COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Mungu ambaye sikubali kwamba yupo nifakubali vipi kwamba ana uwezo wowote?

Ni kazi yako kunielewesha huyo mungu unayemuamini, anayesemwa kuwa na uwezo huo, anewezaje kuumba ulimwengu wenye maovu huku akiwa na uwezo na upendo wa kuumba ulimwengu usio na maovu.

Ni kama unaniambia kuna baba mwenye roho nzuri ajabu na upendo usio kifani, lakini kazaa watoto anawaacha wafe kwa umasikini njaa na magonjwa, wakati yeye ana uwezo wote wa kuwasaidia, na alikuwa na uwezo wa kuwafanya wasuone tabu hata moja tangu wanazaliwa, lakini hakufanya hivyo.

Hilo jambo halitaeleweka.

Kisichoeleweka zaidi ya hilo ni mungu wa aina hiyo.

Kwa sababu, angalau baba tunaweza kusema ni binadamu, labda kuna kilicho nje ya uwezo wake.

Mungu ana uwezo wote na upendo wote.

What's his excuse?

Hivi wewe kiranga tangia uanze shule ya msingi hadi hapo ulipo ulishawahi KUFAULU au KUFELI bila ya kufanya mtihani?
Wewe unataka ulimwengu ambao hauna tabu kwa utaratibu upi?

ULIMWENGU NI DARASA NA MABAYA NI CHUMBA CHA MTIHANI.usii
 
Utaratibu unaoutaka Kiranga ni mfano wa mtu anaekimbia umande.Mtu anapokuwa hataki shule atalalamikia hoo walimu wakali hawajui kufundisha lakini wapo wanafunzi wengine wanasoma shule hiohio na wanasonga.

Qur-an 2:38 shukeni (duniani)wote wawili,pindi nitakapokuleteeni muongo wangu basi atakaeufuata muongo hatakuwa na khofu na wala hata huzunika.
Hapana shaka tutakujaribuni kwa mitihani
ya HOFU, na NJAA, na upungufu
(ukosefu) wa MALI na WATU (umauti kwa
mnaowapenda) na matunda. Na wape
habari (njema) wale wanao subiri
(wanaovumilia), Wale ambao ukiwasibu msiba husema:
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na
kwake Yeye hakika tutarejea.
Quran 2 : 155-156

Sasa wewe Kiranga mbona utaratibu wako wa kutaka mambo mazuri SHORT-CUT mbona haungii akilini.
 
Last edited by a moderator:
"Kipimo cha uthibitisho ni kiwango cha kufikia ili kukuridhisha kwamba huu uthibitisho ni sahihi."

Hakuna cha zaidi katika hiyo tafsiri yako ya kipimo cha uthibitisho zaidi ya maana ya kupambanua uthibitisho uliyosahihi na uthibitisho usiosahihi.

Kwahiyo kuna uthibitisho ambao ni sahihi na kuna uthibisho ambao si sahihi. Kwahiyo suala si wewe kipimo chako ni kipi.

Suala si mimi kipimo changu ni kipi. Wewe ndiye uliyeniuliza mimi, mimi ndiye natafuta namna ya kukupa jibu litakalokidhi vipimo na viwango vyako vya uthibitisho, nisije kukwambia "nimethibitisha kwa macho yangu", halafu ukaniambia "uthibitisho wako hauna nguvu, kwani hauna shahidi na inawezekana macho yako mabovu".

Ndiyo maana nikakuuliza.

Kipimo chako cha uthibitisho mpaka uukubali kwamba huu ni sahihi na unafaa ni kipi?
 
Hivi wewe kiranga tangia uanze shule ya msingi hadi hapo ulipo ulishawahi KUFAULU au KUFELI bila ya kufanya mtihani?
Wewe unataka ulimwengu ambao hauna tabu kwa utaratibu upi?

ULIMWENGU NI DARASA NA MABAYA NI CHUMBA CHA MTIHANI.usii

Unafuatilia mjadala au unasoma juu juu na kujiulizia tu?

Wapi nimesema nataka ulimwengu ambao hauna tabu?

