Confession: Mtanzania kusomea au kuishi Kenya na kurudi Tanzania ni big step

Honestly i was embarassed, Sheria itungwe Tz wazito wasitumie kiingereza wanaporekodiwa

your going to stay on the cell until you provide serious explanation on matter ,because now you cannot play with the government like this ,last time I came here equipment like this ,then you take to another site so your going to stay inside until your give instruction for the equipment you have taken to Dodoma to come back here make sure you have sufficient people to work on the site
 
Sioni ubaya wowote wa mtu kuongea broken english ilhali si lugha yake mama
 
Sioni ubaya wowote wa mtu kuongea broken english ilhali si lugha yake mama

Ni uzembe tu, ukishindwa unajitetea kwamba sio lugha ya mama, ifahamike hata Kiswahili sio lugha ya mama kwa wale hamjatokea Pwani kilikobuniwa.
 
Ni uzembe tu, ukishindwa unajitetea kwamba sio lugha ya mama, ifahamike hata Kiswahili sio lugha ya mama kwa wale hamjatokea Pwani kilikobuniwa.

Hakuna cha uzembe wala nn,upo brainwashed na weupe kuona vyao ndio muhimu.

Mtu wa pwani ipi aliyetokea tz asiyejua kiswahili,utetezi wa kizuzu kabisa huo.

Hata wenyewe hao wenye lugha yao wanawashangaa vile mnavyoshobokea lugha zao na kudharau zenu.

Ndio maana wanawaita nyie ni nyani kwa kutojielewa.
 
Hamna sehemu nimesema watu wa Pwani hawajui Kiswahili, jifunze kusoma na kuelewa unachokisoma.
Nyie wazembe, lugha umeisomea miaka yote halafu unashindwa hata kuitumia kuongea sentensi chache za msingi, halafu unajitetea eti sio lugha ya mama.
Halafu uzembe wenu upo hata kwenye lugha zenu za asili, ni wachache sana huwa mnajua hata salamu kwa kutumia lugha za asili, kingereza kimewapiga chenga, lugha za asili hamzijui na uandishi wenu wa Kiswahili hutia kinyaa, hamna lugha hata moja mnayoimudu kiufasaha, mpo mpo tu ilmradi siku zinasonga, tatizo uzembe.
 
unaongea ongea pumba tu mkuu,lugha za asili si ndio zimewaweka nyie hapo mlipo,na ndio maana mnabaguana,sisi kwetu hata kama kuna watu tunaozijua hizo lugha lakini sio kipaumbele chetu na huwezi kuona mtu anajisifia kujua lugha ya asili yake,endeleeni kubakia kuwa wahanga wa lugha za kigeni na kujiona nyie ni wazungu weusi.
 
Hakuna na haiwezi kutokea watu wakabaguana kwa misingi ya lugha, fahamu ujanja na uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja hupanua maarifa na ndio maana unaona pamoja na kwamba nchi yetu zaidi ya nusu yake ni kame tupu, ila uchumi wetu unaelekea kuwa mara mbili yenu, ukizingatia mna nchi kubwa yenye madini kote.

Watu hubaguana kwa misingi ya kidini, ukabila, uchama, ukanda, jinsia, dini na mengineyo lakini sio lugha.
Somalia wao wanaongea lugha moja, dini moja ila kila siku milipuko na mauaji.
Kwenu huko mna udini, ukanda na uchama sema siku hizi naona hata ukabila umewaingia.
 
Mnatamani sana tuchukiane kama nyie na kamwe haitatokea hivyo,tutapishana kwa hoja ila mwisho wa siku tutaelewana tu na hatutafikia kiwango chenu cha chuki.Hiyo ndiyo tofauti kubwa kati yetu na nyinyi.Sisi ndio watanzania.

Kuhusu maendeleo kijana hilo ni dogo sana na muda utafika na tutakuwa na maendeleo makubwa sana kuliko nyie taifa la wezi wezi,lenye maendeleo bandia. Nyie mnachokiweza ni utapeli na ujanja ujanja tu na zama zenu ndio zinakaribia kuisha.
 
chai ya moto bila vitafunwa haipendezi hata kidogo
 
elimu(ndani na nje ya darasa) ambayo watz wengi huipata Kenya ndio huwa inawapaisha juu ya wenzao wengi wakirudi tz, ila sasa Shida watz wenzangu navowajua mimi ni kwamba ukitaka wapandwe ubishi uliojaa hasira jaribu kuwaambia ukweli
Kuna watu kibao nawafahamu wamesoma kenya na hawana lolote, lakini mimi nimesoma Tz and I have make it kuliko hata hao waliosomea Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni uzembe tu, ukishindwa unajitetea kwamba sio lugha ya mama, ifahamike hata Kiswahili sio lugha ya mama kwa wale hamjatokea Pwani kilikobuniwa.
Hivi unajua maana ya "lugha mama" kwa kiingereza "mother tongue" kweli wewe?

