Constantine Oswald Millinga: Mmoja wa waasisi 17 wa TANU mwaka 1954

Constantine Oswald Millinga: Mmoja wa waasisi 17 wa TANU mwaka 1954

Hotuba ya Samora Machel kuwa hakuna gredi ya mkoloni, wala hatuwezi kujisifia kuwa sisi ni zao la mkoloni mwarabu hivyo ni bora kuliko aliyetawaliwa na mreno, vivyo hivyo hatuwezi kujipiga vifua tulitawali na mjerumani hivyo tu wabora kuliko waliotawaliwa na mwingereza

Ukoloni ni ukoloni tu hauna uafadhali kuwa tujibainishe na wa fulani kwa kuwa tulitupa imani zetu za jadi kijumbatia dini ngeni iliyokuja kwa jahazi mwanzo kabla ya nyingine ikiyofika kwa merikebu .

Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra

Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.

Samoro Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.

Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.

Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.

Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.

Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.

Bagamoyo,
Nakushukuru sana kuweka historia ya Martin Kayamba.

Kwangu mimi imenikumbusha mengi hasa baada ya kusoma wachangiaji wengine wakinishutumu kuwa sina nilijualo kuhusu historia hiyo kama ilivyo katika ''Ten Africans.''

Nimeeleza niyajuayo kuhusu kitabu hicho na nikaweka na kitabu kingine cha nyongeza, ''Modern Tanzanians.''

Kwa kurahisisha naweka kipande kutoka ,''Ten Africans,'' kuhusu Chief Makwaya wa Siha na Sir Ali bin Salim Liwali wa Mombasa kisha nitasherehesha In Shaa Allah:

''Chief Makwaya and Makoni are staunch Mohammedans
and were very particular about food.

Mr. Mitchell arranged with the District Commissioner at Mombasa for Chief Makwaya to consult with Sir Ali bin Salim, K.B.E., C.M.G., of Mombasa in order to remove the scruple from his mind about food.

On 51st March we arrived at Mombasa; the first thing we did was to drive by taxi to the District Commissioner to see Sir Ali bin Salim. The District Commissioner took us to Sir Ali bin Salim, who kindly invited us into his office.

After the matter had been explained to him, he told Chief Makwaya that Mohammedans are not forbidden by their religion to eat food cooked by Christians ormeat of animals killed by Christians or Jews, because Christians have the Gospel (Injili) and Jews have the Deuteronomy (Torati). Both these books come from 'God.

He had been to England himself for one year and during that
period ate the same food which Europeans ate.

The only meat which a Mohammedan is forbidden to eat is pork,
and he strongly warned Chief Makwaya that they should
not touch it.

In confirmation of what he had said he was willing to come on board S.S. Francisco Crispi to lunch with us.

We were very pleased to invite him to lunch.
At 12 noon he arrived on board and had lunch with us.

At 4p.m. he kindly sent his car to take us round Mombasa Island, and we enjoyed the trip very much.''

Chief Makwaya jina lake kamili ni kama lilivyo hapo chini kwenye picha yake.

Walipokuwa safarini kwenda Uingereza yeye alikuwa na hofu na uhalali wa chakula ndani ya meli.

Walipofika Mombasa ikabidi aonane na Liwali wa Mombasa Sir Ali bin Salim apate fatwa.

Sir Ali bin Salim alimtoa hofu.

1710137192770.jpeg

1710132690519.png

Chief Makwaya ndiye aliyeuingiza Uislam Usukumani kwa kuwaleta walimu kutoka Zanzibar.

Angalia mavazi yake.
Bahati mbaya kafariki akiwa na umri mdogo wa miaka 40.

Mtoto wake ambae alikuja kujulikana kama Chief David Kidaha Makwaia akarithi kiti cha baba yake.

Chief Kidaha alibadili dini akatoka Uislam na kuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki.
Akabadili jina lake la Ahmed na kuchukua jina la David.

1710133178704.png

Chief David Kidaha Makwaia​

Mimi nimebahatika kumuona Chief Kidaha Makwaia mwaka wa 1967/68.

Mwanae ambae ndiye chief wa sasa wa Siha, Chief Edward Jonathan Makwaia tukisoma darasa moja St. Joseph's Convent Dar es Salaam yeye ndiye alinichukua kwenda kumsalimia baba yake.

Wakati huo Chief Kidaha alikuwa amehamia Kenya.

Angalia picha hiyo hapo chini huyo katikati ni Edward Makwaia, wa kwanza kulia ni Iddi Mvule na kushoto ni Mwandishi.

Picha hii tulipiga Kilimanjaro Hotel miaka hiyo tuko shule.

1710133643068.png

Chief Kidaha Makwaia ndiye Abdul Sykes akimtaka ajiunge na TAA wamchague President wa TAA na kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kisa hiki nimekieleza hapa mara nyingi.

Naamini wengi mnakifahamu.

Hamza Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere.
Waingereza wana msemo, ''The rest is history.''

Historia hii mimi nimeipokea kutoka kwa Mama Daisy, mke wa Abdul Sykes.

Ni kisa cha kusisimua sana.

Angalia picha nyingine hapo chini Kleist Abdul Sykes na Edward Kidaha Makwaia.

Kulia ni Edward Makwaia na kushoto ni Kleist Sykes nyumbani kwa Kleist Kawe Beach.

Baba zao walikuwa marafiki na watoto wao halikadhalika wakawa marafiki.
Ndipo husema mara kwa mara kuwa mimi ni sehemu ya historia hii.

Sisi ni sehemu ya historia hii.

1710134386623.png
 
View attachment 2931063

View attachment 2930992
Chief Makwaya ndiye aliyeuingiza Uislam Usukumani kwa kuwaleta walimu kutoka Zanzibar.

