CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

Personal sidhani kama tunamtendea haki January na uamuzi wake wa kimaisha hana haki ya kuchagua mwongozo wake wa kimaisha if he has political ambitous let it be. Na lisiwe jukumu letu kuwakatisha wengine tamaa its none of our business honestly with other choices in life.

Lakini vilevile again mimi personal najiuliza iweje huyu January aende huko wakati tayari kuna mmbunge wa chama ambacho yeye anategemea kupata ticket ya kugombea CCM.

Swali je Shelukindo katamka kwamba uchaguzi ujao basi tena agombei au ndio wanaleta utemi wa kumtoa mbunge wao kichama kwa sababu asimamii ulafi wanao u-support CCM.

Hapo ndipo tunapo question abuse of power from IKULU kuingilia siasa za chini kwa uonevu; hivyo hata iletwe CV gani ya huyu bwana au his highest IQ scores still atakua criticised kwa namna ya mfumo unaotaka kumuinua kisiasa.

Hapo ndipo tatizo lilipo ubabe wa viongozi wajuu CCM na wala Januari sio tatizo. Tuseme mtu wa kawaida anaweza kwenda ruhusiwa ku-challenge jimbo kama la Rosta au fisadi mwingine yeyote kwa ticket ya CCM na viongozi wajuu kutoka chama wakatoa ruhusa hizi.

Kama aiwezekani why iwe special case kwa Januari huko Bumbuli aruhusiwe kumuingilia mbunge wa chama chake na kum-challenge kiti. Hivyo hii inatufanya tuone this January is not an ethical man at all kwa kuikubali hii challenge in the first place; therefore he is just another fisadi in the making.

You can fool some people sometimes but you cant fool people all the time.
 
- M-Tanzania yoyote anaruhusiwa kugombea anything, ndio maana Shibuda anagombea urais, uoga wa watu sio muongozo wa CCM, ni simply uoga wa watu tu na it has nothing to do na CCM kama chama wala Ikulu!

es!
 
Mkuu Malafyale,
Sio kwa niko upande wa kumtetea Januari, bali kukumegea kipande kidogo tuu cha professionalism ya kazi ya mshauri, advisor. Mshauri anatoa ushauri kwa mhusika under fidushiary relationship kama ilivyo kwa daktari na mgonjwa, baba na mwana, mwalimu na mwanafunzi, wakili na mteja etc. Kipimo cha uzuri ama efectiveness ni kwenye end results kwa aliyehudumiwa. Hivyo Jan kama mshauri wa Kikwete, hawajibiki kukueleza mimi wewe na sisi amemshauri nini JK, wala si mimi wewe au sisi tunaoweza kuupima ushauri wake zaidi ya JK mwenyewe. Hivyo please don't waste time kuuliza ameshauri nini au kafanya nini, its on the shoulders za mshauriwa.
mnaomtetea Januari, je jamaa ni mshauri au la.
- Kuna wasaidizi na washauri, sasa ni vyema kwenye ishu kama hii a Great Thinker ukawa makini katika kuchanganua nani ni nani among wasaidizi wa Rais, maana politically wasaidizi wa Rais ina-cover eneo kubwa sana, mpaka mawaziri wote ni wasaidizi wa Rais,

- Kama Rais ameharibu uchumi anaye mshauri wa uchumi, mshauri wa nje, mshauri wa utawala Januari ni personal asisstant, sio anything else!

Respect.

FMEs!

sifa ambayo mimi nimeisikia ambayo watu wengi wakimsifia ni moja tu kwamba yeye ni kijana so does masha, ngeleja and nchimbi.

sifa za Januari kiutendaji ni zipi, shule nzuri hata chenge ameenda shule kubwa...
 
FMEs na Libaba sasa mnatoka nje ya mada,kumbukeni mada husika ni kuhusu January Makamba na uamuzi wake wa kugombea jimbo la Bumbuli,lkn nyie sasa mmeigeuza mada na kuanza "person attacks"

My summarization;nakubaliana kabisa na Game Theory na FMEs kwenye kipengele ndani ya katiba kinachosema kuwa"kugombea Ubunge kwa kila mtz mwenye umri wa miaka 18 ni haki yake ya msingi na ya kikatiba",na kwa vile January katimiza kigezo hicho hamna wa kumzuia!

Lkn napingana na nyie akina FMEs kwenye ubora wa January akija kuwa mbunge wa Jamhuri ya TZ,kwa vile hajafanya lolote la maana kwenye nafasi yake kama camp-de-aide wa Rais JK,je atafanya nini jipya akija kuwa Mbunge?huo ndiyo wasi wasi wangu!

