Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Jaribu halitatupata kamwe isipokuwa lililokawaida,lkn katika yote kumbuka Bwana ataleta mlango wa kutokea.....halafu Mungu hapendi ROHO iangamie siyo mwili huu wa nyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nawashangaa sana hawa wanaojiita manabii, mitume na wachungaji kwa kuvuliwa nguo na COVID-19.

corona ndio ilitakiwa iwe kitu ya kuchukulia point tatu za kiubwete katika nyakati hizi.
Boss imani yako ndio itakuponya mimi sio nabii au mtume, ndio maana hata Yesu hakuwa akiponya wasio na imani wale wenye imani ndogo kama punje ya radani.

Unataka kuniambia hujawahi kumuona mtu au hata wewe binafsi ukiwa na dalili zote hizo zinazofanana na corona kabla hata haujagundulika?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji28][emoji28][emoji28]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
We roho mtakatifu wakuweza kukujulisha jambo hilo inamaana huna?

It's Scars
Jambo dogo katika maisha, elezea kwann unaamini baba uliye naye ndiyo baba yako LIMEKUSHINDA umebaki una DUWAA Kama panya aliyezingirwa.

Halafu unajitutumua kujadili jambo kubwa linalohitaji fikra na ufahamu usio na kipimo
 
Umedata kapime Corona pengine imepanda kichwani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kama muislamu najibu kwa mujibu wa uislamu , kwanza tambua kwakuwa unamuabudu M/mungu haina maana hautapata misukosuko hata manabii walipata shida ,wapo ambao waliouawa na binaadamu kwa ajili ya dini , Allah anasema kwenye Quran na tutawajaribu yaani tutawapa mitihani inayotokana na khofu ,njaa ,kupungukiwa mali ,vifo , ila wape bishara njema wale watakaosubiri na kutokufuru Mungu kwa magumu wanayopitia watu ambao watakiri kuwa wameumbwa na Mungu ,na kwa Mungu ndio marejeo yao....

Pili mzee mabalaa mengine yanakuwa ni hasira ya Muumba kutokana mabaya tunayofanya ,labda kukisiri kwa ushoga ,labda serikali zinajiona Miungu watu ,kusiri mauaji ya halaiki na Hapa Muumba anasema akileta balaa lake hatachagua wanaoumubudu na wasiomuabudu wote atawachapa kupembua atafanya baada kufufuliwa

Tatu haya majanga yalitokea au yalitabirirwa kuwa kuna wakati yatatokea mfano Mtume Muhammad alisema "Inapotokea magonjwa kama haya ya maambukizi mfano wa tauni basi watu wa sehemu usika ilioathirika wasitoke ilo eneo mpaka ugonjwa uishe na wale walio nje ya eneo wasiende mpaka ugonjwa uishe the same scenario na hii self isolation ,Swadaqa Rasuulu Llah
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kua habari za mungu sio za kufikirika kama ilivyo spiderman?

Unaweza kuthibitisha?

It's Scars
Kwa sababu habari za spiderman inajulikana kabisa ni kitu kilichobuniwa kwa ajiri ya movie,hakuna hata mtu aliyewahi kudai uwepo wa spiderman nje ya masimulizi ya movie. Lakini habari za madai ya uwepo wa Mungu zipo kwenye maisha halisi wanayoishi watu na zimeathiri maisha ya watu hivyo huwezi kufananisha na movie za spiderman.

Suala la kwamba kuwa kweli Mungu yupo au hayupo ni jambo lenye kujadaliwa hadi sasa.
 
Yani anashindana na viumbe dhaifu alivyoviumba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kushindana na kiumbe dhaifu kama yeye alivyo na maamuzi na alikuumba kwa mfano wake hivyo hivyo nawe unamaamuzi
Kama ambavyo wewe hujaamua kumuamini basi hawezi kukulazimisha your not a robot
MUNGU hawezi kuatafuta Watu kwa kuwahonga vitu ili wawe wake anatafuta wenye utayari

Kazi kwako sasa
 
Unachokihoji wala hakina relation yeyote na hoja yangu, hapa vyoona mwisho wa siku utauliza mbona simzungumzii baba yako

Kwanza kabla ya kutaka kuamisha magoli kwa wakulima nataka nijue hii hoja ya wanasayansi kua na dini tumeimalizaje??

It's Scars
Sio kawaida yangu kabisa kuamisha magoli,nimekuuliza swali hilo likuwa ndani ya tunachojadili. Nimekwambia mwanasayansi kuwa na dini ni sawa tu na mfanyabiashara kuwa na dini au mkulima kuwa na dini,kila mmoja hapo ana shughuli yake. Sasa wewe unahoji tu kwanini huyo mwanasayansi(mwanadini) asitumie dua badala ya sayansi katika kutatua matatizo mbalimbali? Ndiyo nakuuliza mbona auhoji hivyo kwa mkulima kwamba aache kulima na kuomba dua tu? Au kwa mfanyabiashara?
 
Kwa nini kiumbe kimekuwa dhaifu?
 
Hapa naona unaelekea kwenye hoja nyingine fikirishi zaidi. Haya enhe Scars hakuchagua kuwa hivyo alivyo. Hivyo unamaanisha kwa neema ya Mungu scars kapendelewa kwa kuumbwa sio chizi wala sio mwanamke malaya. Lakini hapa duniani kuna machizi na wanawake malaya wengi sana hivyo nao pia hawakuchagua wawe hivyo kama ilivyo kwa scars. Kwa hii nadharia yako inaonesha wazi kuwa
1. Mungu ana upendeleo kwenye uumbaji
2. Anawaonea watu kwenye adhabu ya moto kwasababu yeye Mungu kumbe ndiye anayepanga wawe hivyo walivyo hakuna mtu anayeweza kuchagua awe vile alivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…