Hivi huko kenya huwa mnafundishwa ujinga kwenye shule zenu. Mimi nimezaliwa Mwanza ( kanda ya ziwa) na kiswahili ni lugha mama yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu kibao nawafahamu wamesoma kenya na hawana lolote, lakini mimi nimesoma Tz and I have make it kuliko hata hao waliosomea Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umefanikiwa kwa kipi mkuu, nakuonea Huruma, naona hata akili zako hazipo sawa, hivi kweli mtu umejiita idiot embicile we ni mzima kweli, umetororoka hospitali ya vichaa au
 
Wala hatuwezi kutamani mbaguane, hamna kitu kibaya kama ubaguzi, sio kitu cha kutamani dunia hii, sema tunayaona japo kwa unafiki mnapenda kuficha maradhi kama walivyo Korea Kaskazini.
Kuhusu uchumi naona pengo baina yetu linazidi kuongezeka, wimbo wa kwamba mtatufikia uliimbwa tangu enzi za mababu zenu na naona mtaupokeza kwa vizazi vijavyo ila hali ni ile ile.
 
Hivi unajua maana ya "lugha mama" kwa kiingereza "mother tongue" kweli wewe?

Hivi huko kenya huwa mnafundishwa ujinga kwenye shule zenu. Mimi nimezaliwa Mwanza ( kanda ya ziwa) na kiswahili ni lugha mama yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu huyo ni kituko hadi anatia huruma,ni mjinga lakini anajifanya mwerevu eti kisa kujua kuongea kiingereza kwa ufasaha.

Najiuliza mwanangu je wa std 5 anayejua kiingereza vizuri kuliko mimi eti naye nimwone wa maana sana kisa kujua kiingereza,huo ndio uzwazwa wa hawa ngozi nyeusi wenzetu kutwa kuthamini lugha za watu na kuzipuuza za kwao.
 
Heheeeeee,ngoja nicheke kikwetu mieee,nchi yangu pendwa kimaendeleo inakuja kwa kasi sana bila kukiabudu kiingereza
 
Reactions: Oii
Ukimkuta mtanzania anajua kiingereza... Utagundua kiingereza chake kuwa kitamu zaidi ya hao unaowasifia.

Siku zote juhudi za mwanafunzi ni muhimu kuliko za mwalimu.

Lakini pia usisahau kuwa kujua kiingereza sio kipimo cha akili... Isipo kuwa kukifahamu vizuri kunakupa fursa ya kujiamini zaidi kuwasiliana na watu wa lugha husika.

Mfano kama kweli unahisi unahitaji kujua kiingereza unaweza jiunga English counsel pale posta... Ukihitimu pale kiingereza chako kitakuwa ni worldwide standard na utaweza tambulika popote.

Sio lazima kwenda Kenya kujifunza kiingereza ambacho na huwa na mapungufu kama tunavyo ona ilivyo kwenye kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimkuta mtanzania anajua kiingereza... Utagundua kiingereza chake kuwa kitamu zaidi ya hao unaowasifia.
Mtu akijua kiingereza anajua tu kama ilivyo mtanzania anavyokijua kiswali ambacho hakimpi shida kabisa, Ikumbukwe uzi huu sio wa mashindano mkuu, naona unataka kuanzisha ligi out of topic

Siku zote juhudi za mwanafunzi ni muhimu kuliko za mwalimu.
Again wakenya wengi kiingereza hawajifunzi darasani tu, bali hata wakitoka darasani kwenye jamii napo kinatumika hii inasaidia sana tofauti na hapa kwenye jamii kiswahili kinatumika zaidi, ukiingia darasani nako walimu wanafundishia kiswahili kwa asilimia kubwa sana, unakuta mwalimu ana define kitu kwa english ila anaanza kuelezea kwa kina kwa kiswahili na hii ni hadi vyuonu.

Lakini pia usisahau kuwa kujua kiingereza sio kipimo cha akili... Isipo kuwa kukifahamu vizuri kunakupa fursa ya kujiamini zaidi kuwasiliana na watu wa lugha husika.
Umesahau kwamba kiingereza ni lugha ya kimataifa? Umesahau kwamba kiingereza ni lugha ya biashara za kimataifa? Umesahau kwamba kiingereza kinapanua wigo wa fursa walizopata kina lupita nyongo? Umesahau kwamba kiingereza ni lugha inayofanya hawa ndugu zetu wachukue ajira za hapa tz huko UN arusha? Umesahau kwamba kukijua kiingereza unaweza kusoma karibu nchi yoyote duniani?

Mfano kama kweli unahisi unahitaji kujua kiingereza unaweza jiunga English counsel pale posta... Ukihitimu pale kiingereza chako kitakuwa ni worldwide standard na utaweza tambulika popote.
Hapo english counsel na kwa ras simba washkaji zangu kibao wanaenda wanatoka hapo bado ndio yale yale tu ya kujua kiingereza cha kuandika ila kile cha kuelewana wakiongea na wazungu ni sifuri, wengi wakiongea na mtu tofauti na mtanzania mwenzao au mzambia basi inakuwa shughuli kweli kweli, watu kibao wamesoma hapo wakienda huko UN wanalalamika wazungu wanamungunya maneno

Sio lazima kwenda Kenya kujifunza kiingereza ambacho na huwa na mapungufu kama tunavyo ona ilivyo kwenye kiswahili.
Naona tunarudisha uzi nyuma kwa ubishi badala ya kusonga mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…