Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)


Na wanatuweza kweli na mapichapicha haya! wameshatujua udhaifu wetu

Mlimani city watu waliambiwa hivyo hivyo lakini hamna kinachoendelea pale
 
Ivi imekuwaje kila kitu mkiambiwa hamuamini yaani mumekosa imani na serikali yenu kiasi hicho
Ni mpango mzuri all the best for the planners and those in the project team to make it real
 
Mwenye development software please atuwekee hapa. Asante.
 
Huo ni ujanja wa watawala kujitwalia maeneo nyeti na muhimu zikiwemo fukwe za bahari kwa kigezo cha uwekezaji. Ni aibu na fedheha iliyoje kwa watawala kupanga mikakati ovu ya kuua viwanda ili waweze kujitwalia maeneo kwa faida zao binafsi. Kuna fununu kuwa eneo lote la iliyokuwa TANGANYIKA PACKERS limeshatwaliwa watawala waroho kwa mgongo/kivuli cha NHC
 
Ivi imekuwaje kila kitu mkiambiwa hamuamini yaani mumekosa imani na serikali yenu kiasi hicho
Ni mpango mzuri all the best for the planners and those in the project team to make it real
Ni kweli. Hatuna imani tena na serekali, full stop! Which is very very bad!
 
Tumuulize mbunge husika. Mchoro wenyewe unaonyesha utawameza wananchi wote waishio Kawe. Na ni kwa nini Dar tu? Dodoma makao makuu ya nchi haihitaji maendeleo kama haya?

Nashukuru kwa upande wa Tanga wamepeleka Pongwe Satellite City Project.

Dar walete miradi ya miundo mbinu zaidi kama ujenzi wa reli na meli kwa ajili ya usafirishaji wa abiria.
 
Nani wa kufadhili mradi huo? Kigamboni City imeishia kwenye internet, je hiyo Kawe City Mtaiweza?
Vinginevyo mtaambiwa kwanza muwe mashoga ndipo mfadhiliwe
 
Tanzania kwa mipango hatujambo!mambo yote huishia kwenye karatasi tukishachukua pesa
 
Afadhali imeanza 'series' mpya, maana ile ya 'New City of Kigamboni' ilishaanza kuboa...
 

Hakika unachosema!
Hii ni nchi ya kipuuzi tu! Mtindo mkubwa kabisa wa kipuuzi, kishenzi na kipumbavu ni huu wa kudhani kwamba Tanzania ni Daressalaam tu. Kila siku mijitu hii inayolia kule Bungeni inadhani Tanzania yote itahamia Dar.

Wanachota pesa ya serikali wanampa mtu ananunua UDA, wanachota pesa za serikali wanampa mtu anajenga vituo vya mafuta, sasa wanakuja na upuuzi huu wa kawe, tanzanite, kigamboni, n.k. Yote haya wanafikiria ni Dar tu.

Je wapuuzi hawa wanakumbuka kwamba tangu tupate uhuru hawajawahi kujenga Hospitali hata moja? wanafahamu kwamba watu milioni 5 walioko Dar sasa ni watu wanaohitaji hospitali kuliko shopping molls?

Naanza kutia mashaka juu ya uwezo wa mwafrika. Nadhani kweli sisi ni genetically weak.
 
Nchi hii imeendelea sana kwenye makaratasi,makablasha, mafaili na madokomenti tena ni zaidi ya u.s.a ila kwenye uhalisia ndo balaha.
 
Naomba niwe wa mwisho kuamini kama hii project itafanikiwa nukta
 
JK alipoingia madarakani alisema ataifanya Kigoma kuwa kama Dubai na Mwanza kuwa kama Califonia. Atajenga Machinga Complex kila wilaya! Duuh, si shangai kutengeneza michoro mingi ya kila eneo la Dar ili kuwapa matumaini washinda vijiweni wasirect kwa kukosa ajira, kumbe upepo mtupu ataondoka 2015 hata 10% ya ahadi zake hajatekeleza!

Kiongozi huyu anajua kucheza na akili za wabongo!
 
Jamani, hapa si ndio pale Tanganyika parkers walipobomoa nyumba karibia mia mbili juzi, NHC wamebomoa nyumba za kizamani pale nahisi labda ndio wanataka waanze ujenzi wa mji huu mpya. kama ni hivyo itakuwa safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…