Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

Mi Binafsi,ya Mhe.Rais Ilinifungua sana..........Yq Warioba ilikuwa nzuri lakini ilijifunga.....Ya Presdent ndiyo ilikuwa ina'analyze' yale yaliyokosa 'kuulizika' kwenye hotuba ya Mh.Jaji Warioba...
 
JK hakuwa contextual kabisa. Ameenda kufungua bunge na sio kujadili, kuhoji au kujibu hoja za Rasimu.

Hiyo kazi si yake, hyo kazi ni bunge la Katiba. Ukitaka kuelewa janja ya JK ni pale aliposubiri Warioba awasilishe Rasimu ya Katiba bungen alafu yeye aje baada ya wiki.

Hapo hatuitaji PhD kuelewa nia yake. Hapa kwangu mimi JK amewasilisha rasimu nyingine tofauti na ile inayojulikana kwa wananchi.

Binafsi, nitaki lingine nataka TANGANYIKA ireje. Haijalishi idadi ya serikali being moja, mbili au tatu.

Moto yetu ni : TANGANYIKA KABLA, TANZANIA KWANZA
 
Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....

Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...

Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....

Anyway nawasihi wabunge wa katiba na watanzania wote...angalieni nchi zingine za africa wanavyoyumba migongano ya kila mara, mara kabila hili liko sana juu mara hawa hawatakiwi kuchukua ardhi...kama mnataka tufike huko mkilianzisha ndio limeanza hivyoo....

Ndio hapo mtakapo mkumbuka Nyerere kulia na kusaga meno...

JK amefanya kuwakumbusha mlipotoka...mkitakaa..... myaache...yaani huwa naumia moyoni kweli watu wanaotuka au kumkashifu mkuu wa nchi...hawajui kama wanajitukana wao ni kukosa hekima na busara...lakini tunafanyaje ni uhuru wa kuongea huu.

Sasa kama mmesoma sana kuliko Nyerere ama wazungu wanaoungana kila.kukicha ndio titajua hapo bidae...

Maana naona hapa.kuna watu wanao linganisha viongozi kwa usomi wao...mbona hamuulizi Warioba na Nyerere nani zaidi....jokes.

Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.

Msione vinaelea vimeundwa..

Mungu naomba utupatie katiba iliyobora...itakayo tuweka wananchi watanzania salama...Amina
 
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.

Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.

Sijajua unaangalia vitu gani kusema hotuba ya rais ni ya karne wakati mda mwingi kautumia kupiga vijembe na kutetea kitu ambacho kwasasa hakina uwezo wa kutetewa...zanzibar imeshakua nchi bado mnataka serikali mbili ndani ya nchi mbili...mbona inaonekana kama vile unaona kabisa hii ni nyeupe ila kwa malengo yako binafsi unafumba macho na kusema ni nyeusi..
 
Musulmán terrorista Faiza, ¿Eres alrededor abuela? Muchos líderes islámicos con trasfondos resultó ser gran fracaso en este país y JK es un buen ejemplo de esa falta.

Usted es una mierda cuando usted apenas encuentra un musulmán, pregúntese por qué?

Simplemente porque ypu son un gran pecador y musulmanes no lo son.

Los únicos líderes que transformaron este courty desde los más pobres hasta donde estamos ahora somos musulmanes, ¿qué hicieron sus títeres de la iglesia hacer? que no sea sólo ser dictadores y empujando al país a ser el más pobre de los pobres.

Usted es un buen ejemplo de la manera de su pensamiento y la escritura. ¿Qué puede provocar que no sea el odio de desprestigio? gran mierda.
 
Sijajua unaangalia vitu gani kusema hotuba ya rais ni ya karne wakati mda mwingi kautumia kupiga vijembe na kutetea kitu ambacho kwasasa hakina uwezo wa kutetewa...zanzibar imeshakua nchi bado mnataka serikali mbili ndani ya nchi mbili...mbona inaonekana kama vile unaona kabisa hii ni nyeupe ila kwa malengo yako binafsi unafumba macho na kusema ni nyeusi..

Wewe onesha kimoja ambacho hukukipenda katika hotuba ya Kikwete, weka nukuu, wacha kuandika vya kufikirika. Labda mtu akisema kweli na kwa Kiswahili fasaha, kwako na kwa wale walio kama wewe mnaona ni vijembe?

