CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

Kwa mtazamo wangu, bwana January, ana haki ya kujitokeza kugombea chochote kifaacho kugombewa kwa misingi ya katiba yetu. Ila kusema kama anafaa au hafai, nafikiri wana-Bumbuli waachiwe uamuzi huo, manake sie tutaishia kupiga makelele tu yanayopitiliza masikioni.
Mimi natamani sana kama somo la uraia lingekuwa limepita kwenye vichochoro vya kila kona ya Tanzania yetu, hapo ningesema angalau waTZ tutakuwa tunaongea lugha moja kwenye maeneo fulani. Kwa sababu hizi 'analytics' zinazofanyika hapa jamvini kuhusu uwezo wa viongozi wetu kwenye nyadhifa tunazowabebesha laiti hata robo yake ingekuwa inaeleweka na wananchi wapiga kura, basi hata kura moja tu ya mtu ingekuwa ina tofauti kubwa sana kwenye chaguzi zetu. Sasa hivi vitenge, chumvi na tshirt can make a huge difference kwenye chaguzi zetu.....

Which makes it even more crucial, not less so, that we discuss these issues in detail and depth.

Kuna watu wanataka kutuambia kwa sababu mtu ana haki kikatiba na ni kijana tu basi anafaa, hata kama hana nia ya kuleta maendeleo kama alivyothibitisha kwa kauli zake majununi za "Watanzania ni nzi wala mavi".

Huyu huyu mjinga mjinga ndiye aliyetoa kauli zilizotaka kuleta diplomatic row na Wa-Nigeria katika jitihada zake za kitoto kujikomba kwa waarabu na JK alipoenda na muungwana Saudi Arabia.

Wakazi wa Bumbuli wakimchagua huyu watakuwa wameuziwa kanyaboya.
 
tatizo ni kuwa mleta habari hana facts za what really went on on the ground

pili if anything huyo bwana aliyempa taarifa hakumpa picha kamili na btw mtoa taarifa naye ni member humu jf lakini nashangaa imekuwaje yeye hakuleta habari bali kaamua kumtumia huyu bwana azilete na matokeo yake ni haya ambayo ni half cooked innuendos

maana mwanzo nilifikiri mwanzisha thread ana matatizo ya cherry picking, lakini baadae nikagundui actually its a sign of stupidity, since it is deliberate. It is a sign of dishonesty & na naona hata nyie mmeingia kwenye mkumbo huu wa ku cherry pick even from the quotes he took from points he is attacking...lakini hii ndio home of great thinkers who cant even think straight!

cha ajabu mleta habari hajasema jinsi jm alivyokuwa mobbed kila alipokwenda,na sehemu zingine jm kaenda kwa kualikwa.

mzee naona umeamua kumtetea jm mpaka tone lako la mwisho la damu, wewe unasema jm kaenda kusalimia ndugu zake na hakwenda kwa ufanya kampeni, sasa unasema amealikwa, na nani, wapi? Punguza ushabiki....

pili so cliche kudai kuwa jm katoa jezi za mpira ili hali ukweli ni kuwa hakuzitoa! The so called jezi kwa hiyo hii habari kuwa jm alitoa jezi ni utunzi na mtunzi inaelekea aliskip hata darasa la kiswahili let alone la utunzi!

jezi za jm vijana wamezikataa.

tatu: Jm hakuwahi kuchangia taasisi yoyote ile hiyo 100,000 na hakuwa na kikao na taasisi yoyote ile ya kiislam

jm amechangia ujenzi wa shule shs 100,000 kabla hata hajaenda na siku alipoika alitaka kuitembelea ile shule wa kuomba mwenyewe ufanya hivyo lakini wadau walimsubiri hakutokea bila taarfa yoyote...namba ya mkuu wa shule 0717027490
nne: Narudia tena mleta habari kadai kuwa mzee mkamba aliwahi kumpigia debe jm ukweli ni kuwa hakuwahi kufanya hivyo na mbaya zaidi sisi watu wa mwambao tunajuana kwa hulka zetu na the same applies to watu wa pwani na kwa jinsi sie watu wa bwambao tunavyowajua wasambaa walivyo na tabia zao, they dont protest kwa kutimua watu, bali they just listen to you without a response!

wewe sijui una interest gani na hili swala, hapa jf kulikuwa na thread inayomhusu mzee makamba kwenda kuwapigia debe watoto wake na kiongozi mmoja wa kata ya mbeleibwana ndege alimkemea mpaka kwenye vyomba vya habari....i ask myself what is your motive? Mbona unapinga hata yaliyo wazi kwa hoja changa...

tano you will have to be so stupid ku pursue nafasi ya uongozi kwa kudai eti umetumwa na mtu na in jm's case eti katumwa na jk! Jambo ambalo si kweli na maanayake ni kwamba there is nothing you stand for!

baada ya jm kupewa nafasi ya kuongea pale msikitini aliwaambia nini wananchi,kama mimi unaona natunga basi namba ya diwani wa soni hii hapa alikuwepo 0784400267.....

haya bwana..
 
Huu mjadala umefika mahali umepotosha na fm na gt kwa ushabiki na unazi wao na mapenzi kwa ndugu yao jm, imefika hatua wanapinga hata yale ambayo jm mwenyewe amefanya...hii ni hatari sana.

Lakini lazima tujue hapa kwamba, hakuna anayesema jm hafai kuwa mbunge au hana sifa za kuchaguliwa na wana bumbuli, anazo kila haki na ninasimamia kila taarifa niliyoifikisha hapa katika mzunguko wa bwana jm, kwa kweli hata mimi ningependa vijana tujitokeze kwa wingi sana ili kuleta mabadiliko, lakini kwa hili la jm lina mapungufu yafuatayo;

1. Anatumia ukaribu wake na raisi kujinadi kwamba ndio itakuwa sababu ya yeye kuwasaidia wananchi, na kuthubutu kusema ametumwa na raisi achukue jimbo, lakni kama raisi anamuhitaji sana anaweza hata kumteua, na hata alipoomba kuwasalimia wananchi pale soni kubwa ni hilo kwamba yey yupo sana karibu na raisi wa nchi....hata mh shelukindo aliwahi kujiita kibonyezo, kwamba naye yupo sana karibu na "jikoni"
2. January ameenda kujinadi na kujitambulisha akijua kanuni za chama haziruhusu na huu si muda muafaka, na akitambua kwamba yupo mbunge ambaye hajamaliza muda wake.

