COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Sawa.

Unaweza kuwa na tajiri ana uwezo wa kuwa na nyumba nzuri lakini haishi katika nyumba nzuri.

Rais anayemaliza muda wake wa Uruguay Jose Mujica anaendesha ki Volkswagen Beetle na kupenda maisha ya chini.

Analipwa $ 12,000 kwa mwezi, lakini anatoa sadaka asilimia 90 ya mshahara wake.

Sababu yake ya kufanya hivyo ni kwamba yeye anataka kuishi maisha ya kawaida kama raia wa kawaida wa Uruguay. Anaamini katika usawa wa binadamu na hataki tais awe na maisha tofauti sana na wananchi wake. Ameahawahi kitoa maneno kwamba angependa kuona marais wote wa dunia wanaishi kama wananchi wao wa kawaida.

Kwa hiyo huyu tais kwa atandards za mtu wa kawaida wa Uruguay ni tajiri, lakini anaishi maisha ya kawaida.

Na katoa sababu zake, nzuri tu, kaeleweka kwa nini kaishi maisha ya kawaida.

Maelezo yake hayana major contradiction.

Mungu wenu hamuwezi kumuelezea kwa nini alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu usio na mabaya, lakini hakuumba ulimwengu huo?

Hapa nilichofanya ni kwamba nimekuuliza swali hili, na wewe inajibu kwa kusema "mungu kaamua tu kuumba hivyo ingawa alikuwa na uwezo wa kuumba vingine".

For the sake of argument, hilo si jibu la swali langu.

For the sake of argument, nimekubali kwamba OK, mungu kaumba ulimwengu huu kama ulivyo. Hili si jambo ambalo nataka kuli challenge.

Nilichouliza, ambacho mpaka sasa hujakijibu, ni kwamba, kwa nini mungu kauumba ulimwengu huu na sio ule ambao hauna uwezekano wa mabaya?

Ukinijibu kwamba mungu alikuwa/ ana iwezo wa kuumba ulimwengu usio na mabaya lakini hakuamua tu kuumba ulimwengu huo, bado hujajibu swali langu la kwa nini kaamua kuumba ulimwengu huu na sio ule.

Hujajibu ulichoulizwa, na ulichojibu hujaulizwa.

Hata kama Rais Jose Mujica asingesema ni kwanini anaishi ya aina hiyo hali ya kuwa anauwezo wa kuishi maisha ya kitajiri je,hiyo ingemfanya asiwe tajiri?
 
sisi binadamu ni kama panyabuku wa mzumbe,tuko kwenye research na inavyo onekana pure african ndio wanafaa,sababu wako liquid,najua utauliza research ya nana ? na ya nini ? subilini kidogo nimepata wageni nitarudi.
 
Hata kama Rais Jose Mujica asingesema ni kwanini anaishi ya aina hiyo hali ya kuwa anauwezo wa kuishi maisha ya kitajiri je,hiyo ingemfanya asiwe tajiri?

Angekuwa tajiri, na angekuwa na sababu zake za kuishi hivyo.

Kutokusema hakuna maana hana sababu. Hilo moja.

Lakini huwezi kisema unamkubali na kumuelewa Mujica kama huelewi sababu za yeye kuishi anavyoishi na kufanya anavyofanya.

Ukitaka kukubali tu bila kuelewa unaweza kukuta huyo Mujica hata hayupo umekubali hadithi tu, maana unaweza kuambiwa Mujica anaruka kwa ungo pia, gari kashaliacha sasa. Ukiamini Mujica huyo yupo bila kuelewa anarukaje, utakuwa umeamini Mujica asiyekuwepo kwamba yupo.

La pili, hata kama tusingejua kwa nini rais tajiri kaanua kuishi maisha ya kimasikini, rais tajiri kuanua kuishi maisha ya kimasikini si contradiction.

Rais Mujica hajawahi kusema kwamba hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu akaenda kuishi maisha ya kimasikini.

Angekuwa amesema kwamba hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu akaenda kuishi maisha ya kimasikini, hapo kungekuwa na contraduction. Tungeuliza wote wanaomkubali watueleze huyu tais imekuwaje aseme hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu aende kuishi maisha ya kimasikini.

Hujatuambia kwa nini mungu huyu tunayeambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kiasi kwamba angeweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya hakuumba ulimwengu huo?

Ulimwengu huu una contradict the idea of an all knowing, all capable and all lobing god.

Hujaweza kuondoa hii contradiction.

