Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.
Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.
Musulmán terrorista Faiza, ¿Eres alrededor abuela? Muchos líderes islámicos con trasfondos resultó ser gran fracaso en este país y JK es un buen ejemplo de esa falta.
Sijajua unaangalia vitu gani kusema hotuba ya rais ni ya karne wakati mda mwingi kautumia kupiga vijembe na kutetea kitu ambacho kwasasa hakina uwezo wa kutetewa...zanzibar imeshakua nchi bado mnataka serikali mbili ndani ya nchi mbili...mbona inaonekana kama vile unaona kabisa hii ni nyeupe ila kwa malengo yako binafsi unafumba macho na kusema ni nyeusi..
Uwezi kuwa mtanganyika alafu ukaunga mkono serekali mbili. Ngoja Tanganyika yetu irudi alafu ndio mtajua hatima yenu nyie wazanzibar mlio jisahau hapa Tanganyika
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.
Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.
Kwa hiyo Nyerere na Pengo si Watanganyika?
Leo mnaungana na mimi mkipenda msipende kusema kuwa Nyerere alifanya makosa kuiuwa Tanganyika. Hilo linawashinda nini kusema na mnapata kigugumizi?
Mimi siungi mkono huo muungano wote. Naona ni wa kulazimishwa tu.
Kikwete alienda kufungua bunge kama Raisi wa nchi na ingeeleweka kama angeongelea faida na hasara za serekali tatu au mbili. lakini alichokifanya ni kuelezea misimamo ya CCM au Rasimu ya CCM kama yupo lumumba
duniani kuna aina kuu mbili za utawala: utawala wa kidemokrasia na utawala wa kidikteta.Wanabodi,
Naona mpaka sasa hizi hotuba mbili, zimeleta changamoto ya aina yake kwenye mjadala wa katiba mpya!.
Naomba kuwauliza wale wenye uwezo wa "to read in between the lines", kwa ku compare and contrast hizi hotuba mbili, ya Jaji Warioba akiwasilisha rasimu, na ya Rais Jakaya Kikwete akilizindua Bunge hilo Maalum, ipi ndio hatuba ya maana zaidi?!. Jaji Warioba kawasilisha rasimu ya serikali 3, Rais Kikwete akaiponda hiyo rasimu na kuweka mwelekeo wa serikali mbili!.
Jaji Warioba ametoa sababu za kufikia serikali tatu, jee sababu hizo ni credible?, ni justified?, zinatekelezeka?!.
Rais JK hakuzipangua, bali ametoa angalizo jinsi zisivyotekelezeka!. Jee kati wawili hawa, nani ni mtu credible wa kumuaminia, isije ikawa ni blah blah tuu?!.
Is Jaji Warioba credible?, is he the man of integrity?, ushauri wake wa serikali tatu kuwa utapunguza keri za muungano unaweza kuwa ni kweli?!, au nao ni blah blah za kisiasa?!.
Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.
Pasco
Warioba alihutubia na kuwasilisha rasimu ya katiba, na kutoa hoja za maana na zenye nguvu kudefend kazi ya tume yake!
Kikwete alihutubia with stats za vijiweni na hoja mfu na pia akasahahu kilichompeleka: kuzindua bunge. Kikwete ni rais bogus dunia imewahi pata kuona katika karne ya 21! Yaani lilisahau hata tume ya katiba lilichagua lenyewe na kila step alikuwa briefed.
kama pengo anauunga mkono muungano wa style alio ongelea zaifu ni --------. Swala ni principle tu. kama warioba alivyosema mafuta ya zanzibar ni ya wazanzibar na gari ya Tanganyika niyawote niupumbavu. Muungano alioutaka nyerere na huu zaifu anaouongelea ni tofauti.
Kwa wenye kujua kuwa Mapinduzi ya Znz yalifanywa na Wazaramo, Wandengereko, Wamanyema wakishirikiana na ndugu zao wa unguja sina shaka kuwa wataungana nami nikisema WAPEMBA hawakuwahi kushiriki katika mapinduzi bali walitaarifiwa tu kuwa sasa sultan kashatimuliwa !!! ZNZ ni Sehemu ya Tanganyika! Waasisi wanatambua ukweli huu lakini wengi wako kimya hawataki kuwaambia ukweli wananchi kuwa chokochoko zote za kutaka kututenganisha chanzo chake ni wapemba wachache wasiojua chochote kuhusiana na historia ya nchi hii... the so called muafaka ndo chanzo cha matatizo yote haya....Mimi nasimama upande wa JK kuwa ZNZ ni sehemu ya Tanganyika serikali mbili zinatosha kwa sasa kuelekea serikali moja!!!
Hujui kuwa Warioba pale alikuwa anawasilisha rasimu? na anaelezea yaliokuwa kwenye rasimu? ile si hotuba ewe punguani.
Kikwete kaenda kufunguwa bunge na kutoa hotuba, na hotuba yake ilikuwa safi sana, hakutafuna maneno.
Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....
Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...
Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....
Anyway nawasihi wabunge wa katiba na watanzania wote...angalieni nchi zingine za africa wanavyoyumba migongano ya kila mara, mara kabila hili liko sana juu mara hawa hawatakiwi kuchukua ardhi...kama mnataka tufike huko mkilianzisha ndio limeanza hivyoo....
Ndio hapo mtakapo mkumbuka Nyerere kulia na kusaga meno...
JK amefanya kuwakumbusha mlipotoka...mkitakaa..... myaache...yaani huwa naumia moyoni kweli watu wanaotuka au kumkashifu mkuu wa nchi...hawajui kama wanajitukana wao ni kukosa hekima na busara...lakini tunafanyaje ni uhuru wa kuongea huu.
Sasa kama mmesoma sana kuliko Nyerere ama wazungu wanaoungana kila.kukicha ndio titajua hapo bidae...
Maana naona hapa.kuna watu wanao linganisha viongozi kwa usomi wao...mbona hamuulizi Warioba na Nyerere nani zaidi....jokes.
Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.
Msione vinaelea vimeundwa..
Mungu naomba utupatie katiba iliyobora...itakayo tuweka wananchi watanzania salama...Amina