3. Kitendo cha jm kutumia nguvu ya pesa kutafuta kuungwa mkono ni kufanya wale wengine wasiokuwa na uwezo washindwe kujitokeza kwakuwa yeye ana nguvu ya pesa kutoka different sources, je watoto wa wakulima ambao wanauwezo wana nafasi gani?
Na kwanini jm atumie pesa wakati yeye kama tunavyosema ni smart na huko bumbuli ndio anakotokea na hata baba yake pia ndio kwao...

4.tunataka fair competition katika harakati hizi, jm atumie elimu yake na uzoefu wake kuwaomba wananchi wa bumbuli kura zao wakati itakapo wadia sio kuanza kutoa hongo za chinichini....

Ila hii ni kwa gt na fm, nipo tayari kuweka rehani maisha yangu nawahakikishia january makamba hawezi na hataweza kuchukua jimbo la bumbuli, nyinyi mnajua upinzani anaopata huko anakopita, sehemu anazozomewa...kwa kifupi haungwi mkono na kumbuka kwamba nyoka hazai jongoo....alwayz like father like son....

Ushauri wa bure kwa jm.....just pull out...tumia busara chambua na fikiria kuhusu safari yako ilivyokuwa na jaribu kuona inakupa matumaini gani.
 
You are totally missing the point.

Kitu kibaya, hata kama kinafanywa na wabunge wote kama unavyotaka ku justify, hakibadiliki kuwa kizuri kwa sababu eti kinafanywa na wabunge wote. Kama wagombea ubunge wote wakiwa wanaua, kuloga au kutoa rushwa hili halitafanya kuua, kuloga au kutoa rushwa kwa January kuwe any less an offense.

Two wrongs do not make a right.

Hiyo post yako inakuonyesha kama populist bendera kufuata upepo asiye na principles, kama wale 70% aliowasema muungwana. Eti nitajie mbunge mmoja, kwa hiyo kama hamna mbunge hata mmoja asiyetoa rushwa ndiyo huyu messiah wenu January Makamba asisemwe akitoa rushwa? Si mnasema ndio vijana hawa wanaotuletea mabadiliko tunayohitaji, mabadiliko yenyewe ndiyo kukumbatia rushwa ile ile?

Ndiyo maana nilisema January Makamba = More of the same.

It seems simple logic is not so simple.

- Ninafikiri uwezo mdogo sana ulio nao wa kuelewa ndio unakusumbua, mwanachi yoyote mwenye uwezo wa kusaidia wanachi anaotaka kuwaongoza, anayo haki ya kuwapatia anything hakuna sheria ya jamnuri inayokataza hilo, sasa utawaendeleza vipi wananchi unaotaka kuwasidia kama huwezi hata kutoa vyarahani wakajishonea nguo zao?

- Sasa kama Januari ana uwezo wa kugawia wananchi wa jimbo lake vyarahani asigawe kwa sababu eti ni mtoto wa Makamba amesoma na ni kijana mdogo? Unaelewa maana ya rushwa au unabahatisha tu?

- Wewe umewahi kuniona mimi nikija hapa JF kufuata mikumbo, huyu kijana anakuzidi sana mkuu na anao uwezo wa kuwa mbunge, tumeona magarasha mangapi kutoka huko Tanga yakiingia bungeni kulala tu usingizi, sasa vijana wanataka kuingia mnaanza wivu na majungu, hebu peleka huko muacheni kijana huyu awape mawazo mapya huko Tanga!

Es!
 
..January ana haki ya kugombea ubunge popote pale Tanzania kama ilivyo kwa mimi na wewe.

..I am assuming kwamba atagombea kupitia CCM.

..ninachopenda kujua ni kwamba huko CCM January yuko ktk kundi la CCM-mafisadi au CCM-wapiganaji? hakuna aliye-neutral ndani ya CCM.

..pia si vibaya kwa January kutoa misaada huko Bumbuli. lakini pia ni vizuri tukajua vyanzo vya fedha za misaada hiyo. je, ni fedha zake za mfukoni? je, ni fedha toka kwa wachangiaji ambao ni safi? je, ni fedha za mafisadi?
 
Huu mjadala umefika mahali umepotosha na fm na gt kwa ushabiki na unazi wao na mapenzi kwa ndugu yao jm, imefika hatua wanapinga hata yale ambayo jm mwenyewe amefanya...hii ni hatari sana.

- Huu mjadala umeuleta kwa nia ya kuharibu jina la huyu kijana na ni kawaida yako kuwachukia vijana wote ambao wazazi wao ni viongozi, ndio maana tunajaribu kukuelimisha kwamba watoto wa viongozi ni wananchi wa Tanzania kama wengine wote na wana haki za anything affordable by our laws kwa kila raia wake.

Lakini lazima tujue hapa kwamba, hakuna anayesema jm hafai kuwa mbunge au hana sifa za kuchaguliwa na wana bumbuli, anazo kila haki na ninasimamia kila taarifa niliyoifikisha hapa katika mzunguko wa bwana jm, kwa kweli hata mimi ningependa vijana tujitokeze kwa wingi sana ili kuleta mabadiliko, lakini kwa hili la jm lina mapungufu yafuatayo;

- Sasa tizama, huyu kijana hajawahi kuwa kiongozi Tanzania, sasa hayo unayoyaita mapungufu wewe umeyapata wapi? kama sio majungu wivu chuki na fitina?

1. Anatumia ukaribu wake na raisi kujinadi kwamba ndio itakuwa sababu ya yeye kuwasaidia wananchi, na kuthubutu kusema ametumwa na raisi achukue jimbo, kwamba yey yupo sana karibu na raisi wa nchi..

- Either yupo karibu na Rais au hayupo, na kama unajua siasa basi ulipaswa kujua kwamba katika siasa za taifa anything ambacho ni Symbolic Nationally karibu yako ni muhimu sana katika kujinadi mbele ya public, ndio maana kule US kila siku politicians wanasema walikuwa karibu na Reagan, au JFK, kama ulikuwa huelewi hiyo ni kawaida sana kwenye kampeni za siasa.