Weka nukuu, wacha kuhororoja hovyo.
 
Uwezi kuwa mtanganyika alafu ukaunga mkono serekali mbili. Ngoja Tanganyika yetu irudi alafu ndio mtajua hatima yenu nyie wazanzibar mlio jisahau hapa Tanganyika

Kwa hiyo Nyerere na Pengo si Watanganyika?

Leo mnaungana na mimi mkipenda msipende kusema kuwa Nyerere alifanya makosa kuiuwa Tanganyika. Hilo linawashinda nini kusema na mnapata kigugumizi?

Mimi siungi mkono huo muungano wote. Naona ni wa kulazimishwa tu.
 
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.

Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.

Warioba alihutubia na kuwasilisha rasimu ya katiba, na kutoa hoja za maana na zenye nguvu kudefend kazi ya tume yake!
Kikwete alihutubia with stats za vijiweni na hoja mfu na pia akasahahu kilichompeleka: kuzindua bunge. Kikwete ni rais bogus dunia imewahi pata kuona katika karne ya 21! Yaani lilisahau hata tume ya katiba lilichagua lenyewe na kila step alikuwa briefed.
 
Kwa hiyo Nyerere na Pengo si Watanganyika?

Leo mnaungana na mimi mkipenda msipende kusema kuwa Nyerere alifanya makosa kuiuwa Tanganyika. Hilo linawashinda nini kusema na mnapata kigugumizi?

Mimi siungi mkono huo muungano wote. Naona ni wa kulazimishwa tu.

kama pengo anauunga mkono muungano wa style alio ongelea zaifu ni --------. Swala ni principle tu. kama warioba alivyosema mafuta ya zanzibar ni ya wazanzibar na gari ya Tanganyika niyawote niupumbavu. Muungano alioutaka nyerere na huu zaifu anaouongelea ni tofauti.
 
Kikwete alienda kufungua bunge kama Raisi wa nchi na ingeeleweka kama angeongelea faida na hasara za serekali tatu au mbili. lakini alichokifanya ni kuelezea misimamo ya CCM au Rasimu ya CCM kama yupo lumumba

Hujaisikiliza hotuba kaongea kuhusu Serikali mbili na kataja matatizo yaliokuwepo sasa kwa hizo Serikali mbili tulizonazo na kaongelea kuhusu Serikali tatu.

Si CCM tu aliyoitaja, kaongelea pia CHADEMA, CUF, TLP, ADC, NCCR, hujasikia? au hujasikiliza hotuba?

Wacheni porojo, weka nukuu, tukuchambulie.
 
Nimejitaidi kusikiliza pumba. Na kikubwa alichoongelea ni matatizo ya serekali mbili yanavyo lalamikiwa na wazenj na anayashughulikia bila kupitia bungeni ambapo kwa hilo baazi wanamini anashirikiana na zanzibar kuvunja katiba ya Muungano. Na kuhusu serekali tatu alitishia kwamba jeshi linawezakupindua nchi kama litakosa hela kutoka na serkali ua muungano kukosa hela katika serikali tatu. Huo ni uongo kwa serikali ya muungano inaweza kupata hela kwa kutumia union tax kamaikiwekwa kwenye katiba. Nakama ni kutolibwa mbona hata sasa serekali haikusanyi kondi ipaswavyo.
 
Wanabodi,

Naona mpaka sasa hizi hotuba mbili, zimeleta changamoto ya aina yake kwenye mjadala wa katiba mpya!.

Naomba kuwauliza wale wenye uwezo wa "to read in between the lines", kwa ku compare and contrast hizi hotuba mbili, ya Jaji Warioba akiwasilisha rasimu, na ya Rais Jakaya Kikwete akilizindua Bunge hilo Maalum, ipi ndio hatuba ya maana zaidi?!. Jaji Warioba kawasilisha rasimu ya serikali 3, Rais Kikwete akaiponda hiyo rasimu na kuweka mwelekeo wa serikali mbili!.

