Congo DR ni sehemu ambayo hata shetani hujiuliza mara mbili kwenda

Congo DR ni sehemu ambayo hata shetani hujiuliza mara mbili kwenda

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Ama kweli tembea uone!

Congo DR, ni sehemu ambayo maeneo mengi ili ufanikiwe kutoboa, ni lazima uwe umehitimu ubabe kwa zaidi ya alama 1000%.

DR, ndilo eneo ambalo maovu, umafia na hata unyama hutendwa hadharani!

Mfano, mgeni usafiripo kwa kupitia mpaka wa Kasumbalesa kwa roli kwenda Lubumbashi, na hata mbele zaidi- hakika uwe sawa kisaikolojia kwa matukio ya kibabe kutoka kwa watoto wa mbwa!

Mateso utayoyashuhudia kuanzia Kasumbalesa na kuendelea, hayasimuliki!

Eneo la urefu wa kilomita mia, usishangae ukatumia wiki na hata mwezi kufika.

Congo DR, ndipo eneo ukibanwa na wamba unaweza uchague ima wachukue kila kitu ndani ya gari ama wewe ufanywe vipande vya nyama na gari ibaki ili iwe shuhuda wa ulikuwa nayo Duniani.

Itoshe kusema, huenda shetani akiwa anaongea na simu husimama DR na kutoa maelekezo. Na hata yeye ( shetani ) usishangae huwa anajiuliza mara mbilimbili kutua hapo.

Ulishajiuliza kwa nini Yesu harejei kama alivyo sema? Huenda jawabu lipo Congo na matukio yake ya kinyama!

Anzia Lubumbashi hadi Kamoto, hakika wewe kama ni mtu lege lege- sikushauri uende!

DR, ndiyo mahali unaweza kufumba macho uombe ile unafumbua, unakutana na kope chini!

DR, wewe mwenye miaka 40 kuchinjwa na kitoto cha miaka 10, wala siyo ajabu. Ila ni ajabu endapo kitoto cha miaka 10 kitashindwa kukuchinja wewe mwenye miaka 40.

Umafia uliopo DR, siyo makalio eti kila mtu anayo.

Congo, 🙌!

Hakika, Congo siyo Kongowe.
 
Back
Top Bottom