Unaelewa tofauti ya mimi kutaka ulimwengu ambao hauna tabu na mimi kueleza kwamba mungu wenu tabia zake za kuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote zinapingana na ulimwengu huu mnaosema kauumba ambao umejaa magonjwa, vita, matetemeko, ajali na tabu nyingi?

Unaelewa tofauti ya kifalsafa kati ya habari hizo mbili tofauti?

Au unachanganya madawa tu kwa kukosa tafakari kubwa?

Mungu anayejua yote, kuweza yote na mwenye upendo wote kwa nini ahitaji kuwepo kwa mtihani?

Na kwa nini aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Utaratibu unaoutaka Kiranga ni mfano wa mtu anaekimbia umande.Mtu anapokuwa hataki shule atalalamikia hoo walimu wakali hawajui kufundisha lakini wapo wanafunzi wengine wanasoma shule hiohio na wanasonga.

Qur-an 2:38 shukeni (duniani)wote wawili,pindi nitakapokuleteeni muongo wangu basi atakaeufuata muongo hatakuwa na khofu na wala hata huzunika.
Hapana shaka tutakujaribuni kwa mitihani
ya HOFU, na NJAA, na upungufu
(ukosefu) wa MALI na WATU (umauti kwa
mnaowapenda) na matunda. Na wape
habari (njema) wale wanao subiri
(wanaovumilia), Wale ambao ukiwasibu msiba husema:
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na
kwake Yeye hakika tutarejea.
Quran 2 : 155-156

Sasa wewe Kiranga mbona utaratibu wako wa kutaka mambo mazuri SHORT-CUT mbona haungii akilini.

Anayetaka shortcut ni wewe unayemlimbikizia mungu maswali yote ambayo huna majibu yake, na kutaka kutafuta jibu la kila swali kwenye Quran ambayo yenyewe sio tu inajipinga, bali pia inakubali kwamba inajipinga.

Pia, kufikiri kwamba ulimwengu ambao hauna mabaya ni "utaratibu anaoutaka Kiranga" ni kushindwa kuelewa argument yangu.

Nimeelezea hapo juu kwa nini ulimwengu usiowezekanika kuwa na mabaya si utaratibu anaoutaka Kiranga bali ni ulimwengu ambao mungu wenu, kwa kufuata tabia zake za kuweza yote, kujua yote na kuwa na upendo wote alitakiwa kuuumba.

Tatizo hukuweza kufuatilia logic ya argument yangu kutofautisha nini nataka mimi na nini ni just a logical consistency check on your godhead.

Sometimes I feel like I might as well be talking quantum physics to a goat!

Sipendi ku sound kama najigamba. Lakini maadam umeongelea mambo ya kukimbia umande, ngoja niyaongelee hapa.

Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba watu wengi

1.Hawawezi logical thinking. Mambo kama contradiction, tautology, fallacy, circuitous logic, non sequitur etc ni msamiati

2. Hawana elimu na exposure ya kutosha katika mambo ya falsafa na sayansi (kwa elimu simaanishi vyeti na degrees, namaanisha uelewa mpana, to illustrate this point nikiongelea vitu kama "immanent critique", entropy, the second law of thermodynamics, Heisenberg's Uncertainty Principle au hata "mutual exclusive events" katika kujenga hoja logically, kwa wengi habari hizi hawazijui. Ukiwauliza kuhusu kazi za Anselm, St. Augustine, Aristotle, Socrates, Buddha, Lord Russel au hata Dawkins sio tu hawajazisoma, hata lugha ambayo kazi hizi zimeandikwa ni mgogoro.

3. Kutokana na 2 above, reference nyingi zinaishia kwenye Quran na Bible. Which is not a problem for me, as I can use the Bible and Quran conceptually to show flaws through "immanent criticism". Tatizo ama hawaielewi "immanent criticism" ni nini, au simply wana deep rooted "cognitive dissonance".

