Utaratibu unaoutaka
Kiranga ni mfano wa mtu anaekimbia umande.Mtu anapokuwa hataki shule atalalamikia hoo walimu wakali hawajui kufundisha lakini wapo wanafunzi wengine wanasoma shule hiohio na wanasonga.
Qur-an 2:38 shukeni (duniani)wote wawili,pindi nitakapokuleteeni muongo wangu basi atakaeufuata muongo hatakuwa na khofu na wala hata huzunika.
Hapana shaka tutakujaribuni kwa mitihani
ya HOFU, na NJAA, na upungufu
(ukosefu) wa MALI na WATU (umauti kwa
mnaowapenda) na matunda. Na wape
habari (njema) wale wanao subiri
(wanaovumilia), Wale ambao ukiwasibu msiba husema:
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na
kwake Yeye hakika tutarejea.
Quran 2 : 155-156
Sasa wewe
Kiranga mbona utaratibu wako wa kutaka mambo mazuri SHORT-CUT mbona haungii akilini.
Anayetaka shortcut ni wewe unayemlimbikizia mungu maswali yote ambayo huna majibu yake, na kutaka kutafuta jibu la kila swali kwenye Quran ambayo yenyewe sio tu inajipinga, bali pia inakubali kwamba inajipinga.
Pia, kufikiri kwamba ulimwengu ambao hauna mabaya ni "utaratibu anaoutaka Kiranga" ni kushindwa kuelewa argument yangu.
Nimeelezea hapo juu kwa nini ulimwengu usiowezekanika kuwa na mabaya si utaratibu anaoutaka Kiranga bali ni ulimwengu ambao mungu wenu, kwa kufuata tabia zake za kuweza yote, kujua yote na kuwa na upendo wote alitakiwa kuuumba.
Tatizo hukuweza kufuatilia logic ya argument yangu kutofautisha nini nataka mimi na nini ni just a logical consistency check on your godhead.
Sometimes I feel like I might as well be talking quantum physics to a goat!
Sipendi ku sound kama najigamba. Lakini maadam umeongelea mambo ya kukimbia umande, ngoja niyaongelee hapa.
Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba watu wengi
1.Hawawezi logical thinking. Mambo kama contradiction, tautology, fallacy, circuitous logic, non sequitur etc ni msamiati
2. Hawana elimu na exposure ya kutosha katika mambo ya falsafa na sayansi (kwa elimu simaanishi vyeti na degrees, namaanisha uelewa mpana, to illustrate this point nikiongelea vitu kama "immanent critique", entropy, the second law of thermodynamics, Heisenberg's Uncertainty Principle au hata "mutual exclusive events" katika kujenga hoja logically, kwa wengi habari hizi hawazijui. Ukiwauliza kuhusu kazi za Anselm, St. Augustine, Aristotle, Socrates, Buddha, Lord Russel au hata Dawkins sio tu hawajazisoma, hata lugha ambayo kazi hizi zimeandikwa ni mgogoro.
3. Kutokana na 2 above, reference nyingi zinaishia kwenye Quran na Bible. Which is not a problem for me, as I can use the Bible and Quran conceptually to show flaws through "immanent criticism". Tatizo ama hawaielewi "immanent criticism" ni nini, au simply wana deep rooted "cognitive dissonance".
4. Speaking of cognitive dissonance, this is a serious enough issue kiasi kwamba ina deserve a separate mention. Kuna watu wakishakulia kwenye dini fulani hata uwaambie nini hawawezi kubadilika. Ni kama mtu ambaye amekaa kusubiri basi, na anavyozidi kusubiri basi anazidi kupata shaka kwamba basi haliji, lakini akishasubiri kwa muda mrefu sana anaona akiondoka atakuwa kapoteza muda mrefu sana kusubiri, vipi kama basi likija? Anaendelea kusubiri basi kwa muda mrefu wakati kwa upande fulani anakuwa kashajua haliji. Kuna watu walitabiriwa kwamba Yesu atarudi miaka ya 1842 or around that time. Muda ukafika na kupita Yesu hajarudi. Wengine wakawa washauza nyumba na mashamba yao, lakini kwa sababu walikuwa washajikita sana kwenye imani hiyo, hata ilipokuja kuwa wazi kwamba wametapeliwa, hawakuweza kujiondoa katika imani hiyo. Walizidi kumpa mtume wao excuses tu kwamba he was basically right, kuna mambo mambo tu yametokea. Ndicho tunachokiona hapa, watu washakunywa maji ya dini tangu watotot, sasa leo wewe unataka kuleta mambo yako ya logic na common sense ambayo clearly yanaonesha kwamba imani zao ni potofu wakati kwao ukoo mzima ndio unachoamini, jamii nzima imesimama kwa mujibu wa mambo haya ya dini, hawawezi kukuelewa, hata wakikuelewa wanakupotezea tu, na wengine watakupiga vita kwa maana unawastua sana kuwaambia kwamba walichojua maisha yao yote ni uongo mtupu.
Sasa kudeal na watu ambao hawana elimu inayotakiwa kuanza kuchangia mjadala huu, na hapo hapo wamejawa cognitive dissonance kuhusu dini, sitegemei kwamba watanielewa.
Ila pia, kuna wengine watapata mambo fulani na hata kuchangia zaidi. Hivyo siwezi kuacha mjadala uwe hijacked na hawa waliokimbia umande ambao wanaona wengine wamekimbia umande, huku wao hata set theory hawajui, let alone what a contradiction is.
Tofyo hujajibu, kabla ya kumuumba mwanadamu, mungu alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki kufanyika.
Kwa mujibu wenu, hakuumba huo.
Kaumba huu ambao mabaya yanawezekanika kufanyika.
Kwa nini?