- Januari yupo karibu na Rais ni fact, amemtuma au hakumtuma ni wajibu wa Rais kukanusha lakini kama Januari amesema kweli (which I doubt) lazima Rais amesikia, sasa kama hahusiki basi anatakiwa kukanusha asipokanusha ni kweli ndio siasa za taifa zilivyo mkuu kama ulikuwa huelewi.

2. January ameenda kujinadi na kujitambulisha akijua kanuni za chama haziruhusu na huu si muda muafaka, na akitambua kwamba yupo mbunge ambaye hajamaliza muda wake.

- Hilo ni tatizo la chama chake, ingawa kwenye kichwa chako cha mada hukusema kama anagombea chama gani, sasa unaona tunaposema kwamba una majungu, wivu, chuki na fitina kwa sababu kama hili ni tatizo ni chama chake ndio kinawahusu sio wewe, hayakuhusu haya na hayana anything to do na uwezo wake wa uongozi!

3. Kitendo cha jm kutumia nguvu ya pesa kutafuta kuungwa mkono ni kufanya wale wengine wasiokuwa na uwezo washindwe kujitokeza kwakuwa yeye ana nguvu ya pesa kutoka different sources, je watoto wa wakulima ambao wanauwezo wana nafasi gani?
Na kwanini jm atumie pesa wakati yeye kama tunavyosema ni smart na huko bumbuli ndio anakotokea na hata baba yake pia ndio kwao...

- Januari anao uwezo wa kipesa sio kwa sababu ni mtoto wa Makamba, na pili yeye kuwa na uwezo wa kipesa sio kosa la kisheria, pili kuwapa misaada wananchi anaotaka kuwasaidia sio kuvunja sheria, kuwa au kutokuwa na pesa sio tatizo la mtoto wa Makamba au wa mkulima, haya ndio tunaita majungu na fitina, sasa kama wewe mwenyewe unayetaka uongozi, umeshindwa kutafuta pesa kidogo binafsi au hata ya kuwasaidia wananchi unaotaka kuwasaidia ina maana moja tu kwamba ukipewa uongozi utawapeleka chini an kuwaibia!

- Kijana anayetaka kuongoza ni lazima aweze kusimama mbele ya wananchi na kuwaeleza jinsi alivyohangika na maisha mpaka kufikia uwezo wa kuwa na pesa alizozipata kihalali ambazo anazitumia kwenye kampeni, kama mgombea yoyote hawezi hilo, katika hii nchi ya kibepari basi ni simply kwamba hafai, kwa hiyo hii ya kijana mdogo sana kama Januari kuwa na uwezo wa kipesa tena za halali at his age inapaswa kuwa a plus kwake katika kampeni, unless kama mkuu unaweza kuthibitisha kwamba amezipata kwa njia ya wizi, halafu so far hii habari nzima ni maneno yako tu hakuna popote pa kutihibitisha ukweli wake! Ingawa tunaijadili anyways!

4.tunataka fair competition katika harakati hizi, jm atumie elimu yake na uzoefu wake kuwaomba wananchi wa bumbuli kura zao wakati itakapo wadia sio kuanza kutoa hongo za chinichini....

- Wewe unadai una uchungu na taifa lako, unamuona Januari anatoa hongo kama ulivyosema kwenye hii mada yako, sasa kilichokushinda kukusanya evidence na kumfikisha kwenye sheria ni nini hasa? Badala yake umekimbilia huku kuleta majungu, fitina, wivu na chuki zako za binafsi, mwananchi anayependa fair competition angekimbilia polisi pale pale alipoona hongo ikitolewa, acheni kuharibu majina ya vijana wanaotaka kulisaidia hili taifa!

Ila hii ni kwa gt na fm, nipo tayari kuweka rehani maisha yangu nawahakikishia january makamba hawezi na hataweza kuchukua jimbo la bumbuli, nyinyi mnajua upinzani anaopata huko anakopita, sehemu anazozomewa...kwa kifupi haungwi mkono na kumbuka kwamba nyoka hazai jongoo....alwayz like father like son....

- Hapa sasa ndipo unapoonyesha rangi zako wazi za fitina na chuki, yaani wewe ndiye unayeamua nani awe mbunge huko? Haya ya mtoto na jongoo ni ujinga foolisness, Januari amesoma baba yake hakusoma kama mtoto hizi huwa ni methali za wivu, chuki, majungu na fitina.

- Sasa kama unajua kuwa hatashinda unalia lia nini hapa mkuu, kwani aliyekuambia kugombea ni lazima kushinda nani? Wengine hua wanagombea kuhakikisha kwamba anayeshinda anakumbatia agenda ya maendeleo waliyonayo pamoja na kwamba wanajua watashindwa, hii ya kushinda ua kushindwa ni dhana potofu sana na ni nothing but wivu, fitina, chuki na majungu at best!
Ushauri wa bure kwa jm.....just pull out...tumia busara chambua na fikiria kuhusu safari yako ilivyokuwa na jaribu kuona inakupa matumaini gani.

- Januari hahitaji kusikiliza this kind of advice, maana movtive yake iko wazi ni wivu, chuki na majungu, ninaamini Januari atakua motivated sana kuendelea na juhudi zake hasa kutokana na this kind of jokes, infact leo nitamtafuta nimpe nguvu zaidi, this is great ina maana moja tu kwamba huko kuna dalili za ushindi!

- Mkuu pole sana, hatuko hapa JF ku-create majungu na hatred kwa waliotuzidi maarifa, infact huwa tuna incourage watu wajifunze kutoka kwa wanaozidi akili na maarifa, badala ya yale mambo ya kizamani ya kuwasubiri chini washuke. Taifa hili la sasa tunawahitaji viongozi kama Januari, ambao katika umri mdogo sana walionao tayari wameshafanya mengi sana binafsi na nationally, na tuko wengi tunao unga mkono vijana wengi kujitokeza kama anavyofanya Januari!

