Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....Anyway nawasihi wabunge wa katiba na watanzania wote...angalieni nchi zingine za africa wanavyoyumba migongano ya kila mara, mara kabila hili liko sana juu mara hawa hawatakiwi kuchukua ardhi...kama mnataka tufike huko mkilianzisha ndio limeanza hivyoo....Ndio hapo mtakapo mkumbuka Nyerere kulia na kusaga meno...JK amefanya kuwakumbusha mlipotoka...mkitakaa..... myaache...yaani huwa naumia moyoni kweli watu wanaotuka au kumkashifu mkuu wa nchi...hawajui kama wanajitukana wao ni kukosa hekima na busara...lakini tunafanyaje ni uhuru wa kuongea huu.Sasa kama mmesoma sana kuliko Nyerere ama wazungu wanaoungana kila.kukicha ndio titajua hapo bidae...Maana naona hapa.kuna watu wanao linganisha viongozi kwa usomi wao...mbona hamuulizi Warioba na Nyerere nani zaidi....jokes.Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.Msione vinaelea vimeundwa..Mungu naomba utupatie katiba iliyobora...itakayo tuweka wananchi watanzania salama...Amina
hakuna mtu asiye penda muungano, tatizo ni je upande wa pili wana utaka huo muungano, Jaji kasema upande wa pili wapo pamoja kwenye jambo hilo, iwe wa cuf au wa ccm, kwa hali akawa amekuwa limited na options anazoweza kufanya , ukitilia maanani upande wa pili mpaka katiba yao wame badili, na yeye au sisi wadanganyika/wabara machogo hatuna uwezo wa kubadili katiba yao. na zaidi ya hapo muungano unatakiwa uwe to a certain degree fair say 95%, ikiwa hatuwezi kufikia 100%, na hii inatakiwa kuonekana katika mambo mengi mfano kuchangia katika gharama za muungano, kuteuliwa kwa watu katika nafasi za muungano , mfano mambo ya nje n.k., sasa wewe muungano huu unaona upo fair? wa watu 1.5 wa upande moja kuwa sawa na watu 43 wa upande mwingine kama sio wizi? au theory ya changu ni changu chako ni changu ipo sawa?
 
Mbaya zaidi, katumia takwimu za tume kupinga matokeo yaliyowasilishwa bila ya kujua kwa kufanya hivyo, mathematics of probability zimembeba warioba; unampinga mtu kwa kuja na alternative approach ambayo iliyo scientific;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

..zaidi, wajumbe wa Tume wanasema wao wameangalia pia UZITO WA HOJA zilizotolewa.

..pia kwasababu muungano unahusu wananchi wa nchi mbili, basi ni lazima ktk kuchambua takwimu tuangalie kila upande unauzungumziaje muungano.

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,

Na ni uzito huo huo wa hoja ambao CCM hiyo hiyo uliutumia kwenda kinyume na matakwa ya wengi kufuatia kazi ya tume ya nyalali ambapo 80% ya wananchi walipendelea mfumo wa chama kimoja, huku 20% wakipendelea mfumo wa vyama vingi. CCM ikachukua maoni ya wachache kutokana na nguvu ya hoja.

Ama kweli viongozi wa CCM are long in power and short in memory.

Cc Nguruvi3, FJM Mag3


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
hivi ukicompare RASIMU YA KATIBA na HOTUBA? kuna uelewa gani twapata

maana jaji warioba yeye alipitisha rasimu ya katibu na mkuu wa nchi naye alihutubia
mkuu pasco sijakulelewa ulitaka kumaanisha nini hapa?

na hapa hivi Rais wetu alisomea Ph.D au alitunukiwa?

source: Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.
 
JokaKuu,

Na ni uzito huo huo wa hoja ambao CCM hiyo hiyo uliutumia kwenda kinyume na matakwa ya wengi kufuatia kazi ya tume ya nyalali ambapo 80% ya wananchi walipendelea mfumo wa chama kimoja, huku 20% wakipendelea mfumo wa vyama vingi. CCM ikachukua maoni ya wachache kutokana na nguvu ya hoja.

Ama kweli viongozi wa CCM are long in power and short in memory.

