Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

Badala ya project za haya magorofa ya kichina kwa nini wasitujengee viwanda vikubwa vya kutengeneza products zinazotokana na raslimali zetu angalau kila mkoa ili wakulima huko vijijini wapate soko la kuuzia mazao yao na waliko mjini tupate ajira za kutosha.Hii ndiyo miradi ya msingi kabisa ambayo kila serekali ya nchi masikini kama yetu inatakiwa kuanza nayo,ila kwa ma-genius na first class economists wa ccm hayo maghorofa na misururu ya magari barabarani ndiyo maendeleo .
 
He he he he, niitumie lipstic??

Ubaya lipstick kanunua mwanamme, naye aitujmie

Ukiipatia vizuri matumizi yake, hiyo lipstick itazalisha mchele, nyama, soda, ma-juicy; nini unga wa uji !!
 
hahahahaha.!
bongo bhana, kazi ya kutu tishatisha na 'mapichapicha' tu, plans kibao sasa ona utekelezaji.! on the field hakuna chochote kile, sasa uliza uone maripoti ya tathimini ma-master plan sijui manini nini kibao...
tutaiona serikali iko serious kama tutaanza kuona utekelezaji 'serious' wa kigamboni city sio kila siku kutuletea mipicha yao hii...
ni kweli tunataka maendeleo, but sio kwa stahili hii ya kutulaghai laghai..
 
mkuu n00b, katika miradi inayoendelea labda ungetuwekea na ule wa ujenzi wa uwanja wa taifa almaarufu kama 'SHAMBA LA BIBI' na significance yake ya kuwa na viwanja viwili vikubwa vilivyoungana, wengine hatujajua malengo ya serikali ni nini kwenye hivyo viwanja kama itakavyoweza kuwa kwa hiyo mingine pia. Hii sio siasa tafadhali
Mi nataka tuanze kuongea kisomi mkuu wangu, hujanikwaza. Ni challenge ambayo tunayo kwa sasa kama taifa. Sasa, tukomae tujue status za miradi hii na kama fedha kwa ajili ya miradi hii zipo. Tunaweza kuanza kutembea vifua mbele (hata kama hatuna stake katika projects zenyewe) endapo hii miradi itafanikishwa bila kuvurugwa.

Ikitokea huu ukafanikiwa, wa Kigamboni ukafanikiwa na mingine zaidi, basi kuna afueni tutaiona angalau ukilinganisha na majirani zetu
 
Michoro michoro......
Mipango....vision.....
Dar Chalinze njia sita!
Mji wa Luguruni....
Mji wa Kigamboni...
Mji wa Magomeni, Temeke? and now Kawe??
Wanatumia michoro ya rangi rangi kuwaweka sawa watu...bassssss....
Conceptual design....Argggggh!
Hata Rage nae alikuja na uwanja wa kisasa.....Manji nae na conceptual design....nzuri sana!
Ila on the ground ....sifuri!
 
He he he he, niitumie lipstic??

Ubaya lipstick kanunua mwanamme, naye aitujmie
Kongosho, hapo kwenye RED....ni Kichina, au? Let me guess, cursor huwa ina-jump to anywhere it feels to go! Na kuhusu hilo la lipstick, mbona unanishangaza aisee; we wa wapi?! Siku hizi baadhi ya wababa mambo ya ma-lipstick, sijui ma-lipshines, mbona kawaida tu Kongosho!
 
Last edited by a moderator:
Hii itatokea labda miaka 200-300 ya Uhuru wa Tanganyika

Tutakuwa wote tulishaonja umauti na kurudi tena duniani! inanikumbusha ile hadithi ya kitoto kwamba ukifa Afrika unazaliwa Ulaya!. Kigamboni nimeisikia kabla sijamaliza chuo na bado hata haijaanza na leo tunapigwa kombora lingine; khaaaaa.

Kuna mradi mwingine niliwahi kuuona kwenye magazeti mwaka 2000 ukiwa ni kutoka mjini pale seaview kwenda kule Oysterbay. Huu ulikuwa ni mradi wa kuchukua sehemu ya bahari na kuifanya nchi kavu kisha kujenga maduka na mijihoteli; nikashuhudia picha tamu kama hii ya leo lakini hadi leo ni ndoto tuu! Tuendelee kuota kwa matumaini.
 
