Congo DR ni sehemu ambayo hata shetani hujiuliza mara mbili kwenda

Congo DR ni sehemu ambayo hata shetani hujiuliza mara mbili kwenda

R.I.P Patrice Lumumba balaa lilianzia baada ya kuuwawa Lumumba kwa usaliti wa kina Mobutu.
Na Tshombe alihusika.
Hii habari ya RT juu ya Congo na Lumumba inauma sana
===
 
Ama kweli tembea uone!

Congo DR, ni sehemu ambayo maeneo mengi ili ufanikiwe kutoboa, ni lazima uwe umehitimu ubabe kwa zaidi ya alama 1000%.

DR, ndilo eneo ambalo maovu, umafia na hata unyama hutendwa hadharani!

Mfano, mgeni usafiripo kwa kupitia mpaka wa Kasumbalesa kwa roli kwenda Lubumbashi, na hata mbele zaidi- hakika uwe sawa kisaikolojia kwa matukio ya kibabe kutoka kwa watoto wa mbwa!

Mateso utayoyashuhudia kuanzia Kasumbalesa na kuendelea, hayasimuliki!

Eneo la urefu wa kilomita mia, usishangae ukatumia wiki na hata mwezi kufika.

Congo DR, ndipo eneo ukibanwa na wamba unaweza uchague ima wachukue kila kitu ndani ya gari ama wewe ufanywe vipande vya nyama na gari ibaki ili iwe shuhuda wa ulikuwa nayo Duniani.

Itoshe kusema, huenda shetani akiwa anaongea na simu husimama DR na kutoa maelekezo. Na hata yeye ( shetani ) usishangae huwa anajiuliza mara mbilimbili kutua hapo.

Ulishajiuliza kwa nini Yesu harejei kama alivyo sema? Huenda jawabu lipo Congo na matukio yake ya kinyama!

Anzia Lubumbashi hadi Kamoto, hakika wewe kama ni mtu lege lege- sikushauri uende!

DR, ndiyo mahali unaweza kufumba macho uombe ile unafumbua, unakutana na kope chini!

DR, wewe mwenye miaka 40 kuchinjwa na kitoto cha miaka 10, wala siyo ajabu. Ila ni ajabu endapo kitoto cha miaka 10 kitashindwa kukuchinja wewe mwenye miaka 40.

Umafia uliopo DR, siyo makalio eti kila mtu anayo.

Congo, 🙌!

Hakika, Congo siyo Kongowe.
Kuna watu wamechagua DRC iwe hivyo ili isiweze kusimamia madini yake. Kwa namna ilivyo na serikali isiyo na nguvu katika eneo lote la nchi ndivyo wengine wanavyonufaika.

Mfano, hata hayati Robert Mugabe, sehemu kubwa ya ule utajiri wake ulitokana na madini ya DRC, ikiwa ni biashara walioifanya pamoja na hayati Solomon Mujuru.

Hata jirani zetu Kenya, nao hawavutiwi na utulivu wa DRC, kwani vurugu hizo zinafanya Kenya kuwa ndiyo gulio kuu la madini ya waasi wa DRC. Kama ilivyo kwa Rwanda.

Hiyo nchi haiwezi kuwa na utulivu labda hadi ibaki na mashimo tu, baada ya madini kumalizika, ila kinyume chake, ni vurugu tupu kwa faida ya wezi wa madini.

Ova
 
Ndio maana wenye malori wengi hawakubali mizigo ya congo wakikubali mwisho ni kasumbalesa kutoka hapo utafute usafiri mwingine
 
Ile ni forgotten war
We are distracted by too many things na hatuikumbuki Ile vita.
If we pay attention,we can end that war.
Tatizo kule ni usaliti.
Watu wanaenda kupigana but they are not of one mind.
Huku we are distracted by cabinet reshuffles and people poisoning one another,kiasi kwamba we are forgetting about our international duties.
 
Toka nakua mpaka Leo ni Kongo au Sudan ni vita tu na Mweshimiwa ninaemjua ni Sariva kiirl mpaka Leo hakuiishi vita tu
 
Kuku wa zabanga alionyesha ulimwengu jinsi Congolese walivyo, wizi majivuno na roho mbaya ndio foundation ya Congo, they will never change
 
Toka nakua mpaka Leo ni Kongo au Sudan ni vita tu na Mweshimiwa ninaemjua ni Sariva kiirl mpaka Leo hakuiishi vita tu
South Sudan ni ka Nchi kadogo sana, hata Jimbo la Katanga linaizidi South Sudan kwa ukubwa wa Eneo.
 
Nchi ni kubwa kuliko Marekani a urusi ? Ni ujinga wa wasfrika!
Ni nchi kubwa sana kuliko uchumi wa DRC...

Hawawezi hata kuwa na bajeti hata robo ya kutengeneza miundombinu ya eneo lililo mbali ya mji mkuu (kilometers 2000) ..huko porini hakuna hata Serikali ya kueleweka...wanakaa wahuni na waasi...nk
 
Back
Top Bottom