Conspiracy Theory (MIND SPINNING): Sheikh Ponda Issa Ponda hajapigwa na Polisi

Conspiracy Theory (MIND SPINNING): Sheikh Ponda Issa Ponda hajapigwa na Polisi

Tumechoka sasa wapigwe tu. Kauli ya Pinda

Kauli mujarab punda mkaidi hendi pasina kichapo: yoyote yule anayelenga kuleta uchochezi na ashughulikiwe ipasavyo; Ponda ashukuru tu polisi wenyewe voda fasta kama ingekuwa ni wale polisi wa kweli tungekuwa tunaongea mengine.
 
lane, unaweza kuwa na point, hao wanaokupuuza ni wavivu tu wa kufikiri.
Vyombo vya habari vya magharibi vime capture hilo tukio mapema mno na katika hali ambayo inaweza kutafsiriwa kama wamekuwa appeased na hatua ya kupigwa risadi kwa Shehe ponda.

Inawezekana kabisa ikawa ghilba iliyopangwa kiustadi ili kuwapoza wamagharibi kufuatia kumwagiwa tindikali kwa watu wao.


aaannhaaaa...kama naelewa elewa..
Kwa maana nyingine PONDA katolewa kafara. Kama jumba bovu lilivyomdondokea LOWASSA..?

Na asingepigwa shaba yeye ..
JK ilibidi akajieleze ..au?

Mmmnnhh..!
 
Angekua ni mchungaji, hiyo mikono ingekua na pingu sa ivi akisubiriwa apate nafuu.
Lakini kwa ni yeye, polisi wanaogopa msala wa wafuasi wake.
 
Lane uko sawa, hii issue ya Ponda was planned b4.
Watu hapa wanashindwa kuelewa, fikiria zaidi ya hapo Ponda alivyopigwa risasi tatizo ni nini??
Walishindwa kumkamata kawaida bila kutumia nguvu zote hizo?? Kama kumkamata Ponda hawajashindwa siku nyingi hata hapo walipompiga risasi RPC aliluja na taarifa kwamba siyo polisi waliompigana hata wao hawajui alipo wanaomba wananchi wanaojua wawajulishe polisi mahali alipo Ponda.
Hii ni sawa kweli wananchi wamtoroshe Ponda kiasi kwamba Polisi wasijue alipo mpaka leo tena jioni ndiyo wakajua yuko Muhimbili?? Inawezekana kweli???
Sasa hapa ndiyo mahali pa kufikiria zaidi ya hili, hii ilipangwa na kama ni hivyo ilikusudia nini??
Tunajuaje kama ni wauza sembe walikuwa wanapita zao JNIA na mzigo wa kutosha wakaamua wajamishe watz wote kwenye suala la Ponda???
Au wahamishe mjadala tu wa Sembe uliokuwa unashika kasi ktk majadiliano kila sehemu hapa nchini, leo hii Ponda watu wote tumehama.
Ukiangalia suala la sembe serikali yenyewe(Serokali KUU) inadai ukiwakamata wauza sembe uchumi wa nchi utayumba, moja kwa moja unaona ni jinsi gani serikali inahusika ktk hili suala la sembe.

Na hii inaonyesha ni jinsi gani tunaendeshwa na matukio na anayetuendesha ni Serikali hii hii ya TZ
Jaribu kufikiria zaidi na zaidi, kuna vyombo vya habari vya nje jana viliripoti hili suala instantly sijui walitoa wapi taarifa ila wanadai walipata taarifa polisi, na walihusisha sana na suala la wadada wawili kumwagiwa tindikali Zanzibar.
Hebu fikiria zaidi hapo, Je ni wazungu walikuja kulipiza au ni JK alitaka kusafisha jina kwa Wazungu??
Tujaribu kufikiria zaidi na zaidi.

