COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Kwahiyo mitihani ni kwa faida ya mwalimu au mwanafunzi mwenyewe?

Mtihani unaweza kuwa na faida kwa wote, mwalimu na mwanafunzi.

Utawasaidia wote kujua mwanafunzi anajua nini na hajui nini.

Bila mtihani wanaweza wasijue mwanafunzi anajua nini na hajui nini.

Sasa mungu anayejua yote mtihani unamsaidia nini?

Na kama nia yake ni kumsaidia mtu, kwa nini ahitaji mtihani wakati yeye mungu anajua yote na anaweza kufabya mambi bila kihitaji mtihani wa mabaya ya dunia?
 
Na watu gani wanaosema nothing is impossible under the sun....unataka kuthibitishiwa MUNGU yupo..Huu uthibitisho mmoja tu MUNGU wangu ndio aliyeshika dunia isianguke ikianguka pasipo yeye kutoke basi atakua hayupo....huu ni uthibitisho labda utataka nikuoneshe alivyo ishikiria? ndio swali linalo fata eh?

Ukishasema nothing is impossible, unamaanisha everything is possible.

Ukishasema everything is possible, unamaanisha hata the opposing and mutually exclusive are possible at the same time.

You walk into a contradiction at the same time.

If nothing is impossible, then it is possible that 1=2=3=4=5...

Everything breaks down.

Even your premise that nothing is impossible.

Because if everything equals everything and anything equals anything, you would not know what is nothing to begin with!

Tafadhali nioneshe huyo mungu.

Unanionesha vipi?
 
Umeeleza vizuri kwamba wengi wanafuata mapoleo tu na hawatafakari vya kutosha.

Hicho ndicho kitu ninachokataa mimi.

Ukiaema mungu yupo, kimantiki unatakiwa uweze kuthibitisha.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?

Umeelezea imani yako kama ya Ukatoliki, unaweza kuelezea imekuwaje, kwa mujibu wa imani yako, mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Unapohoji mungu kuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na mabaya je,unaamini kuwa mungu yupo? Kama hauamini basi hoja yako haina msingi, kwa sababu hoja yako inabidi ijibiwe kwa kutumia maneno yake(vitabu vyake) na wewe hata yeye mwenyewe humuamini kama yupo. Ni sawa na kumuuliza mlinzi kwanini boss wake amelala hadi sasa hali ya kuwa unavyojua wewe kuwa boss wake hayupo.
 
That is neither here nor there.

Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Hujanieleza ni kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao ubaya na uovu unawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ubaya na uovu hauwezekani?

pasinge kuwa na ubaya wala uovu kama MUNGU asingekuepo..labda ubaya na uovu ungekua na sura nyingine akilini mwetu..ubaya ndo upi huo na uovu ndo upi uo? labda ubaya unafananaje ama uovu unafananaje?...ni vitu gani hivo ubaya uovu....vina wezekana kila mahali?...vina mantiki gani?...vimetoka wapi?...binadamu anavielewa vipi?...kwanini viwepo?...ninani aliyesema huu ni ubaya?
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Hujaonesha kimantiki imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwanza Unakubali kweli anao huo uwezo?
 
Unapohoji mungu kuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na mabaya je,unaamini kuwa mungu yupo? Kama hauamini basi hoja yako haina msingi, kwa sababu hoja yako inabidi ijibiwe kwa kutumia maneno yake(vitabu vyake) na wewe hata yeye mwenyewe humuamini kama yupo. Ni sawa na kumuuliza mlinzi kwanini boss wake amelala hadi sasa hali ya kuwa unavyojua wewe kuwa boss wake hayupo.

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" katika maisha yako yote?

Unataka nifanyeje ili ujue natumia vitabu vyake?

Vitabu gani?

Nikikwambia nimetumia vitabu vyake bila wewe kuelewa utakubali?
 
Ukishasema nothing is impossible, unamaanisha everything is possible.

Ukishasema everything is possible, unamaanisha hata the opposing and mutually exclusive are possible at the same time.

You walk into a contradiction at the same time.

If nothing is impossible, then it is possible that 1=2=3=4=5...

Everything breaks down.

Even your premise that nothing is impossible.

Because if everything equals everything and anything equals anything, you would not know what is nothing to begin with!

Tafadhali nioneshe huyo mungu.

