Shy land
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 6,208
- 2,767
Imefanyaje?
Nimeuliza kiranga anieleze ni wapi alipozitoa taarifa au chanzo cha habari panaposema mungu ana upendo na uwezo mkubwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imefanyaje?
Kwani we unaujua huo ushahidi ulivyo?
Kwa hiyo mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mateso lakini una huruma?
Isingewezekana kwasababu mateso ndio yanayosababisha huruma, kama kusingekua na mateso kabisa kusingekua na hicho cha kuonea huruma.
Kiranga mimi namwamini Mungu, na kwangu ni Muweza wa yote, hayo unayosema itabidi umuulize mtaalamu wa theology. Mimi nimechagua kumwamini. Kuna maswali mengi sana ambayo muda mwingi tunakosa majibu ila tunaendelea kuamini, wewe kama umechagua kutoamini na kutoona uwezo wake isiwe tabu.
Swali hapa si mfano wa jinsi ya ulimwengu ukawa umepatikana tofauti.
Human ignorance is infinite.
Swali hapa ni jinsi gani ulimwengu hauwezi ukawa umepatikana tofauti.
Mimi sijasema najua ulimwengu ulivyoanza, sasa huwezi kuniuliza hilo swali.
Wewe unayedai kwamba ulimwengu umeumbwa na mungu una wajibu wa kutueleza ni kwa nini ulimwengu huu umeumbwa na mungu na hauwezi kuwa umetokea kwa njia nyingine yoyote.
Mpaka sasa nishakupa swali unieleze imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote kaumba ulimwengu huu, hujanijibu.
Kiranga mtu wangu, sijaimply in anyway that what am saying is a fact, I simply repeated what I have come across.
So yes, I believe in God na kila mtu ana haki ya kuamini anachotaka that's why inaitwa kuamini cause we have not been there tukaona anything, we just chose a path and clearly path uliyochagua ni tofauti kidogo na yangu ndo maana tunashindwa kuelewana.
But I insist hakuna hata kimoja nilichosema kinachoashiria kuwa nina uhakika kile ninachoamini ni sahihi na wengine wanachoamini sio.
Hivi unaweza kuniambia kwanini uliniambia nafikiri sawa na line ya reli ikiwa wewe pia huwezi hata kutoa mfano tu wa fikra tofauti?
Je,vp wewe ikiwa ndiyo umekariri tu kwa kukataa kwa hiyo imani yako ya kwamba mungu hajaumba huu ulimwengu? Maana hakuna hoja uliyotoa yenye kuonesha imani ya kuamini mungu ndiyo aliyeumba ulimwengu si sahihi.
This is refreshing!
Nimeuliza kiranga anieleze ni wapi alipozitoa taarifa au chanzo cha habari panaposema mungu ana upendo na uwezo mkubwa.
Kwa sababu unasema kinachoweza kuwepo ni mbele na nyuma tu wakati hujui habari zote.
Vipi kama ulimwengu haujaumbwa na mungu na ukweli kuhusu nature yake hatutapata teknolojia ya kuujua kwa miaka 1,000 ijayo?
How do you go about that?
I would look at the god theory and all it's holes and discard it, even as I am converging more and more towards the truth.
Wewe umesema mungu yupo na kaumba ulimwengu, nimekupa maswali ya kimantiki kuonesha kwamba huyo mungu wako hawezi kuwa ndiye mungu aliyeumba ulimwengu huu (inherent contradiction of central character). Hujaweza kujibu maswali haya.
Hujaweza kuthibitisha mungu yupo.
Umesema ulimwengu huu ni ushahidi kwamba mungu yupo, nimekuonesha jinsi gani ushahidi huu ni ushahidi kwamba mungu wako hayupo.
Nimekuuliza imekuwaje mungu mwenye ujuzi wa yote, upendo wote na uwezo wote aende kuumba ulimwengu huu? Hujajibu swali.
Habari yako ya mungu kuwapo haiyumkiniki.
Ni hadithi ya kitoto iliyoungwa ungwa kwa maarifa ya kizamani ambayo hayawezi kuhimili uchunguzi wa kimantiki.
Hujajibu maswali.
Unaposema hakuna hoja niliyotoa kuonesha imani ya kuamini mungu si sahihi unataka nifikiri kwamba ama unajiondoa alili tu ama huna akili.
Kwa sababu mmeleta habari ya "ulimwengu huu ni ishahidi kwamba mungu yupo", nikaipangua hoja viziri kuonesha kwamba "ulimwengu huu ni ushahidi kuwa mungu hayupo".
Kwa sababu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kama huu.
Nimekueleza kama kila intelligence ni lazima iwe created, then hiyo intelligence inayo create nato ni lazima iwe created. Hivyo mungu wako naye atahitaji kuwa na muumbaji na muumbaji wake naye atahitaji muumbaji, bila mwisho. Kwa hiyo habari nzima ya kufikiri kila intelligence ni lazima iwe imeumbwa, badala ya kuonesha kwamba mungu yupo, inaonesha kwamba mungu hayupo.
Sasa ukipotezea hoja za msingi kama hizo (hujaijibu) na kusema hakuna hoja niliyotoa inayoonesha imani ya kuamini mungu aliyeumba ulimwengu si sahihi, unajishusha hadhi mwenyewe.
Unajionesha kuwa wewe ama ni muongomuongo ambaye huna nia ya ku dahili hoja, ama ni mjingamjinga ambaye hata nikikuelezea hoja nzito huwezi kuzielewa.
Zaidi ya hapo, unaweza kuwa mjingamjinga na muongomuongo.
Tueleze sasa.
Kipi ni sahihi hapo?
"Kwa sababu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuumba ulimwengu
unaoruhusu mabaya kama huu."
Ulimwengu haufanyi mabaya bali mabaya hufanywa na wanadamu.
Ulimwengu ni kitu chengine na binadamu ni kitu chengine usichanganye hivyo vitu. Maovu yanayofanywa na wanadamu inahusiana vp na kuja kusema kwamba Mungu hajaumba ulimwengu kwa sababu hiyo?
Eleza ni vp madai ya kwamba Mungu ndiyo kaumba ulimwengu hayana ukweli kwa sababu za msingi, lakini sio kuja na hoja ya kwamba et kisa binadamu anafanya maovu et ndiyo ulimwengu haujaumbwa na Mungu. Ni vichekesho vitupu
Na kichekesho cha mwisho ni kusema mungu naye atakuwa na muumba wake,hapa ndiyo unathibitisha maneno niliyokwambia kwamba unapinga usichokijua.
Nilishawahi kukwambia kwamba mungu humjui lakini unampinga, ila ukanibishia ukasema unamjua.
Ungekuwa unamjua usingekuja kusema kuwa mungu naye anahitaji muumbaji, kwa sababu ungekuwa unajua kabisa kuwa yeye pekee ndiyo mwenye sifa ya kuumba na yeye hana mwanzo wala mwisho hajaumbwa.
Lakini kwa kuwa humjui basi wewe umekariri sifa zake za upendo na uwezo wote tu hujui hata kama ana sifa ya kuumba pia.
Blah blah miiiingi lakini hakuna chochote kinaonesha Mungu yupo
Nimekuuliza mungu unayemuamini ni yupi ili nikupe reference zinazokuhusu wewe.
Siwezi kukupa reference za ma Buddhist kutoka kwenye Dhammapada wakati wewe unaamini mungu wa Wakatoliki.
Mungu unayemuamini ni yupi?
Hujajibu hili swali.
Unachoogopa ni kipi?
First thing first, kwa mujibu wa imani yako, unakubali au hukubali kwamba chochote kinachotokea kwenye ulimwengu kinatokea kwa kibali cha mungu?
Kwamba mungu asingekiachia kitokee kisingetokea?
Kwamba mungu wako alivyokuwa anaumba ulimwengu huu alikuwa na uwezo wa kuupa tabia zozote alizotaka yeye?
Unakubali au hukubali?
biolojia nilipata F, siwezi kujibu maswali yako......but am sure yanajibika kisayansi lol..:lol::lol:...mie napenda kusikiliza gospel huwa zinanicalm down nerves,napendaga kuhisi matatizo yangu siku moja kuna ambae anaweza kuyatatua ambae ni God...ila nikisoma bible,uwepo wake na jinsi kristo alivyokufa msalabani....napataga na mushkeli wa kuiamini hii kitu....:noidea::noidea::noidea::noidea::noidea::noidea::noidea::noidea::noidea:
Mimi ni mtu ambaye nampenda mungu sana.
Kuliko unavyofikiria.
Ningependa mungu awepo. Akiwepo, ultimately reaponsibility ya kila kitu ipo kwake. Maana yeye ndiye mwe ye mikoba yote na kaumba vyote.
Kwa hiyo ma hlobal warming, ma Ebola, ma Tsunami yote yanakuwa si mzigo wa mwanadamu. Ni mzigo wa mungu. Mwanadamu anakuwa kipande kidogo tu cha mchezo.
Lakini hata nikimpenda vipi mungu. Hili haliondoi ukweli kwamba kama hayupo, hatuwezi kisema hayupo.
Siwezi kujifariji kwamba mu gu yupo, ni mwema na ana nguvu zote na mimi nionbe na kyimba tu wakati manyiki yote inao esha kwamba hayupo.