Kama ni kumuuwa Ponda, ndiyo iwe jana na kwa style hiyo??
Hivi Ponda na JK hawana uhusiano wowote ule hata ktk dini(ukimsaidia muislam mwenzako unapata thawabu kwa mwenyezi mungu).
JK anajulikana ni mnafiki sana, mtu wa kuuma na kupuliza, na mambo ya u. . .i yumo, kwanini asijionyeshe kwa wazungu kwamba anamshughulikia Ponda kama kuwaridhisha wazungu lkn in real sense Ponda ni jamaa yake kwa hiyo anafanya ambush kuonyesha alitaka kummaliza Pinda lkn akamkosakosa akampa ya bega kidogo, wazungu wanatulia wanaona jamaa kweli anafuatilia.
Tujiulize na kufikiri zaidi na zaidi.
 
Mtoa mada ana hoja.Kutokana na Nchi yetu kuwa Uchi ni rahisi kwa Majasusi wa Nchi zingine kuingia na kufanya hujuma.Mfano wale Mabinti waliomwagiwa Tindikali Zanzibar wana nasaba na Israel;Hujuma za Israel zinajulikana Duniani kote.Vilevile Rwanda ina watu Kibao humu nchini na Generali Kagame alishatoa lugha ya Vitisho kwa hiyo lolote linawezekana.
angalau wewe umemuelewa mtoa mada, yote yanwezekana lakini humu sijui kuna watoto wa shule za msingi
 
lane point yako ya 4 na ya 5.....

Inaongea zaid ya ulichoandikaa...
Natafakari mpaka kichwa kinauma.
 
Last edited by a moderator:
Kauli mujarab punda mkaidi hendi pasina kichapo: yoyote yule anayelenga kuleta uchochezi na ashughulikiwe ipasavyo; Ponda ashukuru tu polisi wenyewe voda fasta kama ingekuwa ni wale polisi wa kweli tungekuwa tunaongea mengine.
Umelewa ushabiki wa kushabikia ccm mpaka huwezi hata kufikiri. Unasema wangekuwa polisi wa kwrli tungeongea mengine, kwamba ulitamani Shehe Ponda auawe au?
Wewe ndio mpuuzi kabisa.
 
Nakubaliana na wewe hata mwangosi hakupigwa na polisi, wale wananchi kule arusha hawakuuwawa na polisi, yue kijana pale morogoro haikuwa polsi pia.
 
Umejichanganya sana ndugu yangu!

Naomba utofauti kati ya serikali na polisi....Kama unakiri serikali ina mkono kwenye tukio la Sheikh Ponda basi polisi ndo wa kwanza kabisa kuhusika kwenye upigaji risasi. Na hili wamelithibitisha wenyewe kwamba walipiga risasi na mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi wa Sheikh Ponda.

Kutokana na matukio yaliyowahi kutokea polisi wakiwa "kazini" nashawishika kusema kuwa haihitaji akili ya chuo kikuu kubaini kuwa serikali kupitia jeshi la polisi iko nyuma ya tukio hili!

Cha ajabu kama wanamtafuta mtu ni kwa nini wasitoe taarifa rasmi kwa mhusika ili kama anaweza kujisalimisha ajisalimishe....Huu utaratibu wa polisi kusaka watu kama majambazi utawagharimu sana...

Polisi kamwe hawataweza kutokomeza uhalifu kwa kutenda uhalifu dhidi ya watuhumiwa! Waanze wao kutii sheria bila shuruti!

SOMA TAARIFA YA JESHI LA POLISI HAPA>>>

Taarifa za Jeshi la Polisi kuhusu Shekhe Ponda.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jeshi la Polisi Tanzania.
Dar es salaam agosti, 10, 2013

1. Mnamo tarehe 10, Agosti, 2013, majira ya saa 8 mchana, maeneo ya shule ya msingi ya kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro kulifanyika kongamano la Baraza la Eid lililoandaliwa na Umoja wa wahadhiri mkoani Morogoro,
Dakika chache kabla ya kongamano hilo kumalizika alifika Shekhe Ponda issa Ponda alizungumza kwa muda mfupi.

