Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Naona mpaka sasa hizi hotuba mbili, zimeleta changamoto ya aina yake kwenye mjadala wa katiba mpya!.

Naomba kuwauliza wale wenye uwezo wa "to read in between the lines", kwa ku compare and contrast hizi hotuba mbili, ya Jaji Warioba akiwasilisha rasimu, na ya Rais Jakaya Kikwete akilizindua Bunge hilo Maalum, ipi ndio hatuba ya maana zaidi?!. Jaji Warioba kawasilisha rasimu ya serikali 3, Rais Kikwete akaiponda hiyo rasimu na kuweka mwelekeo wa serikali mbili!.

Jaji Warioba ametoa sababu za kufikia serikali tatu, jee sababu hizo ni credible?, ni justified?, zinatekelezeka?!.
Rais JK hakuzipangua, bali ametoa angalizo jinsi zisivyotekelezeka!. Jee kati wawili hawa, nani ni mtu credible wa kumuaminia, isije ikawa ni blah blah tuu?!.

Is Jaji Warioba credible?, is he the man of integrity?, ushauri wake wa serikali tatu kuwa utapunguza keri za muungano unaweza kuwa ni kweli?!, au nao ni blah blah za kisiasa?!.

Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.

Pasco
 
Mkuu Pasco na wewe sasa umnateleza. Hauwezi kusema kwamba Kati ya Jaji warioba Na Rais kikwete ni nani mkweli na ni nani Blaah! blaah! Suala hapa sio Ukweli Vs Blaah! bali ni tofauti ya uoni kulingana na mtizamo, upeo na mazingira. Kwa hiyo watu wawili kutofautina na mawazo haimaanishi kwamba mmoja wapo ni hamnazo! au hana nia njema! Lahasha! Hata wewe Pasco ukiamua kutofautiana na wote kama alivyofanya Zitto, bado hatuwezi kukubeza maana utakuwa unaongea kulingana na upeo wako na mtizamo wako.

Kwa hiyo si sahihi kuyafanya mambo haya kama ligi ya mabingwa wa bara, hasa katika suala hili la katiba ambalo kwa kiasi kikubwa linahitaji maridhiano zaidi ya mashindano.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, kitu alichafanya Kikwete ni cha kijinga sana na kama ingekuwa nchi nyingine ambayo wananchi na wasomi wake wako ''awake'' angekiona cha moto. Mimi nachojua ni kuwa kuna timetable maalumu ya kuandika hii katiba, na kipindi cha kutoa mapendekezo kilishapita sasa ni kipindi cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa. Alikuwa wapi muda wote watu wanatoa mapendekezo? Kwa nini hakuyawasilisha kwenye tume na sasa anakuja na rasimu nyingine ambayo hata ilikotoka haijulikani? (labda wameiandaa yeye na mke wake!
 
Mh. Jaji Warioba alikuja na facts zilizotokana na maoni ya wananchi; ndicho wananchi wanachotaka. Na zaidi ameenda mbali zaidi kuonesha sio tu jinsi mfumo unaopendekezwa na wananchi unavyotekelezeka, bali amewaonesha watawala namna ya kuutekeleza. Kwa upande wa Rais, kwanza hana facts zozote kuonesha kwamba muundo hautekelezeki zaidi ya "hisia" tu. It's just a fear of the unknown; hakuna kingine.
 
Be Serious Kaka.
Tuko Mpee Facts / Nondo V/S Mipasho ?!!!!!!!?
 
Huwezi mfananisha warioba na kiazi tafuta mtu wa kumlinganisha naye sio huyo ------
 
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.

Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.

Alafu nyie waznz ndio mnatuchanganya. mnataka znz yenye mamlaka kamili ndio hzo tatu alafu leo huztaki tena? hamtaki kuwa nchi ya kiislam na kujiunga oic? changueni tatu acheni unafiki nyie.msituletee zogo
 
Alafu nyie waznz ndio mnatuchanganya. mnataka znz yenye mamlaka kamili ndio hzo tatu alafu leo huztaki tena? hamtaki kuwa nchi ya kiislam na kujiunga oic? changueni tatu acheni unafiki nyie.msituletee zogo

Naona unabwabwaja bila ya uelewa.

