COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Huwezi kusema kwa uhakika kila mtu amepangiwa siku yake ya kufa wakati hata kuthibigisha kwamba kuna aliyepanga siku hiyo huwezi.

Anza kuthibitisha kwamba yupo kwanza, lbda nitakusikikiza kwenye yanayofuata.

Umemtaja shetani.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao shetani anawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezekani kuwepo?
 
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoruhusu ajali kutokea na viumbe wake kuumia vikali na hata kufa?

Wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao ajali haiwezekani.

Hili swali bado halijajibiwa na wanaosema mungu huyo yupo.

Licha ya kujaribu sana kulipindua pindua.

Jana tu nikikuwa nasikiliza habari tetemeko limepiga Nepal 7.8 on the Richter scale, limepiga just outside Kathmandu watu wamdlisikia mpaka Kolkata kilomita karibu 900 huko. Watu kibao wamekufa, Wa Nepali na watalii. Kuna executive mmoja wa Google, mkuu wa Privacy, alikuwa kaenda kupanda Mt. Everest na yeye kafariki. Kuna watoto kibaonwa ki Nepali watakuwa wanakufa kwenye vifhsi hata hivi njnavyoandika. Picha kama umeona kwenye TV watu wanafukua vifusi vya ngumba kwa mikono. Halafu hakuna hata uhakika kwamba unaposimama ili kufukua kifusi hujamkandamiza mtu na kumuua chini yako.

Wiki ya jana ilikuwa Papua New Guinea, wiki hii Nepal, ukiona hivyo Japan wajitayalishe linakuja kwao, kisha California, kisha Chile litafuata.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, upenxo woye na hjuzi wote kaumba ulimwengu ambao mabaya kama haya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ukimwengu ambao haya hayawezekani?

Swali hili halijapatiwa jibu bado.
 
Ndg yangu kiranga kwa kila jambo hapa duniani na hata Mbinguni KUNA KANUNI ZAKE,usipozijua huwezi kuwa katika nafasi ya kuelezea Chochote hata kama hapa nchini Au duniani tunao uhuru wa kuongea

Unaongelea jambo gani? unaongelea kanuni gani?

Fuguka, hiki ni jukwaa la majadiiano huru, si ushairi uliofichika.

Mungu pia anafuata kanuni?

Kama anafuata kanuni inamaana yupo chini ya kanuni na hawezi kufanya anachotaka?

Kama hayupo chini ya kanuni, je ni kweli kila jambo duniani na mbinguni kuna kanuni zake?

Unawezaje kuamini mungu anayeweza yote na kujua yote (maana yake yuko juu ya kanuni) na hapo hapo ukasema kila jambo lina kanuni?

Huoni kwamba hapo kimsinhi umesema mungu yupo juu ya kanuni na anahitaji kanuni kwa wakati mmoja?

Huoni kwamba umejipinga mwenyewe kabla hata mimi sijakupinga?
 

Ipo siku utapata majibu ya maswali yako yote, tena kwa ufasaha zaidi
 
Ipo siku utapata majibu ya maswali yako yote, tena kwa ufasaha zaidi

Hili unalijua au kuamini?

Na kwa nini nisione hayo ni maneno ya kujifariji kwa mtu asiye na majibu ya maswali yangu tu?

Halafu kufikiri kwmba mtu kupinga uwepo wa mungu ni kutokana na kuwa na maisha mazuri tu ni kukosa exposure tu.

Kamtafute kwenye Google mtu anaitwa Primo Levi, myahudi ambaye alikuwa hamini kuwepo kwa mungu, akapata tabu sana kwenye makambi ya Nazi walivyokuwa wanaua Wayahudi. Lakini hilo halikumfanya akubali kuwepo kwa mungu. Kwa hiyo kusema wanaopinga kuwepo kwa mungu wanapinga hivyo kwa sababu ya maisha mazuri tu ni kjkosa elimu kuhusu hili jambo.

Ila naweza kukukubalia kwamba watu wanaoweza kujitosheleza kwa mambo fulani basic ya maisha wanaweza kupata wasaa zaidi wa kujiuliza maswali makubwa kama mungu yupo au hayupo.

Kama umeshiba na una huduma nzuri za afya, una muda wa kusoma vitabu, unaweza kupata muda wa kujiuliza maswali makubwa kuhusu mungu kwa kina.

Kama unafanya kazj ya minimum wage na unahitaji kufanya kazi masaa mengi sana iki kula tu, na wanao wanaumwa, huna hela za kuwapeleka hospitali, si tu utakuwa huna muda wa kujisomea na kuuliza maswali kuhusu mungu, bali pia mara nyingine matumaini yako yote yanakuwa katika mungu huyu ambaye hata humjui.

Ndiyo maana Ulaya ya kaskazini kwenye maendeleo ya kiuchumi na kielimu watu hawaendi sana makanisani wakati Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kwenye matatizo ya kiuchumi na kielimu watu wanajazana makanisani.
 

Warumi 14:1 "Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake ".
 

Moyo wako haujatahiriwa na ndio maana unampinga Mungu na kusudi lake. Pasipo tohara ta Moyo ni rahisi kupinga uwepo wa Mungu
 
Moyo wako haujatahiriwa na ndio maana unampinga Mungu na kusudi lake. Pasipo tohara ta Moyo ni rahisi kupinga uwepo wa Mungu

Hujajibu uliyoulizwa, na uliyojibu hujaulizwa.
 
Warumi 14:1 "Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake ".

Imani kila mtu anaruhusiwa kuwa nayo, that is uninteresting.

Facts, that is something else.
 
Umeliona hilo tu mkuu?

Mengi sana, hilo ndilo most basic.

Kama nataka kujadiliana nawe falsafa za kina Russell na Aquinas hapa nashindwa kupata confidence ya kuendelea kama mtu ninayejadiliana naye hajui tofauti ya "kujadiri" na kujadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…