CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

wewe hata wakati hii thread inaaza ulibisha kwamba JM hagombei ubunge, sasa hvi kila unachoambiwa unataka ushahidi wewe mbona hutoi ushahidi wa kubisha kwako.....unalazimsha hoja hii iwe ni chuki wa watoto wa wawakubwa....wivu....lazima pale tunapoona kuna mtu anataka kutake advantage ya nafasi yake ili kuwarubuni wananchi tuseme, mungu mkubwa wananchi wa bumbuli wameshaona rangi za january mapema, uongo, ulevi na dharau.....na wameapa kula pesa zake mpaka mwisho lakini ubunge hawampi.....na huwezi kubadilisha misemo ya busara kwamba mtoto wa nyoka ni nyoka....

na kama ukitaka ushahidi, fuatilia kampeni za JM jimboni, timu yake imeshaanza kuparaganyika hata kabla ya muda..

na mzee shelukndo ameshafika jimboni baada ya kusikia michezo michafu inaendelea....ngoja tufuatilie tuone haya mapambano yataishia wapi....

- Huruma sana ndugu Great Thinker!


Es!
 
I don't know much about the state of the opposition in Bumbuli, but I can tell you this much.As long as mbunge ni mmoja wa hawa top contenders wa CCM (January or Shelukindo) wananchi wameumia.
 
Tumjadili Januari kama mtu anayejitegemea,Hatutokuwa tunamtendea haki Januari kama tutakuwa tunamuhusisha na kauli za Baba yake (Mzee Yusuph).Januari ana haki kikatiba kugombea Ubunge!Tumpe ushirikiano kama mwenzetu baada ya kumkatisha tamaa.


Kauli za baba yake zitamuandama popote na kwa chochote atakachojaribu kufanya. Sasa kama Januari ana sifa, je mtoto wa fundi viatu ambaye baba yake Januari alisema atakufa akiwa fundi viatu yeye hana haki ya kugombea?

Sometimes we need to keep our mouth shut, if you open up your mouth, it means you're allowing everything to passthrough (domo la babake Januari)
 
haya ni baadhi ya maazimio ya mkutano mkuu wa ccm uliofanyika mwezi huu....

"Kufanya Kampeni kabla ya wakati
Kanuni za CCM zinaruhusu mwanachama kutangaza nia ya kugombea, hatas hivyo, Halmashauri Kuu ya Taifa , Imekemea vikali mwenendo wa baadhi ya wanachama wa CCM wanaowania kugombea Udiwani, Baraza la Wawakilishi na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa kuanza kutembea matawini na kwenye kata na kufanya kampeni kabla ya wakati.

Halmashauri Kuu ya Taifa imekumbusha kwamba Kanuni za Chama Cha Mapinduzi kuhusu uteuzi wa wagombea wa CCM katika vyombo vya dola hairuhusu mwanachama yeyote kufanya kampeni kabla ya ya wakati uliowekwa rasmi.

Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito mahsusi na imeziagiza kamati za Maadili na Kamati za Siasa za ngazi zote kudhibiti hivyo. CCM inatambua kuwa kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila mwanachama lakini ni lazima kila mwanachama azingatie utaratibu na kanuni zinazotawala shughuli za uchaguzi. CCM haitawavumilia wagombea watarajiwa wanaofanua fujo na vurugu kwa kuvunja kanuni katika kipindi hiki ambacho umakini unahitajika katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa imekemea vikali viongozi wanaofanya kazi ya udalali wa kuwatembeza matawini wagombea watarajiwa kwani viongozi hao nao wanavunja kanuni na wametakiwa kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.


nataka nione nini kitafanywa kwa wale wanaoendelea kumpigia kampeni JM jimboni bumbuli, na kuhusu pia mzee makamba kumnadi mmoja wa wagombea jimbo la korogwe, Je hizi kanuni ni kwa wote?

kwa wale wasio na taarifa ni kwamba wananchi wa Bumbuli wanaye mgombea wanayemtaka na ipo juhudi za kumuomba mzee shelukindo kumu-endorse kijana huyo kwakuwa anamfahamu na alishamkubali kabla, ipo timu ya wazee na wale wote waliomuunga mkono mwaka 2005 kutaka kumpelekea maombi maalum kujitoa na kumpa nafasi kijana wao, mzaliwa wa bumbuli, msomi na anayekubalika katika jamii. kitu kinachotoa matumaini ni kwamba kijana huyo ni mtoto wa swahiba wa karibu na mzee shelukindo, Mzee kaniki wa Soni.
kijana ameshatangaza nia yake jimboni na wananchi wengi wameonyesha kumuunga mkono, kwa hiyo upinzani zaidi unategemewa kuwa kati ya January na Kaniki.

tunatafuta wasifu wa kijana huyu ili tuuweke hazarani, ila kwa sasa ameonekana kumpa shida January kwakuwa timu kubwa ya January inatokea Soni ambako ndio kijana huyu amekulia na anakoishi, kwahiyo wajumbe wengi wanahusiana na kijana huyu na watu wa soni wameahidi kumpa support kijana huyu, ndio maana sasa timu ya Januari imevurugika kwakuwa wanashindwa pia kuwaamini wajumbe.

Taarifa zilizokuwepo ni kwamba hata mpiga debe mkuu wa Januari bwana Mahanyu anamkubali sana Kaniki na anajua upinzani aliosababisha kwa januari, inasemekana upo mpango wa kutaka kumuomba kaniki amuachie nafasi januari,tutafuatilia.

Pia wananchi wengi wa soni waliosoma gazeti la Tazama Tanzania la wiki iliyopita ambalo lilitoa habari ya bw Januari kama mgombea mpendwa jimbo la bumbuli limewasikitisha sana watu kwakuwa habari zilizopo kwenye habari ile nyingi ni za uongo, moja ni baadhi ya watu walioandikwa kwamba wametoa maoni kuyakana maoni yao, lakni ndio siasa na mapambano,

Ubunge at any cost, by any means.....
 
Hawa watoto wa viongozi wanapaswa kupigwa stop kuingia ktk siasa kipindi ambacho wazazi wao wapo madarakani ili kuweka taswira ya usawa.

Simuungi mkono huyo january makamba. namshauri atafute kazi aliyoisomea na si kuwakilisha wananchi. endapo hawa ccm wanarudisha uchifu kwa mlango wa nyuma basi na sisi tutazindua kampeni ya uchifu nchi nzima ili kurudisha enzi zileee za mababu zetu ambapo machifu walikuwepo na walikuwa na nguvu kweli kweli.

Tupinge kwa nguvu zote hizi kampeni za watoto wa vigogo. Na nyie mnaosema wana haki za kikatiba najua mnasema hivyo kwa kuwa mpo kwenye payrol zao hawa mafisadi watoto.
 
Yamekuwa yakijitokeza masuala mengi sana yanaohusishwa na mchakato wa uchaguzi wa ubunge ndani ya jimbo la Lushoto.....

Baada ya January Makamba kujitangaza kuwa yeye ndie aliyeandaliwa na kutumwa na raisi (mtu wake wa karibu)...tukasikia JK akitoa agizo kwamba hakuna aliyemtuma jimboni kugombea nafasi yoyote....

wakati JK anatoa agizo watu wakatangaze nia tu lakini wasipige kampeni....Jana January amekutana na wanachama wa CCM jimboini bumbuli ambao ndio wanaompigia kampeni na kuwaambia atakuwepo jimboni kw siku 3 kuzungukia jimbo na kuwatoa hofu wapiganaji wake kuwa wWASIOGOPA kumtangaza popote bila kificho, wawe huru kufanya kampeni popote jimboni kwa kujiamini....

wakati huohuo Mbunge aliyekosasa madarakani Mh. shelukindo, amewakilisha taarifa kwenye kamati ya siasa ya wilaya kumlalamika January kuhusu kufanya kampeni kabla ya wakati ikiwa ni pamoja na kumchafua, kulalamikia viongozi wa chama kumpigia kampeni za wazi bwana January kinyume na kanuni za chama, lakini taarifa hizo zimepuuzwa na hakuna hatua iliyochukuliwa.
cha kushangaza zaidi wakati mkutano wa kamati ya siasa ukiendelea na Bwana January alikuwa na mkutano wa kambi yake eneo hilohilo.....

kitendo cha viongozi wa chama kumpigia January Makamba kampeni kimekuja baada ya kupata agizo la Mh Yusuph Makamba, katibu mkuu wa CCM, kuagiza kijana wake apewe ushiikiano katika suala hilo na kuhakikisha yeye ndiye mbunge ajaye, suala hili pia limewagawa sana viongozi wa chama ndani ya jimbo, kwakuwa wale wasiomuunga mkono wamepokea vitisho, ikiwa ni pamoja kukosa nafasi zao walizokuwa nazo, tayri baadhi ya madiwani, makatibu wa kata wamepata onyo kwa kutokumuunga mkono kijana wa mzee.

Baadhi ya malalamiko mengi ni kwamba January amekua akifanya mikutano ya kampeni waziwazi na kugawa fedha kwa wananchi lakini hakuna anayemchukulia hatua, tayari ametoa vitu na vifaa mbalimbali katika maeneo ya jimbo na kuchangia baadhi ya shughuli kinyume na kanuni za chama.

1.Je hizi sheria na kanuni za chama ni kwa wote? au wapo waliojuu
2. Je usawa utakuwepo pale watakapo jitokeza wengine kugombea nafasi hiyo kama viongozi wa chama wanalazimisha JM awe ni chaguo la jimbo?

ukiacha hili la mwanae, Mzee Makamba anampigia mgombea mwingine kampeni jimboni korogwe waziwazi bila kujali kwamba anavunja kanuni za chama, na kwa haya yote watu walio karibu na JK wamesema amemwonya Mzee makamba aache kukivuruga chama.....


"Haki sawa kwa wote"
 
WanaCCM ndio waamuzi wa nani awe mgombea wakati wa kura ya maoni. Na wananchi ni waamuzi wakati wa uchaguzi. Haya masuala wakati karibia na uchaguzi huwa kiasi fulani yanachanganya, kuna kuchafuana, kutafuta huruma kwa wananchi nk. Lakini ni kweli chaguzi zetu hutawaliwa na rushwa, hilo sikatai. Na atakaye liondoa hilo ni sisi wananchi wenyewe, sasa kama unanunuliwa kwa muda, una umia miaka mitano akili iko wapi?.

Huyo Shelukindo mwenyewe sio msafi.
 
Taarifa zilizopo ni kwamba Bwana January Makamba amepata msiba wa bibi yake huko Bukoba na ameahirisha ziara yake jimboni bumbuli.
Tunampa Pole sana na kumtakia safari njema, japo kulikuwa na mabishano mwanzoni pale wananchi waliposema January si mzawa wa Bumbuli kama inavyodaiwa na baadhi wa watu kupinga sana suala hili wakati yeye mwenyewe ameweka wazi.
 
Back
Top Bottom