Mkuu,naomba unisome na kunielewa
Nilikuwekea hapo kuwa mantiki inakana vitu kuwepo bila muwekaji sijui hiyo inakuwaje ni assumption
Nasema ni assumption kwa sababu huwezi thibitisha kwamba vitu vyote vina muwekaji, mf Mungu muwekaji wake ni nani?
Nithibitishie kuwa Mungu anafit kwenye hizo maana zako za kitu
Mkuu hebu tuangalie maana ya Mungu.
Katika ukristo God is the
creator and ruler of the
universe and source of all
moral authority; the
supreme being.
Hiyo maana ya Mungu kwa mujibu wa ukristo inafall katika maana hii ya kitu
3. An action, activity, concept or thought
> unspecified circumstances or matter etc.
Nasema hivyo kwa sababu kwa maana ile pale juu Mungu amekuwa defined as a concept.
Pia kuna sifa nyingi sana za Mungu kama ifuatavyo; ambazo zote zinamdefine Mungu
Ni Mwenye nguvu, mtakatifu
(Mwanzo 1:1)
Ni Mwenye nguvu kupita wote na aonaye (Mwanzo 16:13)
Mungu ni wa milele, kumaanisha hakuwa na mwanzo na kuweko kwake
hakutakoma. Hafi na hamaliziki
(Kumbukumbu la torati 33:27, Zaburi 90:2; Timotheo wa kwanza 1:17).
Mpaka hapo nimekuonesha Mungu ni nini, na sifa zote hapo juu zinafall katika maana ya kitu niliyoweka hapo juu.
Ukishindwa utakuwa ume assume tu na humjui Mungu ni nini
Nimekujibu hapo juu maana ya Mungu kwa mujibu wa ukristo.
Pia kuhusu suala la Mungu bado ni assumptions kwa sababu hazijathibitika ingawa zinaaminika kuwa kweli.
Nasema hivyo kwa kuwa an assumption is a thing that is accepted as true or as certain to happen, without proof.
Sijaasume bali hiyo ni kwa mujibu wa mantiki
Au unakana?
Narudia tena hiyo mantiki yako bado ina utata, kama kila kitu kina muwekaji basi na Mungu naye ana muwekaji
Hapana siku assume bali nilikuambia kuwa kama tukianza kudhani nyumba inaweza kutokea bila mjengaji tutakuwa tuna violet kanuni ya mantiki,upo hapo?
Nakubali kabisa kwamba nyumba kutokea bila mjengaji tunaviolate kanuni,
Kama mkuu umeweza kusema nyumba haiwezi kutokea bila mjengaji, vipi kuhusu Mungu aliye mjengaji/muumbaji wa vyote kutokea bila mjengaji?
Hapa ndo kidogo mantiki inaleta utata.
Bahati mbaya sana hukunielewa
Nilikuuliza kama unaweza kujua sababu ya kila kitu kuwa na muwekaji,hujaelewa kabisa hili
Mkuu hiyo mantiki ya kila kitu kuwa na muwekaji umeileta wewe, na hizo sababu wewe ndo unatakiwa kuzijua na kuzitaja hapa ili kujustfy mantiki yako
Lakini pia nilikuambia kuwa umeshindwa kuniuliza maswali ambayo yanaweza kukupa majibu sahihi kwakuwa kuna step umeiruka
Step ipi hiyo nimeiruka? Kama ni kuhusu Mungu ni nini nimeshakujibu hapo juu
Kabla ya kujadili au kurukia kuwa Mungu anaweza kuwa na muwekaji ni lazima kwanza ujue Mungu ni nani
Unaposema ni nani, unamaanisha ni mtu?
Ukitumia neno 'nani/who' you refer to a person.
Kuhusu Mungu ni nani/nini nimeshakujibu hapo juu.
Tunasema binadamu lazima awe na muwekaji la hawezi kuwepo tu kutokana vile ambavyo binadamu tunamuona na viungo vyake vilivyo na mpangilio,yaani ni kama nyumba yenye bafu,choo,jiko,chumba cha kulala n.k useme vyote hivyo vimetokea tu bahati mbaya hata kama umejua kuwa vyote hivyo vipo hapo kwa sababu maalum nayo ni atakaeingia humo atavihitaji
Tunarudi palepale, vipi kuhusu Mungu aliyemuwekaji wa vyote, je unakubali kuwa yeye anaweza kutokea tu from nowhere? Au kuna muwekaji?
Labda nikuambie hivi;gari limewekewa break kwakuwa inahitajika kwenye matumizi na aliyiweka alijua hilo,leo binadamu anaonekana mkamilifu na hakuna kiungo ambacho kimekosekana kwenye hitaji lake,mfano kama angekuwa hana mkono mmoja na ikaonekana kwenye maisha yake ya kila siku anahitaji mkono mwingine hapo tungeweza kuona kirahisi sana kuwa amepungua,iweje aonekane hajapungua?
Bado narudia tena, vipi kuhusu Mungu aliye muwekaji wa vyote hivyo, je yeye anaweza kutokea tu from no where?
Halafu pia bado una assume tu kwamba ni Mungu ndiye muwekaji wa hivyo vyote kwa sababu huwezi kuthibitisha.
Hata mimi naweza kusema/kuassume muwekaji wa vyote hivyo ni babu yangu, nitakuwa sawa na wewe unayesema muwekaji ni Mungu, wote TUNASSUME
Sasa basi kwa mntiki hiyo ndipo tunasema kuwa binadamu aliwekwa na hakujiweka mwenyewe au kutokea tu
Pia kwa mantiki hiyo tutasema Mumgu naye aliwekwa hakujiweka mwenyewe.
Kwenye ishu ya Mungu ni tofauti,hujui Mungu uwezo wake unakomea wapi,halafu kabla ya kwenda kote huko ni lazima kwanza tukubaliane kama yupo ili tuanze kujadili uwezo wake,hatuwezi kujadili uwezo wa gari wakati hatujui au mmoja haamini kama kuna gari
Ni kweli labisa mkuu ili tuweze kujadili gari fulani ni lazima tujue lipo au halipo,
Sasa wewe ambaye unasema kuna gari(Mungu) naomba uthibitishe kwamba lipo, baada ya hapo tuanze kujadili.
Mimi siwezi kusema lipo au halipo, kwa sababu wewe ndo umekuja na wazo la gari kuwepo kwa hiyo naomba unithibitishie kwanza hilo gari, halafu ndo ntajua lipo au halipo
Kitendo cha huyo mtu kuwa na afya dhaifu tayari ni ishara ya uvunjifu wa kanuni,sijui kwanini huoni hili
Kama unajidai huoni na kusoma madhara yanayopatikana kwa hao kufanya hivyo sijui nitakusaidiaje
Labda nikuulize swali mkuu,
Mtu anapougua ugonjwa fulani mf malaria anakuwa amevunja kanuni?
Tuanzie hapo kwanza