Cool James Dandu (Mtoto wa Dandu) - Biography

Cool James Dandu (Mtoto wa Dandu) - Biography

Hayo yalifanyika katika kipindi kifupi sana,na kuna jamaa ambaye alikuwa .mtu wa karibu na marehemu akawa anamega kisela

ni kwamba watu walichukulia tofauti kwa kitendo cha mke wa Dandu (dada anayeonekana katika wimbo wa jaydee USIUSEMEE MOYO) kuolewa na rafiki wa karibu wa marehemu Dandu ambaye toka kabla Dandu hajafariki palikuwapo tetesi kwamba wanatoka tena akaolewa naye katika kipindi kisichozidi mwaka tokea Dandu afe.
 
ni kwamba watu walichukulia tofauti kwa kitendo cha mke wa Dandu (dada anayeonekana katika wimbo wa jaydee USIUSEMEE MOYO) kuolewa na rafiki wa karibu wa marehemu Dandu ambaye toka kabla Dandu hajafariki palikuwapo tetesi kwamba wanatoka tena akaolewa naye katika kipindi kisichozidi mwaka tokea Dandu afe.

Mh aisee, alikuwa mzuri kwl yule mmachame
 
Nyota wa bongo fleva za mwanzo kabisa nyota iliyozimika ghafla kwa ajali ya gari akiwa anapanda kwenye kilele cha mafanikio na umaarufu
Leo hii amesahaulika na hakumbukwi tena
Mke wake mwenyewe kashaolewa na mthungu hamkumbuki ndio sisi wa kando binadamu tumeumbwa kusahau.Anakumbukwa kwa mazuri yake tuu.
 
JAMES Dandu ‘Mtoto wa Dandu' siyo jinageni katika gemu la Bongo Fleva lakini niwangapi wanamkumbuka na wanautambuamchango wake katika gemu la Bongo Fleva ?Ungana nami ili kumjua kwa kina .'
1436909373129.jpg (mtoto wa dandu) enzi za uhai wake .

HISTORIA YAKE KWA UFUPI
James Dandu au kwa jina lingine Cool JamesMassive ' CJ Massive ' alizaliwa Julai 5, 1970,Mwanza nchini Tanzania . Alisoma shule yaMsingi Kurasini na baada ya hapo , yeye ,mama yake na ndugu zake walihamia jijiniStockholm , Sweden alikoishi kwa kipindikirefu.

ALIVYOINGIA KWENYE GEMU
James Dandu aliingia rasmi kwenye sanaaya muziki mwaka 1988 akiwa jijini Stockholmambapo alitoa singo kadhaa zikiwa katikastaili ya Euro -House. Mwaka 1992 aliachiaalbamu yake ya kwanza ambayo hata hivyohaikupata mafanikio makubwa. Mwaka 1993 , aliungana na msanii mwingine kutoka Afrika Mashariki , Andrew Muturi nakuunda kundi lililokwenda kwa jina la SwahiliNation. Wasanii wengine wawili wakajiungakwenye kundi hilo.

Baadaye, James Dandu alijitoa kwenye kundihilo na kuungana na Mkongomani, Jose Masena ' Black Teacher ' na kutoa albamumbili zilizowatambulisha vyema sehemu mbalimbali ; Undercover Lover ( 1992) na Zooming You ( 1995 ) iliyokuwa na wimbo ulioitwa Dr . Feel Good . Wakapata mafanikiomakubwa na kuingiza mkwanja wa maana .

AREJEA BONGO KWA KISHINDO
Kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na mwenzake, Black Teacher , Mtoto wa Dandu aliamua kurudisha majeshinyumbani kwa lengo la kuja kuibua na kuinuavipaji Tanzania na Afrika Mashariki kwajumla. Aliporudi Bongo , alikuja na staili mpya yauimbaji wa nyimbo za taratibu ( R & B ) ambaohaukuwa umezoeleka sana kwa kipindi hicho.Akajipatia umaarufu mkubwa ndani ya kipindikifupi.Hakuishia hapo , aliendelea kuingiza ubunifukatika kazi zake , akawa anachanganya R &Bya kisasa , Rhumba na Ndombolo (staili iliyokuwa maarufu sana nchini Zaire kipindi hicho) . Akatoa albamu nyingine kama Soft Like a Pillow ( 1997 ) , Bi Harusi ( 1998 ) na Sukuma Land ( 2002 ) .

Miongoni mwa ngoma ambazo mpaka leozikipigwa lazima watu watulie ni SinaMakosa ambayo aliurudia wimbo wenye jinahilohilo uliopigwa na Les Wanyika kutokaKenya. Ngoma hii ilimtambulisha kinomaAfrika Mashariki yote , hususan nchini Kenya.Pia alifanya remix ya wimbo wa Mamu akiwana mkali Madilu System ambao ama kwahakika ulibamba mbaya !

TUZO ZA KILI
Mwaka 1999 , James Dandu aliamua kuanzisha tuzo alizoziita Tanzania Music Awards ambazo hivi sasa zinajulikana kama Kili Music Awards baada ya kuanza kudhaminiwa na bia ya Kilimanjaro . James Dandu ndiye aliyefanikisha usajili wa tuzo hizo kwa kushirikiana na Basata chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni ( kipindi hicho).

KIFO CHAKE
Mtoto wa Dandu alifariki Agosti 27, 2002 ,kwa ajali ya gari iliyotokea eneo laMakumbusho jijini Dar es Salaam , nyota yakeikiwa inang ' ara kinoma na kuzusha simanzikubwa miongoni mwa mashabiki wake ,hususan wanawake ambao walikuwamashabiki wake wakubwa.Akaenda kuzikwa nyumbani kwao , Mwanza .Wakati anakufa, alikuwa bado hajamaliza kurekodi kazi zake mpya katika Studio ya Master Jay. Aliacha watoto wawili wakiwabado wadogo pamoja na mjane , Devotha .

MIAKA 12 BAADA YA KIFO CHAKE
Ni miaka 12 sasa imepita tangu Mtoto wa Dandu aliporejea kwenye makazi yake ya milele. Swali ambalo mimi na wewe tunapaswa kujiuliza , je, anapewa heshima anayostahili hata kama alishatangulia mbele za haki ? Familia yake wakiwemo wanaye Caroline -Jamie 'Malaika ' aliyezaliwa mwaka 1994 na Michael James Junior aliyezaliwa 1997 wananufaika na matunda ya kazi za baba yao?

Nawashauri waandaaji wa Tuzoza Kili wamuenzi James Dandu japo kwa tuzo ya heshima!
 
Back
Top Bottom