Huwezi kunisaidia mimi kujua Biblia maana nimezaliwa hadi nafikisha umri huu sijawahi kujisumbua kusoma kitabu cha imani ingine.
Mission ya Yesu ilikuwa ni kuwakomboa wenye dhambi hakuja kuwakomboa wale wanaomjua Mungu mfano Yohana mbatizaji hakuja kwa ajili yake alikuja kwa ajili ya wazinzi, wauwaji kama Petro wasio mjua Mungu na hata kuiheshimu siku ya sabato n.k.
Sasa error hapo ni ipi?
Amin nakuambia ,hata mafarisayo walidhani hivyo
Inakuaje yesu kijana mdogo awafundishe taurati Vijeba vya kiyahudi.
Lakini kumbe mambo sivyo yalivo.
Injili imekuja kuifafanua vyema taurati.
Mfano:-
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja KUITANGUA TORATI AU MANABII; La!, SIKUJA KUTANGUA, bali KUTIMILIZA.
Maelezo
-: BWANA aliposema hakuja kuitangua torati wala manabii bali kuitimiliza…alikuwa ana maana kuwa yeye hakuja kuondoa neno lolote la torati lililosemwa bali alikuja kulifanya kuwa
IMARA ZAIDI..kwa mfano torati iliposema usizini, haikuishia pale tu katika mwili…lakini Bwana Yesu alipokuja alisema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake…si umeona hapo.. hajaiondoa amri ile bali ndio ameikolezea..Ikiwa na maana sio tu kwenda kuchukua hatua ya kuzini ndio iwe kosa hapana bali kitendo cha kumtamani tu tayari ni kosa, hivyo haupaswi kutamani kabisa ili kuitimiliza torati…
Na Qur-an imekuja kufuta makosa ya wajanja waliojipenyeza kwenye dini ya Mungu.
Ili Mungu aabudiwe na waja wake kama Mungu,
Qur an imesema
''walaatakrabu zinaa'' = wala usiikaribie zinaa-
Hivi ndivyo vitabu vya Mungu vinavyowiana,ukiondoa zile hitilafu za kuamini, bado maamrisho ni yale yale.
Soma qur-an ijiongezee maarifa