2. Kongamano hilo ambalo lilifungwa majira ya saa 12:05 jioni,
Ambapo watu walianza kutawanyika, baadhi yao wakiwa wamezingira gari dogo alilokuwa amepanda Shekhe Ponda baada ya kutoka katika eneo hilo, askari wa Jeshi la Polisi walilizuia gari hilo kwa mbele kwa nia ya kutaka kumkamata Shekhe Ponda ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi sehemu mbalimbali hapa nchini yenye mlengo wa kusababisha uvunjifu wa amani.

3. Baada ya askari kutaka kumkamata, wafuasi wake walizuia ukamataji huo kwa kuwarushia mawe askari wa Jeshi la Polisi, kufuatia na purukushani hizo askari walipiga risasi hewani kama onyo la kuwatawanya.

4. Katika vurugu hizo, wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha mtuhumiwa, hivi sasa imethibitishwa kuwa Shekhe Ponda yupo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akitibiwa majeraha katika bega la mkono wa kulia linalodaiwa alilipata katika purukushani hizo.

5. Kufuatia na tukio hilo timu inayoshirikisha wajumbe toka jukwaa la haki jinai ikiongozwa na CP Issaya Mngulu imeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

SSP Advera Senso

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.


998570_488248254592757_534728210_n.jpg
 
Mtoa mada alikuwa na mawazo kama Yangu,kama. Kweli polis wanamtafta kwann wasmfate Moi?wanaishia kutaka ajitokeze,hiz kweli n drama wanacheza kupumbaza wavivu wa kufkir kama ww unaetukana hapa,huyu jamA hayapigwa risas,na kama kapigwa n kapigwa na ndugu zale waliokuwa wamemzunguka,kwan haingii akilin mtu azungukwe na kundi la watu afu risas impate yy tu,jitokezen wengine waliopata majera katka hyo ktu,afu Kwan Ponda ndo nan hasa wa kutufanya tumuongelee kiasi hiki!?Jk utakuka kuilipa huo uoga unaoufanya kwa huyu She+ani!
 
Hakuna ulevi mbaya kama kulewa DINI. Bora hata pombe waweza kuamkia supu ikakutoka. Kwa sababu ya ugumu wa maisha na uelewa mdogo watu wengi wamejiingiza kuwa wakereketwa wa DINI hali inayowafanya kushindwa kupambanua mambo kwa KINA. Hongera kwa kujaribu kusumbua akili mkuu na kufikiri kwa MANTIKI. Waache waliolewa katika ulevi wao.
 
Kama alipigwa riasasi na byunduki ya Policcm kwenye hilo tukio - swali ni je kuna ganda la risasi kwenye crime scene, na je hilo ganda la risasi liko compatible na aina za byunduki walizokuwa nazo askari wa policcm? Theory nyingine inaweza kuwa kwa vile Sheikh ni mpambanaji, yeye na wenzake inawezekana wakaona watumie mwanya huo kwa kumtandika risasi begani ili waamshe hamasa ya wafuasi! Mnakumbuka yule Sheikh wa UAMSHO aliyejiteka?
 
Kwa mtazamo wangu ponda kapigwa risasi na mtu ambaye alikuwa amepangwa,sema tu hakuwa sharp shooter,he/she missed the target...walichokosea police ni kumfukuzia ponda kwa nyuma..wangetaka kumpata vizuri wangemplant snipper maeneo ya pale alipokuwa anahutubia...my take😛onda was to be assasinated by government machinaries but their plan was shallow
 
Umelewa ushabiki wa kushabikia ccm mpaka huwezi hata kufikiri. Unasema wangekuwa polisi wa kwrli tungeongea mengine, kwamba ulitamani Shehe Ponda auawe au?
Wewe ndio mpuuzi kabisa.

