Huu mjadala niliuacha kidogo kwa kuwa niliona kuna watu wanapinga kila hoja inayochangiwa ikionekana inapingana na suala la kumpinga bwana JM.
wiki iliyopita kwenye gazeti la Tazama Tanzania, ukurasa wa mbele kabisa waliandika "MAKAMBA KUMVAA SHELUKINDO", kwenye habari ile kulikuwa na mambo mengi sana ya kumsifia JM na kumshusha mbunge aliyekuwepo, ni kweli kabisa Mzee shelukindo amechoka na hakufanya lolote katika kusaidia maendeleo ya eneo lake, japo yapo machache ambayo nae amechangia.....
Suala kubwa ambalo pamoja na kumsifia sana JM katika habari, wameseme wameshindwa kumpata JM kuthibitisha kuwa anagombea Ubunge kwenye jimbo la bumbuli.
Taarifa za uhakika ni kweli JM anagombea na tayari kashapita jimboni kujitangaza na kashaweka timu ya kumfanyia kazi.
Mambo kadhaa ambayo ninayaping kuhusu ile article ni kama ifuatavyo:
1. kwanza ile ni kampeni ya wazi kwa JM, japo wamejifanya hawajampata kuthibitisha
2.kusema kwamba wananchi wa bumbuli ndio waliomuita JM aje kuwa mbunge wao ni UONGO, JM hajulikani jimboni kabla ya yeye na baba yake kuanza kujinadi, sio mzawa na wala jakakulia jimboni pale na wala hakuna suala ambalo amewahi kulifanya jimboni kabla ya kutangaza nia yake ya kugombea ambalo wananchi wananweza kusema ni zuri.
3. watu wote walioandikwa kwenye habari ile kama ndio waliohojiwa ni watu ambao wamo kwenye kamati ya kumtangaza JM jimboni( shemzigwa,Julius kingazi......) kwahiyo ni propaganda.
4. kusema JM ni mzawa na amekulia jimboni ni uongo kwani watu wa Mahezangulu ambako anatokea baba yake wamemkana kwa kuwa si mzaliwa wa pale na hajakulia pale na mbaya zaidi hata JM mwenyewe kwenye historia yake amekiri kwamba yeye amekulia Bukoba kwa bibi yake,tena akimsaidia bibi yake kuuza pombe za kienyeji, JM ni mtoto wa nje wa mzee makamba, mama yake ni mwenyeji wa bukoba na hili ndio wananchi wanalohoji kwakuwa yeye anadai ni mwenyeji....na ijulikane wazi familia ya mzee makamba inachukiwa sana eneo analotokea kwa tabia za dharau na matusi ya mzee makamba kwa wananchi....na ndio maana mzee makamba mara zote mbili alishindwa kwenye kugombea ubunge....
5. JM kwa mara ya kwanza amefika baadhi ya maeneo ya jimboni mwaka huu na sio kweli kila sehemu wanamfahamu kama nakala inavyosema, mwandishi alikuwemo kwenye safari ile ndio maana ameamua kuandika anavyoona kuwa inampendelea JM.
6. tunaposema watoto wa vigogo wanatumia nafasi za wazee wao vibaya hatuna maana wote na sio kuwachukia, bali inapotokea hali mtoto wa kigogo anagombea nafasi ya uongozi kuna advantage za upendeleo zinatokea ambazo zinamnyima fulsa yule mwananchi wa kawaida mtoto wa mkulima, nitatoa mfano:
i. JM anapigiwa kampeni na viongozi wa chama sasa hivi wakati ambapo sheria za chama zinapinga hivyo kwakuwa bado chama hakijateua wagombea, je hawa wengine watasaidiwa na nani? mpiga kampeni mkuu wa JM ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Lushoto bwana Mahanyu, Mzee shelukindo ameshalalamia hili katika kamati ya siasa na kutaka bwana mahanyu avuliwe uongozi lakni hakuna wakumsikiliza na huyu bwana bado mpaka kesho anafanya kazi hii,na hata pale mwenyekiti wa chama wa eneo moja kwa kuwa hayuko upande wa JM alipokataa JM asifanye kampeni kwakuwa muda bado, alipewa onyo kali kutoka juu, Je unazani kuna usawa hapa?