Hujajibu swali langu.
 
mkuu Kiranga kwa mfano hivi mtu akikupiga na jiwe mahali popote mwilini ukaumia lakin usitoe damu kabisaa wala kuonesha dalili popote kuwa umepigwa..lakin kiuhalisia wewe umepigwa na ukawa na maumivu makali ukaja kwangu kushitaki kuwa umepigwa je mimi nitaamini vipi kwa kweli umepigwa na unasikia maumivu makali saana...hebu niconvince niamini kweli una mamivu makali sana yaliyotokana na kipigo wakati mimi siyaoni....

Swali lako linaanzia kati.

Unaongelea ulimwengu ambao mtu anaweza kukupiga jiwe, ukaumia, usitoe damu tu.

Hujaelewa au hujazingatia kwamba swali langu linaaulizia kuhusu ulimwengu ambao hauna mabaya na hivyo huwezi kupigwa jiwe, kuumia wala kutoka damu.

Katika ulimwengu huo, wewe hutahitaji ushahidi wa kwamba mimi nimepigwa jiwe na kuumia.

Kwa sababu kutakuwa hakuna ubaya wowote.

Hakuna kupigwa jiwe wala risasi, bakina haja ya ushahidi wa kwamba umepigwa. Itatakaje ishahidi kwamba umepigwa wakati kitendo cha kupigwa hakijulikani na hakiwezekani katika ulimwengu huo?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu huo?

Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu huo na akaumba huu ambao mabaya yanawezekana?

Swali hili sijajibiwa.
 
Last edited by a moderator:
anhaa kumbe sahivi hushaamini yupo ila unataka kujua kwann kaumba ulemwengu wenye mabaya.au unataka vyote...au unaona tutashindwa kujibu kwann kaumba ulimwengu wenye mabaya kisa unaamini hayupo?

hilo swali lako la kwanini kaumba ulimwengu wenye mabaya nidhambi kwetu sisi wanaimani kulijadili..nlikutolea mfano wachungu kumuuliza mfinyanzi wake kwanini umeniumba hivi...

siku sio nyingi utaenda kuwauliza wazazi wako kwanini mmenizaa mwaafrika....kiranga husitake kila unachoamini uthibitishiwe vingine prove tu mwenyewe fanya research soma reference mbalimbali unaposhindwa uliza experts..ndo uwanasayansi huo,ndo logical thinking hiyo, hatukukurupuka tu kuamini MUNGU yupo kama wewe ulivyo kurupuka kuamini hayupo

sisi tulishakatazwa kuapa bali majibu yetu yawe ndio au hapana..ukiniuliza MUNGU yupo au hayupo ntajibu yupo,..yupo wapi?anaishi pamoja nasi..mbona simuoni?naamini hivo...kwann unaamini hivo?sababu ya moja mbili tatu....basi kitacho baki hapo ni msimamo wako...

ila nakushauri tu uamini kama kweli MUNGU yupo..MUNGU muumbaji...

kwakua thread yako inataka uthibitisho utaupata tu fanya reseach,..kama unataka kumuona utamuona tu mtafute..

Wapi umeona nimesema naamini kwamba mungu yupo?

In your entire life, have you heard of "immanent criticism" ?

Kwa nini ni dhambi kwa wanadamu kujadili ulimwengu ulivyoanza?

Mungu wa haki na ukweli anaogopa nini kuwa muwazi?

Au umeambiwa ni dhambi kujadili hilo kwa sababu waliotunga hadithi ya uongo ya kuwapo kwa mungu waliona kwamba ukijadili sana utajua ukweli kwamba mungu hayupo, na njia pekee ya kukufunga macho usielewe kwamba mungu hayupo ni kukuambia kwamba kujadili mwanzo wa ulimwengu ni dhambi?

Thread haijakaa kujadili imani zaidi, imekaa kujadili ushahidi zaidi.

Kama imani unaruhusiwa hata kuamini kwamba mungu ni funza aliyekuwa kwenye kidole cha babu yako. Ukiamini hivyo hilo halina tatizo. Unatetewa na "The Universal Declaration of Human Rights" kuanzia 1948.

Thread inajadili ushahidi na uthibitisho.
 
kama unaona walitudanganya kwamba kuna MUNGU..huko ni kutokufikiria....watu toka zamani walikua wanatengeneza nakuabudu miungu yao..watu walikua wakitafuta kitu chakuabudu ili kiwatatulie matatizo yao..

ndipo walipo tokea manabii unaowaita wadanganyifu..na ndio walio tuonesha MUNGU wakweli....MUSA ndo mtume wamwanzo kabisa kuandika kuhusu MUNGU..basi dhumuni lake la kudanya ni nini?

gharika la nuhu mwenyezi MUNGU alidhihirisha kuchukizwa na maovu na kuangamiza binadamu..kwahiyo nuhu alivo waambia MUNGU kasema hivi alidanganya nini pale...