Anyways tuwaachie wana Bumbuli wenyewe waamue nani anafaa kuwa Mbunge wao!Ila kwangu January ni another CCM's failure candidate maana kwa miaka 5 sasa akiwa pale kama msaidizi wa Rais sijaona hicho alichomsadia!
 
Jamani, naomba tuwe objective kidogo!!

Mimi nadhani kwenye masuala ya kugombea kura kutoka kwa wananchi, kila MTanzania mwenye sifa kamili, agombee.

wananchi wa jimbo huko Bumbuli ndio wenye say ya mwisho, kwa hiyo sioni tatizo la January kugombea, kwa sababu ni lazima aende kwa wananchi na kushinda kwanza kura za maoni, then apitishwe na NEC ya CCM, halafu tena wananchi wamchague na ndio awe mbunge.

Kama ana mapungufu, si wananchi wataamua?? Kama Mbunge Shelukindo amefanya mazuri kwa wananchi wake si watamchagua tena??

Hapa ni ridhaa ya wananchi, na mgombeaji afanye atakavyofanya kwa kufuata sheria ili achaguliewe FULL STOP.

Ingawaje sikubaliani na mambo mengi anayofanya JK na Ikulu yake, lakini kwenye hili nampa props January kama atagombea ubunge kwa njia hii, sababu ni very easy kusubiri ubunge wa kuteuliwa na rais kama ni kweli rais anataka kumpa uwaziri.
 
FMEs na Libaba sasa mnatoka nje ya mada,kumbukeni mada husika ni kuhusu January Makamba na uamuzi wake wa kugombea jimbo la Bumbuli,lkn nyie sasa mmeigeuza mada na kuanza "person attacks"

- Mkuu heshima yako sana, haya ni mapambano ya fikra, na sisi ni kawaida yetu kujibu mashambulizi katika kusimamia hoja zetu, ingawa wanatumia kila njia kutuvuruga huwa hatubabaiki tunasimama kwenye hoja bila kuogopa anything!

- Ninachosimamia hapa ni hoja yangu kwamba Januari ana haki zote kama raia wa Tanzania kugombea ubunge wa jimbo lolote la Tanzania bila kubaguliwa kwa sababu ya baba yake, wala kazi yake ya ukaribu na Rais. Na ninaamini kwamba ana uwezo wa kuongoza kwa sababu record yake iko wazi nimeiweka hapo nyuma na besides kuwepo kwake karibu sana na Rais, kunampa an edge ya uongozi hasa wa taifa kutokana kushudia kwake ishus muhimu za taifa zikiamuliwa na huko Ikulu kila siku ya Mungu.

- Kama mimi ni mpiga kura wa Bumbuli nitaweka maanani sana wasifu wa Januari na hasa ukaribu wake na Rais kikazi.

My summarization;nakubaliana kabisa na Game Theory na FMEs kwenye kipengele ndani ya katiba kinachosema kuwa"kugombea Ubunge kwa kila mtz mwenye umri wa miaka 18 ni haki yake ya msingi na ya kikatiba",na kwa vile January katimiza kigezo hicho hamna wa kumzuia!

- Sawa sawa mkuu tupo pamoja sana hapo!

Lkn napingana na nyie akina FMEs kwenye ubora wa January akija kuwa mbunge wa Jamhuri ya TZ,kwa vile hajafanya lolote la maana kwenye nafasi yake kama camp-de-aide wa Rais JK,je atafanya nini jipya akija kuwa Mbunge?huo ndiyo wasi wasi wangu!
Anyways tuwaachie wana Bumbuli wenyewe waamue nani anafaa kuwa Mbunge wao!Ila kwangu January ni another CCM's failure candidate maana kwa miaka 5 sasa akiwa pale kama msaidizi wa Rais sijaona hicho alichomsadia!
- Mkuu historia ya taifa on uongozi hasa ubunge iko wazi sana, sasa labda ungeweka wazi wabunge unaoamini wameweza kazi hiyo kutokana na experience waliyokuwa nayo kabla ya kushika ubunge, na yote waliyoyafanya mazuri kwa wananchi wao na taifa, then ndio utakuwa na ubavu wa kuuliza experience za Januari,

- Otherwise, ubunge ni open kwa mwananchi yoyote yule kugombea na kujifunza kazi akiwa kazini, I mean kwa mantiki yako basi vijana wote wasiruhusiwe kugombea maana hawana experience, hapana mkuu Januari amesoma sana kwa umri alionao, na kazi zake za kila siku, licha ya kutokea kwenye familia ya uongozi wa taifa, inatosha sana kumfanya akawa na uwezo mkubwa sana kiuongozi na hasa the fact kwamba ameamua kuachana na kazi za Ikulu na kwenda kuji-establish independently sio vijana wote wanaweza kufikiri namna hiyo, wengi wetu tungelilia kufia Ikulu.