- Ujumbe wangu kwa Januari, si kweli kwamba hapa tunachukia watoto wa viongozi, au watoto wa wazazi wenye uwezo, na wala hatulaumu umasikini wetu kwa walio na uwezo walioupata kihalali, ingawa pia kwa vile hapa ni nyumba ya Demokrasia, ni rahisi sana kwa wenzetu wengine kujichomeka na kueneza sumu za wivu, fitina na chuki zao binafsi!

- Kwenye Demokrasia tunawavumilia na kujaribu kuwaonyesha njia kwa kuwaelimisha!

es!
 
Wasifu wa Januari Makamba.

1. Mr. January Y. Makamba
, Chair of the Africa Working Group at the Institute for Conflict Analysis and Resolution (ICAR), Fairfax, Virginia.

2. Recipient of the Brenda Rubenstein Scholarship at ICAR, Mr. Makamba is also an International Organization Fellow of the UN Association and Intern at the Academy for Educational Development in Washington D.C.A MS degree in Conflict Analysis and Resolution from George Mason University will be awarded in May 2004,

3. following his BA degree in Peace and Conflict Studies from Saint John's University (Minnesota) in 2002.

4. Mr. Makamba
worked for AFRICARE as Assistant Camp Manager of the Mtabila II Refugee Camp, Kasulu, Tanzania from 1995 to 1997, where he oversaw the management of a camp of more than 60,000 Burundian refugees.

5. Later he worked summers as a Protection Assistant/Intern with the UNHCR Sub-Office in KasuluThe Carter Center (2002), and as a Researcher/Intern in the Ministry of Foreign Affairs of Tanzania, researching conflicts in the Great Lakes region of Africa as they relate to national policy (2003).

6. Mr. Makamba
(2001), as an Election Observer/Human Rights Intern in Atlanta and Sierra Leone with has built an extensive network of activists in politics and civil society in East and Central Africa.

7. Asisstant to the President of Tanzania, since 2005 to this date.
 
WEWE field marshal mbon aunatumia energy nyingi sana kutetea huu mvinyo wa zamani?!do you happen to have any special interest in this fella being an MP?!

wote tunafahamu jinsi gani UTAWALA wa kikwete ulivyofail.kuna post humu watu wanajaribu hata kuonesha connection ya washauri wa kikwete na failures zake.either hawasikilizi washauri au washauri wanamshauri PUMBA.

sasa kama JANUARI ni mshauri wa RAISI kwa miaka mi-5 sasa sidhani kama angefaa kuwepo kwenye kundi la mabadiliko ambayo wananchi wa Tanzania wanayahitaji.
huyu ni more of the same,nothing new hapa.huyo shelukindo naye ni walewale,wanajisemeaga bora afadhali kuliko potelea mbali,sasa sijui yupi ni yupi hapa.

tukirudi kwa JANUARI

1.ELIMU
kila mtu anafahamu kuwa kigezo cha elimu Tanzania ni moj akati ya silaha kubwa wanayoitumia mafisadi kulaghai wananchi wakati productivity ni F.sitampa sifa kwenye hili.elimu aliyonayo naiona kama basic,sio extra-ordinary.

2.UHUSIANO na KIKWETE.
hapa ndio anapokosea,anajihusisha na FAILURE ya uongozi,100 years later wananchi wa Tanzanaia watauuchukulia utawala wa kikwete kama muda ambao TZ ilijikwaa,so far tupo chini,we don't need losers like these to continue to keep us down.

3.FEDHA& MISAADA

huyu kijana hana fedha za kutoa misaada anayotoa,tunafahamu kuwa kuna mkono wa mtu behind those grants he is giving out now,as many others before him have proved.
wananchi wa BUMBULI wajiulize,is 5 years of a mediocre leader worth a few sewing machines?!
nyie mnaokimbilia kutoa mifano ya marekani sijui,ni wapi OBAMA alitoa msaada hata wa baiskeli kwa RAIA yoyote wa marekani?!!
cha zaidi aliweka kampeni ya kuchangiwa na same people waliomchagua.hebu tazameni hili,huyu mkimuachia afanye atakavyo mkishampa huo ubunge itakuwa payback time ya hivyo vyerehani same way watanzania wanalipia Pilau za kikwete hadi kesho!!

wanajua wananchi wa TZ hawana elimu ya uraia,na watafanya kila wawezavyo waipate elimu ya uraia!!

poleni watanzania wenzangu.
 
WEWE field marshal mbon aunatumia energy nyingi sana kutetea huu mvinyo wa zamani?!do you happen to have any special interest in this fella being an MP?!

- Vipi ina maana wewe unamchukia kwa sababu umeshindwa kupata hiyo special interest na ubunge wake nini mkuu? Maana inaonekana mawazo yako ni motivated na special interest sasa unadhani wote tuko hivyo, pole sana mkuu, wengine hwua tunajali facts tu at hand! na hatuogopi wala kutishwa na maneno emptya au hewa! huwa tunatumia haki yetu katika demokrasia kusema our mind as we see fit!

wote tunafahamu jinsi gani UTAWALA wa kikwete ulivyofail.kuna post humu watu wanajaribu hata kuonesha connection ya washauri wa kikwete na failures zake.either hawasikilizi washauri au washauri wanamshauri PUMBA.
- Yaani siku hizi unawakilisha mawazo ya watu wote, wa wapi hao hapa JF au somewhere else?

- Januari sio mshauri wa Rais Kikwete, ni Assistant tu politically tunasema hivi kama Rais ameharibu uchumi basi washauri wake wa uchumi hawafai, wapo wanaotambulwia kishera lakini Januari sio mmojawapo, kama Rais ameharibu kiutawala, washauri wake wa utawala wapo tena wanaotambuliwa kisheria lakini Januari sio mmojawapo, kila sekta Rais anao washauri wanaotambuliwa kisheria, sasa ni vyema ukasema wazi hapa Januari anatambuliwa kisheria kama mshauri wa nini kwa Rais?