YESU alipo eleza habari za MUNGU alidanganya iliiwaje sasa?..au unahisi kuna watu wabaya walitumia nadharia ya MUNGU ili watufanyie kitu kibaya? tueleze....

ni nani hasa alidanganya na kwa lengo lipi?...inabidi ujitosheleze unapotaka kusema kitu kilidanganywa.....

ww kamanimekuelewa vizuri,kwamba hukubali kitu ambacho hujathibitishiwa,..kwan kuna mtu alishawahi kukuthibitishia kwamba ulizaliwa,

kwani kuna mtu alishawahi kukuthibitishia kwamba kuna pumzi?

kwani mchumba wako alisha wahi kukuthibitishia kwamba anakupenda?

kwani kuna mtu alishawahi kukuthibitishia kwanini mawingu pamoja nauzito wake wote lkn haya dondoki?

kuna mtu alishawahi kukuthibitishia mabara yalikua yameonganishana zaman?

kuna mtu alishawahi kukuthibitishia kwanini binadamu ana damu na inatoka wapi?

ni vichache kati yamengi ambayo hujathibitishiwa lkn unaamini tu...kwann ukurupukie tu kuthibitishiwa MUNGU na hapohapo ukatae kuamini..wakati ujajiuliza hayo madogo yaliyoshindwa kuthibitishwa...TULIZA AKILI NDUGU usikurupeke....kunawatu hawalali wanaangaika kuprove MUNGU hayupo..weusha conclude tayar tayar kienyenyi...tena kwanjia yakutaka kuthibitishiwa tena kwaubaguzi wapoint(una neglet imani)....TULIA KWANZA....

Ahsante
 
Kiranga naona unajitoa ufahamu...swali langu limebase katika ulimwengu huu hu tuliopo ambao tayari mabaya yapo na tunayaona.....nieleze ili nikubali kuwa umepigwa jiwe na unasikia maumivu makali....nasubiri jibu
 
Last edited by a moderator:
Jaman hayo mambo yamungu hacheni kuyajadil mwenyez mungu aletewi dhiaka aina yyote ile wala mifano ambayo ni dhiaka kwake hayo ci mafunzo, ci munaona mungu kwa mifano komba Leo Yuko wp?.
 
nijothemaster umetisha mkuu kwa hayo maswali ulompa....yani anaamini kabisa kuwa dunia ni mviringo wakati wala hajawahi kupanda chombo chochote cha angani ili akathibitishe hilo
anaamini kabisa kama baba na mama yake kweli ndo wazaz wake kwa kuambiwa tu...hajawahi kuthibitisha hilo
anaamini moyo wake unadunda na kusukuma damu hata hajawahi kuuona
anaamini kabisa kuwa akiumwa ugonjwa fulani na daktari akamwambia hvo na kumpa dawa anaitumia dawa ile na anapona...kaambiwa tu hajathibitisha kabisaa
afadhali hata wanaosema hawana uhakika na uwepo wa Mungu huku wanaendelea na research zao kujua ukweli kuliko kiranga anahitimisha kwa hoja dhaifu na sababu zile zile za mfumo wa kuuliza maswali yaleyale kila siku... Kiranga jipange asee
 
Last edited by a moderator:
Angekuwa tajiri, na angekuwa na sababu zake za kuishi hivyo.

Kutokusema hakuna maana hana sababu. Hilo moja.

Lakini huwezi kisema unamkubali na kumuelewa Mujica kama huelewi sababu za yeye kuishi anavyoishi na kufanya anavyofanya.

Ukitaka kukubali tu bila kuelewa unaweza kukuta huyo Mujica hata hayupo umekubali hadithi tu, maana unaweza kuambiwa Mujica anaruka kwa ungo pia, gari kashaliacha sasa. Ukiamini Mujica huyo yupo bila kuelewa anarukaje, utakuwa umeamini Mujica asiyekuwepo kwamba yupo.

La pili, hata kama tusingejua kwa nini rais tajiri kaanua kuishi maisha ya kimasikini, rais tajiri kuanua kuishi maisha ya kimasikini si contradiction.

Rais Mujica hajawahi kusema kwamba hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu akaenda kuishi maisha ya kimasikini.

Angekuwa amesema kwamba hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu akaenda kuishi maisha ya kimasikini, hapo kungekuwa na contraduction. Tungeuliza wote wanaomkubali watueleze huyu tais imekuwaje aseme hataki kuishi maisha ya kimasikini, halafu aende kuishi maisha ya kimasikini.

