Hello Great Thinkers wa JF,
Kwanza natanguliza samahani kwa yeyote ambaye nitakuwa nime-mkwaza na title yangu na content ya thread yangu. Lakini naomba mnivumilie na kunisikiliza japo kidogo kwnai nia yangu ni njema kabisa.
Sasa katika kutafakari swala zima linalohusu sheikh ponda, nimejikuta nina maswali yasiyo na majibu ambayo baomba niwashirikishe nyote:
Najiuliza kwamba;
1. Kulikuwa na sababu gani ya polisi kumpiga risasi sheikh ponda? je walishindwa kumkamata sehemu nyingine - mathalani nyumbani kwakwe, ofisini kwakwe au hata kumpta taarifa kwamba natafutwa na polisi na hivyo ajisalimishe? Je, ni kweli walikuwa hawajui alipo au wana agenda nyingine nyuma ya hii?
2. Tukifanya assumption kwamba walikuwa hawajui alipo untill alipojitokeza Morogoro; sasa swali ni kwamba kwanini polisi na maafisa usalama hawakumsubiri mpaka amalize mhadhara wake na pengine kwenda kule msikiti wa mungu mojaa dini moja huku wakimfuatilia hadi kumkamata kiurahisi pasipo kusababisha taharuki? Badala yake waliamua kufanya in a public place tena operation iikiongozwa na afisa mkubwa wa jeshi la polsi kamamda shigolile ambaye naamni anafahamu fika impact ya uamuzi wake.
3. Toka jana jioni baada ya kupigwa risasi alikuwa wapi? huduma ya kwanza alipata wapi?. Kwa ufahamuw wangu mimi penetrating chest injury hasa ya risasi ina hatari ya kusababisha lung collapse, bleeding na ashindwe kupumua na kifo kunyemelea fasta. Sasa mbona habari toka itoke kuanzia jana hadi leo ndio wanatuambia yupo muhimbili kwa sasa.
4. Je, hakuna hata mtu mwingine aliyejeruhiswa au hata kuuwawa na risasi za polisi ambao bila shaka walipiga randomly ili kuwadhibiti wafuasi wa ponda? mbona hakuna
5. Ndani ya muda mfupi vyombo vya habari vya ulaya hasa Uingereza vilipata taarifa ya kupigwa risasi sheikh ponda na to my surprise RPC shigolile alikiri mwenyewe kwamba wao polisi ndio wamempiga risasi ponda jamba yupo at large. Hata hivyo huku kwetu polisi kupitia msemaji wao advera wameshakataa hawahusiki. sasa sijui tumwamini advera ambaye yupo ofisini akisubiri taarifa au kamanda shigolile ambae alikuwa frontline
6. Swali la mwisho na la kizushi ni kwamba toka lini seriali imekuwa against na ponda and the like? Je, hawa si wamekuwa wakitoa hate speech na kuhatarisha uvunjivu wa amani lakini serikali imeweka pamba masikioni? matokeo yake watu wamechomewa makanisa, mapadre, wachungaji kuumizwa na wengine kuuwawa at the same time hata pale ambapo evidence isiyo na shaka inaonesha kwamba chuki ya udini unasambaa bado serikali haikuchukua hatua. Sheikh ponda alitajwa moja kwa moja lakini yupo na anadunda. Leo imekuwaje tena serikali hiyo hyo ghafla iamuae kumpiga risasi kama jambazi sugu na hatari? mhhh hapa inakataa kuingia akilini
7. Mashuhuda wa tukio hili walionekana kutoa stori ndefu na detailed yenye kuelezea matukio kwa uafasaha tena wakipangilia na kuwasliasha mada vizuri. Katika hali ya panic ya tukio kama hili huwa unapata some sort of amnesia mpaka ukisha-cool off ndio unaanza kukumbuka matukio kidogo kidogo.
In summary maoni yangu ni kwamba Sheikh Ponda Issa Ponda - Hajapigwa risasi bali hii ni mind spinning ya dola ili kuondoa focus kwenye mambo ya msingi yanajitokeza kila uchwao mfano swala la madawa ya kulevya, usalama katika uwanja wetu wa JNIA, tindikali kwa wale binti wa volunteers wa Uingereza etc
Na kwa kuwa tangia hapo tayari zipo tension ya kidini iliyobuniwa na kuratibiwa na serikali kama namna ya divide and rule machanism ya chama tawala na serikali yake wameona njia mojawapo ya kutuliza munkari upande mmoja wa dini ambao wanaona wanaonewa na serikali na dini nyingine kupendelewa ni kuratibu what I call a pure daytime bluff.
haya ni maoni yangu, nakubaliana na wewe kama hautakubaliana na maoni yangu lakini nakaribisha input, crtique na matusi
asanteni