- Sometimes JF tunakuwa very contradicting, maana one minute tunasema tunataka viongozi vijana, the next minute hatutaki kuongozwa na wananchi vijana ambao ni watoto wa viongozi, sasa one wonders exactly what is our stand? Kwamba watoto wa masikini ndio wenye uwezo wa kuongoza then kwa nini tumekwama as a nation? I mean Rostam, Lowassa, Ngeleja, na Serukamba baba zao waliwahi kuongoza wapi? Sasa kama baba zao walikuwa ni wananchi wa kawaida then why tumekwama?

- Ndio tunaihisa kuamini kwamba kuna tabia ya wivu na chuki za binafsi kutokana na maendeleo ya watoto wa viongozi walioamua kupigana na kuwa independent na kazi za wazazi wao, I mean dakika moja hatutaki viongozi wazee, dakika ya pili hatutaki viongozi vijana watoto wa viongozi, sasa unaona hii hatred where do you draw the line na ksuema hapa sasa basi? the next thig tutasema hatutaki viongozi wanawake, sijui kesho tutaibuka na nini?

- Kama kweli mkuu unataka ku-predict Januari atakwua kiongozi wa namna gani akiwa mbunge, then jaribu kuweka wazi hapa sifa wabunge wazuri unaowajua, walizokuwa nazo kabla ya kushiika ubunge, ndio Great Thinkers wanatakiwa kujadili na facts, badala ya wasi wasi bila facts!

Respect.

FMEs!
 
Ingawaje sikubaliani na mambo mengi anayofanya JK na Ikulu yake, lakini kwenye hili nampa props January kama atagombea ubunge kwa njia hii, sababu ni very easy kusubiri ubunge wa kuteuliwa na rais kama ni kweli rais anataka kumpa uwaziri.

Unampa props pia kwa kwenda kugawa vyerehani ili kujijengea political capital? Una endorse hizo njia za kifisadi za kujikusanyia 'mtaji wa kisiasa'?
 
- Sasa tunarudia pale pale, yaani hukumu bila facts, tuwekeeni facts za Januari kugawa hivyo vitu na besides kwani sheria inasema nini kuhusu mgombea ubunge kugawa Takrima?

es!
 
Unampa props pia kwa kwenda kugawa vyerehani ili kujijengea political capital? Una endorse hizo njia za kifisadi za kujikusanyia 'mtaji wa kisiasa'?

Vyerehani vinamsaidia nani jamani?? Kutwa tuko hapa tunapiga kelele umaskini ulioko uko vijijini, sasa unataka mtu apeleke vyerehani kijijini mimi nimseme vibaya?? Hapana mkuu, mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro, na tunahamasisha sana watu kupeleka misaada huko kijijini.

Kama wanakijiji wakiona mtoa vyerehani ndio mkombozi wao, siwezi kuwapinga wanachokitaka.

Mbunge aliyepo posho anazopata na yeye si akatoe mashine za kusaga nafaka, power tillers n.k. ndio kumkomboa mwananchi hivyo.

Kamam January angekuwa anakwenda kupambana na mtoto wa maskini huko kijijini ningeweza kubadili mawazo yangu kwenye hili la kutoa misaada, lakini anapambana na mwenyekiti wa kamati moja ya bunge na mbunge wa muda mrefu, kwa hiyo hapa mimi sioni tabu maana kwa kawaida kama mbunge wa jimbo umefanya uliyotakiwa kufanya kwa kuwa mbunge zaidi ya miaka 10, HUNA LA KUOGOPA na kuondolewa ni kazi sana.

Halafu kwa upande wa CCM, nashangaa sana wabunge wanaolalamika kuwa kuna watu wanatembeza pesa kuwangoa. CCM imebadili taratibu za kupata wagombeaji huko majimboni, na kura za maoni safari hii zitapigwa na wananchi wa jimbo zima. Sasa kweli mtu anaweza kuonga jimbo zima mbunge uliyefanya kazi yako kwa ufanisi utolewe?? Hapana, mimi nasema mbunge aliyefanya kazi ipasavyo na aliyekaribu na wananchi , anatakiwa akaribishe wagombeaji wengi wa aina hii ili jimbo linufaike na yeye ni kiasi cha kuwaeleza vizuri wananchi wake na kama anakubalika atapeta tu.

Disclaimer:: I'm not endorsing anyone in this jimbo even though I'm a little bit biased towards the new generation.
 
Haya bana naona watu mna condone tabia za kifisadi fisadi in the name of misaada vijijini. Hamjiulizi watu wanatoa wapi hizo hela za kununulia vitu vyote hivyo. Oh well...it is what it is....kwanza sisi wengine si wabongo tena wala nini. Mtajiju....
 
Msaada miaka yote watu hawajatoa mpaka 2010, huoni kwamba msaada una jambo huu?
 
- Mkuu Moelex, saafi sana, mimi ninaomba mtu mmoja hapa amtaje mbunge mmoja tu, wa kuchaguliwa na wanachi ambaye hajawahi kutoa hata senti moja kwa wananchi katika kugombea ubunge wa jimbo na akawa mbunge anyways? Mention just one!

Respect.

FMEs!
 
JM kutoa misaada kwao kuna shida gani jamani?...........cha msingi kujiuliza ni kama nguvu/juhudi hiyo ni yake kihalali.........

Sitegemei mshikaji wangu afanye "BIASHARA YA MANYANI"........hii simulizi kama sikosei ilitolewa na Mwanakijiji.............
 
- Lakini ithibitishwe kwanza kama ni kweli ametoa, maana so far ni speculation tu! au?

Respect.

FMEs!
 
Tumjadili Januari kama mtu anayejitegemea,Hatutokuwa tunamtendea haki Januari kama tutakuwa tunamuhusisha na kauli za Baba yake (Mzee Yusuph).Januari ana haki kikatiba kugombea Ubunge!Tumpe ushirikiano kama mwenzetu baada ya kumkatisha tamaa.

- Duh! hoja nzito sana, saafi sana Mkulu Mwawado, tupo pamoja sana hapo!

Respect.

FMEs!
 
Haya bana naona watu mna condone tabia za kifisadi fisadi in the name of misaada vijijini. Hamjiulizi watu wanatoa wapi hizo hela za kununulia vitu vyote hivyo. Oh well...it is what it is....kwanza sisi wengine si wabongo tena wala nini. Mtajiju....

- Duh! very interesting!

es!
 
- Lakini ithibitishwe kwanza kama ni kweli ametoa, maana so far ni speculation tu! au?

Respect.

FMEs!

....ikithibitika kivyovyote vile then what?..........

awe ametoa au hajatoa au yuko mbioni kutoa au ana idea ya kutoa.........the point is.........kuna ubaya gani?....mana hapa ndio mjadala unaendelea hivo..........hata akigombea huo ubunge Bumbuli kuna ubaya gani?..........
 
- Mkuu Moelex, saafi sana, mimi ninaomba mtu mmoja hapa amtaje mbunge mmoja tu, wa kuchaguliwa na wanachi ambaye hajawahi kutoa hata senti moja kwa wananchi katika kugombea ubunge wa jimbo na akawa mbunge anyways? Mention just one!

Respect.

FMEs!

You are totally missing the point.

Kitu kibaya, hata kama kinafanywa na wabunge wote kama unavyotaka ku justify, hakibadiliki kuwa kizuri kwa sababu eti kinafanywa na wabunge wote. Kama wagombea ubunge wote wakiwa wanaua, kuloga au kutoa rushwa hili halitafanya kuua, kuloga au kutoa rushwa kwa January kuwe any less an offense.

Two wrongs do not make a right.

Hiyo post yako inakuonyesha kama populist bendera kufuata upepo asiye na principles, kama wale 70% aliowasema muungwana. Eti nitajie mbunge mmoja, kwa hiyo kama hamna mbunge hata mmoja asiyetoa rushwa ndiyo huyu messiah wenu January Makamba asisemwe akitoa rushwa? Si mnasema ndio vijana hawa wanaotuletea mabadiliko tunayohitaji, mabadiliko yenyewe ndiyo kukumbatia rushwa ile ile?

Ndiyo maana nilisema January Makamba = More of the same.

It seems simple logic is not so simple.
 
Kwa mtazamo wangu, bwana January, ana haki ya kujitokeza kugombea chochote kifaacho kugombewa kwa misingi ya katiba yetu. Ila kusema kama anafaa au hafai, nafikiri wana-Bumbuli waachiwe uamuzi huo, manake sie tutaishia kupiga makelele tu yanayopitiliza masikioni.
Mimi natamani sana kama somo la uraia lingekuwa limepita kwenye vichochoro vya kila kona ya Tanzania yetu, hapo ningesema angalau waTZ tutakuwa tunaongea lugha moja kwenye maeneo fulani. Kwa sababu hizi 'analytics' zinazofanyika hapa jamvini kuhusu uwezo wa viongozi wetu kwenye nyadhifa tunazowabebesha laiti hata robo yake ingekuwa inaeleweka na wananchi wapiga kura, basi hata kura moja tu ya mtu ingekuwa ina tofauti kubwa sana kwenye chaguzi zetu. Sasa hivi vitenge, chumvi na tshirt can make a huge difference kwenye chaguzi zetu.....
 
Back
Top Bottom