- Na je unaweza kuweka mfano mmoja tu wa ushauri mbovu ambao Januari amewahi kumpa Rais wetu in the last five years!

sasa kama JANUARI ni mshauri wa RAISI kwa miaka mi-5 sasa sidhani kama angefaa kuwepo kwenye kundi la mabadiliko ambayo wananchi wa Tanzania wanayahitaji.
huyu ni more of the same,nothing new hapa.huyo shelukindo naye ni walewale,wanajisemeaga bora afadhali kuliko potelea mbali,sasa sijui yupi ni yupi hapa.
- Januari aliwahi kumshauri nini Rais unachokijua, kiweke hapa tukione ili tuamini!

tukirudi kwa JANUARI

1.ELIMU
kila mtu anafahamu kuwa kigezo cha elimu Tanzania ni moj akati ya silaha kubwa wanayoitumia mafisadi
kulaghai wananchi wakati productivity ni F.sitampa sifa kwenye hili.elimu aliyonayo naiona kama basic,sio extra-ordinary.

- Elimu ni either unayo au huna, lakini sio a crime kuwa nayo kama alivyonayo Januari, na si wananchi wote wa Tanzania wanayo na hai okotwi mtaani, it takes a lot kua nayo ndio maana tunamuheshimu yoyote yule aliyenayo elimu kama ya Januari Makamba!

2.UHUSIANO na KIKWETE.
hapa ndio anapokosea,anajihusisha na FAILURE ya uongozi,100 years later wananchi wa Tanzanaia watauuchukulia utawala wa kikwete kama muda ambao TZ ilijikwaa,so far tupo chini,we don't need losers like these to continue to keep us down.
- Sio siri kwamba huelewi tofauti ya Presidency as an insitution na Presidency on a personal level, ambako ndio unakuta ishu ya uongozi ni vitu viwili tofauti sana na an instituion, sasa as long ni wewe ndiye utakayeandika history ya 100 years to come, sio siri kwamba Januari atakuwa a loser, lakini thanks to God kwamba hutaandika hiyo history!

3.FEDHA& MISAADA

huyu kijana hana fedha za kutoa misaada anayotoa,tunafahamu kuwa kuna mkono wa mtu behind those grants he is giving out now,as many others before him have proved.
wananchi wa BUMBULI wajiulize,is 5 years of a mediocre leader worth a few sewing machines?!
nyie mnaokimbilia kutoa mifano ya marekani sijui,ni wapi OBAMA alitoa msaada hata wa baiskeli kwa RAIA yoyote wa marekani?!!
cha zaidi aliweka kampeni ya kuchangiwa na same people waliomchagua.hebu tazameni hili,huyu mkimuachia afanye atakavyo mkishampa huo ubunge itakuwa payback time ya hivyo vyerehani same way watanzania wanalipia Pilau za kikwete hadi kesho!!
- Kumbe wewe ni muweka hazina wake kwamba unajua hela alizonazo na asizonazo, duh! kweli nimekuvulia kofia mkuu!

- Obama hawezi kuwapa wamarekani baisikeli, kwa sababu huko US unaweza kwenda Salvation Army ukapata hata baisikeli za bure au kwa dola moja mpaka tano, labda tu ungeeleza zile hela zote dola Million karibu 300 alizifanyia nini wakati wa kampeni? Na alipewa na nani na hao waliompa atawalipa je? na kwa nini ile kampuni ya silaha ya Chenney ilikuwa inapewa sana tenda kuliko zingine kama huko majuu hakuna haya mambo yetu ya bongo?

wanajua wananchi wa TZ hawana elimu ya uraia,na watafanya kila wawezavyo waipate elimu ya uraia!!poleni watanzania wenzangu.
- Elimu ya uraia haiwezi kuwa proven na wivu, chuki, majungu na fitina, kwamba ukiweza kuyapanga yakawa kama kweli basi ndio una elimu nzuri ya uraia, Tanzania tunahitaji vijana kama Januari kusimama na kuchukua uongozi wa taifa, yaani walete mawazo mapya!

- Pole sana mkuu, hapa ni Demokrasia tunaruhusiwa kufikiri na kusema for ourselves sio kuamuliwa na wengine!

es!
 
- Huu mjadala umeuleta kwa nia ya kuharibu jina la huyu kijana na ni kawaida yako kuwachukia vijana wote ambao wazazi wao ni viongozi, ndio maana tunajaribu kukuelimisha kwamba watoto wa viongozi ni wananchi wa Tanzania kama wengine wote na wana haki za anything affordable by our laws kwa kila raia wake.

- Sasa tizama, huyu kijana hajawahi kuwa kiongozi Tanzania, sasa hayo unayoyaita mapungufu wewe umeyapata wapi? kama sio majungu wivu chuki na fitina?

- Either yupo karibu na Rais au hayupo, na kama unajua siasa basi ulipaswa kujua kwamba katika siasa za taifa anything ambacho ni Symbolic Nationally karibu yako ni muhimu sana katika kujinadi mbele ya public, ndio maana kule US kila siku politicians wanasema walikuwa karibu na Reagan, au JFK, kama ulikuwa huelewi hiyo ni kawaida sana kwenye kampeni za siasa.

- Januari yupo karibu na Rais ni fact, amemtuma au hakumtuma ni wajibu wa Rais kukanusha lakini kama Januari amesema kweli (which I doubt) lazima Rais amesikia, sasa kama hahusiki basi anatakiwa kukanusha asipokanusha ni kweli ndio siasa za taifa zilivyo mkuu kama ulikuwa huelewi.

- Hilo ni tatizo la chama chake, ingawa kwenye kichwa chako cha mada hukusema kama anagombea chama gani, sasa unaona tunaposema kwamba una majungu, wivu, chuki na fitina kwa sababu kama hili ni tatizo ni chama chake ndio kinawahusu sio wewe, hayakuhusu haya na hayana anything to do na uwezo wake wa uongozi!

- Januari anao uwezo wa kipesa sio kwa sababu ni mtoto wa Makamba, na pili yeye kuwa na uwezo wa kipesa sio kosa la kisheria, pili kuwapa misaada wananchi anaotaka kuwasaidia sio kuvunja sheria, kuwa au kutokuwa na pesa sio tatizo la mtoto wa Makamba au wa mkulima, haya ndio tunaita majungu na fitina, sasa kama wewe mwenyewe unayetaka uongozi, umeshindwa kutafuta pesa kidogo binafsi au hata ya kuwasaidia wananchi unaotaka kuwasaidia ina maana moja tu kwamba ukipewa uongozi utawapeleka chini an kuwaibia!

- Kijana anayetaka kuongoza ni lazima aweze kusimama mbele ya wananchi na kuwaeleza jinsi alivyohangika na maisha mpaka kufikia uwezo wa kuwa na pesa alizozipata kihalali ambazo anazitumia kwenye kampeni, kama mgombea yoyote hawezi hilo, katika hii nchi ya kibepari basi ni simply kwamba hafai, kwa hiyo hii ya kijana mdogo sana kama Januari kuwa na uwezo wa kipesa tena za halali at his age inapaswa kuwa a plus kwake katika kampeni, unless kama mkuu unaweza kuthibitisha kwamba amezipata kwa njia ya wizi, halafu so far hii habari nzima ni maneno yako tu hakuna popote pa kutihibitisha ukweli wake! Ingawa tunaijadili anyways!

- Wewe unadai una uchungu na taifa lako, unamuona Januari anatoa hongo kama ulivyosema kwenye hii mada yako, sasa kilichokushinda kukusanya evidence na kumfikisha kwenye sheria ni nini hasa? Badala yake umekimbilia huku kuleta majungu, fitina, wivu na chuki zako za binafsi, mwananchi anayependa fair competition angekimbilia polisi pale pale alipoona hongo ikitolewa, acheni kuharibu majina ya vijana wanaotaka kulisaidia hili taifa!

- Hapa sasa ndipo unapoonyesha rangi zako wazi za fitina na chuki, yaani wewe ndiye unayeamua nani awe mbunge huko? Haya ya mtoto na jongoo ni ujinga foolisness, Januari amesoma baba yake hakusoma kama mtoto hizi huwa ni methali za wivu, chuki, majungu na fitina.

- Sasa kama unajua kuwa hatashinda unalia lia nini hapa mkuu, kwani aliyekuambia kugombea ni lazima kushinda nani? Wengine hua wanagombea kuhakikisha kwamba anayeshinda anakumbatia agenda ya maendeleo waliyonayo pamoja na kwamba wanajua watashindwa, hii ya kushinda ua kushindwa ni dhana potofu sana na ni nothing but wivu, fitina, chuki na majungu at best!

- Januari hahitaji kusikiliza this kind of advice, maana movtive yake iko wazi ni wivu, chuki na majungu, ninaamini Januari atakua motivated sana kuendelea na juhudi zake hasa kutokana na this kind of jokes, infact leo nitamtafuta nimpe nguvu zaidi, this is great ina maana moja tu kwamba huko kuna dalili za ushindi!

- Mkuu pole sana, hatuko hapa JF ku-create majungu na hatred kwa waliotuzidi maarifa, infact huwa tuna incourage watu wajifunze kutoka kwa wanaozidi akili na maarifa, badala ya yale mambo ya kizamani ya kuwasubiri chini washuke. Taifa hili la sasa tunawahitaji viongozi kama Januari, ambao katika umri mdogo sana walionao tayari wameshafanya mengi sana binafsi na nationally, na tuko wengi tunao unga mkono vijana wengi kujitokeza kama anavyofanya Januari!

- Ujumbe wangu kwa Januari, si kweli kwamba hapa tunachukia watoto wa viongozi, au watoto wa wazazi wenye uwezo, na wala hatulaumu umasikini wetu kwa walio na uwezo walioupata kihalali, ingawa pia kwa vile hapa ni nyumba ya Demokrasia, ni rahisi sana kwa wenzetu wengine kujichomeka na kueneza sumu za wivu, fitina na chuki zao binafsi!

- Kwenye Demokrasia tunawavumilia na kujaribu kuwaonyesha njia kwa kuwaelimisha!

es!

SIR,YOU WILL DO ANYTHING TO DEFEND YOUR FRIEND....HALAFU KILA WAKATI UNAJICHANGANYA, MARA HUTAKI KUAMINI KAM JM ALIENDA KUJITANGAZA JIMBONI, MARA UNATAKA KUJUSTIFY KWAMBA SIO KOSA, MARA HUAMINI KAMA AMEPANGA KUGAWA VYEREHANI HAPOHAPO UNAJUSTIFY KWA UWEZO WAKE WA FEZA.....

I NOW CONCLUDE KWAMBA WEWE NI JANUARY MAKAMBA....HUWEZI KUTETEA KILA HOJA NA KUPINGA KILA KITU KINACHOSEMWA, MALUMBANO YAKO HAYANA TIJA NA KAMA WEWE SIO JM BASI KWA TAARIFA YAKO HUMSAIDII KWA HILI UNALOFANYA.....SAVE YOUR ENERGY SON....
HAKUNA MWENYE CHUKI,WIVU KWA JM WALA WATOTO WENGINE WA WAKUBWA IL WEWE UNATAKA KUONYESHA IWE HIVYO....KAMA JM ATAKUSIKILIZA HAUTAMSAIDIA HATA KUFIKIA HIYO NI YAKE...

KULUMBANA NA WEWE SIWEZI MANA HATUMSAIDII YEYOTE HAPA....
 
- Woow! Hillarious! na ni very entertaining!

es!
 
Hii thread yanikumbusha ile thread ya kijana mwingine iliyowahi kuanzishwa humu ndani - Lawrence Masha. Maswahiba wetu wanapoguswa swala haliwi tena nguvu za hoja bali hoja za nguvu lakini pamoja na yote mwishowe ukweli hufichuka. Pia kwa mbali nakumbuka mwaka 2005 - sitasahau yaliyotupata tuliokuwa na ujasiri wa kuhoji huyu bwana katufanyia nini hadi tumpe Uraisi. Bahati mbaya sana ni kuwa Watanzania siku zote tunakuwa na matumaini ya kuvuna tusichopanda. Kawaida yetu ya kukumbatia viongozi wa kufinyangwa inavyozidi kukomaa ndivyo na taifa linavyozidi kudidimia na bado hatujifunzi, inasikitisha.
 
- Nilitetea background ya Masha ambayo ninaifahamu sana pale ilipotaka kupotoshwa kwa makusudi, lakini sikutetea uwezo wake wa kazi kama waziri, na besides mengi yalikuwa ni majungu kuliko facts kama hii thread, lakini unaweza kuanzisha mjadala wa Masha huu ni Januari Makamba.

- Kuhusu Mtandao nilikuwa wa kwanza kule BCS kuwatahadharisha wananchi na hili kundi, lakini nikatukanwa sana kwamba wananchi wa Tanzania wanataka viongozi vijana, na matokeo yako very clear ya viongozi vijana.

- Sasa hapa sitetei mtu, ninatetea principle, kwamba mtoto wa Makamba au wa mwananchi yoyote wa Tanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote Tanzania, kama ana makosa kiuongozi yasemwe hapa tuyaone lakini sio kuleta chuki, wivu, na fitina na kujaribu kulazimisha majungu kwa nguvu kwamba wote hapa tuwachukie watoto wa viongozi hayo ni mawazo finyu sana na ni umasikini ambao binadam anauruhusu kumuingia mpaka kwenye ubongo, yaani unaanza kuwachukia watu wengine kwa sababu wamezaliwa na watu wenye uwezo kuliko wako,

- Au kwa sababu wana uwezo wa akili na wamefanikiwa makubwa sana kwenye maisha wakiwa na umri mdogo kuliko wako, basi unageuka kua na chuki wee halafu unajaribu kutumia kila njia kulazimisha na wengine wawe na sumu kama zako kwa visingizio vya ajabu ajabu ambavyo wala huwezi kuvitolea ushahidi, huo ni umasikini wa akili na ni hatari sana kwa taifa ndio maana hili taifa limekwama, watu wenye uwezo wa kuongoza siku zote hutengenezewa majungu na fitina kama haya kwenye hii thread!

- Eti ni wapi Januari aliwahi kuongoza taifa kwamba sasa unaweza kumuhukumu? Fitina fitina tu na roho za kimasikini mnajaribu hata bila aibu kuzihalalisha hapa, kama hamuwezi kugombea nafasi waachieni wanaoweza kina Januari, lakini sio kuja hapa na kutaka kutulazimisha wote hapa tuwe na chuki na watu wengine bila sababu, ni mawazo mufilisi na ya hatari sana na ni lazima kuwaogopa sana wale wote wenye haya mawazo ya chuki na watu!

Respect.

FMEs!
 
- nilitetea background ya masha ambayo ninaifahamu sana pale ilipotaka kupotoshwa kwa makusudi, lakini sikutetea uwezo wake wa kazi kama waziri, na besides mengi yalikuwa ni majungu kuliko facts kama hii thread, lakini unaweza kuanzisha mjadala wa masha huu ni januari makamba.

- kuhusu mtandao nilikuwa wa kwanza kule bcs kuwatahadharisha wananchi na hili kundi, lakini nikatukanwa sana kwamba wananchi wa tanzania wanataka viongozi vijana, na matokeo yako very clear ya viongozi vijana.

- sasa hapa sitetei mtu, ninatetea principle, kwamba mtoto wa makamba au wa mwananchi yoyote wa tanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote tanzania, kama ana makosa kiuongozi yasemwe hapa tuyaone lakini sio kuleta chuki, wivu, na fitina na kujaribu kulazimisha majungu kwa nguvu kwamba wote hapa tuwachukie watoto wa viongozi hayo ni mawazo finyu sana na ni umasikini ambao binadam anauruhusu kumuingia mpaka kwenye ubongo, yaani unaanza kuwachukia watu wengine kwa sababu wamezaliwa na watu wenye uwezo kuliko wako,

- au kwa sababu wana uwezo wa akili na wamefanikiwa makubwa sana kwenye maisha wakiwa na umri mdogo kuliko wako, basi unageuka kua na chuki wee halafu unajaribu kutumia kila njia kulazimisha na wengine wawe na sumu kama zako kwa visingizio vya ajabu ajabu ambavyo wala huwezi kuvitolea ushahidi, huo ni umasikini wa akili na ni hatari sana kwa taifa ndio maana hili taifa limekwama, watu wenye uwezo wa kuongoza siku zote hutengenezewa majungu na fitina kama haya kwenye hii thread!

- eti ni wapi januari aliwahi kuongoza taifa kwamba sasa unaweza kumuhukumu? Fitina fitina tu na roho za kimasikini mnajaribu hata bila aibu kuzihalalisha hapa, kama hamuwezi kugombea nafasi waachieni wanaoweza kina januari, lakini sio kuja hapa na kutaka kutulazimisha wote hapa tuwe na chuki na watu wengine bila sababu, ni mawazo mufilisi na ya hatari sana na ni lazima kuwaogopa sana wale wote wenye haya mawazo ya chuki na watu!

respect.

fmes!

ndugu yangu fmes....hiki kiapo cha kumlinda na kumtetea jm kama kingetumika pia kwa viongozi wa nchi yetu basi tungekuwa mbali sana....lakini kinachonishangaza katika hoja zako ni kulazimisha kwamba kuna chuki na wivu na roho mbaya juu ya jm....you are very wrong.....tulichofanya hapa ni kutoa taarifa kwamba jm ameenda kujitangaza jimboni bumbuli na kwa taarifa yake alikuwa ameweka ahadi ya kufanya hivyo kabla kwani sio kwamba ndio ameanza kampeni...kwani hata pikipiki alishapeleka kule jimboni zaidi za mwezi sasa umepita....
hakuna asiyetaka vijana wajitokeze na hakuna aliyempinga jm so far, ila tunaangalia namna anavyofanya shughuli na kuangalia kama je ni katika mwenendo ambao unaleta matumaini kwa demokrasia ya nchi yetu....

nakushangaa unapopinga kwamba:
1. Jm hakwenda bumbuli kujitambulisha
2. January hajawahi kuchangia ujenzi wa shule
3.jm hakuchangia vijana
4. Jm hakutoka pesa kila alipopita....
5. Jm hakutoa pikipiki.....

lakini unatetea kwamba jm ni kijana mwenye uwezo....smart...hapo hapo unasema anasaidia jamii yake.....ndio maana nimesema humsaidii jm kwa hili kwa kukanusha kila alilofanya....unaweza ukawa au ukahisi kwamba wewe ni mjuaji sana lakini kumbe sivyo....unapinga hata kwamba jm anataka kugombea ubunge bumbuli.....
nimekuwekea hata namba za simu za watu wa kupigia kama unataka ushahidi..piga uulize kila sehemu anayopita jm anasema nini na anataka nini na jaribu pia kuchukua mawazo ya watu kuhusu mtizamo wao kuhusu jm.......

at my own humble conclusion, i think u have done more harm to jm than u think u helped....so long....

sijui na wewe unagombea wapi ndugu yangu....i wish u all the best....
 
