Congo DR ni sehemu ambayo hata shetani hujiuliza mara mbili kwenda

Hivi bado mtanzania anahitajika kuwa na visa kuingia DRC?. Mwanzoni mwa mwaka huu nikiwa Gisenyi Rwanda nilipanga kuingia Goma, ubabe nilioukuta kule "Grand barrier" kulinifanya niachane na mpango huo.

Nitarudi huko tena mwakani nikiwa nimejipanga kisawa sawa.

 
Hakuna Serkali baadhi ya maeneo na yako mengi so hilo ulilosema lipo sana
 
Grand barrier unasema pa kijinga?! Je, ungekutana na ubabe wa Petit barrier?!

Anyway, hizo border mbili za upande wa Gisenyi na Goma ni za kitakatifu sana. Hata Rusizi 1 na Rusizi 2 za Kamembe nazo u Yesu ni mwingi pia. Vivyo hivyo, hata border ya Bugarama na Kamanyola-napo salamu Maria ni nyingi pia.

Ngoma ipo Kasumbalesa, wenyewe wanakwambia bulaya yaani Ulaya. Huko ndiyo lilipo ungua shoka mpini ukabaki!

Kila nikikumbuka visa vya wale watoto wa mbwa pale Kanyaka, aisee sina hamu na DR.

Congo, 🙌!!
 
Acha kuogopeshana
Akuogopeshe nani sasa? Wewe si wa kiume, nenda ukajionee.

Kule ukijifanya mjanja eti kioo juu wamba wanakimwaga chote na adhabu yake wanakumiminia rundo la mavi ndani ya gari halafu ndiyo mnaanza upyaaaa.

Mifuko iliyojaa kinyesi kwao wao ni moja ya silaha. Ulishawahi kukutana na harufu ya mkojo wa siku nyingi? Basi ukijifanya mjanja kinywaji chako cha kushushia utapewa mkojo wa miezi hata mitatu nyuma unywe.

Tunaposema DR ni kama Serena Hotel kwa ajili ya lunch ya shetani, elewa basi!

Congo, 🙌!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…