Angalia mavazi yake.
Bahati mbaya kafariki akiwa na umri mdogo wa miaka 40.

Mtoto wake ambae alikuja kujulikana kama Chief David Kidaha Makwaia akarithi kiti cha baba yake.

Chief Kidaha alibadili dini akatoka Uislam na kuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki.
Akabadili jina lake la Ahmed na kuchukua jina la David.

View attachment 2931012
Chief David Kidaha Makwaia​

Mimi nimebahatika kumuona Chief Kidaha Makwaia mwaka wa 1967/68.

Mwanae ambae ndiye chief wa sasa wa Siha, Chief Edward Jonathan Makwaia tukisoma darasa moja St. Joseph's Convent Dar es Salaam yeye ndiye alinichukua kwenda kumsalimia baba yake.

Wakati huo Chief Kidaha alikuwa amehamia Kenya.

Angalia picha hiyo hapo chini huyo katikati ni Edward Makwaia, wa kwanza kulia ni Iddi Mvule na kushoto ni Mwandishi.

Picha hii tulipiga Kilimanjaro Hotel miaka hiyo tuko shule.

View attachment 2931022
Chief Kidaha Makwaia ndiye Abdul Sykes akimtaka ajiunge na TAA wamchague President wa TAA na kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kisa hiki nimekieleza hapa mara nyiingi.
Naamini wengi mnakifahamu.

Hamza Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere.
Waingereza wana msemo, ''The rest is history.''

Historia hii mimi nimeipokea kutoka kwa Mama Daisy, mke wa Abdul Sykes.
Ni kisa cha kusisimua sana.

Angalia picha nyingine hapo chini Kleist Abdul Sykes na Edward Kidaha Makwaia.

Kulia ni Edward Makwaia na kushoto ni Kleist Sykes nyumbani kwa Kleist Kawe Beach.

Baba zao walikuwa marafiki na watoto wao halikadhalika wakawa marafiki.
Ndipo husema mara kwa mara kuwa mimi ni sehemu ya historia hii.

Sisi ni sehemu ya historia hii.

Shukrani story ya Martin Kayamba ilikosa picha muhimu za Chifu wa Shinyanga Makwaia, Sir Ali Bin Salim Al Busaidi wa Mombasa na sasa historia inazidi kukaa sawa.
 
Shukrani story ya Martin Kayamba ilikosa picha muhimu za Chifu wa Shinyanga Makwaia, Sir Ali Bin Salim Al Busaidi wa Mombasa na sasa historia inazidi kukaa sawa.
Bagamoyo,
Miaka imekwenda.

Chief Kidaha Makwaia ana historia muhimu sana kati ya machifu wakubwa wa Tanganyika.

Angelitaka angekuwa ndiye Waziri Mkuu wa kwanza Tanganyika.

Huwa najiuliza ingekuwaje historia ya Abdul Sykes kama Chief Kidaha angeingia TAA kisha TANU badala ya Nyerere?

Huwa nilikuwa nawaangalia Kleist na Edward kisha hujichekea mwenyewe moyoni.

Sisi tumekuwa marafiki toka udogo wetu na tunaijua historia ya wazee wetu.

Angalia hiyo picha hapo chini na soma majina utajua kuwa nisemayo ni kweli:

1710174750021.png

Kulia waliosimama: Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza.
Kulia waliochutama: Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kaisi.
Picha hii tumepiga nyumbani kwa akina Edward Makwaia, Upanga Road 1968.​
 
Hui..
Lakini wenye kuchapa vitabu hivyo ni wachapaji wakubwa ulimwenguni kama Oxford University Press.

Haiwezekani hawa na wao kama mie wakawa hawana kitu.

Hawa hawachapi mambo ya dini.

Iweje wachape kitabu changu?
Kwa hiyo wachapa vitabu wanajuwa kuliko sisi Watanzania?
 
Kwa hiyo wachapa vitabu wanajuwa kuliko sisi Watanzania?
Hui...
Oxford University Press wana wataalamu wa kila fani uijuayo duniani.

Wachapaji wengine katika nchi zetu wana nafasi ya kuwapata wataalamu waliopo nchini na nchi jirani kwa kila somo.

Nakuambia haya kwa kuwa mimi ni mwandishi nimechapa na Oxford University Press Nairobi na Oxford University Press New York.

Nimechapa na Phoenix Publishers Nairobi na wengine; na nimechapa na wachapaji kadhaa wa hapa nyumbani.

Nakueleza kitu ninachokijua.
 
Haya Mzee ukiwadanganya wewe kwa vile wanakuamini basi inatosha. Lakini ukweli Watanzania wanaujua kuwa Tanzania ni nchi ya wote: Wapagani, Waislamu na Wakristu.

Japo wewe unachuki na Wakristu lakini huma namna wataemdelea kuwapo sambamba na watanzania wengine.
 
Kweli Tanzania ni nchi ya wote lakini historia yake katika kukabiliana na ukoloni imejikita kwa watu maalum ambao historia yake mimi nimeitafiti na kuiandika.

Historia ya African Association kwanza kabisa imeandikwa na Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Katika historia hiyo kaeleza kuwa waasisi wa African Association ni yeye, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Katika hawa hakuna Mpagani.
Waislam wako 6 na Wakristo 3.

Kleist kaeleza sababu ya Waislam kuwa wengi.

Kasema sababu ni kuwa wamishionari wakiwakataza waumini wao kujihusisha na siasa.

Historia ya TANU nimeieleza kupitia Nyaraka za Sykes na hizi nyaraka zipo mpaka leo.

Baada ya kifo cha Kleist 1949 mwanae Abdul akawa Secretary wa TAA halikadhalika akiwa mfadhili pamoja na mdogo wake Ally, Dossa Aziz na John Rupia.

Historia hii hivi sasa ni maarufu.

Abdul Sykes akampokea Nyerere 1952 na TANU ikaundwa 1954.

Hakuna Wapagani wanachama wa TANU wala hawamo katika viongozi.

Tanganyika nchi ya wote lakini waliopambana na ukoloni historia yao ndiyo hii.

Kuwa hii ndiyo historia ya kweli ya Tanganyika na mimi nimeiandika kama ilivyokuwa haina maana imesababishwa na chuki yangu kwa Wakristo.
 
Duh mbona tuliaminishwa TAA & TANU ilikuwa ya Waislam ?.Sasa huyu Mgalatia katokea wapi tena au yule Ustadhi Mohamed Said alimsilimisha maana hata katika kitabu chake cha hustoria ya Kariakoo hajamtia Bwana Millinga kabisa.
acha uchochezi mbona wagalatia walikuwepo kina Mareale,Abel Makaranga,John Rupia,Germano Pacha,Kunambi,Kasela Bantu
 
United Africa

Tuesday, May 7, 2019​

Mtemi Kibete: Shujaa wa Kinyamwezi​

1723305321631.png

Tanzania ina mashujaa wengi katika historia yake. Mashujaa wengi wanasahaulika jinsi muda unavyozidi kupita. Ingawa wakina mama walipata nafasi kubwa za kuchukua uongozi na kufanya kazi kubwa kupinga ukoloni, ni wachache sana wanakumbukwa kwa uongozi wao au jitihada zao katika harakati za kupinga utawala wa kikoloni.

Mmoja ya mashujaa hao ni Mtemi Kibete wa Unyamwezi. Historia ya maisha ya Mtemi Kibete inatufundisha mengi kuhusu maisha yake na historia ya Tanzania, tunajifunza kuhusu baba yake Chifu Mirambo alikuwa ni mtu wa aina gani, na tunajifunza kuhusu ujasiri wa kina mama, nafasi waliyopata kwenye jamii na michango yao kwa taifa letu.

Mtemi Kibete alisahaulika kwa miaka mingi mpaka ilipofika mwaka 1976, wakati huo alikuwa na kama miaka tisini na nne; Mwalimu Nyerere alisafiri kwenda Tabora kumkabidhi nyumba mpya Mtemi Kibete Mwanamirambo, mmoja ya watoto wa Mtyela Kasanda, aliyejulikana zaidi kama Chifu Mirambo. Mtemi Kibete alikuwa ni mmoja ya watoto wa Chifu Mirambo waliokua hai mwaka huo.

Kibete alizaliwa mwaka 1882 na alifariki tarehe 25 mwezi was 12, mwaka 1982. Inasemekana alikuwa bado msichana mdogo wa miaka kumi na mbili baba yake, Chifu Mirambo, alipofariki mwaka 1894. Mtemi Kibete alikuwa mmoja ya watoto saba waliozaliwa na mama mmoja. Baba yake alikuwa na wake wengi walioka katika maboma yake matano, Isela, Meta, Ikonogo, Ukerebe, na Kiburuga. Kibete aliishi na mama yake katika boma la Isela homa.

Boma la Isela lilikuwa na ulinzi mkali. Chifu Mirambo aliweka askari wake hodari waliojulikana kama Warugaruga kulinda boma hilo na maboma yake mengine. Chifu Mirambo alikuwa anahama mara kwa mara kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Alikuwa anaenda boma la Isela na kukaa hapo kwa kama mwezi mmoja kila mwaka. Chifu Mirambo alikuwa anawapenda sana watoto wake. Alikuwa anacheza na Kibete na watoto wake wengine alipoenda kwenye boma lake la Isela. Alikuwa anacheza nao na kuwapa watoto wake wote upendo mkubwa. Hili alilisema Mtemi Kibete baadae. Wavulana wote walichukuliwa walipofika umri fulani na walipelekwa kujiunga na jeshi.

Mtemi Kibete alipewa bangili za shaba alizipata kama urithi kutoka kwa baba yake. Bado alikuwa na bangili hizo mwaka ilipofika akiwa na miaka kama tisini na nne. Hizo bangili za shaba zilitengenezwa na Watusi. Mtemi Kibete alipata kuwa Chifu wa kabila lake kwa kipindi kifupi kabla hajaondolewa na Waingereza. Mtemi Kibete alisahaulika kwa miaka mingi mpaka Mwalimu Nyerere aliposikia kuhusu taabu anazopata mwaka 1976 na uamuzi ukafanywa ajengewe nyumba.

Kibete alipata shida sana kipindi cha utawala wa Wajerumani. Wajerumani walituma wanajeshi waende kuvunja ofisi ya chifu wa Wanyamwezi. Wajerumani walipofika Ulyankulu wakamkuta Chifu Katunga, kaka yake Mtemi Kibete. Chifu Katunga alikuwa anapatana sana na mmoja ya wakoloni waliemwita Bwana Mzuri.

Hakupatana kabisa na mkoloni mwingine aliyejulikana kama Bwana Toronto. Mama yake Mtemi Kibete alikuwa mjasiri sana. Siku moja alitofautiana na mama mmoja alieitwa Machunija. Machunija alikuwa rafiki wa Mabruku, aliyetumwa Tabora na Sultani Said Barghash kutoka Zanzibar. Mama yake Mtemi Kibete alimpiga Machunija. Mabruku akaenda kumshitaki kwa Wajerumani.
Mama yake Mtemi Kibete alikimbia na kujificha Kwande.

