifa za Mungu kabla ya kuzungumzia mambo ya huu ulimwengu,mambo ya dini yako ya zamani kwamba "ana hukumu watoto na vitu kuu kwa makosa ya mababu zao" hii sio sifa ya Mungu. Sijakwambia uanze kuelezea matukio kwanza.
Kwahiyo tuanze kujadili sifa zake kwanza kwa ujumla wake na utoe tafsiri ya kujipinga.
Twende taratibu tu mkuu.