4. Speaking of cognitive dissonance, this is a serious enough issue kiasi kwamba ina deserve a separate mention. Kuna watu wakishakulia kwenye dini fulani hata uwaambie nini hawawezi kubadilika. Ni kama mtu ambaye amekaa kusubiri basi, na anavyozidi kusubiri basi anazidi kupata shaka kwamba basi haliji, lakini akishasubiri kwa muda mrefu sana anaona akiondoka atakuwa kapoteza muda mrefu sana kusubiri, vipi kama basi likija? Anaendelea kusubiri basi kwa muda mrefu wakati kwa upande fulani anakuwa kashajua haliji. Kuna watu walitabiriwa kwamba Yesu atarudi miaka ya 1842 or around that time. Muda ukafika na kupita Yesu hajarudi. Wengine wakawa washauza nyumba na mashamba yao, lakini kwa sababu walikuwa washajikita sana kwenye imani hiyo, hata ilipokuja kuwa wazi kwamba wametapeliwa, hawakuweza kujiondoa katika imani hiyo. Walizidi kumpa mtume wao excuses tu kwamba he was basically right, kuna mambo mambo tu yametokea. Ndicho tunachokiona hapa, watu washakunywa maji ya dini tangu watotot, sasa leo wewe unataka kuleta mambo yako ya logic na common sense ambayo clearly yanaonesha kwamba imani zao ni potofu wakati kwao ukoo mzima ndio unachoamini, jamii nzima imesimama kwa mujibu wa mambo haya ya dini, hawawezi kukuelewa, hata wakikuelewa wanakupotezea tu, na wengine watakupiga vita kwa maana unawastua sana kuwaambia kwamba walichojua maisha yao yote ni uongo mtupu.

Sasa kudeal na watu ambao hawana elimu inayotakiwa kuanza kuchangia mjadala huu, na hapo hapo wamejawa cognitive dissonance kuhusu dini, sitegemei kwamba watanielewa.

Ila pia, kuna wengine watapata mambo fulani na hata kuchangia zaidi. Hivyo siwezi kuacha mjadala uwe hijacked na hawa waliokimbia umande ambao wanaona wengine wamekimbia umande, huku wao hata set theory hawajui, let alone what a contradiction is.

Tofyo hujajibu, kabla ya kumuumba mwanadamu, mungu alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki kufanyika.

Kwa mujibu wenu, hakuumba huo.

Kaumba huu ambao mabaya yanawezekanika kufanyika.

Kwa nini?
 
Suala si mimi kipimo changu ni kipi. Wewe ndiye uliyeniuliza mimi, mimi ndiye natafuta namna ya kukupa jibu litakalokidhi vipimo na viwango vyako vya uthibitisho, nisije kukwambia "nimethibitisha kwa macho yangu", halafu ukaniambia "uthibitisho wako hauna nguvu, kwani hauna shahidi na inawezekana macho yako mabovu".

Ndiyo maana nikakuuliza.

Kipimo chako cha uthibitisho mpaka uukubali kwamba huu ni sahihi na unafaa ni kipi?

Utaongea mbwembwe zote ila ni vilevile tu kuna uthibitisho sahihi na usio sahihi.

"Kusema nimethibitisha kwa macho yangu". Itakuwa umejithibitishia mwenyewe na wala sie hatuwezi kuita huo ni uthibitisho. Ni sawa na mie niseme jana usiku nilimuona Kiranga bar anakunywa bia,halafu nikiambiwa nithibitishe niseme nimethibitisha kwa macho yangu.
Itakuwa bado sijathibitishia.
 
Ahaa kumbe nimeelewa leo kwamba wewe unasema mungu yupo kwa kiwa tu ulizaliwa ukakuta watu wanasema mungu yupo basi na wewe umekariri hivyo bila hata kushughulisha ubongo wako.,

Ikiwa ni hivo kwa wote kwamba tuwe na uvivu wa kufikiri mambo kwa kina basi hata leo tusingekuwa umeme,radio active waves,ndege magari n.k na hata tungekuwa tunaamini kwamba dunia ni bapa kama walivyoamini zamani.