Wajerumani wakamuamuru Chifu Katunga amkamate mama yake Kibete. Katunga akakataa. Bwana Toronto akaja na askari wake Ulyankulu. Askari waliwapiga risasi kaka watatu wa Mtemi Kibete, Maswa, Kihana, na Kapaya na kuwaua hapo hapo. Zaidi ya Wanyampala mia nne walikamatwa. Wengine sitini wakakamatwa, wote walifungwa na minyororo na kupelekwa geraza la Wajerumani Tabora.

Bwana Toronto aliamua kuwaadhibu familia yote ya Chifu Katunga. Askari walichukua bunduki zote, ng’ombe wote walioweza kuwapata, pembe za ndovo zilizomilikiwa na familia na wakachoma moto vijiji vitano. Katika heka heka hizo, Watusi walikuja na kuchukua ng’ombe wote waliobaki wakaondoka nao.

Mtemi Kibete na kaka yake Chifu Katuga na wake zake wawili walienda Uha. Askari wa Kijerumani walikuwa wanawafuata wakijaribu kumkamata Katuga mpaka walipofika Lukela. Watu wengi kwenye kundi lao waliuliwa. Safari hio ya kuwakimbia Wajerumani ilikuwa ngumu sana.

Walipata shida sana kupata maji. Njia moja ya kupata maji ilikuwa ni kufuata aina fulani ya ndege waliojua wapi pa kupata maji. Walitumia bunduki moja ya Chifu Katuga kuwinda wanyama kwa chakula. Walikuwa wanaweka kambi kwa siku tatu wakitafuta maji, kama kulikuwa hamna maji, basi waliendelea na safari yao. Pia walikuwa wanakula matunda waliyopata porini. Watu wengi walikufa kwa njaa katika msafara wao.

Kibete bado alikuwa mdogo. Kuna wakati Chifu Katuga ilibidi ambebe Kibete mgongoni wakati wanasafiri. Afya ya Kibete ilikuwa imezoofika sana. Katuga alihakikisha Kibete alikuwa na maji kidogo, ingawa wengine wengi walikuwa hawana maji. Uamuzi huo ulifanya baadhi ya watu kwenye msafari kuamua kuondoka na kwenda kwingine. Walisafiri kwa mguu mpaka Mana za Mlole, sehemu iliyokuwa inatawaliwa na Watusi kipindi hicho.

Chifu wa Watusi aliwakaribisha wote na kuwapa chakula na sehemu ya kukaa.
Bwana Toronto akaja na mpango mwingine wa kumkamata Chifu Katuga. Alituma ujumbe kwa Katuga kumuomba warudi Ulyankulu na kwamba atawajengea kijiji kipya. Katuga na watu wengine 80 walikamatwa na Wajerumani walipofika Bunampanda wakati wakijaribu kurudi Ulyankulu. Mama yake Kibete pia akamatwa Kwande alipokuwa amejificha.

Wajerumani walipanga kumnyonga Katuga, mama yake, na wafuasi wake wengine. Kwa bahati nzuri Bwana Mzuri aliekuwa safarini akarudi. Akafanya uamuzi wasinyongwe na wapelekwe Dar es Salaam. Chifu Katuga akaishi Dar es Salaam kama mkulima wa minazi mpaka alipokufa.
Chifu Katuga alimtuma Kibete na wengine warudi Ulyankulu akiwa Dar es Salaam. Walipofika nyumbani wakamkuta Kaibuka amepewa Uchifu.

Hawakupatana kabisa na Kaibuka, wakaamua kwenda Tabora na kudai haki yao kwa viongozi wa kikoloni. Walipofika Tabora walifanikiwa na Mtemi Kibete akapewa uchifu. Hili lilikuwa jambo la kijasiri sana wakati huo. Kaibuka alikuwa anasaidiwa sana na wamisionari na wakoloni walikuwa wanataka yeye awe kiongozi. Mtemi Kibete alikuwa kiongozi wa nne kushika madaraka tangu Chifu Mirambo alipofariki.

Waingereza hawakutaka kabisa Mtemi Kibete awe Chifu. Wakafanya njama za kumtoa na wakafanikiwa baadae
Mtemi Kibete aliolewa na Kigao, mtoto wa Chifu Ntinginya wa Usongo na Nyawa. Alifanikiwa kupata watoto watatu, wavulana wawili na msichana mmoja. Alikuwa na wajukuu 15 na watukuu 6 mwaka 1976. Aliishi kwa miaka 6 zaidi mpaka alipofariki mwaka 1982 akiwa na kama miaka mia moja na mbili.

Maisha ya Mtemi Kibete yanatupa nafasi nzuri ya kupitia tena historia ya Tanzania. Kuna wengi wametoa mchango mkubwa wakati wa harakati za kupambana na wakoloni. Wachache sana kama Mtemi Kibete wanatambulika kwa mchango wao. Mtemi Kibete ni mfano mzuri wa kuonyesha kwamba wakina mama walipata nafasi za uongozi na walitoa mchango wao mkubwa kwa jamii.
© Azaria Mbughuni
azmbughuni@gmail.com
 
Safari za Lawi Sijaona mwenyewe huko

Maisha ya Lawi Nangwanda Sijaona

View: https://m.youtube.com/watch?v=82xOyiMkHJQ
Mtoto wa Mzee Lawi N. Sijaona aitwae Sijali Adam Lawi Sijaona aliyezaliwa Tarehe 20 June 1955 leo mwaka 2024 katika mazungumzo exclusive na mwandishi mahiri wa historia Tanzania mzee Mohamed Said ..

Mzee Lawi Sijaona alizaliwa mwaka 1928 kijiji cha Mnima wilaya ya Newala nchini Tanganyika karibu na mpaka wa Mozambique.

Mzee Lawi Sijaona alisoma shule maarufu ya St. Andrews College Minaki na kuhitimu ngazi ya Senior Cambridge Overseas Certificate hivyo kupata nafasi ya kujiunga na chuo Kikuu cha Makerere University lakini akaghairisha kujiunga chuo kikuu ili aajiriwe asaidie wazazi wake.

