Content Creators mnaoanza (Episode I): Unatumia camera gani kutengeneza maudhui yako?

Content Creators mnaoanza (Episode I): Unatumia camera gani kutengeneza maudhui yako?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu, especially mnaopenda tasnia ya "content creator" kwenye social media, naanza kwa kuwauliza, unatumia camera gani kurecord video?
images (13).jpeg

Iwe ni kwaajili ya YouTube, au kwaajili ya Instagram au TikTok, quality ya video na audio jumlisha na storyline nzuri ndio vitakavyokuweka tofauti na wabwatukaji wengine mitandaoni.

Topic za mic nzuri na storyline tuziweke za siku nyingine, leo tuangalie camera nzuri ya bei rafiki na accessories zake utakazo weza kutumia kutengeneza high quality video.
images (12).jpeg

Hatutaongelea camera kubwa kama DSLR tutajaribu kuongelea izi aina tatu portable, if possible na accessories zake (sio lazima hizi):

1. Smartphone:

Hii ndio namba moja na haina mpinzani. Kwanza portable, battery zinakaa sana na chaji, haiitaji accessories nyingi, na kila siku zinazidi kuadvance.
images (14).jpeg

Unavyochagua simu kwaajili ya kurecord tunaangalia sana resolution, ukubwa wa lensi, frame rate na ..
  • Resolution angalau 1080p ila 4K sahivi ni muhimu.
  • Ukubwa wa lensi (itasaidia kurecord wakati wa giza)
  • Frame rate utaona wameandika 30fps, 60fps kubwa is better na ndogo ni best wakati wa slo-mo record.
  • Stabilization (ingawa ni digita) ila tunaweza kusolve kwa gimbal.
images (6).jpeg

Kumbuka, kama unarecord kwaajili aya YouTube shorts, Instagram Reels au TikTok, hakikisha simu yako iko vertical (imesimama/portrait) na sio vertically.
images (15).jpeg

Kama una record kwaajili ya YouTube video, utatakiwa kuilaza camera (landscape).

Accessories zinazoendana na simu itategemea unarecord ndani au nje, na stationary au upo on motion.
images (8).jpeg

Kama ndani utahitaji chanzo cha mwanga (hii topic ya siku nyingine) na stand ya kushika simu yako.
be81d1a77ef57047e317010628217726.jpg_720x720q80.jpg

Kama una record nje mchana, unaweza kutumia mwanga wa jua na ukatumia stabilizer (gimbal) kufanya video iwe nzuri.
images (7).jpeg

Recommendation: Ikijaga kwenye ishu ya video recording, iPhone hana mpinzani. Sio lazima ununue latest model, ila kwa sasa (2024) ukipata kuanzia iPhone 8Plus au X kuja juu sio mbali. Ingawa kuna video nzuri tu nimeziona za iPhone 7 na ukioneshwa unaweza usiamini.

Mbali na iPhone, Samsung nae siku hizi ameanza kumkatamata iPhone kwenye tasnia ya video kama budget sio issue, hizi kuanzia S20 kuja juu nazo zipo vizuri kwenye Video.

Pixel ni mkali kwenye picha, kwa vifeo labda hizi latest models (Pixel 7 kuja juu)!

2. Action Camera

Hii kama unapenda kurecord video katika extreme conditions (sports) kama vile jogging, baiskeli, pikipiki, racing, kuogelea, etc.
images (4).jpeg

Hizi camera zina stabilization kubwa sana, zina himili mazingira ambayi simu haiwezi ata kusogea, etc.
images (5).jpeg

Hizi hazihitaji accessories nyingi, zaidi itataka mount kama unaiweka kwenye helmet au unaiweka kwenye dashboard.

Challenge kubwa ni bei na battery zake hazikai sana na chaji, unless uwe na battery za ziada, na pia kuna case ya overheating (GoPro ugonjwa wake)!

Recommendation: Hapa hapana utata, mkali ni GoPro angalau kuanzia GoPro 7 (wali introduce hypersmooth kwaajili ya stabilization, ile kitu muhimu sana). Hii bei inaanzia 500k.
images.jpeg

Ila kama budget iko vizuri wacheki na wakali wa camera DJI Action especially 3 kuja juu. Kwa Action 3 bei inaanzia kama 500k na inaweza kushuka zaidi kwani Action 5 inatambulishwa huu mwezi (September)!
images (2).jpeg

Kama unapenda majonjo wacheki na Insta 360 nishawahi ijaribu sikuipenda ila kwa wanaofanya kuendesha pikipiki ni tamu sana.
images (3).jpeg

Nilipenda sana invisible selfie stick unakua kama umepiga picha na mtu mwingine kumbe umejipiga mwenyewe.

Ila zote ni nzuri, kikubwa unataka nini kwenye video zako.

3. Travel camera/Stabilization camera

Hivi vizuri kwa wazee wa vlog za kutembea kwani ni portable, na vidogo sana ila vinatoa video zenye quality ya hali ya juu na stabilization matata kwasababu zimetengenezwa na mechanical stabilization zake sio kama digital stabilization za kwenye simu na action camera.
images (9).jpeg

Hapa hadi sasa sijaona zaidi ya DJI Pocket series ingawa kuna wachina wenzake wameanza kutoa cheaper version mfano Feiyu Pocket 3 ila bado bei ya moto kiasi, kwa sasa Feiyu ni Tsh 900k nimeona.
images (10).jpeg

DJI Pocket 3 ni latest na bei Mil 2+ ila unaweza chukua Pocket 2 sio mbaya kwa Mil 1.

Addition:

Unaweza kuongeza B-Roll cameras (hizi sio main cameras) mfano Drones kuongeza utamu kwenye video zako, especially video za nje.

Kama una swali au kitu cha kuongeza unaweza weka kwa kudiscuss.

Episode II nitaongelea Lightings especially kwa simple video za ndani (sio ulivyofikiria).
 
Gimbal model gani ni nzuri na inaanza kucheza kwenye ngapi i mean ya simu
Gimbals za DJI ndio the best, zinaitwa Osmo Mobile ndio flagship. Zipo 1 hadi sasa latest OM 6. Hapo unakuta hadi laki 5 kwenda juu.

Ila kwa matumizi ya kawaida unaweza chukua za makampuni mengine, mfano Zhiyun, Feiyun wanatengeneza gimbals nzuri za 150k hadi 100k.

Ila itabidi ununue AliExpress maana kibongo nilikuta moja inauzwa Tsh 250k used wakati AE mpya full combo 120k.
 
Na mzgo unaweza chukua mda gani mpaka kufika bongo?
 
Kama unatumia simu kurekodi video usiulize swali lolote wewe nunua iPhone tu. Hata kama ni picha za biashara kupiga bidhaa nunua iPhone. Kama ni nature na landscape ndio fikiria hao kina Sony na Google Pixel.
 
Nilikuwa na underestimate sana hii tasnia ya video recording, ila baada ya kuwa mpenzi wa youtube channels nimekuja kujua kuna watu wanatumia very expensive equipments kwenye recording, hasa camera na drones, video drones zinafika hadi 40000 usd!!
It is, a very expensive hobby
 
Wengi siyo hobby, ni kazi inawaingizia pesa nyingi sana.
 
Umenena. Kwenye video iPhone hana mpinzani.
 
Nilikuwa na underestimate sana hii tasnia ya video recording, ila baada ya kuwa mpenzi wa youtube channels nimekuja kujua kuna watu wanatumia very expensive equipments kwenye recording, hasa camera na drones, video drones zinafika hadi 40000 usd!!
It is, a very expensive hobby
Ni moja ya hobby ambayo kila siku unaona kitu flani kinamiss unataka uwe perfect.

Mi napenda vlog mambo yakikaa nitanunua Osmo Pocket 3. Aisee ile kitu ina high quality video.
 
Wengi siyo hobby, ni kazi inawaingizia pesa nyingi sana.
Unajua nini kaka,

Influencers na content creators "wetu" wa IG, YT na TikTok wanakosea kitu kimoja.

Wanaanza kutengeneza video kwa madhumuni ya kuget paid. Ila ni vizuri kuanza kwanza kama hobby kisha mapato baadae.

Kuna dada nishawahi kwenda nae shopping ya vifaa vya kurecord ni content zake za TikTok aisee, ananunua kwa hisia na ushauri.

Niliangaika sana kumshauri.
 
Back
Top Bottom