Haya bwana, umeshinda

Ngoja nisubiri kwa hamu matunda ya lipstick

Kongosho, hapo kwenye RED....ni Kichina, au? Let me guess, cursor huwa ina-jump to anywhere it feels to go! Na kuhusu hilo la lipstick, mbona unanishangaza aisee; we wa wapi?! Siku hizi baadhi ya wababa mambo ya ma-lipstick, sijui ma-lipshines, mbona kawaida tu Kongosho!
 
Tutakuwa wote tulishaonja umauti na kurudi tena duniani! inanikumbusha ile hadithi ya kitoto kwamba ukifa Afrika unazaliwa Ulaya!. Kigamboni nimeisikia kabla sijamaliza chuo na bado hata haijaanza na leo tunapigwa kombora lingine; khaaaaa.

Kuna mradi mwingine niliwahi kuuona kwenye magazeti mwaka 2000 ukiwa ni kutoka mjini pale seaview kwenda kule Oysterbay. Huu ulikuwa ni mradi wa kuchukua sehemu ya bahari na kuifanya nchi kavu kisha kujenga maduka na mijihoteli; nikashuhudia picha tamu kama hii ya leo lakini hadi leo ni ndoto tuu! Tuendelee kuota kwa matumaini.
Mradi huo mkuu wangu Kimbunga hawezi kutekelezeka ima faima coz' yale maeneo washajigea! Kwa mradi ulikufa automatically Che Ben alipoamua kuwagea wenzake nyumba za serikali!
 
Last edited by a moderator:
Kongosho, hapo kwenye RED....ni Kichina, au? Let me guess, cursor huwa ina-jump to anywhere it feels to go! Na kuhusu hilo la lipstick, mbona unanishangaza aisee; we wa wapi?! Siku hizi baadhi ya wababa mambo ya ma-lipstick, sijui ma-lipshines, mbona kawaida tu Kongosho!
unaowasema wewe labda ni wale wababa wa kwenye mchezo wa comedy
 
Michoro michoro......
Mipango....vision.....
Dar Chalinze njia sita!
Mji wa Luguruni....
Mji wa Kigamboni...
Mji wa Magomeni, Temeke? and now Kawe??
Wanatumia michoro ya rangi rangi kuwaweka sawa watu...bassssss....
Conceptual design....Argggggh!
Hata Rage nae alikuja na uwanja wa kisasa.....Manji nae na conceptual design....nzuri sana!
Ila on the ground ....sifuri!

Mkuu hii nasikia iko njiani kwa mtindo wa PPP
 
Mkuu hii nasikia iko njiani kwa mtindo wa PPP

Yap....imetangazwa zabuni tayari!
Unakumbuka daraja la kigamboni? PPP ilishindikana hadi wakailazimisha NSSF iwekeze!
 
Mkuu,

Si ndoto. Na nikufahamishe ni kuwa tayari eneo la Kawe pale Tanganyika Peckers pamesharejeshwa ardhi kwa asilimia nadhani zaidi ya 50.

FYI, kuna project nyingine inakuja. Tanzanite Mall na itakuwa inaonekana kama inavyoonekana hapa chini (nimefuatilia Brela, naona kuna kampuni imesajili 2011 inaitwa "Tanzanite Mall Ltd" nahisi ndio wenye hii project):
hongera kwa kufuatilia, hebu fuatiliaa dar waterfront na dar village, ikikamilimka hiyo aaaaaaaaaaaaahn ya kawe kwisha
 
Wabongo wanapenda picha, so wape picha. Ndio maana wanafunga safari kwenda kupiga picha Mlimani City na Quality Centre kisha wanarudi kwao Buguruni Mnyamani, Tandale Mtogole au Manzese kwa Mfuga Mbwa na ku-chilll tu wala hawawi-inspired! Business as usual. Na serikali inalijua hilo vizuri sana.

Tunataka vitu halisi na sio mapicha picha tuuuu.
 
Hizi project ni wizi mtupu Kigamboni haijaisha sasa wanakuja na project nyingine hilo eneo walikuwa wanalitolea macho sana na ndio maana nimeona maeneo ya jirani na hapo tumewekewa vigingi kwamba tuko karibu na mto nyuma ya makao makuu ya jeshi kwamba tuhame kwa ajili ya kupisha ujenzi sh**i type hii nchi
 
Mimi natoka kazini saa 11 jioni nafika kwangu Boko saa nne usiku je wakiweka hayo magoorofa yao si nitakuwa nafika saa tisa kabisa maana wakazi kibao barabara hamna, maji hamna, sewage mbovu, umeme ndio duh kero
 
Back
Top Bottom