Lawi Sijaona akajiunga na gazeti la Habari za Leo na kupanda ngazi kuwa mhariri wa gazeti. 1955 akajiunga na halmashauri ya wenyeji wa Newala (Newala Local Council) kama katibu wa Council hadi kufikia ngazi ya mwenyekiti wa District Local Council....

Akajiunga na TAA, baadaye TANU YOUTH LEAGUE (UVCCM), TANU ...1958 mkutano wa Tabora pamoja na Mzee Rashidi Kawawa wakapewa jukumu zito ...

Great piece of informative historical commentary about late Mr. Lawi Nangwanda Sijaona
 
By kitoto blog​

Wednesday, 20 July 2016​

LAWI SIJAONA MFANO WA NAMNA TUSIVYOTHAMINI KUMBUKUMBU ZETU​

1733876972424.jpeg

Wabunge wa TANU mwaka 1959. Picha ya Facebook.
Moja ya mambo makubwa niliyojifunza Ughaibuni ni namna wenzetu, (hasa weupe) wanavyothamini mambo YAO ya kale. Na tunaposema “kuhifadhi” si tu watu maarufu au kadhia fulani fulani za kiserikali.
Chukua vyakula. Zamani Wazungu walikuwa wakioka mikate katika majiko ya mikaa, kama leo Afrika. Majiko hayo yalikuwa aina ya tanuri. Kuna kipindi kilioneshwa mwaka jana kuhusu historia ya mapishi. Wakachagua wapishi wanne wa kisasa. Wakawavalisha magwanda ya karne ya kumi nane na kumi na tisa. Tukaoneshwa wakikanda unga na huku ule mvuke na moshi vikiwaghasi. Wapishi wa “kizazi kipya” wakapata shida sana. Mikate ilipokuwa tayari wakaionja. Wakasema mitamu sana.
Lakini ilikuwa pia na chumvi. Ambapo siku hizi kuna uchaguzi Uzunguni wa chakula chenye chumvi au kisichokuwa nayo. Chumvi si kitu kizuri sana kiafya hasa moyo. Moja ya mafunzo hapo ikawa kuwa leo tunaishi kwa afya zaidi kuliko zamani. Wastani wa maisha ya wananchi karne hizo ulikuwa miaka arobaini kama ilivyo nchi maskini. Leo Uzunguni ni miaka 80.
Tuje kwenye umaarufu.
1733877132862.jpeg

Kanisa la Westminster Abbey, London
Makaburi ya wafalme, wasanii, na wagunduzi yamehifadhiwa. Mjini London kuna kanisa maarufu la Westminster Abbey ambapo watu muhimu wamezikwa toka karne nyingi. Afrika bado tunasoma vitabu vya mwanariwaya Charles Dickens, mtunzi Mwingereza aliyeng’aara karne ya 19. Kaburi lake lipo Westminster Abbey. Nyumba aliyoishi imehifadhiwa . Ukiitembelea shurti malipo.
Mwanafasalfa mashuhuri wa Kirumi (Italia) aliyeishi karne ya 15 na 16 ni Nicollo Machiavelli. Mwanafasalfa huyu aliyefariki 1527 anasomwa na takriban kila kiongozi duniani.
Kitabu chake mashuhuri “The Prince” ni kama msahafu kwa wanasiasa:
“Ni bora kuogopewa kuliko kupendwa; kama huyawezi yote mawili bora zingatia la kwanza.”
Ama: “ Ukitaka kujua akili au uerevu wa mtawala chunguza wale waliomzunguka.”
Ingawa aliandika vitabu vingi, The Prince (Mwana wa Mfalme) kinafahamika zaidi.
Kimehifadhiwa (pamoja na chumba na hata meza) aliyoishi mjini Florence, Italia. Miaka mingapi?
Piga hesabu. Toka 1527!
Linganisha na sisi.
Karibuni tunaweza kuhesabu mangapi tuliyoyaenzi?
Kaburi la Mtemi Mkwawa, pale Kalenga , Iringa. Safi. Mti alionyongwa Mangi Meli wa Old Moshi, Uchagani, na wakoloni wa Kijerumani, mwaka 1892. Safi. Mengine, je? Je ukitaka kusoma magazeti ya Uhuru na Mzalendo- niliyokuwa nikiyaandika mwaka 1976?- Je, ukirudi nyuma zaidi hadi Raha Leo aliloandikia Shaaban Robert miaka ya 1940 na 1950? Je kaburi la Shaaban Robert? Je ni kweli kwamba ukitaka kusoma magazeti yetu ya nyuma yameishia mwaka 1982? Je Radio Tanzania? Je ukitafuta sinema aliyoigiza mmoja wa waasisi wa taifa, Rashid Mfaume Kawawa (Muhogo Mchungu) utaipata?
Lazima tujiulize maswali.
Maana sasa hivi kuna mgogoro na kero inayowasakama watoto, wajukuu na familia ya aliyekuwa zamani Waziri katika awamu ya kwanza ya Tanzania. Wangapi wanamkumbuka Lawi Nagwanda Sijaona?
1733877051570.jpeg

Lawi Sijaona ...picha ya Mtandao wa Wazalendo.
Karibuni nilisoma ukuta wa Facebook ambapo picha iliyopigwa mwaka 1959 Bunge la kikoloni, inawaonesha vijana wa enzi hizo, Waafrika wa kwanza kwanza kuingia Bungeni.
Legco. Kirefu chake ni “Legislative Assembly of Mainland Tanganyika.”
Lilianzishwa mwaka 1926 na aliyekuwa Gavana wa Waingereza nchini, Bwana Donald Cameron. Jumla wabunge 20. Picha hiyo ya 1959 inao Richard Wambura, George Kahama, Amir Jamal, Paul Bomani, Rashid Kawawa na Lawi Sijaona. Vijana hawa walikuwa miongoni mwa timu iliyokuwa sambamba na Mwalimu Nyerere kugombania Uhuru wa Tanganyika. Baadaye tukashinda Uhuru. Wakafanywa Mawaziri.
Mishahara yao ililipwa hela ya malkia, yaani Paundi. Rais alipata paundi 3,000 kwa mwaka na Mawaziri wake, £2,300.
Leo mtu akikupa paundi 3,000 ni shilingi milioni 8 na nusu. Ndiyo ni nyingi kwa mtu wa kawaida. Lakini enzi hizo ilikuwa nadra sana kwa mtu kutafuta uongozi wa kisiasa ili kuiba fedha au kufisadi. Walikuwepo “kupe” (neno Mwalimu Nyerere alilotumia kwa “mafisadi” ) lakini ukweli hakikuwepo kitu cha kuiba. Nchi ilikuwa bado inaanza kutembea.
Sikiliza mwandishi wa Facebook:“Lawi Nang'wanda Sijaona ni mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, akifanya kazi kubwa ya kuasisi vyama vya siasa vya ukombozi, tangu TAA, TANU na hatimaye CCM. Alikuwa kiongozi na mzalendo wa mfano wa aina yake, Akifanya mambo mengi makubwa na ya kukumbukwa....Hakuwa "Fisadi", "Mwizi" wala "Mla Rushwa", alikuwa mwadilifu na mtu aliyelinda kwa nguvu kubwa Rasilimali za Nchi hii. Kumbe, mwisho wake akafa, akazikwa na mema yote. Akasahaulika!.”
Hiki ni kimoja cha visa vingi.
Tumesikia baadhi ya viongozi kuuawa kutokana na kujaribu kutekeleza siasa za nchi. Mathalan Dk Wilfred Kleruu aliyepigwa risasi na mkulima wa Iringa mwaka 1972. Baadaye, Saidi Mwamwindi alinyongwa. Uzuri wa kisa hiki ni watoto wawili wa marehemu ( Eva Kleruu na Amani Mwamindi – Meya wa Iringa) kukutana mwaka juzi na kufanya maridhiano – yaani kusameheana.
Hii inakumbusha pia mtoto wa Nduli Idi Amin na Mwalimu Nyerere ambao wamekuwa wakiwasiliana miaka mingi kufuta tofauti za baba zao.
Haya ni machache ya historia yetu.
Lakini je mmesikia barua iliyoandikwa na mtoto wa Waziri huyo wa zamani Lawi Nagwanda Sijaona , mwezi jana kumtaka Mheshimiwa Rais John Magufuli ajaribu kusuluhisha jambo linaloikera familia yake?
Barua inazungumzia kisa cha Mwenge mwaka 1998 maeneo ya Newala, Mtwara. Mheshimiwa Waziri mstaafu Sijaona enzi hizo (kwa mapenzi yake ya taifa) aliazima jenereta la umeme kusaidia shughuli za kukimbiza mwenge. Hadi alipofariki, 2005- barua ya mwanae inadai-mashine haikuonekana. Barua inadai :
“Jenereta ilipotea ingali mikononi mwa Serekali na shauri hilo kufikishwa Mahakamani kama inavyosomeka hati ya hukumu,kesi ya jinai namba 322/1999 na inaeleza thamani yake kwa makadirio ya shs 1,500,000 na kwamba mmiliki wake ni Mzee Lawi Nangwana Sijaona.”
Barua inaendelea kwamba hadi leo, viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa awamo ya nne walielezwa mgogoro. Uamuzi wa kuandika barua ya wazi kwa Rais Magufuli unasisitiza kumbukumbu ya mzee huyo kutothaminiwa, anadai mwanae.
Bila shaka wapo wananchi wengi waliofanya mema na ya maana nchini ambao hawakumbukwi. Marehemu Sijaona ni mmoja wa wanaotukumbusha haja ya kuwaiga wenzetu wanavyoweka heshima za mababu na mabibi zetu kwa karne nyingi.
Habari zaidi wasiliana na Adam Sijaona simu 06581-45681 au 0782704208.
Ilitoka Mwananchi Jumapili
 
MAKALA ZANGU

my regular newspaper writings in East Africa
(Move to ...) Home KITOTO BLOG ▼

Wednesday, 20 July 2016​

LAWI SIJAONA MFANO WA NAMNA TUSIVYOTHAMINI KUMBUKUMBU ZETU​

1734047209827.jpeg

Wabunge wa TANU mwaka 1959. Picha ya Facebook. Picha hiyo ya 1959 inao Richard Wambura, George Kahama, Amir Jamal, Paul Bomani, Rashid Kawawa na Lawi Sijaona

Moja ya mambo makubwa niliyojifunza Ughaibuni ni namna wenzetu, (hasa weupe) wanavyothamini mambo YAO ya kale. Na tunaposema “kuhifadhi” si tu watu maarufu au kadhia fulani fulani za kiserikali.
Chukua vyakula.

Zamani Wazungu walikuwa wakioka mikate katika majiko ya mikaa, kama leo Afrika. Majiko hayo yalikuwa aina ya tanuri. Kuna kipindi kilioneshwa mwaka jana kuhusu historia ya mapishi. Wakachagua wapishi wanne wa kisasa. Wakawavalisha magwanda ya karne ya kumi nane na kumi na tisa.

Tukaoneshwa wakikanda unga na huku ule mvuke na moshi vikiwaghasi. Wapishi wa “kizazi kipya” wakapata shida sana. Mikate ilipokuwa tayari wakaionja. Wakasema mitamu sana.