Unanionesha vipi?

ninacho amini nikimoja tu MUNGU yupo...unataka kumuona mwangalie binadamu mwenzako machoni kwa nusu saa...utamuona....
 
Kwanza Unakubali kweli anao huo uwezo?

Mungu ambaye sikubali kwamba yupo nifakubali vipi kwamba ana uwezo wowote?

Ni kazi yako kunielewesha huyo mungu unayemuamini, anayesemwa kuwa na uwezo huo, anewezaje kuumba ulimwengu wenye maovu huku akiwa na uwezo na upendo wa kuumba ulimwengu usio na maovu.

Ni kama unaniambia kuna baba mwenye roho nzuri ajabu na upendo usio kifani, lakini kazaa watoto anawaacha wafe kwa umasikini njaa na magonjwa, wakati yeye ana uwezo wote wa kuwasaidia, na alikuwa na uwezo wa kuwafanya wasuone tabu hata moja tangu wanazaliwa, lakini hakufanya hivyo.

Hilo jambo halitaeleweka.

Kisichoeleweka zaidi ya hilo ni mungu wa aina hiyo.

Kwa sababu, angalau baba tunaweza kusema ni binadamu, labda kuna kilicho nje ya uwezo wake.

Mungu ana uwezo wote na upendo wote.

What's his excuse?
 
Hili la wengi wasioamini mungu kutokewa na hali hiyo unalijua au unabahatisha tu kama imani yako ya mungu?

Unamuasa mwenzako kutumia akili vyema na kutafuta ukweli wakati ukweli uliofunulowa na maswali yangu kwako unaukimbia?

Uliyoyaeleza hapa ndiyo niliyomwambia mkuu hapo.
Wewe ndiyo kwanza unajisifu kuuliza maswali. Hali ya kuwa wewe ukiulizwa maswali maswali unajibu kirahisi tu "mie kutokujua jibu la swali hilo haithibitishi kuwa mungu yapo" hapo ushamaliza mwenyewe kirahisi kabisa kujibu.
 
ninacho amini nikimoja tu MUNGU yupo...unataka kumuona mwangalie binadamu mwenzako machoni kwa nusu saa...utamuona....

Sijakuuliza unachoamini ni nini.

Unaweza hata kuamini kwamba mungu ni funza aliye mguuni mwa babu yako. Sikusudii kukutusi, nakuonesha tu nisivyojali nini unaamini, as long as unakubali kwamba ni imani tu.

Imani zina kinga ya haki ya bunadamu zinazotambuliwa ba umoja wa mataifa.

Kwa hiyo sijaja kukuhoji unaamini kipi.

Ukianza kusema unajua, unachoamini ndicho cha kweli, hapo ndipo unahigaji kutoa uthobitisho na ushahidi.

Kichwa cha thread kinao gelea ushahidi wa juwepo mungu, si imani ya kuwepo mungu.

Naona umekosea thread.
 
Uthibitisho mwingine,..michapio kwenye kile unaandika ni uthibitisho tosha kwamba MUNGU yupo..unataka mwingine?
 
Hata nikishindwa kuthibitisha kilichokuwepo, hilo halithibitishi kwamba mungu yupo.

Mimi nataka uthibitishe kwamba mungu yupo.

Hata ukishindwa au umeshindwa?

Nyoosha maelezo.
 
Mtihani unaweza kuwa na faida kwa wote, mwalimu na mwanafunzi.

Utawasaidia wote kujua mwanafunzi anajua nini na hajui nini.

Bila mtihani wanaweza wasijue mwanafunzi anajua nini na hajui nini.

Sasa mungu anayejua yote mtihani unamsaidia nini?

Na kama nia yake ni kumsaidia mtu, kwa nini ahitaji mtihani wakati yeye mungu anajua yote na anaweza kufabya mambi bila kihitaji mtihani wa mabaya ya dunia?

Je,mitihani anayotoa mungu itakuwa faida kwa nani?
 
Niambie wewe unayeamini mungu yupo, mimi sikubali mungu yupo na hivyo siwezi kukubali kwamba mungu ambaye hayupo anatoa mitihani.

Hata nikijilazimisha kuamini mungu yupo kwa sekunde, bado swali langu la kwa nini mungu mwenye kujua yote na kuweza yote ahitaji mtihani?

Kwa nini mungu ahitaji kutumia mtihani?
 
Hata ukishindwa au umeshindwa?

Nyoosha maelezo.