Hujatuambia kwa nini mungu huyu tunayeambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kiasi kwamba angeweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya hakuumba ulimwengu huo?

Ulimwengu huu una contradict the idea of an all knowing, all capable and all lobing god.

Hujaweza kuondoa hii contradiction.

Hujajibu swali langu.

"Hujatuambia kwa nini mungu huyu tunayeambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kiasi kwamba angeweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya hakuumba ulimwengu
huo?"

Mara ngapi tumeeleza kuwa haya maisha ya hapa ulimwenguni Mungu ameyafanya kuwa ni mtihani kwetu? Kwahiyo angetaka kufanya huu ulimwengu usiwe na maovu basi angefanya hivyo kwa sababu uwezo anao. Kama ilivyo kama Rais Jose Mujica angetaka kuishi maisha ya kitajiri angefanya hivyo uwezo huo anao,ila akaamua kuishi maisha ya kawaida kama raia mwengine tu wa kawaida. Hiyo ndiyo sababu yake.

Na mungu pia angetaka kusiwe na uovu angefanya hivyo. Ila yeye sababu yake ni kutupa mtihani,hivyo haya matatizo tunayoyaona ni sehemu ya mtihani.

Na Mungu hajasema kwamba ameyafanya haya maisha ya ulimwenguni ni ya raha yani kwamba hayana matatizo yeyote.

Kwa sababu kuna watu ambao tunasema wanaishi maisha ya raha,labda kutokana na utajiri wao,lakini ukichunguza unaweza kukuta mtu ambaye tunasema anaish maisha ya raha ukakuta ana tatizo lake kubwa kuliko hata matatizo aliyonayo masikini. Yote ni sababu mungu akuyafanya haya maisha kuwa ni ya raha.
 
Jaman hayo mambo yamungu hacheni kuyajadil mwenyez mungu aletewi dhiaka aina yyote ile wala mifano ambayo ni dhiaka kwake hayo ci mafunzo, ci munaona mungu kwa mifano komba Leo Yuko wp?.

mwambie kiranga huyo anataka kututoa imani.mwezi huu....
 
Kwa nini mungu anayejua yote, kuweza yote na kuwa na upendo wote ahitaji mtihani au ahitaji tuwe na mtihani?

Unaposema angetaka kuumba ulimwengu huo usio na mabaya angeumba, hujajibu swali langu la kwa nini kaumba hivi na si vile.

Unaposema kaamua tu kuumba hivi na si vile, hujatupa sababu. Usipotupa sababu, unakubali kwamba hujajua sababu na kama hujajua sababu,humuelewi mungu huyo, na kama humuelewi mungu huyu kwa kitu cha msingi kama hiki, unaweza kufikiri yupo wakati hayupp no hadithi tu.

Nafikiri hujaelewa kabiaa maana yangu ninapoandika "ulimwengu usiowezekana mabaya". Inatafsiri kwamba mtu anaweza kuwa na raha halafu ile raha ikawa na tabu.

Naomgelea ulimwengu ambao mabaya yamepigwa marufuku kabisa.

Kwa nini mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote hakuumba hivyo?
 
Jaman hayo mambo yamungu hacheni kuyajadil mwenyez mungu aletewi dhiaka aina yyote ile wala mifano ambayo ni dhiaka kwake hayo ci mafunzo, ci munaona mungu kwa mifano komba Leo Yuko wp?.

Kabla ya kumuongelea sana mungu, unaweza kuthibitisha kwamba yupo?
 
Kwa nini mungu anayejua yote, kuweza yote na kuwa na upendo wote ahitaji mtihani au ahitaji tuwe na mtihani?

Unaposema angetaka kuumba ulimwengu huo usio na mabaya angeumba, hujajibu swali langu la kwa nini kaumba hivi na si vile.

Unaposema kaamua tu kuumba hivi na si vile, hujatupa sababu. Usipotupa sababu, unakubali kwamba hujajua sababu na kama hujajua sababu,humuelewi mungu huyo, na kama humuelewi mungu huyu kwa kitu cha msingi kama hiki, unaweza kufikiri yupo wakati hayupp no hadithi tu.

Nafikiri hujaelewa kabiaa maana yangu ninapoandika "ulimwengu usiowezekana mabaya". Inatafsiri kwamba mtu anaweza kuwa na raha halafu ile raha ikawa na tabu.

Naomgelea ulimwengu ambao mabaya yamepigwa marufuku kabisa.