Lakini ilikuwa pia na chumvi. Ambapo siku hizi kuna uchaguzi Uzunguni wa chakula chenye chumvi au kisichokuwa nayo. Chumvi si kitu kizuri sana kiafya hasa moyo. Moja ya mafunzo hapo ikawa kuwa leo tunaishi kwa afya zaidi kuliko zamani. Wastani wa maisha ya wananchi karne hizo ulikuwa miaka arobaini kama ilivyo nchi maskini. Leo Uzunguni ni miaka 80.

Tuje kwenye umaarufu.

1734047347697.jpeg

Kanisa la Westminster Abbey, London
Makaburi ya wafalme, wasanii, na wagunduzi yamehifadhiwa. Mjini London kuna kanisa maarufu la Westminster Abbey ambapo watu muhimu wamezikwa toka karne nyingi. Afrika bado tunasoma vitabu vya mwanariwaya Charles Dickens, mtunzi Mwingereza aliyeng’aara karne ya 19. Kaburi lake lipo Westminster Abbey. Nyumba aliyoishi imehifadhiwa . Ukiitembelea shurti malipo.

Mwanafasalfa mashuhuri wa Kirumi (Italia) aliyeishi karne ya 15 na 16 ni Nicollo Machiavelli. Mwanafasalfa huyu aliyefariki 1527 anasomwa na takriban kila kiongozi duniani.

Kitabu chake mashuhuri “The Prince” ni kama msahafu kwa wanasiasa: “Ni bora kuogopewa kuliko kupendwa; kama huyawezi yote mawili bora zingatia la kwanza.”
Ama: “ Ukitaka kujua akili au uerevu wa mtawala chunguza wale waliomzunguka.”

Ingawa aliandika vitabu vingi, The Prince (Mwana wa Mfalme) kinafahamika zaidi.
Kimehifadhiwa (pamoja na chumba na hata meza) aliyoishi mjini Florence, Italia. Miaka mingapi? Piga hesabu. Toka 1527! Linganisha na sisi.

Karibuni tunaweza kuhesabu mangapi tuliyoyaenzi?
Kaburi la Mtemi Mkwawa, pale Kalenga , Iringa. Safi. Mti alionyongwa Mangi Meli wa Old Moshi, Uchagani, na wakoloni wa Kijerumani, mwaka 1892. Safi. Mengine, je?

Je ukitaka kusoma magazeti ya Uhuru na Mzalendo- niliyokuwa nikiyaandika mwaka 1976?- Je, ukirudi nyuma zaidi hadi Raha Leo aliloandikia Shaaban Robert miaka ya 1940 na 1950? Je kaburi la Shaaban Robert? Je ni kweli kwamba ukitaka kusoma magazeti yetu ya nyuma yameishia mwaka 1982? Je Radio Tanzania? Je ukitafuta sinema aliyoigiza mmoja wa waasisi wa taifa, Rashid Mfaume Kawawa (Muhogo Mchungu) utaipata?

Lazima tujiulize maswali.
Maana sasa hivi kuna mgogoro na kero inayowasakama watoto, wajukuu na familia ya aliyekuwa zamani Waziri katika awamu ya kwanza ya Tanzania. Wangapi wanamkumbuka Lawi Nagwanda Sijaona?

1734047612430.jpeg

Lawi Sijaona ...picha ya Mtandao wa Wazalendo.
Karibuni nilisoma ukuta wa Facebook ambapo picha iliyopigwa mwaka 1959 Bunge la kikoloni, inawaonesha vijana wa enzi hizo, Waafrika wa kwanza kwanza kuingia Bungeni.
Legco. Kirefu chake ni “Legislative Assembly of Mainland Tanganyika.”

Lilianzishwa mwaka 1926 na aliyekuwa Gavana wa Waingereza nchini, Bwana Donald Cameron. Jumla wabunge 20. Picha hiyo ya 1959 inao Richard Wambura, George Kahama, Amir Jamal, Paul Bomani, Rashid Kawawa na Lawi Sijaona. Vijana hawa walikuwa miongoni mwa timu iliyokuwa sambamba na Mwalimu Nyerere kugombania Uhuru wa Tanganyika. Baadaye tukashinda Uhuru. Wakafanywa Mawaziri.

Mishahara yao ililipwa hela ya malkia, yaani Paundi. Rais alipata paundi 3,000 kwa mwaka na Mawaziri wake, £2,300.

Leo mtu akikupa paundi 3,000 ni shilingi milioni 8 na nusu. Ndiyo ni nyingi kwa mtu wa kawaida. Lakini enzi hizo ilikuwa nadra sana kwa mtu kutafuta uongozi wa kisiasa ili kuiba fedha au kufisadi. Walikuwepo “kupe” (neno Mwalimu Nyerere alilotumia kwa “mafisadi” ) lakini ukweli hakikuwepo kitu cha kuiba. Nchi ilikuwa bado inaanza kutembea.

Sikiliza mwandishi wa Facebook:“Lawi Nang'wanda Sijaona ni mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, akifanya kazi kubwa ya kuasisi vyama vya siasa vya ukombozi, tangu TAA, TANU na hatimaye CCM.

Alikuwa kiongozi na mzalendo wa mfano wa aina yake, Akifanya mambo mengi makubwa na ya kukumbukwa....Hakuwa "Fisadi", "Mwizi" wala "Mla Rushwa", alikuwa mwadilifu na mtu aliyelinda kwa nguvu kubwa Rasilimali za Nchi hii. Kumbe, mwisho wake akafa, akazikwa na mema yote. Akasahaulika!.”

