Colabo ya Joel Na Diamond haina afya kabisa kutokana na maadili ya Diamond

Madam christina alionekana yuko karibu sana na diamond ikadhaniwa anataka kufanya collabo naye
 
Wanamuziki wa injili ambao wako likelly kufanya collabo na wanamuziki wa kidunia wako wengi wala si joel tu. Joel alishafanya collabo na barnaba hakupigiwa kelele, labda barnaba ni muadilifu
 
Collabo za waimbaji wa injili na wanamuziki wa kidunia inategemea imani ya waimba injili ikoje. Kama muimbaji wa nyimbo za injili anaona ni biashara kufanya collabo na mwanamuzi wa kidunia poa tu. Kuna mmoja alishirikishwa kwenye tuzo za kampuni ya bia na akashika chupa ya bia wakati wa kupokea tuzo, waumini walimuona sio, wakavunja vunja cd zake majumbani mwao, mpaka leo hawana imani na muimba injili huyo maarufu
 
Wako wengi waimbaji wa injili wanaotamani kufanya collabo na wanamuziki wa kidunia. Wanaona ni fasheni mpya kushirikiana na watenda dhambi ili ujumbe ufike. Cha ajabu verse wanazoimba wa kidunia haziko kiinjili kama verse za wainjili, unakuta wimbo ni mmoja ila ni mix injili mix kidunia japo mukhtadha ni mmoja, wimbo kama omoyo remix wa jane miso feat harmonize na huu wa joel lwaga feat diamond. Hawa wa kidunia kumtaja Yesu kwenye verse zao ni shughuli pevu
 
Joel lwaga na barnaba mbona hamkupiga kelele, kwani nyie ndo watoa hukumu mpka mumwone diamond ni mchafu kuzidi wengine? Una uhakika gani huyo pastor wako ni msafi kuliko diamond au kwa vile anakuombea kanisani ndo unasema ana kibali mbele ya Mungu??
 
 
Kwamba kosa la Joel lwaga ni kushirikiana na diamond kufanya mziki si ndio? Kwahiyo Leo wenye dhambi inabidi tuwatenge?? Au tusishirikiane nao kivyovyote?? Au ndo mpka watubu na kuondoka ndo tuwaamini?? Acheni kuhesabu haki asee hicho mnachofanya ni ujinga
 
Hapa Afrika hakuna mtu ambaye tunaweza kusema unau practise ukristu katika ukamilifu wake wote, wengi ambao wanajiita wakristu are not full Christians ila still wana guts za kukosoa na kuwaona wengine kama mashetwani.
 
Itokee collabo ya Rose Muhando feat J melody au jux au marioo au rayvanny, Angel Bernard feat Nandy, Bella Kombo feat Fina, Bony Mwaitege feat Christian Bella, Masanja mkandamizaji feat Dulla makabila, vipi hapo?
 
Wanaona ni fasheni mpya kushirikiana na watenda dhambi ili ujumbe ufike
Njia mojawapo ya kukufanya uendelee kuwa na imani ni pamoja na kujiweka mbali na hawa watumishi wa nyumba za imani. Unajua ni kwanini ipo hivyo ?
 
Hata maandiko yanasema sikuja kwaajili ya wema bali kwajili ya wenye dhambi Yesu mwenye alisema pia sio wote wasemao bwana bwana watauona ufalme wa mbingu
 
Yesu mwenyewe alisema,ajaja kwa ajili ya watakatifu Bali wenye dhambi.
Yesu alikosea kuingia nyumbani kwa zakayo
Kuoshwa miguu na kahaba
 
Wewe ni mtakatifu sana? Wee mbona una dhambi ya UONGO, juu ya sakata la usajiri wa Aziz Ki, na uzi wako uko humu.

Asiyekua na kosa na awe wa kwanza kurusha mawe.
Hasibu bhana, khaaah
 
Wanamuziki wa injili ambao wako likelly kufanya collabo na wanamuziki wa kidunia wako wengi wala si joel tu. Joel alishafanya collabo na barnaba hakupigiwa kelele, labda barnaba ni muadilifu
Nani kakuambia Barnaba ni muadilifu? Na uwadilifu wa mtu unapimwaje?
 
wimbo wa joel uliopokelewa vema ni ule wa kwanza tu, zilizofuata zikawa hazina mvuto, ni baridi mpaka akaanza kushirikiana na wanamuziki wa kidunia. Unaambiwa hukumu ya bwana huanzia nyumbani kwake acheni ahukumiwe na wakristo wenzake. Wakristo ukienda nje ya code zao kitakulamba tu wala msimtee na asijitetee aombe radhi jamii yake, asishupaze shingo kama anavyotoa povu jingi kwa wanaomuhukumu
 
Joel si mpole wala mnyenyekevu, huo si ukristo, kama anaona anahukumiwa isivyo angeomba radhi/samahani kwa jamii ya kikristo ambayo ndiyo wasikilizaji wakubwa wa nyimbo za injili. Anakuwa mkaidi huku anajua kaenda nje ya code za muimba injili. Waimba injili wanajulikana misimamo yao kiimani.
 
Wapi hiyo track. Mwenye nayo ashee please.
 
Uislamu haukubaliani na mashoga. Kwa hiyo, hawakubaliani na Diyamond hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…