hakuna mtu asiye penda muungano, tatizo ni je upande wa pili wana utaka huo muungano, Jaji kasema upande wa pili wapo pamoja kwenye jambo hilo, iwe wa cuf au wa ccm, kwa hali akawa amekuwa limited na options anazoweza kufanya , ukitilia maanani upande wa pili mpaka katiba yao wame badili, na yeye au sisi wadanganyika/wabara machogo hatuna uwezo wa kubadili katiba yao. na zaidi ya hapo muungano unatakiwa uwe to a certain degree fair say 95%, ikiwa hatuwezi kufikia 100%, na hii inatakiwa kuonekana katika mambo mengi mfano kuchangia katika gharama za muungano, kuteuliwa kwa watu katika nafasi za muungano , mfano mambo ya nje n.k., sasa wewe muungano huu unaona upo fair? wa watu 1.5 wa upande moja kuwa sawa na watu 43 wa upande mwingine kama sio wizi? au theory ya changu ni changu chako ni changu ipo sawa?Kwa mtazamo wangu nimefurahishwa sana na mchakato mzima wa katiba....Hotuba ya Warioba na Jk zote nilizisikiliza...kwa kweli kwa mtazamo wangu Warioba hotuba yake ilikuwa imejifunga sana na alichofanya JK ni kuweka wazi zaidi kwa sisi ambao hatupo karibu sana na siasa na tumezaliwa tumekuta muungano...Mimi najiuliza serikali.tatu itaudhoofisha Muungano na kwanini Warioba ama watu wanania.ya kuudhofisha Muungano...tutengane ili.iweje? Kwanini.tusiungane tuongeze nguvu...maana tunajua kwamba umoja ni nguvu....ukiona mataifa huko ulaya wanaungana....sisi tunafikiria kutengana...WHAT IS THIS....Anyway nawasihi wabunge wa katiba na watanzania wote...angalieni nchi zingine za africa wanavyoyumba migongano ya kila mara, mara kabila hili liko sana juu mara hawa hawatakiwi kuchukua ardhi...kama mnataka tufike huko mkilianzisha ndio limeanza hivyoo....Ndio hapo mtakapo mkumbuka Nyerere kulia na kusaga meno...JK amefanya kuwakumbusha mlipotoka...mkitakaa..... myaache...yaani huwa naumia moyoni kweli watu wanaotuka au kumkashifu mkuu wa nchi...hawajui kama wanajitukana wao ni kukosa hekima na busara...lakini tunafanyaje ni uhuru wa kuongea huu.Sasa kama mmesoma sana kuliko Nyerere ama wazungu wanaoungana kila.kukicha ndio titajua hapo bidae...Maana naona hapa.kuna watu wanao linganisha viongozi kwa usomi wao...mbona hamuulizi Warioba na Nyerere nani zaidi....jokes.Jamani hakuna kitu kibaya kama kuvunja msingi...vunja msingi wa nyumba yako uone kitakacho tokea...vunja msingi wa ndoa uone kitakachotokea...mama arudi saa tisa usiku aondoke asubui baba nae asionekane siku mbili..uone kitakachotokea kwa familia..msingi wa Tanzania ni Muungano.Msione vinaelea vimeundwa..Mungu naomba utupatie katiba iliyobora...itakayo tuweka wananchi watanzania salama...Amina