Hiki ni kimoja cha visa vingi.
Tumesikia baadhi ya viongozi kuuawa kutokana na kujaribu kutekeleza siasa za nchi. Mathalan Dk Wilfred Kleruu aliyepigwa risasi na mkulima wa Iringa mwaka 1972. Baadaye, Saidi Mwamwindi alinyongwa. Uzuri wa kisa hiki ni watoto wawili wa marehemu ( Eva Kleruu na Amani Mwamindi – Meya wa Iringa) kukutana mwaka juzi na kufanya maridhiano – yaani kusameheana.

Hii inakumbusha pia mtoto wa Nduli Idi Amin na Mwalimu Nyerere ambao wamekuwa wakiwasiliana miaka mingi kufuta tofauti za baba zao.
Haya ni machache ya historia yetu.

Lakini je mmesikia barua iliyoandikwa na mtoto wa Waziri huyo wa zamani Lawi Nagwanda Sijaona , mwezi jana kumtaka Mheshimiwa Rais John Magufuli ajaribu kusuluhisha jambo linaloikera familia yake?
Barua inazungumzia kisa cha Mwenge mwaka 1998 maeneo ya Newala, Mtwara. Mheshimiwa Waziri mstaafu Sijaona enzi hizo (kwa mapenzi yake ya taifa) aliazima jenereta la umeme kusaidia shughuli za kukimbiza mwenge. Hadi alipofariki, 2005- barua ya mwanae inadai-mashine haikuonekana.

Barua inadai :“Jenereta ilipotea ingali mikononi mwa Serekali na shauri hilo kufikishwa Mahakamani kama inavyosomeka hati ya hukumu,kesi ya jinai namba 322/1999 na inaeleza thamani yake kwa makadirio ya shs 1,500,000 na kwamba mmiliki wake ni Mzee Lawi Nangwana Sijaona.”

Barua inaendelea kwamba hadi leo, viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa awamo ya nne walielezwa mgogoro. Uamuzi wa kuandika barua ya wazi kwa Rais Magufuli unasisitiza kumbukumbu ya mzee huyo kutothaminiwa, anadai mwanae.
Bila shaka wapo wananchi wengi waliofanya mema na ya maana nchini ambao hawakumbukwi.

Marehemu Sijaona ni mmoja wa wanaotukumbusha haja ya kuwaiga wenzetu wanavyoweka heshima za mababu na mabibi zetu kwa karne nyingi.
Habari zaidi wasiliana na Adam Sijaona simu 06581-45681 au 0782704208.
Ilitoka Mwananchi Jumapili
 
Watu wamedanganywa sana na historia ya upande mmoja ya mzee Mohamed Said iliyojikita kwa "wazee wake" wa Kariakoo zaidi
 
Mzee Said hawezi kuwataja sana watu kama hawa, kisa kivuli cha dini.
Yaani kwa akili za mzee Said, Uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya juhudi za waislamu wa Pwani (watu ambao kielimu na kivita) walikuwa nyuma sana, anasahau kabisa juhudi kamili za kupigania Uhuru zilipiganwa zaidi na wapagani wengi na wagalatia wa Tanganyika.
Pia inaonekana wagalatia wengi ndio walikuwa na elimu dunia ya kuijenga nchi baada ya kupata uhuru.
 
By Martin Kayamba, 1935

My Life and Work in East Africa

I was born on 2nd February, 1891, at Mbweni, Zanzibar. I am the first son of Hugh Peter Kayamba. He is one of the sons of Chief Mwelekwanyuma of Kilole, son of Kimweri Zanyumbai (Kimweri the Great) King of Wakilindi. The Wakilindi are a ruling clan, who ruled over the Wasambaa and other tribes in the coastal areas of Tanga prior to the German occupation of these countries. The first Mkilindi named Mbega came from the hills in the Handeni area. He was a famous hunter and through his hunting prowess and generosity was chosen by the Wasambaa to be their ruler. Chief Mwelekwanyuma was appointed by his father as Chief over the Wabondei and the Coastal section from Pangani to Vanga.
View attachment 2929489

View attachment 2929491
Source: TEN AFRICANS : MARGERY PERHAM : Free Download, Borrow, and Streaming : Internet Archive

TAA, TANU na CCM waliaminisha historia isiyo sahihi kuwa wasomi ni wale tu waliokuwepo miaka ya 1950 wakati usomi Tanganyika umeanza tangu 1895

Page-105-pic-6-Hugh-Peter-Kayamba-Henry-Masibu2-179x300.jpg

Photo : Martin Kayamba’s father Hugh Peter Kayamba (left) and Henry Masibu (right). Photo courtesy of www.bloxhamschool.com

Pointi muhimu sana hii katika vuguvugu la kuleta harakati za kujitawala Tanganyika ambayo haiongelewi kabisa wakati Martin Kayamba pamoja na wenzie wakafikia kwenda Uingereza mwaka 1924 kuiwakilisha Tanganyika katika kuzungumzia mustakabali wa Tanganyika.

Mambo kama haya hatuwezi kuyapata kwa mzee Mohamed Said !
 
Mambo kama haya hatuwezi kuyapata kwa mzee Mohamed Said !
Yoda,
Martin Kayamba mimi nimemsoma zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Naijua historia yake vizuri.

Martin Kayamba kutokana na taazia iloyoandikwa na Erica Fiah alipofariki kaelezwa kama mtu aliyekuwa akijipendekeza kwa Waingereza.

Erica Fiah anasema katika taazia hiyo katika gazeti lake Kwetu kuwa Waafrika hawakunufaika na chochote kutoka kwake.

Yapo mengi uwezayo kuyapata kutoka kwangu.
 
Huna kitu wewe babu zaidi ya agenda ya Uislamu na unaowaita wazazi wako. Tulishakupuuza na tunaendela kukupuuza
 
Back
Top Bottom