Mimi ni Mtanganyika tena wa ukweli kabisa, nilizaliwa Tanganyika mara nikastukia nimebadilishwa Uraia naitwa Mtanzania (jina alilotoa Mhindi wa Tanga).

Nikiuliza Tanganyika yangu iko wapi? naambiwa Nyerere ndiyo aliiuwa Tanganyika.
 
Mkuu Pasco,

So far suala la nani mkweli halipo relevant bali nani ana hoja zenye ushawishi na zinazoakisi matakwa ya umma wa watanganyika (watanzania bara) na wazanzibari walio wengi? Mimi ni mmoja wa wanaoshawishika zaidi na hoja za warioba kwani picha mgando, picha za videos, na sauti za wananchi waliotoa maoni yao zipo; licha ya ccm kujaza watu wake kwenye mabaraza ya katiba, takwimu zao zipo wapi (ccm) zinazo prove wrong hoja ya warioba? Hakuna; Jinsi ccm inavyozidi kuponda takwimu za warioba ndivyo probability of mathematics zinavyozidi kumbeba warioba;nimejadili hili kwa kina kwenye uzi wa Nguruvi3 ambao lengo lake ni kutafuta maoni ya wananchi humu juu ya hotuba ile; unakaribishwa katika mjadala;

Vinginevyo so far,takwimu za ccm ni wingi wao katika bunge la katiba, na huko ndiko JK amewekeza kupitia hotuba yake, akitarajia kwamba hata kwenye kura ya maoni, waliopangwa kuhimiza hoja za JK ndani ya bunge la katiba watafanikiwa;

Baada ya bunge la katiba kumalizika - iwapo litamalizika, mkweli atakuwa ni wananchi;tusubiri kura ya maoni kwa matumaini kwamba itakuwa ni fair and transparent; kura hiyo will provide us with answers;



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Huu uzi ni wa kutaka kutafuta kujulikana. Elimu ni ufunguo wa maisha. Usijikombee. Simamia hoja za kitafiti.
 
Kauli mbiu yetu vijana ambayo tunawaasa vijana nchi nzima to embrace towards kura ya maoni ni:

TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA;

Tunafanya hivyo kwa hoja;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu PAsco, kwanza hapakuwa ni ushindani wa hoja maana majuku yao yalikua tofauti. Kama Kikwete alisoma vizuri ToR (kufungua bunge la katiba) yake iliyompeleka bungeni basi hajaifuata hivyo kama ni mtihani amefail. Warioba alisoma vizuri Terms of Reference (kuwasilisha hoja ya Rasimu ya katiba na kuelezea maudhui yake) alifuata na ndio maana hakutoka nje ya mada wala hakufanya mipasho japo alishafahamu misimamo mbali mbali. Hivyo hatuwezi kusema chcochote zaidi ya hapo. Cha kusikitisha zaidi aliyeajiri Tume ni Rais ayetoa ToR kwa Tume Rais na Report alikabidhiwa yeye kabla ya kuipeleka kwa wananchi, je kama aliona mapungufu ya kitakwimu mbona hakuwauliza mapema? ama lengo lake lilikua ni kuidhalilisha tume
 
Mkuu Pasco na wewe sasa umnateleza. Hauwezi kusema kwamba Kati ya Jaji warioba Na Rais kikwete ni nani mkweli na ni nani Blaah! blaah! Suala hapa sio Ukweli Vs Blaah! bali ni tofauti ya uoni kulingana na mtizamo, upeo na mazingira. Kwa hiyo watu wawili kutofautina na mawazo haimaanishi kwamba mmoja wapo ni hamnazo! au hana nia njema! Lahasha! Hata wewe Pasco ukiamua kutofautiana na wote kama alivyofanya Zitto, bado hatuwezi kukubeza maana utakuwa unaongea kulingana na upeo wako na mtizamo wako.

Kwa hiyo si sahihi kuyafanya mambo haya kama ligi ya mabingwa wa bara, hasa katika suala hili la katiba ambalo kwa kiasi kikubwa linahitaji maridhiano zaidi ya mashindano.

huyo zito umemuingiza kwenye mada kama nani kwenye hoja ya pasco
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom