haya ni baadhi ya maazimio ya mkutano mkuu wa ccm uliofanyika mwezi huu....
"Kufanya Kampeni kabla ya wakati
Kanuni za CCM zinaruhusu mwanachama kutangaza nia ya kugombea, hatas hivyo, Halmashauri Kuu ya Taifa , Imekemea vikali mwenendo wa baadhi ya wanachama wa CCM wanaowania kugombea Udiwani, Baraza la Wawakilishi na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa kuanza kutembea matawini na kwenye kata na kufanya kampeni kabla ya wakati.
Halmashauri Kuu ya Taifa imekumbusha kwamba Kanuni za Chama Cha Mapinduzi kuhusu uteuzi wa wagombea wa CCM katika vyombo vya dola hairuhusu mwanachama yeyote kufanya kampeni kabla ya ya wakati uliowekwa rasmi.
Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito mahsusi na imeziagiza kamati za Maadili na Kamati za Siasa za ngazi zote kudhibiti hivyo. CCM inatambua kuwa kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila mwanachama lakini ni lazima kila mwanachama azingatie utaratibu na kanuni zinazotawala shughuli za uchaguzi. CCM haitawavumilia wagombea watarajiwa wanaofanua fujo na vurugu kwa kuvunja kanuni katika kipindi hiki ambacho umakini unahitajika katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa imekemea vikali viongozi wanaofanya kazi ya udalali wa kuwatembeza matawini wagombea watarajiwa kwani viongozi hao nao wanavunja kanuni na wametakiwa kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
nataka nione nini kitafanywa kwa wale wanaoendelea kumpigia kampeni JM jimboni bumbuli, na kuhusu pia mzee makamba kumnadi mmoja wa wagombea jimbo la korogwe, Je hizi kanuni ni kwa wote?
kwa wale wasio na taarifa ni kwamba wananchi wa Bumbuli wanaye mgombea wanayemtaka na ipo juhudi za kumuomba mzee shelukindo kumu-endorse kijana huyo kwakuwa anamfahamu na alishamkubali kabla, ipo timu ya wazee na wale wote waliomuunga mkono mwaka 2005 kutaka kumpelekea maombi maalum kujitoa na kumpa nafasi kijana wao, mzaliwa wa bumbuli, msomi na anayekubalika katika jamii. kitu kinachotoa matumaini ni kwamba kijana huyo ni mtoto wa swahiba wa karibu na mzee shelukindo, Mzee kaniki wa Soni.
kijana ameshatangaza nia yake jimboni na wananchi wengi wameonyesha kumuunga mkono, kwa hiyo upinzani zaidi unategemewa kuwa kati ya January na Kaniki.
tunatafuta wasifu wa kijana huyu ili tuuweke hazarani, ila kwa sasa ameonekana kumpa shida January kwakuwa timu kubwa ya January inatokea Soni ambako ndio kijana huyu amekulia na anakoishi, kwahiyo wajumbe wengi wanahusiana na kijana huyu na watu wa soni wameahidi kumpa support kijana huyu, ndio maana sasa timu ya Januari imevurugika kwakuwa wanashindwa pia kuwaamini wajumbe.
Taarifa zilizokuwepo ni kwamba hata mpiga debe mkuu wa Januari bwana Mahanyu anamkubali sana Kaniki na anajua upinzani aliosababisha kwa januari, inasemekana upo mpango wa kutaka kumuomba kaniki amuachie nafasi januari,tutafuatilia.
Pia wananchi wengi wa soni waliosoma gazeti la Tazama Tanzania la wiki iliyopita ambalo lilitoa habari ya bw Januari kama mgombea mpendwa jimbo la bumbuli limewasikitisha sana watu kwakuwa habari zilizopo kwenye habari ile nyingi ni za uongo, moja ni baadhi ya watu walioandikwa kwamba wametoa maoni kuyakana maoni yao, lakni ndio siasa na mapambano,
Ubunge at any cost, by any means.....