Corona imefutika Tz, mara wagonjwa ni wanne tu, mara wamesalia wagonjwa 66. Majirani mnakwama wapi?

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Duh! Kama kuna nch imejichokea kwenye hili la corona basi ni Tz, yaani wakuu wote wanapishana kauli, hakuna anayesema kimoja na mwenzake, halafu wataalam wote walishajipigia kimya. Mkulu kasema juzi corona imefutika kabisa kwao, wazri wa masuala ya afya akasema wamesalia wanne, waziri mkuu jana akasema wamesalia 66, wananchi nao hamna cha tahadhari tena, full misongamano, halafu idadi kubwa ya raia wao wanaojaribu kuingia kwenye mataifa majirani wanakutwa na kirusi.

Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Halafu yote hayo, video zinaendelea kutupiwa kwenye mitandao, kama hii ya BBC ambayo madaktari wa Tz wanaeleza ukweli wa hali ilivyo japo kwa kujificha.

Hili ni taifa LA Mungu, tunalindwa na Mungu pekee. Nyie Endeleeni kutegemea wanadamu wenzenu.

Dunia yote inategemea hekima iliyopewa na Mungu, yaani unamshika simba kidevu halaafu unajisifia kulindwa na Mungu??? Watu bado mnasongamana kwenye vilabu vya pombe na machangudoa na kuendelea kujisifia...
 
Wivu na kijiba cha roho kitakuua, kuishi Tz raha sana. Achana na sokoni, njoo uone kumbi za starehe, mpira uwanjani kama kawa, live bendi bar kama kawaida, nyama choma ndo usiseme. Hata hao wazungu mnaowaabudu huko huku bongo wanajichanganya katikati ya umati wa watu. Na hakuna maambukizi mapya. Tukiwaambia Mungu hachunguziki muwe mnaelewa.
 
Wanasubiri maiti zao kuokotwa mitaani . Hakuna tena anayejua ukubwa wa janga hili nchini. Wanaougua hawaendi hospitali bali kupiga nyungu mwanzo mwisho. Akipona heri, na asipopona pia yote heri .
 
Baadhi ya majirani zetu hawa ni washamba kupindukia, ona hizi comment zao humu. Alafu viongozi wao sasa ndio washamba zaidi yao, eti waziri mkuu anasema bila aibu kwamba anayestahili sifa ni Magufuli. Utadhani Magufuli ni jina la chanjo flani hivi au tiba.
 
MK254,

Sina uhakika Kama hujui kuwa status ya covid 19 kwa Kila nchi "is a moving Target". Data ya leo ni tofauti na ya Jana. Ungekuwa na hoja ya msingi Kama viongozi wetu hawa wawili yaani waziri wa afya na waziri mkuu wangetoa data tofauti kwa siku huyo hiyo moja.

China wagonjwa walipugua hadi kuwa chini ya 50 lakini leo wako zaidi ya 200!!

MK254 njoo hapa utueleze wachina wameikimbia Kenya kwa ajili ya Nini? Au huna habari hiyo? maana wewe haujambo kwa kujitoa ufahamu!
 
Baadhi ya majirani zetu hawa ni washamba kupindukia, ona hizi comment zao humu. Alafu viongozi wao sasa ndio washamba zaidi yao, eti waziri mkuu anasema bila aibu kwamba anayestahili sifa ni Magufuli. Utadhani Magufuli ni jina la chanjo flani hivi au tiba.

Ndio hawa hawa

2404415_IMG-20200520-WA0032.jpg
 
Sina uhakika Kama hujui kuwa status ya covid 19 kwa Kila nchi "is a moving Target". Data ya leo ni tofauti na ya Jana. Ungekuwa na hoja ya msingi Kama viongozi wetu hawa wawili yaani waziri wa afya na waziri mkuu wangetoa data tofauti kwa siku huyo hiyo moja.

China wagonjwa walipugua hadi kuwa chini ya 50 lakini leo wako zaidi ya 200!!
@MK254 njoo hapa utueleze wachina wameikimbia Kenya kwa ajili ya Nini? Au huna habari hiyo? maana wewe haujambo kwa kujitoa ufahamu!

Wachina kuikimbia Kenya sio issue kubwa maana sisi hatufanyi ujinga kama wa kwenu kujichokea na kuacha kuendelea kupambana dhidi ya corona, tunaitangaza kama ilivyo, iwe ikulu au gheto.

Hivyo tunaitangaza ilivyo ndio kama ukiona kama vipi ihame nchi urudi kwenu kisha utakuja siku itatulia, ila nyie hapo mnang'ang'ania muingie kwenye nchi za watu bila kupimwa.
 
Corona ipo na haishi leo wala kesho chukua tahadhari
 
Baadhi ya majirani zetu hawa ni washamba kupindukia, ona hizi comment zao humu. Alafu viongozi wao sasa ndio washamba zaidi yao, eti waziri mkuu anasema bila aibu kwamba anayestahili sifa ni Magufuli. Utadhani Magufuli ni jina la chanjo flani hivi au tiba.
Wewe imekuuma nn?
 
Wachina kuikimbia Kenya sio issue kubwa maana sisi hatufanyi ujinga kama wa kwenu kujichokea na kuacha kuendelea kupambana dhidi ya corona, tunaitangaza kama ilivyo, iwe ikulu au gheto.

Hivyo tunaitangaza ilivyo ndio kama ukiona kama vipi ihame nchi urudi kwenu kisha utakuja siku itatulia, ila nyie hapo mnang'ang'ania muingie kwenye nchi za watu bila kupimwa.
Wachina wa Bongo wapo ila walio Kenya wanataka kukimbia! Halafu jua hawa watu wana mtandao hivyo wanajuana vizuri waliopo huku na waliopo huko. Shida ni kubwa huko kwenu jomba!
 
Hao wapo Bongo maana hawajui kulikoni, nch mshajichokea kila kiongozi na tamko lake, mara corona festival eti imefutika, mara wagonjwa wanne mara sitini na sita, ilhali kila mkiingia kwenye majirani zenu wote mnakutwa na corona.

Sasa wageni wote walioko huko hawajui wala hawana namna ya kujua kichwa wala mkia mpo mpo tu mumejichokea kisa umaskini, na ndio maana kwa mataifa yote duniani nyie ndio Ulaya na Marekani wamewapa watu wao tahadhari ya kutotoka nje hovyoo.
 
Hao wapo Bongo maana hawajui kulikoni, nch mshajichokea kila kiongozi na tamko lake, mara corona festival eti imefutika, mara wagonjwa wanne mara sitini na sita, ilhali kila mkiingia kwenye majirani zenu wote mnakutwa na corona. Sasa wageni wote walioko huko hawajui wala hawana namna ya kujua kichwa wala mkia mpo mpo tu mumejichokea kisa umaskini, na ndio maana kwa mataifa yote duniani nyie ndio Ulaya na Marekani wamewapa watu wao tahadhari ya kutotoka nje hovyoo.
Si kweli US hajatoa alert kwa Tz peke yake!
Kwa sasa Uganda ndo anatupa mwanga nchi ipi imekubuhu kwa maambukizi ya #covid19;You always take the lead
 
Back
Top Bottom