CONCERN: Why are all car manufacturers setting up shop in Kenya? Iko wapi Tanzania ya viwanda?

so make me understand, how will small start ups survive before their big breaks?, did you know in Kenya you can own a company and file nil returns?
Brother you will take a century to educate a fools who is bewitched, this is economic issue which need intellectual/strategic discussion which will bring about changes in our country but he/she is brings about political view of point.
 
Back in the 90's Kenya used be the power house for motor assembly in EA, 2nd hand cars imports is what killed the industry but I can see we are slowly getting back on our feet. Welcome Volvo.
Bravo jirani zetu kwa hatua hizi
 
Mtu mmoja nchi hii anaweza akaamka asubuhi . . ,akala maharage yake ya koromije, akaamua kufunga kiwanda ama biashara ya watu kwa kutangaza tuu ktk TV au radio . .
 
Sera za uwekezaji Tanzania bado hazijakaa vizuri. Sera zinabadilika badilika, kila raisi anaekuja anakuja na yake. Utitiri wa regulators, rushwa, kutothamini wawekezaji, utekelezaji mbovu wa sheria za kodi, ana kubwa zaidi taifa kwa ujumla halina business mindset. Watanzania wengi wanachukia matajiri au watu waliofanikiwa sana. Ule msemo wa alie juu msubirie chini unawagusa watu wengi. Kwa nini alie juu usimfate huko huko juu. Pengine ni kwasababu wapo wengi walifanikiwa kwa njia za udanganyifu so tunahisi kila mwenye mafanikio kapitia huko. Tatizo lingine ni ulimbukeni...mambo madogo yanakuzwa na kuonekana makubwa kupita kiasi. Tunakosa global perspective, matokeo yake watu wanaridhika mapema. Biashara hazikui kuvuka mipaka. kampuni nyingi za kenya zimewekeza hapa, ni ngapi za Tanzania zimewekeza kwao. We must change the business mindset. We must think big and see the bigger picture. Matajiri wakubwa Tanzania ni wahindi na waarabu. CEOs kwenye makampuni makubwa kama ya simu, mabenki e,.t.c ni wahindi, waarabu au wageni. Key positions zinakamatwa na expatriates. Lazma tukubali pale Kenya walipotuzidi, ndo njia pekee ya kuwakimbiza na hatimae kuwapita. Tujue wanafanya nini kinachovutia wawekezaji, sisi tufanye zaidi kuwapita.
 
Mi sidhani kama kodi ni tatizo.
It should be that hata kodi iwe kubwa vipi mwekezaji bado atataka kuja Tanzania.
Solution sio kupunguza kodi, in my view. Mi naona infrastructure. That is where Kenya wametupiga bao.
Brother . . ,

Be serious . . , kodi ni tatizo kubwa kabisa kwa business . .

TRA wanatangaza kuwa kuji register kupata TIN na VAT certificates ni bure, lakini ukisogea Ofisini kwao kupata usajili ndio utajua kuwa kutoa rushwa ni lazima . .
Kwanza watakudai uonyeshe wapi umepata Capital yako, na hiyo wataitumia kukufanyia makadirio ya kodi, watataka uonyeshe mkataba wa kupanga Ofisi . . , nao unalimwa kodi . . , msururu wa makodi hata kabla ya kuanza biashara unaendelea . . Bado 30% Corporate tax . .

Kuwekeza TZ lazima uwe ngangari sana . .
 
acha tukose tu mavitu mazuri hii nchi yetu bhna sielewi sasa kama hata prado yangu jmn ya kutumia mwenyewe si ya biashara ila bandarini inalipiwa 30Milion as kodi
 
Umeona aliyechaguliwa kuwa CEO wa TIC? Alikuwa mkuu wa Wilaya Singida Sishangai kampuni kwenda Kenya niko disappointed for sure.
-Hivi CEO alifunguliwa kesi ya nini? Tabili mshindi
-Manji ana kesi za nini vile?
-TDL wamezalisha viroba bulks & bulks na ipo kwenye long & short term plans za kampuni anakuja mtu bila kutaja sheria iliyovunjwa anasema tarehe 1 sitaki kuona na inakuwa.

-Kwa taarifa tu, serikali haitanunua magari mapya toka Kenya bali itaendelea kununua toka SA & Japan kwa "keshi"
 
Tuna kosa sifa ya uchapakazi, ni watu wa kuongea zaidi kuliko kutenda, watu wa kutoa sababu zaidi kuliko kufanya kitu kitokee. Mbaya zaidi uwizi, ufisadi, mfano mzuri ni yule Mhasibu wa takukuru!!!Kibongo bongo jamaa ni mchapa kazi na anajua kuzitafuta pesa!!
 
Hapo umenena mkuu, kuna watu magari yalichakaa mwaka 47 walishauza scrapper na wamesahau kama waliwahi kumiliki hayo magari walipoenda TRA kulipia magari mengine waliyonunua wakadaiwa kodi inayozidi thamani ya gari alilokwisha lisahau.
Huu ni wizi wa mchana kweupeee . . , na unafanywa na Serikali dhidi ya wana wa nchi . .
 
Tuna Vi-Wonder Tanzania ,viwanda tuwaachie watu serious kama kenya,Rwanda,South Africa ,Ethopia etla
Kabla ujawekeza katika kiwanda lazima ukague Gharama za umeme,uhakika wa umeme,uhakika wa wafanyakazi makini wenye nidhaamu ya kazi, taarifa hizi zote zinapatikana ktk business inteligence forums/reports na balozi za nchi husika zinaandaa taaarifa hizo hizo kwa kutumia vyanzo rasmi na magazeti na trends in the street.
hivyo basi kiwanda kama Volvo ,hyundai ,Toyota na VW lazima kutumia report za tafiti kabla ya kuwekeza.

Wafanyakazi wa Tanzania nidhamu ya kazi ndogo sana,akishaajiriwa tu baada ya miezi 5 anaanza longolongo na kumfukuza kazi siyo jambo dogo.
Sera zetu hazina sheria nzuri za kulinda mwekezaji halali .mwekezaji anayepaweza tanzania ni Mchina Tu,na yeye anatatizo la ajira kwao china.
Mheshimiwa Raisi ,Magufuli Angalia uhakika wa Umeme na Sheria za uwekezaji.ikiwezekana kuwepo na industrial zones zenye umeme wake nje ya Gridi ya Tanesco,mfano kuweka industrial zone karibu na maporomoko ya maji,au mgodi wa makaa ya mawe.
 
Imagine mtu unafungua stationery office halafu ukienda TRA unatakiwa ulipe si chini ya 60,000. Next year wanapandisha hata ukiwaambia biashara sio nzuri wao wanakomaa tu, sjui tutafika lini.
 
And what will happen if we will not purchase those fabricated car's from your country?
 


Well said.
 
Akili zako na baba yako mmefungua kiwanda gani zaidi ya kutopea kwenye umasikini.
Nikitaja kiwanda na biashara nnayofanya itakusaidia nini wewe kijana wa ccm . . ?! Nyie ccm hampendi kabisa maendeleo ya wanaowakosoa . . Tazama mnavyomwandama Mbowe na biashara zake, tazama mnavyotaka kumfilisi Manji kwa visingizio vya kipumbavu na visasi . .

Wachina tuu ndio watakaoifadi hii nchi . . , nafikiri ndio strategy yenu ya kuendelea kupata support ya kuendelea kungangania madarakani .
 
Hivi Tz tuliahidiwa Tanzania ya Viwanda au Tanzania ya Vi-wonder?!
Kama ni ya viwandad hiyo sahau mpaka jamaa aondoke ila kama ya Vi-wonder tayari tunayo!!
 
Umesema mambo mazuri vile
 
Obviously, wawekezaji wanaenda kuwekeza sehemu iliyo more favorable kwao. Inatakiwa tuifanye Tanzania iwe favorable kuwekeza wakati huo huo tukihakikisha "win win" situation, yaani mwekezaji ana faidika na nchi inafaidika.

Kwa hali iliyopo bongo leo, it will take a great leader ili angalau tuanze kuelekea in the right direction, bahati mbaya sana tumekuwa tukipata MEDIOCRE leaders kwa muda mrefu sasa, na tunaendelea kuanao, na sioni dalili ya hili kubadilika.
 
Tanzania ya vi wonder ipo! Ipo ipo sana. Ingoje tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…