Hamas, Hezbollah, Iran na makundi mengine hapo Syria, Iraq na Yemen wanatengeneza kitu kinaitwa Axis of Evil.
Mkakati wa Iran ni kuwapa silaha na mafunzo maadui wote wa Israel ili ikifikia hatua Israel inapigana na Iran basi makundi mengine yaisaidie Iran. Lengo ni Israel awe na fronts nyingi, mpaka wa Kusini anapigana na huyu, mpaka wa Kaskazini huyu, reserve yote iitwe na wanajeshi wazidiwe majukumu.
Hayo makundi yananunua ugomvi wa Israel na Iran yakimtegemea boss wao Iran atawatetea wakipigwa. Iran naye anawategea anawatumia kwa mahesabu.
Serikali ya Bashar al Assad wa Syria nayo ilisaidiwa mno na Hezbollah kwenye kupigana na waasi na kundi la ISIS. Lengo ni kwa kuwa Syria ni adui wa Israel hivyo muda muafaka naye angeisaidia Hezbollah. Badala yake mataifa haya yanaogopa yameufyata.
Hamas imeanza mbwembwe zikiwa nyingi (haikuwashirikisha wenzie ili shambulizi liwe la siri). Na kwa sasa nimeelewa approach ya Hamas ilikuwa sahihi, wao wana usiri kwao kuliko Hezbollah ilivyokuwa infiltrated na Israel intelligency. Usiri wa Hamas ukafanya waanze vizuri mwanzoni, baadae walitakiwa waingie Hezbollah na Iran ila sasa kila siku wakawa wanasema onyo la mwisho Israel ikiingia Gaza, Israel inaingia. Onyo la mwisho ikiingia kambi fulani, inaingia. Onyo la mwisho kufika Khan Younis, Israel inafika. Mpaka Hamas imechakaa bila washirika kuingilia kusaidia.
Sasa Hezbollah inashambuliwa Hamas hawana nguvu tena. Iran ndio anatakiwa aingie ila hesabu za Rais mpya zinakataa, aliyekuwepo angalau angefanya kitu ila ndio alikufa kwa "helikopta kuanguka kwenye ukungu".