ii. Chama kinakataza mgombea yeyote kutoa hongo ama namna yoyote ya ushawishi wa kutimia pesa, vitu ama zawadi kwa wapiga kura wakati wa kujitangaza, kwani kwa kufanya hivyo mgombea anaweza akawadisqualified, katika kampeni za JM tayari ametoa pikipiki 3 jimboni, na amekuwa akitoa hela kwa wananchi kila sehemu anayokwenda ili kuwaomba wananchi wa mkubali, ameahidi vitu vingi na watekelezaji ni wajumbe wa CCM, je hili nalo hawajaona? au kwakuwa ni mtoto wa mzee?
iii. JM alipoenda kujitangaza jimboni alipewa kadi za CCM za uwanachama zaidi ya 8000, amabazo zimekabidhiwa bwana Mahanyu ili zigawiwe kwa wanachama wapya wa CCM ili ifikapo siku ya kula maoni wamchague yeye, je chama sikimekataza mgombea kudhamini kadi za wanachama kwa nia ua ushawishi? na hili je? je watoto wasio wa viongozi wana nafasi gani kwenye hili? je hapa panaweza kuwa na ushindani wa haki? au ni kwamba anapewa nafasi kwakutumia jina la baba yake...
najua kwenye hili kuna watakao taka kusema leta ushahidi kwakuwa wako tayari kutetea suala la JM kwa kuwa ni Smart na msomi, lakini pia JM katika maongezi yake mengi na wananchi analiweka mbele sana suala la yeye kuwa KARIBU na raisi kama ndio kigezo pekee kitkacho mpa yeye nafasi ya kuwaletea maendeleo jimboni humo, lakini watu wanahoji kama yeye ni mtu wa raisi kwanini raisi asisubiri akamteua kuwa mbunge kama kweli anamitaji kwenye balaza lake la mawaziri?
lazima tuache ushabiki pale kwenye ukweli na sio kila mtu anayekuwa anampinga JM anachuki binafsi naye, ila lazim ijulikane kwamba anatumia nafasi ya mzee wake tu kama daraja, na hata wapiga kmpeniwake ni watu w mzee makamba wa karibu na hata kwenye baadhi ya mikutano ya siri mzee makamba anahudhuriana kutoa maagizo kama yale ya kutaka mzee shekulamba atolewe kwnye kamati ya kampeni baada ya kuonekana hakubaliki kwenye eneo lake kwenye mkutnao wa morogoro......
labda mwisho niseme tu mwandishi yule alionyesha kana kwamba JM anakubalika sana jimboni kitu ambacho si kweli na hakuonyesha kwamba kuna upinzani wowote isipokuwa kutoka kwa shelukindo kitu ambacho si kweli, JM anapata upinzani mkubwa sana kutoka kwa wagombea wengine na sababu ambazo nimezipata ni kama ifuatavyo;
i. wapiga debe wa JM wengi hawakubaliki katika jamii, na mbaya zaidi ni kumtumia bwana mahanyu kama mpiga kampeni mkuu wakati akijua bwana mahanyu si mwenyeji wa jimbo lile, na hajulikani.
ii. wakati wa kugawa pesa kwa wananchi bwana JM hatofautishi viongozi na wananchi, zipo sehemu alitoa 3000(ngongoi na mgwashi) kwa kila mtu na sehemu hata 1000, viongozi wengi waliona kama ni dharau kwao(huu ni mtazamo wa viongozi wengi,maana natoa tu taarifa).
iii. kila alipotembelea maeneo mengi kwakuwa mwenyeji wake hajulikani basi amekuwa akikutanishwa na watu amabao wengine si viongozi na wazee wa eneo husika, kwa hiyo alijikuta akitumia pesa kuwapa walevi tu.
iv.........................ahhh basi,
IJULIKANE KWAMBA NIA YETU NI KUJENGA NA SI KUBOMOA WALA KUKOMOA.......NAWAKILISHA.....