CONFIDENTIAL: Barua Pepe zaonesha Maafisa 62 wa Serikali ya Tanzania akiwemo IGP walihongwa Fedha na ACACIA (2008/2015)

Mstiri marehemu [emoji1787]
 
"NTF inadaiwa kuundwa na maafisa kutoka Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, na Jeshi la Wananchi."

Hakuna sehemu iliyobaki salama kila mtu ni mwizi hakuna hbr ya uzalendo
Unaweza kuwa namba sita duniani kwa wizi na si kwa kulinda
Huu ni ukoo wa panya.
 
Nimeshangaa sana .
Ikiwa idara nyeti hizo ambazo wananchi tunaamini zina watumishi wenye weledi na uzalendo wa hali ya juu zimefikia hatua hiyo, maana yake tupo mahali pabaya sana.
Bado wapo ambao ni waaminifu...Kila sehemu Kuna normal distribution Kwa karibu Kila issue iwe wema au ubaya
 
Ila wakati wa Mkwere watu walipiga sana pesa akiwemo yeye mwenyewe.
Kwangu mimi ndo naona ni rais mbovu kuwahi kutokea katika taifa letu hili na hii ni pale utakapotanguliza uzalendo mbele.
 
Simply walinda maslah ya nchi walijipa jukumu la kuibia nchi wanayo ilinda. [emoji86][emoji17][emoji24]
 
Who is the Director Ngowi?
 
Magufuli alikuja kurekebisha makosa ina maana hakuwaona hawa mafisadi?
Una uhakika Magufuli hakuwa fisadi?
Aliwezaje kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake kwa mabilioni ya fedha za walala hoi ambao hawana maji wala huduma za afya tena kwa kutumia kampuni ya familia.yake Mayanga construction.
 
Kama viongozi wakubwa wa serikali ya Tanzania wakiwemo maafisa wa jeshi la polisi kama IGP wanakuwa kwenye payrolls za kampuni za madini ambao wao wanawaita "wawekezaji" tunategemea wananchi tufanye nini pale haki zetu zinapokiukwa ikiwemo maji ya sumu toka migodini kutiririshwa kwenye vyanzo vya maji (North Mara/Tarime) au wananchi kunyang'anywa ardhi zao (kama kule Loliondo na Ngorongoro) ili wanaojiita "wawekezaji" wapewe?

Katika scenario hii ya migodini, hivi tunadhani kwenye ishu ya mkataba wa bandari na waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World na kwenye hifadhi zetu (reference: Ngorongoro & Loliondo cases) hawa viongozi watakuwa wamelipwa na wanaendelea kuhongwa kiasi gani Kwa gharama ya maisha na damu za wananchi wasio na hatia?

Sasa ndo tujue tunaongozwa na watu wa namna Gani..!!
 
Ndugu, dunia sasa hivi imeharibika imegeuka imekuwa si tambara bovu tena bali ni jitambara libovu.

Zile enzi za utaifa, uzalendo na maslahi ya taifa kulindwa zimepotezwa na serikali ambazo zipo kwa ajili ya kuwakilisha wenye dunia na wenye pesa.

Sisi wananchi wa kawaida akili ni nywele tuzitumie.
 
Mkuu, waifahamu uzuri Acacia na walokuwa nyuma yake?

Kuna watu wazito sana na si watu wa kawaida.

Kisha kuna ile Twiga iloanzishwa kwa lazima na mgao uwe 50/50 baada ya Acacia kutupwa nje na kuja Barrick.

Baadae Acacia akatupwa nje na kurudi kwake hadi leo ni kimya.

Maana hayo yote yalifanyia kabla ya 2015.

Haya mazingira ni magumu mno.
 
1. Hiyo ya akina Bulembo ni kwamba alianza kupambana na walokuwa wakiponda mali za chama khasa jumuiya hizo kama jumuiya ya WAZAZI ambayo Bulembo alikuwemo, hivyo ni lazima chamani kungeibuka makundi yale yanomuunga mkono na yake yanochukizwa na hatua alokuwa akizichukua.

Na mashahidi si wapo ingawa hatufahamu ni kwa jinsi gani kampeni ya usafi ndani ya CCM ilifanywa.

2. La "nature" ya uongozi wake hilo sipingi alikuwa na kasoro ya kutochunga ni kauli ipi yafaa mahali gani na kwa nani. Kw ahilo alikosea sana kwani aliweza kusikika hadi nje ya nchi kwamba amekataa dawa za chanjo ya Covid na pia hatofanya Lockdown.

Hii inafanya aonekane hana tofauti na Tundu Lissu kwenye kutoweza kuchunga kauli ingawa hii yaweza kusemwa kuwa ni aina fulani ya siasa za kelele ambazo wahusika huitwa "firebrand".

"Firebrand politicians" wapo akina Julius Malema, alikuwepo marehemu mzee Mugabe na Hugo Chavez lakini hawa wawili waliweza kizimwa kwa kukosa muongozo. Patrice Lumumba aliuawa kwa kauli zake khasa hotuba yake siku Congo wanakabidhiwa uhuru. Malema yajulikana hawezi kuja kuwa raiai wa Afrika Kusini lakini wamemruhusu kuwa msemaji.

Hivyo ukiwa mwanasiasa ambae ni "Firebrand" watakiwa uwe mjanja na uwe na timu nzuri ya watu wanokupa mwongozo ili "project" unoitaka ifanikiwe iweze kutekelezwa.

Ukiwa huna timu nzuri yaani ile "inner circle" basi weye hutoboi tena kwa kuzingatia ni "outsider" au "wild card" kwa wale wacheza tennis.

La mwisho kuhusu ukichukua hatua utagombana na chama kizima, hili ni jambo zito sana. Jaribu kuangalia nchi kama za Uchina na Urusi na sasa India ni hatua zipi wamechukua ili kuinua uchumi wa nchi zao na kuondokana na upuuzi wa Ufisadi?

India ni mfano latest kuhusu kuchukua hatua kuinua nchi kiuchumi na kiteknolojia maana hivi huendana pamoja. India sasa wameweka chombo chao cha satelite mwezini na siku si nyingi India wataweza kuwa na ni moja ya nchi zenye nguvu kubwa duniani, khasa baada ya mkutano wa G20 ulifanyika mjini Delhi.

Lakini Narendra Modi ana watu wanomzunguka (Inner Circle) ambao kazi yao ni kuandaa sera za ndani uchumi, siasa, afya na zingine na zile sera za mambo ya nje ambazo ni pamoja na msimamo wa India wa kutoilaani Russia kwa kuivamia Ukraine.

Lakini ni chama cha Modi cha Bharatiya Janata ndicho chenye kuhakikisha India yafika mbali kimaendeleo na kuwa moja ya mataifa makubwa duniani yenye nguvu ya kiuchumi.

Ufunguo (key) ni watu walo nyuma yako (si wa kuimba tu tupo nyuma yako) ni timu khasa ya watu wa kazi kwa ajli ya mradi au project. Hawa wakikuweka uzuri basi weye watoboa kiulaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…