Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
We mbona unachekesha! Wapi niliposema hivyo?
Mie nimekwambia hizo zote ni sifa zake. We vp mkuu hebu onyesha niliposema hayo uliyosema.
Mungu anawezaje kuwa na sifa zinazopingana?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We mbona unachekesha! Wapi niliposema hivyo?
Mie nimekwambia hizo zote ni sifa zake. We vp mkuu hebu onyesha niliposema hayo uliyosema.
Duh, I was watching the movie "Exodus: Gods And Kings".
I meant to watch this nikasahau, labda watairudia.
Ukisoma sana falsafa ya dini lazima ugundue kwamba huyu mungu wa ukristo na uislamu ni kujiliwaza tu, hayupo.
Yeah nadhani watairudia tu kwa sababu mara nyingi huwa wanafanya hivyo.
Impression niliyoipata ni kwamba imani atheism inazidi kuongezeka hususan huku kwenye Bible Belt.
Halafu kumbe mtoto mmoja wa Reagan naye ni atheist!
Mungu anawezaje kuwa na sifa zinazopingana?
Nitaitafuta.
Atheism inao geza kukubalika kadiri ujinga unavyozidi kufutika, tatizo ni kwetu huku ambako watu hawajafuta ujinga, ukuongelea atheism unaonekana kama umetoka Andromeda galaxy.
Yule mtoto wa Reagan niliona tangazo moja kasema yeye atheist, hata mimi nilikuwa sijui.
Watu wengi ni atheists ila wako pragmatic about it kwa sababu za kijamii tu.
Leo usiku 9 ET CNN wana special report kuhusu wakana mungu - Atheists: Inside the World on Non-Believers.
Nimeona snippets kadhaa na mojawapo ni ya pastor mmoja ambaye yuko kwenye 'closet' i.e. ni atheist lakini waumini wake hawajui. Kwenye mahojiano ilibidi waizibe sura yake na kuibadilisha sauti yake ili asigundulike.
Nilipoona hiyo nikakumbuka ulichowahi kusema kuhusu Papa Francis kwamba inawezekana jamaa ni bonge moja la atheist (for which I can see because he appears to be too smart, practical, sensible and realistic to just believe in something that doesn't make sense by most standards) lakini kwa sababu fulani fulani hawezi tu kusema wazi.
Sounds like it's gonna be an interesting program and I intend to watch it.
Ni wewe ndiye unayesema hivyo kuwa zinapingana. Na hapa naomba ufafanuzi zaidi kujipinga ni kupi.
Halafu hadi sasa sioni ushahidi wa kuthibitisha kuwa hakuna Mungu. Naona malalamiko ya sifa za Mungu kujipinga.
Mungu wako anasemwa kwamba ni wa upendo, mwenye huruma kuu, mtawala mkuu, chanzo cha amani, mtoa vyote, mjua yote, mkarimu, muelewa yote , mwenye nguvu zote
Sifa hizi zipo katika majina 99 ya Allah.
Hapo hapo tunaambiwa ni mdhalilishaji (majina 99 ya Allah).
Inakuwaje mungu mwenye upendo, huruma, uwezo wote, mwenye nguvu zote, chanzo cha amani etc awe mdhalilishaji?
Imekuwaje mungu mwenye ujuzi wote, upendo mkuu, uwezo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ilhali alikuwa na kila uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
mara kadhaa papa francis ashawai sema mungu hajaumba kila kitu humu duniani, ni wajinga wachache tu ndio bado wnakomaa na kitu kisichokua halisi.........Pope Francis declares evolution and Big Bang theory are real and God is not 'a magician with a magic wand' - Europe - World - The Independent
Ndiyo maana uislamu unapigwa vita sana kwa sababu hakuna nafasi ya mafreemason kama huyo Pope kujipenyeza na kuingiza mambo yao kama wanavyofanya kwn ukristo.
Endelea kufuatilia zaidi mkuu utaelewa mengi.