Nakuonesha kwamba you are going in a blind alley, on a wild goose chase. Your non-argument is puttering around with no direction.

The worst that could happen ni kwamba nitashindwa na niseme sijui, siwezi kuthibitisha kilichopo kipo.

Ikiwa nasema hivyo, nashindwa kuthibitisha chochote kilichopo kipo, hilo litathibitisha vipi kwamba mungu yupo?

Kumbuka issue yetu ni kuthibitisha kwamba mungu yupo.

Sasa mimi kushindwa kuthibitisha kilichopo kipo kutathibitisha vipi kwamba mungu yupo?
 
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" katika maisha yako yote?

Unataka nifanyeje ili ujue natumia vitabu vyake?

Vitabu gani?

Nikikwambia nimetumia vitabu vyake bila wewe kuelewa utakubali?

Hujajibu swali langu mkuu.

Haiwezekani kitu ambacho hakipo ukahoji kwanini kimefanya hivi mara vile. Na ndiyo maana ukijibiwa unasema uthibitishiwe kwanza kama hicho kitu kipo.
 
Mungu ambaye sikubali kwamba yupo nifakubali vipi kwamba ana uwezo wowote?

Ni kazi yako kunielewesha huyo mungu unayemuamini, anayesemwa kuwa na uwezo huo, anewezaje kuumba ulimwengu wenye maovu huku akiwa na uwezo na upendo wa kuumba ulimwengu usio na maovu.

Ni kama unaniambia kuna baba mwenye roho nzuri ajabu na upendo usio kifani, lakini kazaa watoto anawaacha wafe kwa umasikini njaa na magonjwa, wakati yeye ana uwezo wote wa kuwasaidia, na alikuwa na uwezo wa kuwafanya wasuone tabu hata moja tangu wanazaliwa, lakini hakufanya hivyo.

Hilo jambo halitaeleweka.

Kisichoeleweka zaidi ya hilo ni mungu wa aina hiyo.

Kwa sababu, angalau baba tunaweza kusema ni binadamu, labda kuna kilicho nje ya uwezo wake.

Mungu ana uwezo wote na upendo wote.

What's his excuse?

Sasa ikiwa hata haumini kuwa mungu yupo basi iweje uhoji uwezo wake hali ya kuwa hata haumini kama mungu? Na ndiyo tunashindwa kuelewana.
 
Niambie wewe unayeamini mungu yupo, mimi sikubali mungu yupo na hivyo siwezi kukubali kwamba mungu ambaye hayupo anatoa mitihani.

Hata nikijilazimisha kuamini mungu yupo kwa sekunde, bado swali langu la kwa nini mungu mwenye kujua yote na kuweza yote ahitaji mtihani?

Kwa nini mungu ahitaji kutumia mtihani?

Sasa kama hujui hilo je,hoja yako ni nini sasa? Na kwanini uhoji hekima ya kitu kisichokuwepo? Huoni kuwa hilo ni tatizo.
 
Nakuonesha kwamba you are going in a blind alley, on a wild goose chase. Your non-argument is puttering around with no direction.

The worst that could happen ni kwamba nitashindwa na niseme sijui, siwezi kuthibitisha kilichopo kipo.

Ikiwa nasema hivyo, nashindwa kuthibitisha chochote kilichopo kipo, hilo litathibitisha vipi kwamba mungu yupo?

Kumbuka issue yetu ni kuthibitisha kwamba mungu yupo.

Sasa mimi kushindwa kuthibitisha kilichopo kipo kutathibitisha vipi kwamba mungu yupo?

Bado haujanyoosha maelezo.

Ni Wewe tu ndiyo unashindwa kuthibitisha kitu kilichopo au pia kilichopo nacho hakithibitishiki kama kisichokuwepo(kama usemavyo)?
 
Umetoka nje kabisa ya swali nililokuuliza.

Whether ni mimi tu nikishindwa kuthibitisha kilichopo kipo au hata kama kilichopo hakithibitishiki kwamba kipo.

Either way.

How does either eventuality prove that god exists?

Tuseme option ya kwanza.

Mimi siwezi kuthibitisha kilichopo kipo.

Hilo linathibitishaje kwamba mungu yupo?

Au option ya pili.

Kilichopo hakithibitishiki kwamba kipo.

Hilo linathibitishaje kwamba mungu yupo?

Hujajibu swali.
 
Back
Top Bottom