Control Number imepunguza Wizi

Pesa inakusanywa kisawasawa. Tumepunguza utegemezi wa bajeti
 
Wahasibu siku hizi hata tai hawavai tena kama zamani tuko nao karume tunagombea tishirt form six
Labda hao waliovamia fani. Au unamaanisha makarani? Maana kila mtu anajiita mhasibu. Angalia kwenye bodi ya wahasibu NBAA mhasibu ni mtu mwenye sifa zipi.

Hao hela ipo. We utapataje hela na mhasibu akose?
 
From the income side YES
What about the expenditure side. Huko ndio Kuna madudu, gari ya kawaida kabisa inanunuliwa kwa shilingi milioni Mia Saba badala ya milioni sabini.
Weka control number na huko
 
Labda hao waliovamia fani. Au unamaanisha makarani? Maana kila mtu anajiita mhasibu. Angalia kwenye bodi ya wahasibu NBAA mhasibu ni mtu mwenye sifa zipi.

Hao hela ipo. We utapataje hela na mhasibu akose?
Wahasibu wanaisoma
 
Wizi umepungua ila haujaisha kwani hujasikia hela za miradi zinaliwa na miradi inatekelezwa chini ya kiwango na C. A. G akikagua hesabu unasikia halmashauri zinapata hati chafu maana yake kuna hela zimeliwa.
 
Umeshawahi chukua police loss report!?
Kwanza gharama halisi ni 2,500/- kwa item moja... ipo hivi
1. Ukienda polisi kutaka loss report, utaelekezwa kwa wale wenye laptop na printer pembeni ya kituo cha polisi
2. Utaombwa kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA, then watakwambia kukutengenezea CONTROL NUMBER utaambiwa 1,000/-
3. Utatengenezewa then utaenda kulipa kwa wakala... 500/-
4. Utaambiwa kulipa 1,000/- kukuprintia hard copy ya loss report

Jumla 2,500/-.

Sasa itokee una items mbili za kuziandikia loss report. Kwanza utaambiwa kila moja na control namba yake... Ndo utaishia kulipa 5,000/-... Mfano umepoteza simu ya laini mbili... kila namba watakutaka utengeneze control namba take
 
Unaongea nn wewe? Loss report Ni Tsh. 500/= huko kwingine Ni kwasabu wewe Ni Ngumbaru
 
Unaongea nn wewe? Loss report Ni Tsh. 500/= huko kwingine Ni kwasabu wewe Ni Ngumbaru
Asante mkuu...!!
Ila nimekupa uhalisia..
1. Hata passport ya kusafiri ni Tshs 150,000/-.. Sasa wewe uwe na hiyo tu, uone kama utaipata.
2. Driving licence ni Tshs 70,000/- nenda nayo hiyo uone kama utaipata
etc

Kuna hidden costs ambazo pengine nyingine ni rasmi na nyingine siyo rasmi, process nzima ikaoelekea hayo ya ongezeko la gharama yatokee

Kuna kuingia mtandaoni kwenye page ya polisi na unajaza mwenyewe

Kuna kwenda polisi kupewa hiyo control namba

Kuna kufanya printing ili upate hard copy...

Hiyo proces inakuvusha kwenye hiyo 500/-.
 
Mkuu inaonekana unpenda sana short cuts ndio maana unapigwa.
Passport ni 150000 na nimepata kwa bei hiyo sikuongeza hata mia labda usafiri tu na 5000 ya mwanasheria .
Loss report ni 500 unaongeza na 500 ya kuprint, hii loos report unaitengeneza mwenyewe mtandaoni hadi kufikia kupata control number ,uwe tu na details zako hata kwenye simu unafanya.
 
Asante kwa kumuelimisha huyo Miss Ngumbaru. #Elimu kwa Walioikosa#
 
So ulitakaje?
 
Huo ni ujinga wako ndo maana unapigwa hiyo 2500
Kikawaida inatakiwa utumie 1000 tu
500 kulipia 500 print
 
kweli isee tena pale mawasiliano kituo cha polisi nimetoa pesa imeniuma sana...
 
Zama za ujima zimekujaa kichwani
 
Huo ni ujinga wako ndo maana unapigwa hiyo 2500
Kikawaida inatakiwa utumie 1000 tu
500 kulipia 500 print
Haya bwana... ila at least wewe pamoja na kupinga, bado umesema hiyo 1,000/- na si anayeng'ang'ania 500/-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…