CONCERN: Why are all car manufacturers setting up shop in Kenya? Iko wapi Tanzania ya viwanda?

Umekosea swali lako ilitakiwa kuuliza hivi nini tunacho sisi watz ambacho Kenya awana kinacho sababisha wawekezaji kuwekeza Kenya Jibu ni ili Tanzania tulichonacho kinacho kimbiza wawekezaji ni CCM NA MZEE WA PHD
Ongeza na hii Tzee Kuna amani while Kenya hakuna.
 
The most suprising thing to me is that if you have a dormant company in tz, you can file nil returns lazima ulipe tax even without doing business, very funny
Tatizo ni kwamba tunataka kuiga everything the world has done before... just copy and paste... it wouldn't be shocking kwamba hilo neno 'dormant' pia maana yake kikamilifu hatuelewi...
 
Nilisafiri kwenda Rwanda ku survey biashara ya kufanya mwishoni mwa mwaka jana . . Kwa bahati mbaya sikukumbuka kuchukua Passport yangu, kwa hiyo nikatumia pasi ya (karatasi) dharura ya East Africa . .

Lengo langu lilikuwa kwenda mpaka boarders za Rwanda na Congo kuona biashara huko inaendaje . .

Sasa, kwa sheria . . , huwezi kupata nafasi ya kuvuka mpaka nje ya nchi za EA kwa temporary pass, kwa hiyo ikanibidi kwenda ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda kuomba pasi nyingine ya muda kwa nchi za SADC . .

Nilisikitishwa sana na huduma za ubalozi wetu kwa kweli, kwanza hawajali muda kabisaaa.
Niliingia ofisini kwao Ijumaa saa 3 asbh , nikaeleza shida yangu na haraka niliyokuwa nayo . Nikaambiwa kusubiri, muhusika anakuja kunisikiliza . Nilisubiri kuhudumiwa mpaka saa 7 mchana . . , kwa kuelezwa kuwa eti nikapige picha halafu ndio nijaze form za kuomba pasi . .
Kurudi saa 8:30 mchana na picha zangu, nikaambiwa nilipie Pass fee halafu nirudi Jtatu asubuhi kuchukua pasi yangu . .

Jtatu saa 3 asbh niko ubalozini, nikaambiwa kusubiri karatasi zinashughulikiwa, nikawakumbusha kuwa ninataka kusafiri mapema kabla ya saa 6 mchana, nikaambiwa bado kusubiri .. Nikaanza kusoma machapisho ya biashara za Tanzania pale Ubalozini mpaka nikayamaliza yooote . . Nikasinzia pale ktk waiting room yao baada ya kuishiwa cha kufanya . .
Karatasi za pasi nilikuja kupewa saa 9 mchana . . , kwa hiyo sikuweza tena kusafiri Jtatu hiyo, ikanibidi kusafiri Jnne asubuhi . .

Nilipoteza Siku 3 nzima Kigali kwa sababu ya Tz Embassy . . , na hawakuonyesha ku regret kwa lolote . . , waliniona kama msumbufu fulani hivi . .

Tanzania Tanzania Tanzaniaaa . .
 
Have y
Ndugu yangu hujui maisha ya hao.jorani zetu. 75% ya cake yao ni mali ya middlemen wa UK 25% ndio Wahindi na mixtures zinginge. Mswahili wao hana kitu anachojua ni kuwatumikia Mabwana tu. Kuhusu uwezo wa kununua Magari weka mbali na TZ sisi ndio tuna uwezo huo kwa Raiya wetu kuzidi wao. Na kila biashara wanayofungua soko wanaloangalia ni TZ, and thus why wanapambana kuhakikisha km sio kutuhujumu tusipate investors ili kulinda masoko ya bidhaa zao.
 
Pole sana, binafsi nimeshawahi kuwa na interactions na balozi zetu katika nchi nyingi sana duniani, na kote huko siwezi kutoa sifa yoyote. Zamani sana nikiwa trainee wa JICA huko Japan tulikuwa na International day ambapo tuliambiwa tuonyeshe jambo lolote kuhusu nchi zetu. Nikaenda ubalozini kuomba picha na bidhaa zozote zinazotangaza nchi. Nilipata packet moja majani ya chai ya Brooke Bond wakati huo, kop[o moja la kahawa ya Africafe na viroba viwili vya Chibuku kwa masharti kuwa nirudishe vyote ubalozni baada ya maonyesho. Hakukuwa na picha zozote, ikabidi nipewe picha na mjapani mmoja aliyewahi kuwa volunteer Tanzania. Iliumiza sana kwa vile jamaa wa kenya alikuwa akitoa free samples kwa watu wote wanaoitembelea meza yake wakati mimi nikiwa naonyesha sura tu. Inawezekana mambo yamebadilika kidogo lakini balozi zetu bado siyo aggressive kiasi cha kulinganishwa na Kenya
 