Nimekuomba tafsiri ya kujipinga kwanza. Hata usiwe na wasi.
Na bado nasubili ushahidi wenye kuthibitisha kuwa hakuna Mungu.
Hujajibu swali la kwa nini mungu anatujaribu viumbe wake dhaifu wakati anajua kila kitu?
Mwalimu wa sekondari akitoa mtihani ili kujua wanafunzi wake wameelewa nini na wana uwezo gani nitaelewa, kwa sababu inawezekana mwalimu anataka kujua uwezo wa wanafunzi wake na hana namna ya kujua hilo nje ya mtihani.
Mungu anayejua yote na kuweza yote kwa nini atupe mtihani?
Nashukuru sasa umenielewa na ukatoa mfano wa mwalimu wa sekondari lakini kosa unalifanya kusudio halisi ya kukuleta kwenye mfano wa mtihani lilikuwa ni mwanafunzi kufaulu tu.
Wewe Kiranga unajaribu kubadilisha kusudio na kuingiza mwalimu kutazama uwezo wa wanafunzi.sipingi kwa upande wa mwalimu bali mimi napinga kwa upande wa Mwenyezi Mungu.
Mungu anakipima kitu anachokijua ili kisipate sababu siku ya kiama ya kwamba niliachwa tu.
Hivi anadhani kuwa mtu ataachwa bure bure tu! Qur-an(75:36) ...
Mwenyezi Mungu ANAMTAHINI mwanadamu kwakua amempa akili.Mwanadamu sio KUKUwalaHakika tumemtukuza mwanaadamu... Qur-an(17:70).
uislam na ukristo wote lao moja kuja na idea ya mungu mjua kila kitu eti aliyeumba kila kitu!!! wote wanaabudu mungu hewa, aisyethibitishika achilia mbali kuelezeka wala kuonekana so in essence they are just the same!!!
uislam na ukristo wote lao moja kuja na idea ya mungu mjua kila kitu eti aliyeumba kila kitu!!! wote wanaabudu mungu hewa, aisyethibitishika achilia mbali kuelezeka wala kuonekana so in essence they are just the same!!!
Kujipinga ni kuwa na mielekeo ya msingi miwili tofauti.
Kama pembetatu kuwa duara wakati mmoja na mahali pamoja.
Mungu wenu anajipinga kwa kuwa kwa upande mmoja ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, lakini upande wa pili kaumba ulimwengu wenye kuwezekana mabaya mengi sana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaqezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili kwa ufanisi wa kuondoa kujipinga huku.
Nimekuwa nikisema hili kitambo hapa.
Kwa mtu anayesoma falsafa ya dini na juchambua dini tofauti, hususan za Asia, unavyozidi kusoma dini tofauti ndivyo unavyozidi kugundua kwamba Uislamu na Ukristo, licha ya tofauti zao cosmetic, vimechangia mengi sana kutoka katika shina la Uyahudi.
Mielekeo ya msingi miwili tofauti ndiyo nini mkuu? hebu fafanua,halafu na huo mfano wako wa pembe tatu hata sioni kuendana na hiyo tafsiri ya "mielekeo ya msingi miwili tofauti" hebu tuliza mapepe usitake kutoa tafsiri zenye kukidhi unayoyataka kusema wewe.
Pia usisahau kuwa bado nasubili ushahidi wa kutokuwepo kwa Mungu.
Tatizo wote nyie mmetoka kwn ukristo na kufuata huko mliko.
Mwenye upendo mkuu na uwezo woye hawezi kuumba ulimwengu unaoqezekana kuwa na mabaya.
Hiyo ni contradiction.
Mungu wako ana mielekeo miwili ya msingi inayopingana.
Huku tunaambiwa ana upendo, huku kaumba ulimwengu ambao unaruhusu watoto masikini wafe kwa ebola.
Huyu mungu ni wa kufukirika zaidi, ukimchekecha katika logic anabaki kuwa chuya.
Mpaka sasa hujaniambia ni kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezeka i.