Cc Nguruvi3, FJM Mag3


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Kusema kweli CCM wanashangaza; wakati Kikwete anatetea mfumo wa serikali mbili akitoa ahadi kuwa matatizo yaliyopo yatashughulikiwa, anasahau kwamba under his watch kulitokea tatizo kubwa zaidi la kuibuka kwa nchi ya Zanzibar ndani ya Muungano. Muungano tulioachiwa na waasisi wetu ni serikali mbili ndani ya nchi moja na pamoja na mapungufu yake umoja wetu kama taifa haukuyumba kwani ulilindwa na Katiba ya Jamhuri hadi pale yeye Kikwete aliporuhusu ichezewe na upande moja katika Muungano. Kama tunakiri kuwepo kwa matatizo kabla, je, kuibuka kwa serikali mbili na nchi mbili zenye Katiba zinazopingana, kulipunguza tatizo?

Kikwete alianza kuonesha dalili ya hila iliyogubikwa na woga pale alipoiagiza Tume kutoruhusu maoni yanayohoji huu Muungano wetu, matatizo yake na namna ya kuyaboresha. Pamoja na kuwaacha wananchi hoi wakijiuliza hiyo nguzu na huo ujasiri wa kuwafunga midomo wananchi wasiujadili Muungano wao Kikwete kautoa wapi! Lakini baya zaidi ni ukimya wake kuhusu kitendo cha Zanzibar kutokuheshimu Katiba na badala yake kutunga Katiba yake inayopingana na ile ya Jamhuri. Kwamba mpaka sasa si Kikwete wala mwanachama yeyote wa CCM ameweza kukemea kitendo hiki cha kihaini hadharani, ni dalili tosha kuwa CCM imechoka na imekosa uhalali wa kuendelea kutawala.

Tutatengenezaje Katiba mpya wakati hatuna ustaarabu wa kuziheshimu sheria tulizojiwekea sisi wenyewe na hasa sheria mama kama Katiba. Nilitegemea kitu cha kwanza Kikwete angefanya alipopewa fursa ya kuzindua BMLK, ni kuwaomba radhi wananchi kwa kitendo hicho cha Zanzibar kutoheshimu Katiba ya Jamhuri. Baada ya hapo angetoa amri, kama Raisi wa Jamhuri na Amiri Jeshi Mkuu, Katiba hiyo isitishwe mara moja, isitumike. Halafu angehakikisha waliohusika wanawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua kali kama fundisho kwa wale wote wenye mawazo potofu kama hayo...ndiyo, huo ndio utawala, utawala unaoheshimu sheria, utawala uliopo Kikatiba.
 
Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....

Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...


Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.

Msione vinaelea vimeundwa..

Micho, inaelekea hujapata vizuri tofauti ya matukio haya mawili. Warioba alitoa MATOKEO ya UTAFITI (wa maoni ya wananchi). Rais Kikwete katoa maoni tu kama raia Mtanzania na hasa kama mwanasiasa. Hakujali facts. Wenye facts ni kina Waryoba. Yeye ana DHANA toka kwa washauri wake.

Mfano; Zanzibar yajulikana kuna wizara ya kilimo, huku bara ipo pia wizara kama hiyo. Sheria inayoipa hii ya huku bara mamlaka ya kujidhani ndiyo wizara ya kilimo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni IPI wakati zote sio za muungano? Masuala haya yanakwaza mawaziri na wizara zote zisizo za muungano huku zile za bara zikibeba joho la kama vile zenyewe ndiz za Jamhuri ya Muungano. Mada hii sumbufu na nyeti aliiongea Waryoba tuu. JK hakuigusa na wala hakutoa wazo kipi kifanyike. Waziri mkuu wa Serikali ya Muungano anajulikana kuwa hana madaraka yoyote huko zenj. Na wala hafiki kukagua kitu huko. Na hapa hata JK alikaa kimya. Rais wa zenj ni waziri tu kwenye baraza la mawaziri la Muungano. Sio Makamu wa rais. JK kimya. Hii point hata Mohammed Raza kasema hadharani inamkera.

Kwa hiyo wawili hawa SI SAWA. Mmoja ni mtafiti lazima aseme KWELI 100% na mwingine ni mwanasiasa tuu ambaye siku zote huwinda RIDHAA.
 
Last edited by a moderator:
Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....

Micho, hapa ama kwa makusudi una ajenda ya kumtusi Jaji Waryoba au una lengo tofauti. Kwanza, Yeye alikuwa Mwenyekiti wa TUME na MATOKEO yaliyokusanywa na kufanhyiwa kazi na TUME ndio alipewa jukuma la kuyawakilisha. Kumlemga yeye binafsi ni sawa na kusema vita ya Kagera alipigana Generali Musuguri peke yake, na lengo lako ni ni ili iwe rahisi kwako kumkosea Waryoba heshima na kumdhalilisha yeye pekee lakini Jaji Agostino Ramadhani na wajumbe wengine Ukawawacha bila kuwagusa. Pili katika hadidu rejea walizopewa, Tume waliambiwa bayana masuala yote ya KUUA au kudhoofisha Muungano NO. Tatu serikali ya Zenj lazima ibaki.Sasa walipoenda kinyume ni wapi? Mbona huongelei Muungano wa Mkataba? wakati uliungwa mkono na asilimia 60 ya wazenj?

Au kosa lake Waryoba ni kule kusogea kunako microphone na kusoma report ya Tume?
 
Last edited by a moderator:
Na wengine huku tulishanyimwa fursa kwa kuwa tulizaliwa baada ya muungano tena kipindi cha Mwinyi so hatuna hadhi ya kuiulizia Tanganyika...........Mzee wangu alifariki nikiwa na mwezi sikumjua zaidi ya picha so sina haki ya kutumia jina lake kwa kuwa sikumjua.
 
Kama ni utafiti warioba anatisha kwanza kaja na existing situation, Analysis, na mwisho katia recomendation and suggestion. Napata shida kuuelewa mtiririko aliotumia JK

Jakaya alitumia mtiririko wa Kisanii ambao ndio mfumo sahihi wa CCM! Tatizo unaliona halafu unafungia macho ndio mtindo wa CCM. JAkaya ukimfikiria huwezi pata picha halisi sana sana utaishia kutukana tu!! Unaapa kuilinda na kuitetea katiba halafu ndani ya himaya yako anatokea mhuni mmoja upande wa muungano anasigina katiba kwa makusudi nawe unakaa kimya pamoja na kuwa unakila njia ya kuzuia kwa muda! Halafu leo unakuja na semina elekezi ambayo nayo iko kisanii sanii ni HATARI sana!!
 
Wanabodi,

Naona mpaka sasa hizi hotuba mbili, zimeleta changamoto ya aina yake kwenye mjadala wa katiba mpya!.

Naomba kuwauliza wale wenye uwezo wa "to read in between the lines", kwa ku compare and contrast hizi hotuba mbili, ya Jaji Warioba akiwasilisha rasimu, na ya Rais Jakaya Kikwete akilizindua Bunge hilo Maalum, ipi ndio hatuba ya maana zaidi?!. Jaji Warioba kawasilisha rasimu ya serikali 3, Rais Kikwete akaiponda hiyo rasimu na kuweka mwelekeo wa serikali mbili!.

Jaji Warioba ametoa sababu za kufikia serikali tatu, jee sababu hizo ni credible?, ni justified?, zinatekelezeka?!.
Rais JK hakuzipangua, bali ametoa angalizo jinsi zisivyotekelezeka!. Jee kati wawili hawa, nani ni mtu credible wa kumuaminia, isije ikawa ni blah blah tuu?!.

Is Jaji Warioba credible?, is he the man of integrity?, ushauri wake wa serikali tatu kuwa utapunguza keri za muungano unaweza kuwa ni kweli?!, au nao ni blah blah za kisiasa?!.

Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.

Pasco
Kijana naona hivyo viroba unavyokunywa bora uachane navyo maana vinakupa hangover mpaka unajisahau na kuanza kuweka povu humu ndani, jaribu kumcompare baba yako kwanza na sio JK mwehu weee
 
Hotuba za kujitetea kwa watuhumiwa!?
Ndo tatizo la ukosefu wa akili hilo linalokusumbua kiac kutofikiri, mnaropoka tu waka hamjui hotuba ndo nini, dada FaizaFoxy kaeleza vyema majibu ya hilo swali nawashanga nyie vipofu wa akili, kheri uwe kipofu wa macho kuliko kuwa kipofu wa akili poleni sana nyie vijana wa Ukawa.
 
Back
Top Bottom