Wajenge Kenya halafu soko wategemee Tanzania ndio plan zao. Tanzania one piga bana ya kueleweka hizo gari ziwe na kodi kubwa kuliko hata bei za magari yenyewe wapuuzi hao. Tutaenda Japan au South maana hakuna namna.
Anza biashara ujue nguvu uliyonayo kwenye hizi deal
 
I will love to here you report this to our Ministry. Napenda watu km ninyi mnaosaidia kuonyesha tunakwamishwa na nini, kuliko wale wanaopinga pinga kila lifanywalo Nchini huku tunawaona humu wakisifia yaleyale lkn yanafanywa kwa jirani.
 
Wajenge Kenya halafu soko wategemee Tanzania ndio plan zao. Tanzania one piga bana ya kueleweka hizo gari ziwe na kodi kubwa kuliko hata bei za magari yenyewe wapuuzi hao. Tutaenda Japan au South maana hakuna namna.
Akili za ki CCM CCM hizi . . , yaani tuache sasa kufuata Sera za biashara za EAC market na EA customs tariff structure . . , kisaa ?!

Tuache kununua Kenya kwa sababu tuu tuna wivu wa ki CCM . . ?

What don't you grow up you Bashitezz . . ??!
 
Tatizo ni kwamba tunataka kuiga everything the world has done before... just copy and paste... it wouldn't be shocking kwamba hilo neno 'dormant' pia maana yake kikamilifu hatuelewi...
Mimi si mtanzania boss,and by dormant I mean a company that isnt doing business,lakini bado mnalipia tax kwa TRA,sisi kenya as long as unafile nil returns haulipi anythin
 
nimekaa nairobi six years..nimeongea kwa maono niliyoyaona mimi.its true hali za weusi si nzuri ila huwezi fananisha na TZ...vipato vya kenya kwa kazi moja na mtu afanyae TZ kuna utofauti mkubwa sana. kuwa na nyumba kenya ni matatizo sana kwa sababu ardhi ni bei sana maeneo ya mijini. viwanda vingi ni kwa sababu ya uchumi mzuri kuliko TZ na Uganda..
 

Si kampuni za magari tu, all multinationals who choose to have a presence in the region, wanachagua Nairobi for very obvious reasons. Google, IBM, etc. Wote wanachagua Nairobi. Nairobi is more business friendly/more entrepreneurial than any other place in the region. Siasa za Kenya ni more business friendly (japo husababisha machafuko mara kwa mara). Wanasiasa wa Kenya wanaelewa biashara kuliko wanasiasa wa kwetu. Na kikubwa wanachotuzidi wenzetu ni human resources. Nafikiri hii ni factor kubwa inayovuta mitaji - watu wenye sifa za kufanya kazi. Huwezi kupeleka mtaji mahali ambapo utapata shida ya wafanyakazi wenye sifa. Hatuwezi kuishinda Nairobi for quality human resources. Kenyans are more technologically savvy than Tanzanians. They are more business minded than Tanzanians. Sisi bado tunadumazwa na nationalistic ideas, which are not well thought of. We need to invest in our people + rethink our education.
 
Mimi si mtanzania boss,and by dormant I mean a company that isnt doing business,lakini bado mnalipia tax kwa TRA,sisi kenya as long as unafile nil returns haulipi anythin
Bwana Kenpaulite, I know that you're not a Tanzanian.... I was talking about us here in Tanzania... anyways, the point got through hopefully to the rest..
 
Umenena vizuri sana.. Sisi tutaendelea kupata wawekezaji kwenye shughul zenye kuitaji technology kidogo na nguvu nyingi na ndio vyenye tija kwetu sbb vinatoa ajira nyingi kwa watu wa chini mfano viwanda vikubwa zaidi EAC vya cement vitakuwa Tz viwanda vikubwa vya chuma, viwanda wa material ya ujenzi kama kile cha vigae..
 
LATEST: Nissan Eyes Bigger East African Market With Kenya Auto Plant
 
TANZANIA YA VIWANDA MY FOOT!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…