Jaji Warioba ametoa sababu za kufikia serikali tatu, jee sababu hizo ni credible?, ni justified?, zinatekelezeka?!.
Rais JK hakuzipangua, bali ametoa angalizo jinsi zisivyotekelezeka!. Jee kati wawili hawa, nani ni mtu credible wa kumuaminia, isije ikawa ni blah blah tuu?!.

Is Jaji Warioba credible?, is he the man of integrity?, ushauri wake wa serikali tatu kuwa utapunguza keri za muungano unaweza kuwa ni kweli?!, au nao ni blah blah za kisiasa?!.

Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.

Pasco
duniani kuna aina kuu mbili za utawala: utawala wa kidemokrasia na utawala wa kidikteta.
Utawala wa kidemokrasia una nguzo mbill muhimu:
1. Mgawanyo wa madaraka, yaani serikali, bunge na mahakama. Kila muhimili unakuwa huru na unausimia muhimili mwingine ili kuleta manufaa kwa wananchi.
2. Utawala wa sheria. Nguzo hii ni muhimu sana ktk utawala wa kidemokrasia. Utafsiri sheria zilizotungwa na kupitishwa na bunge kisha serikali kuidhinisha zitumike. Mgogoro unapotokea kati ya serikalil na raia, raia kwa raia ama kati ya muhimili mmoja na mwingine. Nguzo hii ikifanya kazi vzr utaona utamu wa demokrasia.
Utawala wakidikteta. Utawala uko wa aina mbili:
1. Udikteta wa mtu mmoja km vile ilivyokuwa uganda enzi za idd amini, bokkas huko afrika ya kati.
2. Udikteta wa chama. Huu ni udikteta maarufu sana na nchi nyingi za afrika ziliufuata baada ya uhuru na bado upo 75% afrika.
Udikteta wa chama unaojificha ndani ya mwanvuli wa demokrasia ndio km huu wa ccm na tanzania. Tunaona tuna democrasia: serikali ya watu kwa ajili ya watu, mgawanyo wa madaraka, utawala bora na uchaguzi huru lakini sio kweli ni janjajanja na ulaghai kwa wananchi. Huu ni utawala wa kidikteta wa chama.
Hotuba ya kikwete ilidhihirisha hivyo na alitamka waziwazi kuonyesha udikteta wa chama.
Hotuba ya mzee wa warioba inafuata misingi ya kidemokrasia ya kuheshimu mawazo ya watu: serikali ya watu kwa ajili ya watu.
Kulinganisha hotuba hizi ni kulinganisha udikteta wa kichama na demokrasia ya kweli. Nawasilisha.
Natumia simu hivyo makosa ya kiuandishi yavumiliwe.
 
Warioba alihutubia na kuwasilisha rasimu ya katiba, na kutoa hoja za maana na zenye nguvu kudefend kazi ya tume yake!
Kikwete alihutubia with stats za vijiweni na hoja mfu na pia akasahahu kilichompeleka: kuzindua bunge. Kikwete ni rais bogus dunia imewahi pata kuona katika karne ya 21! Yaani lilisahau hata tume ya katiba lilichagua lenyewe na kila step alikuwa briefed.

Hujui kuwa Warioba pale alikuwa anawasilisha rasimu? na anaelezea yaliokuwa kwenye rasimu? ile si hotuba ewe punguani.

Kikwete kaenda kufunguwa bunge na kutoa hotuba, na hotuba yake ilikuwa safi sana, hakutafuna maneno.
 
kama pengo anauunga mkono muungano wa style alio ongelea zaifu ni --------. Swala ni principle tu. kama warioba alivyosema mafuta ya zanzibar ni ya wazanzibar na gari ya Tanganyika niyawote niupumbavu. Muungano alioutaka nyerere na huu zaifu anaouongelea ni tofauti.

Kikwete kaongelea muungano wa Serikali mbili ulipo sasa na kasema hivi kuhusu Serikali tatu:

- Ningependa kama mnaamua tuwe na serikali tatu, basi ziwe tatu zinazosimama na thabiti!

- Nimeeleza niliyoeleza kwa muhtasari; ninyi wajumbe ndio mna maamuzi juu ya aina ya muundo wa Serikali unaotufaa!

Nawaomba wajumbe mnapojadili aina ya Muungano unaofaa Tanzania muwe watulivu! Epukeni jazba!