Wewe ndiyo mpuuzi Ponda atakuwa shekhe kwako wewe usiyeijua dini kwangu mimi Ponda ni mtu wa kawaida anayetafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutumia dini; kwenu mtu akivaa kanzu nyeupe, kofia ya kitunga na kusoma surat al baqarah basi ndio amekuwa shekhe? Kama umekosa fikra na hekima huwezi kuwa shekhe hata siku moja na huyo mtu hana sifa hata moja ya kuwa shekhe; wewe mtu ni mpuuzi sana mtu anataka kulazimisha mauti yake mimi nimuonee huruma ya nini? huyo hafi shahidi hata siku moja hatetei uislamu ana ajenda zake binafsi hivi haya ni mapandikizi ya kihutu na kitusi yana ajenda nyingine wanataka tu kutumia dini kuvuruga amani yetu; haya ndiyo yale aliyozungumza Mtikila; jiulize amezukia wapi?
 
Kama alipigwa riasasi na byunduki ya Policcm kwenye hilo tukio - swali ni je kuna ganda la risasi kwenye crime scene, na je hilo ganda la risasi liko compatible na aina za byunduki walizokuwa nazo askari wa policcm? Theory nyingine inaweza kuwa kwa vile Sheikh ni mpambanaji, yeye na wenzake inawezekana wakaona watumie mwanya huo kwa kumtandika risasi begani ili waamshe hamasa ya wafuasi! Mnakumbuka yule Sheikh wa UAMSHO aliyejiteka?

Ukimtazama vizuri sheikh poda machoni unagundua anaigiza, hii ni drama Kama ya babu wa loliondo. Yawezekana hamjui risasi ni kitu gani Afya mbovu kama ya ponda apogwe risasi huo mdenge usidondoke

Natoa miaka 1000 ijayo, kama Tanzania itayafikia maendeleo japo nusu yake ya yaliyofikiwa hivi sasa na Japan, Singapore, Taiwan au Korea, basi watakaokuwepo waje kwenye kaburi langu Singida walichape fimbo tu nami nitafufuka kushuhudia maendeleo hayo. Nchi imejaa watu ambao wanajiona wana akili na kujilinganisha na akina Newton. Lilipigwa bomu kanisani, kina "Newton" wakadai waislamu hao!-adui wa kweli akasepa. Lilipigwa bomu mkutano wa Arusha akina "Newton" wakadai wamejilipua ili wapate popolarity na kura za huruma! Adui halisi akasepa. Akatekwa Dkt Ulimboka, Newtons wa Tanzania wakaja na theory nyingii-wengine mara wamechukuliana wanawake, wengine fedha, wenggine alijiteka, wengine alitekwa na watu haki za binadamu ili chama fulani kipate popularity-alimuradi wingi wa wanachoita "conspiracy theory".

Cha kushangaza, leo hii mtu aliyeshuhudia yoooote hayo yaliyotokea na kuendelea anakuja tena na conspiracy theory eti ni "drama" au "wafuasi wake wamempiga risasi ili waamshe hamasa za wafuasi wake"! (Sasa mbona hawajaamka hii hypothesis inaendeleaje kuwapo?) Isitoshe wao wakati nyie "mnadhani" na kuandika kupitia Keyboard, kuna watu wameandika kupitia kuwapo kwenye tukio na kushuhudia kwa macho. Bado mtu anakuja na "conspiracy theory" Aisey. Narudia tena, hata miaka 1000 ijayo kwa akili hizi za kinewton hazitakuja kubaini matatizo ya umaskini wa Tanzania na kuyatatua. This is what we call products of thoughts-the way you think, the way it becomes, the way you conclude, then the way problem is over!

Ndio maana haishangazi kuona baada ya miaka mingi ya ugunduzi wa hesabu, akina Newton wetu hapa hawana jibu la moja+moja kama jawabu ni ngapi (1+1=?), imekuwa hesabu ya midahalo makongamano, warsha nk; but no solution yet.
 
Kauli mujarab punda mkaidi hendi pasina kichapo: yoyote yule anayelenga kuleta uchochezi na ashughulikiwe ipasavyo; Ponda ashukuru tu polisi wenyewe voda fasta kama ingekuwa ni wale polisi wa kweli tungekuwa tunaongea mengine.
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom