battawi said:
Hapa umeniamsha Ndugu yangu
Mimi nakuthibitishia
35:
3. Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnako geuzwa?
5. Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu.
9. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma Pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyo kufa (mvua ikanyesha), tukaifufua ardhi( kwa mvua hiyo) baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyo kuwa kufufuliwa (siku ya mwisho, Na Je ni nani anayeweza kuyafanya hayo asie kuwa Mungu?).
11. Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu (cha Mungu). Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu. (je ni nani mwengine ayafanyaye hayo asiekuwa Mungu ikiwa unamjuwa)?
34:38. Na wanao jitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu ( hapa duniani kabla ya kufa na siku ya kiama).
Hebu kiri ukweli huu kama kuna yeyote anaye yamiliki haya
huu ndio ushahidi wangu, nipe wa kwako basi