- Madai ya Serikali Tatu si jambo jipya! Mwaka 1984 ilikuwa hoja iliyopelekea machafuko huko Zanzibar.

- Suala la Serikali Tatu Wajumbe mlizungumze limalizike. Kama zinakubaliwa, zikubaliwe; kama kukataliwa ijulikane!

Source: https://www.jamiiforums.com/katiba-...-hotuba-ya-rais-uzinduzi-wa-bunge-maalum.html

Ni nini usichokipenda hapo?

Kuhusu Serikali mbili, Nyerere ndiyo aliiuwa Serikali ya Tanganyika, mbona hilo hamlisemei?

Kwa wenye kujua kuwa Mapinduzi ya Znz yalifanywa na Wazaramo, Wandengereko, Wamanyema wakishirikiana na ndugu zao wa unguja sina shaka kuwa wataungana nami nikisema WAPEMBA hawakuwahi kushiriki katika mapinduzi bali walitaarifiwa tu kuwa sasa sultan kashatimuliwa !!! ZNZ ni Sehemu ya Tanganyika! Waasisi wanatambua ukweli huu lakini wengi wako kimya hawataki kuwaambia ukweli wananchi kuwa chokochoko zote za kutaka kututenganisha chanzo chake ni wapemba wachache wasiojua chochote kuhusiana na historia ya nchi hii... the so called muafaka ndo chanzo cha matatizo yote haya....Mimi nasimama upande wa JK kuwa ZNZ ni sehemu ya Tanganyika serikali mbili zinatosha kwa sasa kuelekea serikali moja!!!

Hii ni historia mpya kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika. Sijui ulifundishwa na nani. Kwa hiyo kama Wapemba hawakushiriki Mapinduzi (propaganda za uwongo) wasidai haki zao?
 
Hujui kuwa Warioba pale alikuwa anawasilisha rasimu? na anaelezea yaliokuwa kwenye rasimu? ile si hotuba ewe punguani.

Kikwete kaenda kufunguwa bunge na kutoa hotuba, na hotuba yake ilikuwa safi sana, hakutafuna maneno.

Punguani ni wewe unayebisha mambo usiyoyajua; completely nonsense; bottom line is: Warioba alihutubia na hotuba yake ipo hapa: http://www.katiba.go.tz/attachments/article/188/HOTUBA YA MKITI WA TMK_ BUNGE KATIBA_.pdf

Usiwe unabisha mambo ya kijinga!
 
Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....

Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...

Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....

Anyway nawasihi wabunge wa katiba na watanzania wote...angalieni nchi zingine za africa wanavyoyumba migongano ya kila mara, mara kabila hili liko sana juu mara hawa hawatakiwi kuchukua ardhi...kama mnataka tufike huko mkilianzisha ndio limeanza hivyoo....

Ndio hapo mtakapo mkumbuka Nyerere kulia na kusaga meno...

JK amefanya kuwakumbusha mlipotoka...mkitakaa..... myaache...yaani huwa naumia moyoni kweli watu wanaotuka au kumkashifu mkuu wa nchi...hawajui kama wanajitukana wao ni kukosa hekima na busara...lakini tunafanyaje ni uhuru wa kuongea huu.

Sasa kama mmesoma sana kuliko Nyerere ama wazungu wanaoungana kila.kukicha ndio titajua hapo bidae...

Maana naona hapa.kuna watu wanao linganisha viongozi kwa usomi wao...mbona hamuulizi Warioba na Nyerere nani zaidi....jokes.

Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.

Msione vinaelea vimeundwa..

Mungu naomba utupatie katiba iliyobora...itakayo tuweka wananchi watanzania salama...Amina

Tongotongo
 
Huwezi kulinganisha facts alizotoa jaji Warioba tena kwa utulivu na hotuba aliyoitoa mkuu wa nchi kwa mipasho na hisia kali. Mkuu wa nchi alienda mbali sana mpaka kufikia hatua ya kuongea msimamo wake na wa chama chake. Mkuu wetu hakutumia busara na weledi ktk hotuba yake , alijisahau na kufikiri anaongea na wajumbe wa ccm.
 
Back
Top Bottom