Kwa mfano hadi sasa sasa kwenye articles zenu zote za kumtetea Kijana January bado hujanionyesha kwenye nafasi yake kama mshauri wa Rais wa Jamhuri wa TZ kafanya nini kuwaletea maisha bora watz
January atuambie,kwa nafasi yake ya ushauri wa Rais kawafanyia nini watz?Haya maneno kama ni modern intelluctual wa chuo maarufu USA haina uhusiano wa kuja kuwa effective kuwahudumia watz kwani hata Chenge au Balal nao walisoma vyuo maarufu USA!
Tunataka rekodi ya uchapa kazi wa January Makamba kama mshauri wa Rais kwa miaka hii 5 ya utumishi wake,lkn hivi hivi kwa maneno yenu akina Game Theory na FMEs "sidanganyiki ng'o"
.
Mkuu Malafyale,
Sio kwa niko upande wa kumtetea Januari, bali kukumegea kipande kidogo tuu cha professionalism ya kazi ya mshauri, advisor. Mshauri anatoa ushauri kwa mhusika under fidushiary relationship kama ilivyo kwa daktari na mgonjwa, baba na mwana, mwalimu na mwanafunzi, wakili na mteja etc. Kipimo cha uzuri ama efectiveness ni kwenye end results kwa aliyehudumiwa. Hivyo Jan kama mshauri wa Kikwete, hawajibiki kukueleza mimi wewe na sisi amemshauri nini JK, wala si mimi wewe au sisi tunaoweza kuupima ushauri wake zaidi ya JK mwenyewe. Hivyo please don't waste time kuuliza ameshauri nini au kafanya nini, its on the shoulders za mshauriwa.
Ukienda kwa daktari ukasema unaumwa, unachoumwa ni siri yako na daktari wako, atakuambia unachoumwa na atakutibia, ukipona wewe ndio utajua wasifu wa daktari huyo na utamrecomend kwa wengine, usipopona, utatafuta daktari mwingine kuendelea kuhangaika.
Vivyo hivyo kwa wakili, mtenda ana uhuru hadi kumweleza wakili kuwa ni kweli aliuwa na jinsi alivyouwa, na bado wakili akamshauri a plead not guilty na kumtetea. Hawajibiki kusema ukweli wowote, ni siri na kuaminiana.
Bahati nzuri kijana simfahamu zaidi ya kumsoma, kama ilivyo kwa Nape, the guy seems smart. Huhitaji kujua Zitto amewafanyia nini Kigoma kujua he is briliant, hivi kabla hajaingia bungeni, alifanya nini kustahili kuchaguliwa.c
Hoja ya msingi ni kila mtu ahukumiwe on his own merit na sio kwa sababu ya jina la baba yake japo jina kisiasa ni mtaji sometimes jina hilo hilo linaweza lisiwe mtaji, bali liability.
Nape, Ridhwan, January etc wanasimama wenyewe kwa merits zao wenyewe regadless ni watoto wa nani, naomba tuwahukumu wao kama wao na sio kwa majina ya baba zao.