January makamba yupo soni, lushoto, jimbo la bumbuli (linaloshikiriwa na shelukindo) leo hii akijinadi kwa wapiga kura.
January ambaye alishaanza kujitangaza jimboni humo kwa kumwaga pesa na pikipiki za kampeni leo aliwasubiri watu wa soni wamalize kuswali ili apate nafasi ya kusalimia, lakini kitendo hicho kilichukiwa na wengi na wengi kuondoka bila kutaka kumsikiliza.
Jioni hii anaenda kutembelea shule mpya ya waislamu ambapo mwanzo alichangia shilingi laki moja ya ujenzi.

Safari ya january imekumbwa na vikwazo vingi kwani amekuwa akipata mapokezi mabovu moja ni vijana kukataa vifaa vya michezo kama jezi na kumuambia hawahitaji.....

Mapokezi haya mabaya ya january ambaye anasema ametumwa na raisi kuchukua jimbo hilo, yanasababishwa na chuki waliyokuwa nayo wananchi dhidi ya baba yake mzee makamba ambaye mara ya kwanza naye alitimuliwa na wananchi alipojaribu kumnadi kijana wake....

Wengi wamekuwa wakisema january hajulikani na si mwenyeji wa eneo hilo japo baba yake ni mkazi na alishawahi kugombea jimbo hilo zaidi ya mara 2 na kushindwa.

Wadau wanasema january atatumia jeri ya pesa, wakati wananchi wanasema hawadanganyiki tena......

Mzee shelukind nae amekuwa akizomewa kila anapokwenda jimboni, wananchi wamemuambia basi kwa kuwa kwenye kampeni za 2005 yeye na mke wae waliomba na kuahidi ingeuwa ni awamu ya mwisho hatagombea tena pamoja na kutofanya lolote jimboni humo.......

Naona wanajf wameshaanza kujitokeza.....je tumuunge mkono january???

Ningefurahi kupata uchambuzi yakinifu kutoka kwa wazoefu hapa janvini.....

January ni mzalendo kama kweli ameamua kwenda kugombea mimi binafsi nampongeza kwa nia yake, nampiga mwandishi huyu juu kwa maneno yake ya kukatisha tamaa vijana walio na mwiyo ya uthubutu ninatamani vijana wengi zaidi wasomi na walio na mtazamo mpya wajitokeze . katika kusoma kwangu naona alie andika habari hii anamtazamo hasi kwa Januari na siyo mwelewa wa haki za kiraia na historia ya za siasa nyumbani na dunia ajipange. Mtu hawezi kuhukumiwa kwa nia yake nzuri kwakuwa eti baba yake au mama yake hakufanikiwa kitu fulani kama anachuki na mzee makamba adeal na huyo huyo asihamishie deni la chuki kwa mwanae, usitende kitu ambacho hungependa kutendewa. EJR
 
january ni mzalendo anahaki zake binafsi za kirai, ninampongeza kwa uthubutu wake kama kweli anayo nia ya kugombea jimboni kwao. nivema kuunga mkono vijana wasomi na wenye mitazamo kushiriki katika maamuzi ya maendeleo ya nchi yetu kuliko kusambaza maneno ya kuvuja mwiyo ya vijana eti kwasababu baba zao na mama zao walishindwa kufanikiwa. Mwamndishi wa habari hii ni wazi kuwa anamtazamo hasi kwa January na siyo mwelewa wa historia za siasa nyumbani na duniani kama ana deni la chuki kwa mzee makamba asihamishie kwa kizazi chake. Vijana wengi jitokezeni tubadili mwelekeo wa taifa letu. EJR
 
Muacheni kijana wa watu apigane kuingia bungeni. He is smart and prepared to enter this politics game na nina uhakika jimbo lolote nchini litamtaka, tuache fikra za chuki na wivu kwa watoto wa viongozi au vibosile wa TZ.

Uwepo wao na elimu zao ni matokeo ya wazazi wao ambao waliukimbia umaskini na kufanikiwa ktk siasa na biashara. I don't care how. Isn't this young man the model of what every Tanzanian should be? In terms of wealth of knowledge!

The fact that wewe (an elite Tanzanian) unasoma JF sasa ni kielelezo tosha kuwa nawe watoto wako watakuwa na nafasi ya kuwa na potential kama ya au zaidi ya J Makamba, na watoto wasomi wengine wa vibosile wa TZ.
 
Hv kwani ukitaka kugomea ubunge au kiti chochote cha kisiasa ni lazima uanze kwa kutoa misaada kwa nguvu zote.... mantiki iko wapi... mi nafikiri hapa ndipo tunaokosea.... ikiwa ww ni jimbo lako..... iweje unapotaka kugombea ndio utoe misaada (mi naona ni takrima a.k.a rushwa ya kificho) kwani ulikuwepo wapi mwanzo na hukuona matatizo yao.... hii ni aina ya kasumba iliyojaa vichwani mwetu (viongozi na waongozwaji) sijasikia wenzetu(wazungu) japo sijatembea.. kuwa na staili hii... kuna njia flani za kujifikisha kwa wananchi sio lazima utoe mali... ukiwa una strong FACTS watu watakupa tu... kwa wneye akili ndefu ukianza kutanguliza hivyo wanakuwekea doubt kama utaweza kuleta mabadiliko......

SIASA za BONGO NI ZA KIPEKEEEE.... wote hawajielewe wapiga kura na wapigiwa kura... ndio mtajua kuwa nchii hii ilipaswa kuwa eneo la makaburi(no offence) haiwezekani mijitu iko kama mazezeta haielewi na haitaki kubadilika
 
Back
Top Bottom