MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Siyo kwamba corona haipo ipo sana tu na jana tu nimemsikia waziri Ummy akitoa semina kwa wahudumu wa afya jamii watakaokuwa wakitoa elimu alisema kwa siku mbili tatu ni kana kwamba watu wamerelax hawachukui tahadhari, nadhani wanajiaminisha kana kwamba limeisha ila kubwa kinachotusaidia na hili ndiyo mara zote Rais amekuwa akilijenga kwenye akili za watu ni kuondoa hofu maana hofu ndiyo mbaya zaidi kwenye haya mapambano ingawa tahadhari zote ziendelee kuchukuliwa tutalishinda tu
Ni vigumu kuchukua tahadhari bila hofu, fahamu hofu ni hisia za kibiolojia na iliumbwa kwenye miili yetu ili ituwezeshe kuchukua tahadhari panapostahiki, usingekua na hofu hata unaweza kwenda kumshika simba kidevu maana huogopi chochote, lazima jamii iingiwe na hofu ya kufahamu hiki kitu kipo na kinaua, hapo watatia akili na kuchukua tahadhari.