Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Mungu ni hadithi zilizo nje ya uhalisia

Uhalisia unao uzungumzia wewe ni upi ? Unaujua ?
ndio maana uwepo wake hauthibitishiki nje ya masimulizi yakufikirika

Hivi ushawahi kujiuliza kwanini unawaona watu fulani na unaweza kujifunza kupitia wao kwa kuwaona, lakini huwezi kujiona wewe mwenyewe kwa kile kitendo cha kuona ? Huu tunauita MPAKA/MIPAKA,kama yalivyo macho kwayo huwezi kuona nje ya upeo na ndivyo vivyo akili ina ukomo wake, nyinyi mmeifanya akili ndio kila kitu hali ya kuwa akili ina ukomo wake na majukumu yake, sasa unajaribu kuipa kazi ambayo haiiwezi matokeo yake mnakanusha mambo ambayo hamjui na msio weza kuthibitisha kutokuwepo kwake, huu ni ujinga ulio komaa.

Lakini masimulizi ya kufirika yana sifa gani ? Je mfano wake ni kama yale ya "The Big Bang Cosmology" au "Solar System" au "Landing on the Moon" au "Philosophical Ligic" za kina Plato na Aristotle ?
The same goes with Spiderman
Tatizo la mifano bado lina wasumbua sana nyinyi watu.

Ahsante.
 
Nini maana ya neno "dini"?
Dini ni mfumo wa imani inayoamini kuna muumba wa vitu vyote ambaye ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Dini huusisha ibada ya kuabudu na kuomba huku wakiamini huyo muumba atawasikiliza na kuwatatulia hayo maombi yao

Kwani shehe alikufundisha dini ni nini?

It's Scars
 
Kwa hiyo hilo gonjwa la town mungu alilileta kisha akasubiri aombwe ndio aliondoe?, usiniambie hakujua lilipotoka hadi likaua watu wakamuomba ndio akaliondoa.

Mungu hawezi kuzuia gonjwa kabla halijaua watu wake ama hua hajui linapotokea anakija kushtuliwa na maombi?😀😀.

Ukimwi, kansa bado maombi hayajamfikia ili ayaondoe kama alivyoondoa town au hajui kama yapo?

Tuendelee kuomba mkuu.
Kwa hiyo maswali yanayomhusu Mungu unaniuliza mimi? kwamba kwa nini Mungu anaamua kutoa adhabu watu waangamie halafu baadaye ndo aingiwe na huruma au kutokana na maombi ya watakatifu wake azuie maafa zaidi. Haya mambo yapo wazi kwa kila mtu kutambua wala huhitaji kuniuliza mimi maswali, sana sana na mimi nitakwambia sijui..
 
Dini ni aina ya siasa lengo lake mama ni kumtawala mtu
Mimi niliacha kuamini dini miaka karibu 7 iliyopita angalia sasa hivi hivi wanavyotapata ombeni mtapewa ombeni basi wagonjwa wa corona wapone wakina gwajima mwamposa wezi wakubwa na kodi inaitwa sadaka
 
Mkuu Scars, tambua ya kwamba yapo majaribu kutoka kwa Mungu na mengine ni ya Ibilisi. Jaribu kutoka kwa kwa Mungu humfanya mtu mwenye imani akapate kuthibitika, bali jaribu la Ibilisi humfanya mtu kukufuru na hata kuangukia dhambini.

Hata siku moja kiongozi wa dini hawezi kutenda miujiza endapo jambo likija kwa makusudi yake. Jaribu litoke kwa Mungu ama Ibilisi, mwenye imani ya kweli tu ndiye atakayeweza kusimama.

Ona mwenyewe, viongozi wa kidini uliowataja, ijapokuwa hujitambulisha kwa vyeo vya kidini lakini hawana jinsi zaidi ya kuitegemea sayansi na teknolojia yake ilete majibu juu ya janga hili la COVID-19 badala ya kusimama ktk maombi yenye kuleta miujiza.

Amini, amini nakwambia, kama vile ambavyo dunia iliumbwa kwa Neno, mwanadamu akaumbwa kwa Neno, wafu hufufuliwa kwa Neno, wenye magonjwa na shida mbalimbali huponywa kwa Neno basi tambua janga hili si kitu chochote mbele za Mungu.

Kiinachokosekana ni watu sahihi wenye kulibeba Neno la kweli katika kipindi hiki cha sasa cha nyakati za kanisa. Kipindi ambacho kinaitwa Laodikia, kipindi chenye imani vuguvugu, si baridi wala si moto. Kwa uvuguvugu huo kwa hakika kimeshatapikwa kutoka kinywani kwa mwenye kulimiliki Neno (Ufunuo 3:14-18).

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu mjuzi wa yote hawezi kua na sifa ya kumjaribu kiumbe wake

Unaweza kuangalia marudio ya mechi ya yanga na simba iliyofanyika wiki tatu zilizopita kwa kutegemea simba haitofungwa na yanga?

Mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye hakuna kitu kinaweza fanyika bila yeye kujua, mungu huyu kumjaribu binadamu kwa kutegemea ataenda kinyume na alivyoona kunamfanya eidha ainekane ni mbahatishaji katika ujuzi wake au Mungu ni mnafiki.

It's Scars
 
Nachoamini Mimi mungu yupo na anamakusudi na sisi watu wake, hata kuja kwa corona ni mpango wa mungu vilevile kuna kitu mungu anataka tujifunze kupitia janga hili la corona,,, kwa uhai nilionao na pumzi ya bure nayofuta bila kulipia chochote naamini kuwa mungu yupo hai na anatenda,, tumshukuru mungu kwa kila jambo hata Kama ni magumu.
Kama corona ni mpango wa mungu basi watu wa dini ni wanafiki maana katika maombi yao tunawaskia kua wakisema corona ni kazi ya shetani hivyo wote tusali ili mungu atuepushie

Lakini ikiwa kama kweli hoja yako ya kusema Corona ni mpango wa mungu, na tunaona corona ikiiua hadi watoto wadogo basi utakubaliana na mimi kua shetani ni bora zaidi kuliko Mungu



It's Scars
 
SHETANI MWENYEWE ANAJUA UWEPO WA MUNGU NA ANAMWOGOPA SEMBUSE WEWE SISIMIZI? NI WAKATI WAKO KUMJUA MUNGU NA KUTUBU SIKU YA HUKUMU YAJA.
Ukinithibitishia kua yupo, mbona fasta tu

It's Scars
 
Mungu ni hadithi zilizo nje ya uhalisia na ndio maana uwepo wake hauthibitishiki nje ya masimulizi yakufikirika

The same goes with Spiderman

It's Scars
Suala la spiderman linajulikana na ndiyo maana hukuti watu wakibishana kuhusu spiderman ila suala la Mungu ni tofauti ni kitu ambacho kina athari kwenye maisha na ndiyo maana watu hudai ushahidi wa uwepo wa huyo Mungu,ni tofauti na na suala la spiderman.
 
Hao Viongozi wa dini pia Usisahau walikemia ebola haikufika nchini sijaona uzi wako ukipongeza dini kufanya maombi kuzuia ebola.

Kama siyo unafiki nini? Watu wanafiki utawajuwa kwa maneno yao.

Dini zimetabili siku za mwisho Kuna majanga yatatoke, janga lazima litoke ili maandiko yatimie. Unaanza kukashifu dini.
 
Kijana swali gani au maswali gani hujajibiwa ?

Hii mada tulishaimaliza kitambo sana, nashangaa unaposema hujajibiwa maswali yako. Siku ukiamua kuwa mkweli ujinga ulio nao utaondoka.
Mada haiwezi kumalizwa kwa kukimbia maswali, nakukumbusha mara ya mwisho umekimbia kwa kuandika "poa" na hii ndiyo slogan yako pindi ukikutana na maswali magumu

Nilikupa option ya kuwauliza masheikh endapo hutaweza kuya handle maswali yangu, nadhani ujio wako wa saizi ni muendelezo wa yale maswali ambayo uliyaweka kiporo

Haya sasa tuambie masheikh wamesemaje juu ya hayo maswali?


It's Scars
 
Ujui ukiandikacho we mbwa mwitu. Na
Usipotubu utakufa hakika.
 
hata kipindi cha manabii wa zamani.
Kulikuwepo na magonjwa ya mlipuko kama haya
NA watu walikufa wengi tu..
IMANI YA KWELI IPO,NA INAANZIA KWAKO.
nadhani kwa vizazi viliyopita Mungu/Allah alikuwa anasikiliza maombi ya wanadamu na kuyafanyia kazi haraka.

ila kwa kizazi hiki cha wachungaji wanzinzi(kama gwajima), matepeli(kama wale mashehe wa instagram),Mungu kaamua kula pozi kidogo ili tunyoke.

Mungu kazia hapohapo ili hawa manabii na wachungaji feki wa kizazi hiki wapate kuumbuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kua wanapona na sio kwamba ni script iliyochezwa na padre/sheikh ili kuwateka watu kiakili?

It's Scars
Kijana naona umekariri ndiyo maana unashindwa kunielewa,narudia tena mie sizungumzii masheikh wala mapadri bali nazungumzia dua na dua hufanywa na muumini yeyote sio suala la masheikh wala mapadri hapa. Na kuhusu kupona kweli ni kuondoka kwa hilo tatizo,maana kama hilo tatizo haliji tena maana yake ugonjwa umepata tiba.
 
Naweza kujadili chochote kile kwa namna ambavyo kimesimuliwa hadithini bila kujali uhalisia wake.

nikiandika kauli hapa inayozungumzia uwezo wa spiderman kupanda kwenye maghorofa marefu, pamoja na jitihada zake za kuzuia treni kwa nyuzi za buibui, hiyo itamaanisha kwamba spiderman is real and not fictional character?


Unaweza kuthibitisha huyo huyo Mungu mmoja yupo?

It's Scars
Ndio
 
Back
Top Bottom