Kwa nini mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote hakuumba hivyo?

Kiranga umeuliza KWANINI ulimwengu una maovu lakini mungu amesema ana upendo na uwezo wote? Nimeshajibu swali.

Ukiuliza kwanini Mungu mwenye uwezo na upendo aweke mitihani?hili ni swali lengine kabisa ni sawa ni sawa na kuuliza kwanini Rais Jose Mujica ni tajiri halafu aamue kuishi maisha sawa na raia wengine,kwanini atake maisha ya usawa wakati yeye uwezo anao?kwanini asingejenga jumba la kifahali na kununua gari la kifahali?

Hoja ilikuwa ni mtu tajiri lakini anaishi maisha ya kawaida na Mungu ana uwezo na upendo lakini ulimwengu una matatizo.

Kuna anayemlazimisha Rais Jose Mujica kuishi hivyo?
 
Kiranga naona unajitoa ufahamu...swali langu limebase katika ulimwengu huu hu tuliopo ambao tayari mabaya yapo na tunayaona.....nieleze ili nikubali kuwa umepigwa jiwe na unasikia maumivu makali....nasubiri jibu

Unataka nikijibu swali langu wakati wewe hujajibu swali langu, wakati mimi ndiye niliyeanza kuuliza?

Unaona sawa hilo?

Mimi nimekuuliza, kwa nini mungu kaumba ulimwengu huu ambao mabaya yanaweza kucanyika na mtu akamrushia mwi gine juwe wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki kufanyika na mtu mmoja hawezi kumtupia mwingine jiwe?

Hujanijibu swali hili, unataka nikijibu lako?

Unasema unataka nijibu swali lako la ulimwengu huu tunaouona, halafu hapo hapo unataka nikubali kuwapo kwa mungu ambaye hayupo katika ulimwengu huu wa kuonekana?

Hivi unaelewa umesimamia wapi wewe?

Katika ulimwengu huu au huo?

Huwezi kutaka kujibiwa maswali yako tu yaliyokuja baadaye wakati yangu ya awali hujayajibu.

This is a two way street.

Have some sense of reciprocity.
 
Last edited by a moderator:
Kiranga umeuliza KWANINI ulimwengu una maovu lakini mungu amesema ana upendo na uwezo wote? Nimeshajibu swali.

Hata swali hujalielewa mpaka sasa. Sijauliza kwa nini ulimwengu una maovu. Nimeuliza kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaamua kuumba ulimwengu ambao unaruhusu maovu wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu maovu.

Maswali mawili haya ni tofauti, na kama huelewi tofauti yake, sitegemei kwamba utaweza kujibu swali langu.

Ukiuliza kwanini Mungu mwenye uwezo na upendo aweke mitihani?hili ni swali lengine kabisa ni sawa ni sawa na kuuliza kwanini Rais Jose Mujica ni tajiri halafu aamue kuishi maisha sawa na raia wengine,kwanini atake maisha ya usawa wakati yeye uwezo anao?

Hujajibu swali. Kama unamuelewa mungu unatakiwa ujue reasoning yake.Kama huwezi kujibu huelewi reasoning.Kama huelewi reasoning ya mungu humuelewi idea ya mungu huyo, kama huelewi idea ya mungu huyo unaweza kufikiri yupo wakati hayupo, katungwa tu na watu.

Hoja ilikuwa ni mtu tajiri lakini anaishi maisha ya kawaida na Mungu ana uwezo na upendo lakini ulimwengu una matatizo.

Nilichohoji ni sababu zilizomfanya mungu kuumba ulimwengu ambao unawezekana kuwa na mabaya na matatizo wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauna matatizo.

Hujajibu swali hili.

Jibu la kutupa mitihani linapwaya, kwa sababu mungu anayejua yote, kuweza yote na mwenye upendo wote hahitaji kutupa mitihani ya kutuua na kututesa ili kuweza kufanya chochote anachotaka.

Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao binadamu anaumia na kuteseka sana kwa maovu, tena wengine watoto wadogo ambao hata hawana hatia, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya?

Huyu mungu hana huruma? Mbona mnasema ni mwingi wa huruma?

Sasa vile vitoto vinavyokufa kwa mafuriko Shinyanga (tumeona picha zinatisha) hakuvihurumia alipoumba ulimwengu ambao mafuriko yanaweza kutokea na kuua vitoto masikini?

Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao mafuriko hayawezi kutokea wakati alikuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kwa mujibu wenu?

Hujanipa sababu zinazoeleweka kimantiki.
 
Back
Top Bottom