Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!


Samahani ningependa kujua msimamo wako ni upi kati ya serikali mbili, tatu na moja. Mwanzo umesema Kikwete alitoa hotuba murua ukilinganisha na Warioba ila hapa ni kama hukubaliani na walioipoteza Tanganyika.Kama upo upande wa Kikwete, Je unadhani Tanganyika inaweza kurudi katika mfumo wa serikali mbili?
 
Jaji Warioba amewasilisha rasimu ya katiba kufuatana na maoni ya wananchi waliochangia. Rais ametetea hoja ya serikali mbili na kuonyesha ugumu wa kutekelezwa kwa serikali tatu. Sikumbuki kusoma kwenye hotuba yake aliposema analifungua bunge la Katiba. Napata tabu kidogo kwamba naona kama walikuwa wanaumbuana vile wakati Rais kama taasisi ingetoa majibu aliyoyatoa na kuwakilisha kwenye Kamati alipopokea rasimu ya kwanza. Hoja za Rais ni Valid lakini naona kama kulikuwa na mapungufu kiutawala.
 
mnanishngaza...nyie mlitegemea kikwete aongee jambo la maana? hamwez mfananisha kikwete na warioba. na ndo maana warioba amenyamaza hajataka kubishana. nmeshndwa kumwelewa kikwete nguvu anayoitumua kuitetea zanzibar. dr bana smetme inabid kwanza ajipange namna ya kutetea hoja za kikwete. wazanzibar watu wa ajab na wanafiki sana. wanapiga kelele hawatak muungano huku wanautaka nmeshangaa ijumaa walivyokuwa wanapiga makofi kumshangilia kikwete akiponda serikal 3
 
Kikwete ameshindwa kuelezea kwa nini Katiba ya Zanzibar inaeleza wazi kwamba,Zanzibar ni nchi kamili kuonyesha kwamba sio serikali mbili tu,bali kuna nchi mbili tofauti.ilitakiwa atuchambulie hapo,kama alivyochambua Warioba kwamba hizi ni nchi mbili sio nchi moja yenye serikali mbili ni nchi mbili zenye serikali mbili,kwa maana nyingine kila nchi ina serikali yake
 
Warioba alituletea maisha ya kufikirika na matumaini ya hewani wakati raisi ametuletea uhalisia.ila nchi hii ya wa kukopi na kupest tuna shida ya utambuzi na hatuko tayari kupokea uhalisia sisi ni ma alinacha wa kujenga ghorofa hewani vile tuna dhahabu, almasi, gas, maji na tunapumua, everything is simple and come what may.
 
Hivi kufanya Waryoba awasilishe kabla ya JK kuzindua ilikuwa imepangwa?
 
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.

Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.
Tume ya Warioba walikusanya maoni ya wananchi, wakafanya uchambuzi, wakafanya utafiti, wakarefer historia ndio wakaja na hiyo rasimu,

Hebu JK naye awaeleze watanzania amekusanya maoni wapi, amefanya uchambuzi wapi, amefanya utafiti gani na historia gani iliyomfanya aamue kutaka serikali mbili?
 
Warioba hakutoa hotuba, Warioba amewasilisha rasimu ya katiba ya tume aliyoiongoza.

Kikwete ametoa hotuba murua kabisa na ni hotuba ya karne.

Ya Warioba ni maoni yetu wananchi,ya kikwete ni yake na mkewe.Hivyo wengi wape
 
Hivi mmefuatilia hotuba ya Rais aliposema kero au matatizo ya katiba ya Zanzibar ambayo yameibua hili suala la serikali tatu yatapatiwa ufumbuzi kati ya 2015 na 2018?. Yaani kurekebisha katiba kwa kuodoa kipengele cha Zanzibar ni nchi inahitaji muda wote huo? Au wanataka kuwabembeleza hao wenzetu kwa kumpa uraisi kwanza mzanzibari halafu yafanyike mabadiliko hayo? sioni sehemu likijadiliwa hili.:eyebrows:
 
Msingi unamojengwa hoja ya serikali tatu ni hasira zaidi kuliko kutatua tatizo. Mhe. Jaji Sinde Warioa pamoja na tume yake ya kukusanya maoni ni kuwa kwa sababu Wazanzbar wamevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusema Zanzibar ni nchi basi Tanganyika nayo iwe na nchi yake. Kuwe na serikali ya tatu itakayoshughulikia mambo ya muungano.
Hoja hiyo nidhaifu kwa sababu huwezi kuondoa sheria kwa sababu kuna mtu au kikundi cha watu kinaivunja.Bdala yake mvunja sheria anapaswa kuadhibiwa au la akemewe.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Jakaya Mrisho Kikwete hajui anaongea nini. Tume ya kukusanya maoni ya Katiba ni yake kwa msingi kuwa ameiteua yeye na kabla ya kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba rasimu ile iliwasilishwa kwake kwanza. Hivyo kama angalikuwa na maoni kinzani angaliweza kuyaeleza mbele ya Tume kabla ya kuwasilishwa. Kuipinga baada kuiwasilisha ni sawa na kusema awali alikubaliana na Tume bila kujua athari za maoni aliyokubaliana nayo. Amekuja kujua athari zake baadaye. Maana yake ni kuwa anakumbuka shuka kumekucha.
Pili kiini cha Watanganyika kudai Tanganyika ni yeye JK KUTOLINDA KATIBA ALIYOAPA KUILINDA. Matokeo ya kutolinda Katiba ni madai ya serikali tatu. Kwa kifupi ni kuwa yeye ama kwa kutojua ama kwa uzembe amezalisha hoja ya serikali tatu. Itakuwa ngumu sana kwake kuzuia mkondo wa maji mafuriko baada yakuyafungulia njia. Wote wawili hawana hoja, lakini kama ni kulinganisha ni afadhali Jaji Warioba. Lakini mizania tunayotumia kulinganisha sio sawia. Utalinganishaje mwanasheria mwenye LLM, Jaji, Waziri Mkuu Mstaafu,aliyepata kuwa Mwenyekiti wa sheria za majini (marine law) na mwenyekiti wa Tume ya kero za rushwa na Gentral man mwanasiasa tu hata chapisho moja hana na hotuba anaandikiwa na msaidizi wa raisi tena sio mwepesi wa kujisomea. Bora ungemlinganisha Jaji Warioba na Jaji Amos Wako wa Kenya. Kwa mambo ya kisiasa nisawa lakini mambo ya kitaaluma kama kuandika Katiba ni mzigo mzito kwa JK. Ninacho kiona hapa ni kama amepata shinikizo kutoka kwa washauri wake. Bahati mbaya washauri wake ama wamechelewa ama yeye mwenyewe kwa hulka yake ya kuchelewa amechewa kuelewa somo
 
Pasco,

..hotuba ya JK imekuwa ni mbovu kiasi kwamba hata Dr.Benson Bana ameshindwa kuitetea!!

..mambo mengi aliyoyasema JK hayana ukweli, lakini sidhani kama alikuwa amedhamiria kutosema ukweli.


cc Mchambuzi, betlehem, Nguruvi3
Mbaya zaidi, katumia takwimu za tume kupinga matokeo yaliyowasilishwa bila ya kujua kwa kufanya hivyo, mathematics of probability zimembeba warioba; unampinga mtu kwa kuja na alternative approach ambayo iliyo scientific;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco, any layman can notice the hell of difference between the two.......... Kikwete anasema ameambiwa, kila kitu ameambiwa... while Warioba and his teammates collected the data, analyze them and do the presentation ; ur president was no less than a failure who want to show the weakness of their hard work..... I'm not known to such a cynical president..!
 

Ivi Moshi Mwenyekiti Wa Halmashauri Ni Chadema Na Alipata Kutokana Na Uwingi Wa Madiwani Wa Cdm ! Ivo Uwingi Ndo Kigezo!
 
Ivi Mnafikiri Rais Kama Rais Angesema Nn Yaani Akae Kimya 2! Hakna Rais Mjinga Namna Hyo!
 
Bwana ki.wete ile siku alikua anacheka cheka na kutoa mipasho kama mwimba taarab!!! Huwez walinganisha maana hawafai wala haiwezekani walinganisha!!!
 
Bunge la katiba ni Kama haikuzinduliwa hv ! Maana Mh Rais alienda Kutoa maoni yake Binafsi huku akijua Tume imemaliza kazi yake . Mh Rais aende akazindue Bunge sasa ile ya kwanza hakuzindua alichambua rasimu tu mda mwingi alitumia kudadisi na Uchambuzi ! Kwa kweli Hakuna jinsi zaidi ya kuludi tena pale Dodoma kuzindua Bunge Upya kumbuka hata Warioba Aliludia Mara ya pili baada ya kwanza kukumbwa na walakini na sitofahamu ya Six
 
Hotuba Zote Mbili Zinathamani Kubwa Kwa Watanzania! Rais Kimsingi Alikuwa Anaelimisha Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ivo Kufumbua Waliokuwa Wanaupeo Mdogo!
 
Ivi Mnafikiri Rais Kama Rais Angesema Nn Yaani Akae Kimya 2! Hakna Rais Mjinga Namna Hyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…