Sasa nadhani unazungumza toka katika kichwa chako, huna ushahidi wowote wa kuweza kufunga mkono hoja zako.
Mara baada ya huu ugonjwa kuingia, uliona jinsi wabunge na watangazaji wa TBC na wakuu wa wilaya walivyokufa haraka haraka, na vifo vyao vilitangzwa, ina maana bado wabunge wanakufa lakini hawatangazwi?, bado watangazaji na watu wengine mashuhuri pamoja na viongozi wanaendelea kufa lakini hawatangazwi?, wewe mtaani kwenu wamekufa wangapi?.
Wacha kufikiria vitu bila kutumia akili. Jinsi Tanzania tunavyojiachia bila kuchukua tahadhari, tayari nyumba na familia zingekuwa zimepukutika, na enzi hizi za mitandao ya Kijamii, huwezi ficha vifo vya vingi. Kelele za wapinzani hakuna mtu angeweza kuzizuia.