Shughulisha ubongo wako kijana acha uvivu,mungu ni Idea aliyoiumba mwanadamu.Naanza kuamini kwamba hakuna uhonjwa mbaya kama ugonjwa wa imani.

ndugu, unazungumzia kushughulisha akili kama wanasayansi sio?..assumptions zote zile za physics, leo unataka kubisha mimi kufanya assumption MUNGU yupo

basi twende kisayansi,utavyo fanya assumption kwamba kuna force of gravity which pull all things downward,mimi nitafanya assumption kuna MUNGU anaye wapa watu pumzi ili watembee.,ukithibitisha kwamba force of gravity ilitokea wapi mimi nitathibitisha pumzi ilitokea wapi

ukifanya assumption kwamba mtu mweusi na mweupe wanaweza kuzaa mtoto mweupe au mweusi kutokana na tabia ya genes,nami ntafanya assumption kuna MUNGU anaweza kuumba mtu kilema au mzima,utavyoweza kunithibitishia kwann gene iamue atoke mweusi au black basi nami ntakuthibitishia kwanin MUNGU aumbe black au white

bado mpo miaka mingi nyuma sayansi ya sasahivi inaamini MUNGU yupo nawala haina uwezo wakumpinga uwepo wake hayupo,.ila watacho jaribu ni kumpinga KRISTO..

na watachokua wakiamini MUNGU yupo lkn ni MUNGU wamjuaye wao,hivo nyinyi ambao hamuani MUNGU yupo sio wanasayansi,sio wanasiasa,sio waumini,sijui mpo kundi gani and your free to go..

imani yetu mnaiita idealisn yakwenu materialism lkn bado ina idealism kibao.........

Ahsante
 
Utaongea mbwembwe zote ila ni vilevile tu kuna uthibitisho sahihi na usio sahihi.

"Kusema nimethibitisha kwa macho yangu". Itakuwa umejithibitishia mwenyewe na wala sie hatuwezi kuita huo ni uthibitisho. Ni sawa na mie niseme jana usiku nilimuona Kiranga bar anakunywa bia,halafu nikiambiwa nithibitishe niseme nimethibitisha kwa macho yangu.
Itakuwa bado sijathibitishia.

Mtu kaniuliza, kutoka Dar mpaka Arusha ni umbali gani?

Simjui huyu mtu katoka wapi, wala vipimo vyake ni vipi, naweza kumjibu kwa umbali wa hatua, viwanja vya mpira, kilomita, maili, light years etc

Naweza kumjibu jibu ambalo kwake halitakuwa na maana na hivyo kuzidi kuchanganya mazungumzo tu.

Ili kuepuka hilo, naamua kumuuliza, unataka nikujibu kwa kipimo gani cha umbali?

Nakuja kugundua kwamba mtu mwenyewe hata kipimo cha umbali anachotaka nimjibu kwa kukitumia hakijui.

Kimsingi alichofanya ni kutaka kupindua hoja zangu na kunirudishia mimi mwenyewe.

Kwa kuwa nimesema kisichopo hakithibitishiki anataka kunipindulia mie Jiu-Jitsu. Wakati mie ndo Marcus Almeida.

Matokeo yake jaribio lake la Jiu-Jitsu limemrudia mwenyewe pale anapoomba kujulishwa umbali wakati hajui hata anaombwa kujulishwa umbali kwa kipimo gani.
 
ndugu, unazungumzia kushughulisha akili kama wanasayansi sio?..assumptions zote zile za physics, leo unataka kubisha mimi kufanya assumption MUNGU yupo

basi twende kisayansi,utavyo fanya assumption kwamba kuna force of gravity which pull all things downward,mimi nitafanya assumption kuna MUNGU anaye wapa watu pumzi ili watembee.,ukithibitisha kwamba force of gravity ilitokea wapi mimi nitathibitisha pumzi ilitokea wapi

ukifanya assumption kwamba mtu mweusi na mweupe wanaweza kuzaa mtoto mweupe au mweusi kutokana na tabia ya genes,nami ntafanya assumption kuna MUNGU anaweza kuumba mtu kilema au mzima,utavyoweza kunithibitishia kwann gene iamue atoke mweusi au black basi nami ntakuthibitishia kwanin MUNGU aumbe black au white

bado mpo miaka mingi nyuma sayansi ya sasahivi inaamini MUNGU yupo nawala haina uwezo wakumpinga uwepo wake hayupo,.ila watacho jaribu ni kumpinga KRISTO..

na watachokua wakiamini MUNGU yupo lkn ni MUNGU wamjuaye wao,hivo nyinyi ambao hamuani MUNGU yupo sio wanasayansi,sio wanasiasa,sio waumini,sijui mpo kundi gani and your free to go..

imani yetu mnaiita idealisn yakwenu materialism lkn bado ina idealism kibao.........

Ahsante

Assumptions ni mbaya au nzuri?

Kama ni nzuri huna point kuishutumu physics kwa kufanya assumption.

Kama ni mbaya huna point kusema mungu yupo kwa assumption.
 
Mtu kaniuliza, kutoka Dar mpaka Arusha ni umbali gani?

Simjui huyu mtu katoka wapi, wala vipimo vyake ni vipi, naweza kumjibu kwa umbali wa hatua, viwanja vya mpira, kilomita, maili, light years etc

Naweza kumjibu jibu ambalo kwake halitakuwa na maana na hivyo kuzidi kuchanganya mazungumzo tu.

Ili kuepuka hilo, naamua kumuuliza, unataka nikujibu kwa kipimo gani cha umbali?

Nakuja kugundua kwamba mtu mwenyewe hata kipimo cha umbali anachotaka nimjibu kwa kukitumia hakijui.

Kimsingi alichofanya ni kutaka kupindua hoja zangu na kunirudishia mimi mwenyewe.

Kwa kuwa nimesema kisichopo hakithibitishiki anataka kunipindulia mie Jiu-Jitsu. Wakati mie ndo Marcus Almeida.

Matokeo yake jaribio lake la Jiu-Jitsu limemrudia mwenyewe pale anapoomba kujulishwa umbali wakati hajui hata anaombwa kujulishwa umbali kwa kipimo gani.

Asante kwa hadithi yako nzuri ila hapa tunazungumzia uthibitisho.

Huyo amekuuliza tu umbali wa Dar hadi Arusha ila hajakwambia masuala ya kuthibitisha.
 
I doubt you have the capacity to capture the analogy, or if you do, that your cognitive dissonance will let you be generous with the right comments.

Wewe unaponitaka nikupe uthibitisho bila kunipa kipimo chako cha uthibitisho unaoweza kuuelewa na kuukubali ni sawa na mtu anayeniuliza umbali wa Dar mpaka Arusha halafu mimi nikitaka kujua nimueleze umbali kwa kipimo gani hataki kuniambia nitumie kipimo gani.

Wewe ama huna haja ya uthibitisho ama hata huelewi unachouliza ni nini.
 
Assumptions ni mbaya au nzuri?

Kama ni nzuri huna point kuishutumu physics kwa kufanya assumption.

Kama ni mbaya huna point kusema mungu yupo kwa assumption.

unajua kabisa huwezi kufanya assumption bila experience..ata physics hufanya hivo..kene physics hakuna 100% machine efficence..lkn calculations zao wanaweka assumptions kwamba 100% efficience ipo na inawasaidia kusolve problem zao.

na mimi je nikiamini MUNGU yupo na ananisaidia matatizo yangu kuna kosa..
 
Sina tatizo unaposema unaamini mungu yupo.

Hilo una haki ya kusema kwa kutetewa na mazimio ya Umoja wa Mataifa na jamii zote zinazopenda utawala wa wema wa kimataifa.

Nina tatizo unaposema mungu yupo, kwani hapo umetoka katika duru la imani na kutoa statement ya fact.

Na kwa sababu hiyo, utatakiwa uthibitishe hilo.

Thread hii haijajikita kwenye imani kama ilivyojikita kwenye ushahidi.

Kichwa cha thread hakiongelei imani.Imani kila mtu ana yake na kama nilivyosema, ni jambo la binafsi zaidi.

Hata mtu akisema anaamini mungu ni funza aliyeko kidoleni mwa babu yake, sina tatizo naye. Kashajipa leseni ya imani tayari, siwezi kumshikia bango.

Ukianza kuondoa neno "naamini mungu yupo" na ukasema "mungu yupo" habari nzima inabadilika.
 
I doubt you have the capacity to capture the analogy, or if you do, that your cognitive dissonance will let you be generous with the right comments.

Wewe unaponitaka nikupe uthibitisho bila kunipa kipimo chako cha uthibitisho unaoweza kuuelewa na kuukubali ni sawa na mtu anayeniuliza umbali wa Dar mpaka Arusha halafu mimi nikitaka kujua nimueleze umbali kwa kipimo gani hataki kuniambia nitumie kipimo gani.

Wewe ama huna haja ya uthibitisho ama hata huelewi unachouliza ni nini.

Hivi kwanini unaamini unachokiongea kinamaana?

Nishakwambia hadithi yako ya umbali wa Dar hadi Arusha si ya kuthibitisha.

Hivi uthibitisho hauwi wa ukweli kama hakijatumika kipimo cha mwenyekutaka huo uthibitisho au uthibitisho unaweza ukawa wa ukweli ila usikubaliwe kwa sababu kipimo cha mtaka huo uthibitisho hakipo?

Hebe naomba unijibu hapo kwanza.
 
Mimi naweza kukwambia nimethibitisha kitu ndotoni, kwa sababu nimeota ni uthibitisho wangu wa kwamba, kwa mfano, mungu hayupo.

Utaukubali uthibitisho huo?
 
Sina tatizo unaposema unaamini mungu yupo.

Hilo una haki ya kusema kwa kutetewa na mazimio ya Umoja wa Mataifa na jamii zote zinazopenda utawala wa wema wa kimataifa.

Nina tatizo unaposema mungu yupo, kwani hapo umetoka katika duru la imani na kutoa statement ya fact.

Na kwa sababu hiyo, utatakiwa uthibitishe hilo.

Thread hii haijajikita kwenye imani kama ilivyojikita kwenye ushahidi.

Kichwa cha thread hakiongelei imani.Imani kila mtu ana yake na kama nilivyosema, ni jambo la binafsi zaidi.

Hata mtu akisema anaamini mungu ni funza aliyeko kidoleni mwa babu yake, sina tatizo naye. Kashajipa leseni ya imani tayari, siwezi kumshikia bango.

Ukianza kuondoa neno "naamini mungu yupo" na ukasema "mungu yupo" habari nzima inabadilika.

kwahiyo hapo majibu yangu yanakua kati ya haya
1.naamini MUNGU yupo
2.MUNGU yupo
jibu langu namba 1.kwasababu tuliambiwa tuishi kwa imani

nawewe je majibu yako ni yapi kati ya haya
1.unaamini MUNGU hayupo
2.MUNGU hayupo.

then kila mmoja ataomba uthibitisho wamajibu yamwenzie ilitujue tunaulizana nini.

uthibitisho wangu utatokana najibu langu pale juu.kwakua thread yako inakataa jibu langu..basi nami ningependa kujua jibu lako hapo juu ilijiridhishe,kama kweli nipo nje ya mada

Hiwezi kusema unaamini mungu yupo halafu hapo hapo ukaaema mungu yupo.

The two are mutually exclusive.

Ama unasema unaamini mungu yupo, ama unasema mungu yupo.

Unaelewa tofauti yake ni nini?

Hujathibitisha kuwepo kwa mungu.

Hujaeleza imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
 
hakika kama angeumba ulimwengu huo unausema nisinge amini yupo kwaajili ya hayo mabaya naamini yupo..

afu ulichoniuliza kule juu si nikama naami MUNGU yupo au MUNGU yupo na nimejibu mbona unaruka...nawewe naomba jibu nadhani nimekuuliza pale
 
Mimi naweza kukwambia nimethibitisha kitu ndotoni, kwa sababu nimeota ni uthibitisho wangu wa kwamba, kwa mfano, mungu hayupo.

Utaukubali uthibitisho huo?

Duh! Yani kwa ulichokiandika naona aibu mie.

Halafu mambo kama hayo ndiyo unataka watu tuyakubali tu,tukikataa basi tunaonekana hatuna elimu.
 
hakika kama angeumba ulimwengu huo unausema nisinge amini yupo kwaajili ya hayo mabaya naamini yupo..

afu ulichoniuliza kule juu si nikama naami MUNGU yupo au MUNGU yupo na nimejibu mbona unaruka...nawewe naomba jibu nadhani nimekuuliza pale

Kwa hiyo angeumba ulimwengu huo, huyo mungu muweza yote angeshindwa kykufanya uamini kwamba yupo?

Mungu wenu sio tu hayupo, kimantiki hawezekaniki kuwepo kwa sababu anajipinga yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom